Tuesday, December 25, 2012

Maisha ya Maonyesho na Ubatili




Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? 
(Yeremia 17:9).


Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. (Wagalatia 6:4).


Katika somo lililopita nililoliita Nia ya Ndani ya Moyo niligusia kuhusu umuhimu wa kuwa makini na nia zetu pale tunapomwendea Mungu, maana Mungu anajali sana hizo nia ambazo ndizo zinazoamua endapo atayakubali maombi yetu au tutaishia kupata hasara.


Katika somo hili namwomba Mungu anisaidie kufafanua kwa uwazi zaidi kile ambacho hasa kinaweza kuwa kinaendelea ndani ya mioyo yetu, ambacho ndicho anachokiona Mungu wetu pale anapotutazama.

Monday, December 24, 2012

Ushuhuda wa Adelaida Juu ya Mbingu na Kuzimu



Mwanamke mmoja kutoka Bolivia aitwaye Adelaida De Carrillo alipelekwa Mbinguni na Kuzimu na Yesu Kristo. Kule alionyeshwa ni Utakatifu gani anaotakiwa mtu kuwa nao ili aweze kuingia kwenye UFALME WA MUNGU, na pia ni dhambi gani (ambazo wengi wetu tunadhani kuwa ni ndogo), zinaweza kumfanya mtu aingie Jehanamu.

Friday, December 21, 2012

Maswali kwa Maalim Moses na Ndugu Hamudi




Nawashukuru ndugu Hamudi na Maalim Moses kwa majibu na maswali yenu kuhusu makala yangu ya Ndugu Waislamu Nisaidieni. Mimi naamini lengo letu sote ni kumtafuta na kumtii Mungu wetu aliyetuumba, huku tukiwa na imani kuwa, mwisho wa safari ya maisha haya tutafika kwake mbinguni. Hata hivyo, leo ninayo maswali mengine kwao na kwa Waislamu wengine.

Nia ya Ndani ya Moyo




Tunapofanya jambo lolote, mara nyingi huwa tunasukumwa na nia fulani iliyomo ndani yetu. Kwa mfano, mtu anaweza kumpatia mtu mwingine fedha ili:
  •  Kumsaidia katika mahitaji yake,
  • Kujionyesha mbele za watu kwamba yeye ni mwema,
  • Aweze kuja kumwomba jambo fulani, n.k.

Kwa mfano, katika biashara nyingi utakuta makampuni yakitangaza kwamba: Mteja kwetu ni mfalme; Tuko hapa kwa ajili yako; Tunakuthamini na kukujali; Tumekuandalia bidhaa kabambe kwa ajili yako na familia yako, n.k.

Wednesday, December 12, 2012

Majibu ya Maalim Moses - Sehemu ya II







5. Maalim Moses anasema: Quran ni kitabu pekee duniani ambacho muumini anaweza kukihifadhi kwa moyo. Hamlioni hilo?

Jibu langu:
Ndugu yangu Mzizimkavu, hivi kweli unaweza ukaona fahari na ukajisifia suala la KUKARIRI? Hebu nenda katika taasisi yoyote ya elimu duniani (of course, ukiacha elimu ya Uislamu) – kukariri ni jambo linalopigwa vita. Kukariri hakuna faida yoyote! Kukariri kunamfanya mtu asiwe na tofauti yoyote na roboti au kaseti ambazo ukifungulia zinaanza kutoa tu kile kilichoko ndani ingawa zenyewe hata hazielewi kitu.

Sunday, December 9, 2012

Majibu ya Maalim Moses – Sehemu ya I




Katika makala niliyotoa ambayo yana kichwa Ndugu Waislamu Nisaidieni, wapo ndugu zangu Waislamu ambao wamejibu. Mmojawapo ni Maalim Moses – Mzizimkavu. Nakushukuru Maalim Moses kwa yale uliyosema. Basi na mimi nimeona niseme kuhusiana na kile ambacho amekisema Maalim Moses huku nikiamini kuwa huu utakuwa ni mwanzo na mwendelezo wa mjadala wenye manufaa kwetu sote.


