Muda Unaisha
Haraka!
Huu ni ufupisho wa
ushuhuda wa Victoria Nehale
Nilizaliwa na kuishi Namibia maisha yangu
yote; na niliyatoa maisha yangu kwa Yesu tarehe 06 Februari 2005. Bwana Yesu
Kristo ameshanifunulia mambo mengi katika ulimwengu wa roho ikiwa ni pamoja na
safari za kuzimu. Bwana alinipa maelekezo kwamba niwashirikishe watu uzoefu
wangu; pia alinionya kuwa nisiongeze wala kupunguza chochote katika vile
alivyonionyesha na kuniambia. Wakati nikiandika kitabu hiki, mwishoni mwa 2006,
nilishatembelewa mara 33 na Bwana Yesu Kristo. Kila aliponitembelea, Bwana
alikuwa akiniambia kabla ya kuondoka: MUDA
UNAISHA HARAKA!
Safari ya kwanza
kuzimu
Katika wikiendi ya tarehe 23 Julai 2005, nilipanda taksi kwa ajili ya safari
ya dakika thelathini kutokea mji wa Ondangwa ambako ndiko ninakofanya kazi na
kuishi, hadi kijijini kwetu, kwa lengo la kwenda kuwa na wazazi wangu wakati wa
wikiendi ile. Wakati nikielekea nyumbani, nilipata hisia kwamba kuna jambo
lisilo la kawaida ambalo lingetokea jioni ile. Nilifika nyumbani kwenye saa 12
jioni; na hapo watu walikuwa wanaandaa chakula cha jioni. Nilikuwa jikoni
pamoja na familia yetu, huku nikiwa nimelala kwenye mkeka. Watoto wa hapo
nyumbani walikuwa wakiimba nyimbo zao za Shule ya Jumapili. Ghafla nilijisikia
upako mzito ukinishukia; mwili wangu ukawa dhaifu sana; na nikawa nimetoka
kwenye mwili kutokana na nguvu za Mungu. Nilimwona mwanamume amevaa joho jeupe
refu likiwa limefungwa kwa kamba ya rangi ileile; akiwa anatembea kuelekea pale
nilikokuwa nimelala. Kulikuwa na nuru imemzunguka kana kwamba ilikuwa ikitokea
kwake. Alikuwa amevaa viatu vya wazi vya kahawia. Mwonekano wake ulikuwa kama
wa watu wa Mashariki ya Kati, huku akiwa na ngozi nzuri ya hudhurungi. Uso wake
ulikuwa mpole sana na umejaa utukufu lakini sikuweza kumtazama machoni.
Alipoongea, sauti yake ilikuwa ya upole, na upendo, lakini pia yenye mamlaka; mawimbi ya upendo yalikuwa
yakitoka kwake.
Alinyoosha mkono wake kwangu na kuninyanyua kutokea pale nilipolala. Ghafla
nilijiona nikiwa nina mwili mzuri sana. Nilijiona niko kama nilivyokuwa ningali
na miaka kumi na nane. Nilikuwa nimevaa joho jeupe na kamba nyeupe. Japokuwa
joho langu lilikuwa jeupe, lilitengenezwa kwa matirio tofauti na ya joho la
yule mwanamume. Joho lake lilikuwa la hariri
huku liking’aa kiasi kwamba hata nashindwa namna ya kuelezea.
Alisema, kwa sauti ya upendo na upole sana: “Victoria, nataka uende nami; nitakuonyesha
mambo ya kuogopesha na ninakupekela mahali ambako haujawahi kufika katika
maisha yako.” Alinishika
mkono wa kulia na tukaondoka. Nilijiona kama vile tunatembea hewani na muda
wote tulikuwa tukielekea tu juu. Baada ya muda, nikawa nimechoka sana, na
nikamwambia kuwa nisingeweza kuendelea na safari. Hivyo nikamsihi aniruhusu
nirudi. Hata hivyo, alinitazama kwa upendo na kusema, “Haujachoka
– uko sawa tu. Kama ukichoka, nitakubeba, lakini kwa hivi sasa uko tu sawa.
Amani iwe kwako. Tuendelee.”
Tulifika mahali ambako ni pakavu sana; pakavu kuliko jangwa lolote analojua
binadamu; hakukuwa na dalili zozote za uhai. Hakukuwa hata na mti mmoja au hata
jani au kiumbe chochote hai. Lilikuwa ni eneo linalofadhaisha sana.
Hatimaye tulifika kwenye geti moja na yule mwanamume alinigeukia na kusema:
“Victoria, tutaingia kupitia
geti hili na mambo ambayo utayaona yatakuogopesha na kukufadhaisha – lakini uwe
na uhakika kuwa kokote nitakakokupeleka, utakuwa na ulinzi mkamilifu. Wewe
fungua tu macho yako na kutazama kila nitakachokuonyesha.” Nilijawa na
hofu na kuanza kulia. Nilikuwa nalalamika na kumwomba anirudishe. Nilimwambia
kuwa sikutaka kuingia kwenye sehemu ile maana tayari nilikuwa naona kupitia
getini kile kilichokuwa kikiendelea ndani. Aliniangalia na kusema, “Amani iwe nawe; niko pamoja nawe. Ni lazima tuingie ndani, maana muda
unakimbia haraka.”
Tuliingia kupitia getini. Siwezi kukusimulia utisho wa mahali pale. Nina
uhakika kabisa