Niwie radhi kwa kuwa sikuweza kukujibu mara moja. Hii ni kwa sababu niliibiwa laptop yangu, hivyo nikawa sina uwezo wa kufanya kazi hii. Hata hivyo, namshukuru Bwana wangu Yesu kwa kuwa amenipatia laptop nyingine na sasa naweza kuendelea tena.

Saturday, December 8, 2012

Je, Walikuwa Binadamu Kama Sisi?




Tunasoma katika maandiko juu ya mambo makubwa yaliyofanywa na watu wa nyakati za Biblia. Mambo hayo yalimfurahisha Mungu kiasi kwamba walioyatenda ilibidi Roho Mtakatifu ayaandike kwenye Biblia. Tunapoyasoma mambo hayo tunatiwa changamoto kiasi kwamba wakati mwingine tunajiona labda sisi ni wa hali ya chini sana na huenda Mungu hatufurahii. Mambo hayo ni pamoja na yafuatayo:

Majibu ya Hamudi – Sehemu ya IV



Adamu na Hawa walifukuzwa Edeni


Ndugu Hamudi, nilikuwa nimeahidi kuwa ningetoa jibu la jumla ili kuweza kuweka maisha ya mwanadamu katika picha yake sahihi; na ili tuweze kuona tulikotokea, tuliko na kwa nini tuko hapa; na ni wapi tunaelekea.


Tunaweza kujadiliana na kubishana sana kuhusu suala la Yesu kuwa Mungu au mwanadamu hadi mwisho wa dunia. Lakini jambo moja ni dhahiri – hatuwezi sote tukawa sahihi. Lakini hebu tuangalie uhusiano wa mwanadamu na Mungu kwa ujumla.

Saturday, November 24, 2012

Mwana Mpotevu




Hadithi ya mwana mpotevu inafahamika kwa wasomaji wa Biblia. Vilevile, inafahamika kwa habari ya uhusiano wake na mtu yeyote asiyeokoka; yaani mwana mpotevu anawakilisha watu ambao hawajaamua kumpokea Kristo awe Bwana na Mwokozi wao binafsi. Hadithi hii inaashiria jinsi ambavyo Mungu amempa mtu wa aina hiyo uzima, afya na baraka nyinginezo, lakini badala ya kukaa nyumbani mwa Baba, ameamua kwenda kule duniani na kuishi maisha ya utapanyaji. Hata hivyo, pale anapotambua kuwa amepotea na kuamua kurudi kwa Baba, muda wote Baba yuko tayari kumpokea kwa furaha na upendo mwingi. Sote tuko hivyo. Hapo ndiko tunakoanzia.

Sunday, November 4, 2012

Kuteswa kwa Ajili ya Kristo





Tunaweza kufikiri kuwa tunapita kwenye hali ngumu maishani mwetu. Lakini mara nyingi huwa tunanung’unika tu kwa sababu hatuna nguo, fedha au chakula.

Lakini wapo watakatifu wa Bwana ambao wamepitia mateso mengi kutokana na ushuhuda wao kwa Kristo, Bwana wetu. Ni kwa sababu walimwamini Kristo, matokeo yake wakajikuta kwenye mateso.

Hata leo wapo Wakristo wengi duniani ambao wanateseka kutokana na imani yao kwa Mwokozi. Lakini kwa neema ya Bwana, wameng’ang’ania imani hii.

Majibu ya Ndugu Hamudi - Sehemu ya III


Leo ningependa kuendelea na kujibu maswali ya ndugu yetu Hamudi ambayo aliuliza kufuatia makala niliyoandika katika blog hii, yenye kichwa kisemacho Ndugu Waislamu Nisaidieni.


ROHO MTAKATIFU


Hamudi anauliza: Sehemu pekee katika Biblia alipotajwa Roho Mtakatifu ni katika Yohana 14:26; “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote niliyowaambia. Ni kipi kile ambacho Roho Mtakatifu ameleta au kufundisha kwa miaka 2000 iliyopita?

Tuesday, October 23, 2012

Majibu ya Ndugu Hamudi - Sehemu ya II



Katika sehemu hii ya pili, ninaendelea na kujibu maswali aliyouliza ndugu Hamudi kutokana na makala yangu niliyotoa katika blog hii yenye kichwa: Ndugu Waislamu Nisaidieni.

Kwa kuwa Bwana Hamudi aliuliza maswali mengi, nimeona ni vema niwe nayajibu kwa mafungu kulingana na yeye alivyoyaweka katika mafungu. Leo tutaangalia fungu la pili la maswali hayo.

Sunday, October 21, 2012

Majibu ya Ndugu Hamudi – Sehemu ya I





Katika blog hii kuna makala yanayosema “Ndugu Waislamu Nisaidieni.” Nashukuru kwamba ndugu Hamudi amejitokeza kujibu maswali yangu kadhaa niliyokuwa nimeuliza. Lakini pia, baada ya kufanya hivyo, ndugu Hamudi ameuliza maswali si machache. Nami nimeona kuwa niyaweke hapa pamoja na kile nilichojibu, kama makala ili kwamba, hata mtu mwingine anayependa kuchangia, afanye hivyo.

Ndugu Hamudi, asante tena kwa maswali yako yenye kutikisa akili na fahamu za mtu. Ni lazima nikiri kuwa haya ni maswali ambayo, hakika, kama hujui sawasawa kile unachokiamini, ni lazima ama utachanganyikiwa au utakimbia.

Sunday, October 14, 2012

Nilihisi kama Mungu Amenisaliti!




Utangulizi kutoka kwa blogger

Je, unahisi kuwa una huzuni kubwa isiyoweza kuondoka, umekata tama, unajiona huna maana, unahisi kama vile Mungu amekudanganya au amekuacha; unahisi kama vile  Mungu si wa kuaminiwa au Neno lake si la kuaminiwa, unahisi kuwa Mungu hasikii maombi yako, hakupendi; unahisi kwamba umeshapoteza wokovu wako, au unahisi kuwa umetenda sana dhambi kiasi kwamba Mungu hawezi kukusamehe tena?

Napenda nikuletee habari njema kwamba, bado liko tumaini, tena kubwa sana kwa ajili yako. Karibu usome ushuhuda huu ambao, si tu ni ushuhuda wa mpendwa aliyepita kwenye mapito kama hayo, lakini pia ni somo zuri mno kiasi kwamba, kama kawaida, Mungu anayo mengi ya kutufundisha kupitia mambo ambayo wengine walipitia kama sisi na wakashinda kwa neema ya Mungu ambayo iko kwa ajili ya kila mwanadamu, ukiwamo na wewe. Pendo la Mungu ni zaidi ya maji ya bahari, hivyo hakika kabisa unayo sehemu yako humo ambayo inakungoja uingie na kupokea.

Tuesday, October 9, 2012

Imam wa Msikiti Aokolewa na Yesu





Zak Gariba ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yao. Kwa sababu ya kulitaja jina la Yesu msikitini, Zak Gariba, ambaye alikuwa ni imam alitupwa si tu nje ya msikiti, bali pia nje ya familia yake. Alikataliwa na kujikuta hana tena ndugu; na akapoteza kila kitu. Matokeo yake alifika mahali ambapo aliamua kujiua. Lakini Yesu Kristo mwenyewe alienda kugonga mlango wa nyumba yake na akayabadili kabisa maisha yake kutoka mautini na kumwingiza uzimani.

Wednesday, October 3, 2012

Jinsi Ibilisi Anavyozuia Maombi Yako


Ndugu msomaji wa blog hii, kati ya makala au masomo ambayo nimeyaandika humu, hili ni somo na ushuhuda mmojawapo wenye nguvu sana ambao, kila mwana wa Mungu atakayeusoma, atapata msukumo wa rohoni usio wa kawaida. Haya ni mafunuo yenye nguvu mno ambayo, hakika yatakuinua kwa kiwango cha juu sana nawe utamshukuru Mungu. Nilipouona ushuhuda huu kwenye mtandao, moyo wangu ulianza kuwaka niweze kuutafsiri harakaharaka na kuuweka kwenye blog hii ili yamkini uweze kuwafikia wapendwa wengi iwezekanavyo.

Friday, September 28, 2012

Ushuhuda wa Victoria Juu ya Kuzimu




Muda Unaisha Haraka!

Huu ni ufupisho wa ushuhuda wa Victoria Nehale
Nilizaliwa na kuishi Namibia maisha yangu yote; na niliyatoa maisha yangu kwa Yesu tarehe 06 Februari 2005. Bwana Yesu Kristo ameshanifunulia mambo mengi katika ulimwengu wa roho ikiwa ni pamoja na safari za kuzimu. Bwana alinipa maelekezo kwamba niwashirikishe watu uzoefu wangu; pia alinionya kuwa nisiongeze wala kupunguza chochote katika vile alivyonionyesha na kuniambia. Wakati nikiandika kitabu hiki, mwishoni mwa 2006, nilishatembelewa mara 33 na Bwana Yesu Kristo. Kila aliponitembelea, Bwana alikuwa akiniambia kabla ya kuondoka: MUDA UNAISHA HARAKA!

Friday, September 21, 2012

Muujiza wa Bwana Yesu Ndani ya Msikiti




Huu ni ushuhuda wa dada mmoja wa kutoka Indonesia ambaye, japokuwa zamani alikuwa Mwislamu (na sasa ni Mkristo), Bwana Yesu alimwokoa kimiujiza yeye pamoja na watu wengine kutoka kwenye janga na mauti ya sunami na tetemeko ambavyo vilisababisha vifo vya mamia kwa mamia ya watu.[Japokuwa video si jambo lenyewe halisi kabisa, lakini imeigizwa kuakisi kile ambacho ndicho kilitokea kabisa].


Je, ni nini kilisababisha hadi Bwana Yesu akaingilia kati wakati ule ambapo kifo kilikuwa hakikwepeki?

Friday, September 14, 2012

Kutoka Kwenye Kundi la Kigaidi Hadi Kwa Yesu





Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa kutoka kwa kijana wa Kimisri ambaye Bwana Yesu mwenyewe alimtoa kutoka kwenye uasi na kumfanya kuwa mtu mpya kabisa anayempenda Bwana Yesu pamoja na wanadamu wenzake wote.

Monday, September 3, 2012

Je, Umechoka?



Bwana wetu Yesu alisema wazi: Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. (Mt. 16:24).
Maisha tunayoishi hayaishi mitihani na majaribu mbalimbali. Mitihani hiyo inaweza kuwa inahusu maeneo ya kiafya, kimahusiano, kiuchumi, kiroho, nk.

Kila mwanadamu katika wakati wowote ule, ni lazima anapambana na uhitaji wa namna moja au zaidi. Mtume Petro anatuambia kwamba tumpinge shetani kila wakati kwa imani thabiti: ... mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. (1 Pt 5:9).

Wednesday, August 29, 2012

Ulinzi Kutoka kwa Waganga wa Kienyeji



Naamini umeshasikia mara kadhaa watu wakitaja kile kinachoitwa “sayansi ya kiafrika”. Kwa kifupi maneno haya yanaongelea kazi za waganga wa kienyeji. Ni wazi kuwa yanamaanisha upigaji ramli, uaguzi, usafishaji nyota, na hata ulozi na mengine kama hayo.

Siku hizi watu wengi wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kupata “mafanikio”, wakiwamo wanasiasa, wafanyabiashara, wafanyakazi, wake, waume, wapenzi, wachumba, wanamuziki, na hata wale wanaotaka  kuwakomesha wabaya wao.

Tuesday, August 28, 2012

Jicho lako likiwa bovu



Bwana wetu Yesu alisema kwamba:
Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza. Angalia basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.

Basi kama mwanga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu iliyo na giza, mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikiapo kwa mwanga wake. (Luka 11:34-36).
Kati ya mambo ambayo adui yetu shetani anajaribu sana kuyafanya ni kuiba muda ambao tunatakiwa kuwa na Bwana – iwe ni katika kumwomba, kutafakari, kusoma Biblia, kusikiliza ibada, n.k. Adui anajua kuwa, kama akiweza kutufanya tutumie muda mwingi kwa ajili ya mambo mengine badala ya Bwana Yesu, basi mwisho wa safari atakuwa ametunasa, maana Biblia inasema wazi:

Sunday, August 26, 2012

Msalaba wa Kristo



Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ndilo jambo kubwa kabisa katika maisha yetu, maana unamaanisha wokovu. Na wokovu ni kila kitu - uponyaji, msamaha wa dhambi, uzima wa milele!

Mimi ninapenda 'country gospel songs'. Naamini nawe utafurahia. Bwana wetu Yesu akubariki.


Thursday, August 23, 2012

Ndugu Waislamu Nisaidieni



Allah katika sura Al-Nisa 4:82 anasema kwamba:

Then do they not reflect upon the Quran? If it had been from [any] other than Allah, they would have found within it much contradiction.

Yaani:

Je, hawaitafakari Quran? Kama isingekuwa imetoka kwa Allah, hakika wangekuta ndani yake sehemu nyingi zinazopingana.

Wednesday, August 22, 2012

Waislamu Wanamgeukia Yesu





Video hii inamwonyesha mtu ambaye ni mzaliwa wa ukoo wa Abu Bakr Saddiq, ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa Mtume Mohammad. Abu Bakr Saddiq pia ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kwenye ulimwengu wote wa kiislamu baada ya kifo cha Mtume Mohammad.

Mzaliwa huyu anaitwa Dk. Nasir Siddiki. Yeye pia ametokea kwenye familia tajiri. Akiwa na umri wa miaka 35 alikuwa tayari ni milionea, huku akimiliki kila kitu cha kupendeza ambacho unaweza kukifikiria – iwe ni magari ya kifahari, majumba, nk.

Monday, August 20, 2012

Free E-Books

Je, umeiona sehemu mpya ya  
Free E-Books hapo juu? 

Fungua sehemu hiyo ujipatie 
E-Books 
za bure ili uweze kujiendeleza 
na kukua kiimani. 

Mungu akubariki.

Saturday, August 18, 2012

Chapa ya Mpinga Kristo - 666


 Kifaa cha kuwekwa kwenye mkono
chini ya ngozi

Makala haya niliyatoa kwenye blog nyingine, inawezekana umeshayasoma, lakini nimeona kuwa ni vema niyatoe tena hapa kwa ajili ya yeyote ambaye hakupata nafasi ya kuyasoma. Hii ni kwa sababu ni makala ya muhimu sana, yanayotuonyesha tuko wapi katika ratiba ya nyakati, majira na unabii.

Utakaposoma kilichoandikwa humu, itakuwa ni jambo jema kuwapatia hata wengine unaowafahamu, ama kwa kwa njia ya baruapepe au kwa kuwaambia wasome makala haya wao wenyewe katika blog hii. Mungu akubariki kwa hilo.

Tuesday, August 7, 2012

Je, Watakatifu Hutuombea Tulio Duniani?



Kanisa Katoliki limekuwa likifundisha kwa miaka na miaka kwamba tunaweza kuwaomba watakatifu walioko mbinguni watuombee kwa Mungu. Je, jambo hili lina ukweli kibiblia? Je, hili ni fundisho la Mungu au ni la wanadamu? Je, mtu anayefanya hivyo anampendeza Mungu au anamuudhi?

Hakuna mahali popote katika Biblia ambapo tumeagizwa kuwaomba watakatifu ili watuombee kwa Mungu. Sasa haya mafundisho yanatoka wapi? Unawezaje kuwafundisha watu kitu kisicho kwenye Biblia halafu usiwe na hatia ya kuongeza au kupunguza ujumbe wa Mungu; maana Bwana anasema kuwa atakayeongeza au kupunguza katika neno lake ana hatia. (Ufunuo 22:19).

Thursday, August 2, 2012

Wana wa Mungu


Nani ni "heroes" wa watoto wako. Je, ni wacheza mieleka? je, ni washika bunduki na wauaji wa kwenye sinema na video? Ukimnunulia zawadi mwanao, je, unamletea nini? Je, ni "toy" ya bunduki au ni nini?

Hatima ya mwanao iko mikononi mwako. Kile unachofanya au usichofanya angali bado mchanga ndicho kitakachoamua maisha yake ya baadaye; na hata uzima au mauti ya milele ijayo.


Contina

Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, ambayo baba zetu walituambia. Hayo hatutawaficha wana wao, huku tukiwaambia kizazi kingine, sifa za BWANA, na nguvu zake, na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya. Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu wawajulishe wana wao, ili kizazi kingine wawe na habari, ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao. (Zaburi 78:3-5).


Kanon Tipton

Wanao wakiyashika maagano yangu, na shuhuda nitakazowafundisha; watoto wao nao wataketi katika kiti chako cha enzi milele. (Zaburi 132:12).

Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, watoto wake watabarikiwa baada yake. (Mithali 20:7).

Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili. (Mithali 20:11).



Kanon Tipton

Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. (Mithali 22:6).

Monday, July 30, 2012

Bikira Maria wa Fatima



 Picha ya kubuni kuonyesha jinsi Bikira Maria
alivyowatokea watoto watatu kule Fatima

Duniani humu yako mambo yanayoendelea chini kwa chini bila wengi wetu kujua. Wengi tuko kwenye harakati za kuishi na labda hata kustarehe tu bila kujali nini kiko mbele yetu.

Kuna mahali katika ratiba ya nyakati ambako tunaelekea hakika. Ni jambo lililo wazi kabisa kwamba tulikotoka kulikuwa na unafuu mkubwa kuliko tuliko na tunakoelekea. Misingi mikuu ya kijamii kama vile uaminifu, upendo, kuvumiliana, kushirikiana na kusaidiana ilikuwa na nguvu sana huko nyuma kuliko sasa, na kuliko huko mbele tuendako.

Tuesday, July 17, 2012

Je, ni kweli hatutakiwi kuhukumu?


Naamini umeshasikia mara nyingi watu wakisema, “Usinihukumu bwana. Wewe si Mungu.”

Lakini swali ni kuwa, je, dhana hii hutumiwa na watu kwa jinsi ilivyo sawa? Kabla hatujajibu swali hili, hebu tuchunguze maandiko yafuatayo:

Sunday, June 17, 2012

Sikuja Kutangua Torati



Bwana Yesu alisema: Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. (Mt. 5:17-18).

Sunday, June 10, 2012

Dini na Madhehebu: Mzigo Usio wa Lazima


MAANA YA DINI

Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford: 2004) inaeleza neno ‘dini’ kama mfumo fulani wa imani inayohusiana na mambo ya kiroho na njia ya kuabudu, kusali au kuheshimu/kutii Muumba.

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa kifupi kwamba, dini ni utaratibu anaotumia mwanadamu katika kumwabudu Mungu.

Friday, June 1, 2012

Mwanadamu ni Nini Hasa?



Wewe hujawahi kujiona hata siku moja! Biblia inasema kwamba sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu alipopanga kumwumba mwanadamu alisema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu. (Mwa. 1:26).

Sunday, May 27, 2012

Je, Sabato Ni Siku Katika Juma?



Sabato ilianzia wakati wa uumbaji ambapo baada ya siku sita za uumbaji, Mungu alipumzika siku ya saba. 

Imeandikwa: Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya, akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. (Mwa. 2:2-3).

Hatimaye ulifika wakati ambapo Mungu aliwatoa wana wa Israeli kutoka utumwani Misri; ndipo aliwapa amri juu ya sabato. 

Monday, May 21, 2012

Furaha Katika Roho Mtakatifu



Mara kadhaa nimesikia watu wakisema, “Nikienda kanisani najisikia raha kweli; lakini nikitoka, hali ya uzito wa moyo inanirudia tena.”
Ndugu, Biblia inasema: Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Rum. 14:17).

Hebu tujiulize swali hapa. Sehemu nyingine tunaposoma, Bwana anasema kwamba:

  • Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo. Mimi nimeushinda ulimwengu. (Yohana 16:33)
  • Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. (Mt. 10:22);

Sunday, May 13, 2012

Kuishi Maisha ya Aina Mbili


UTANGULIZI

Mwandishi mmoja alimwuliza Bwana Yesu: Katika amri zote ni ipi iliyo kuu? (Mk. 12:28).

Bwana alimjibu: Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. (Mk. 12:29-30). Hicho ndicho kipimo cha utimilifu wa utii.

Monday, April 2, 2012

Nitashindaje Dhambi Inayonisumbua?


Baba yangu mmoja wa kiroho alipenda kusema, “Jiachie tu kwa Mungu naye atafanya.”

Neno hilo lilinisumbua kwa muda mrefu sana kujua maana yake. Nilikuwa najiuliza, “Jiachie maana yake nini? Mbona mimi najaribu kuishi maisha matakatifu lakini nashindwa? Ina maana mimi sijaokoka?”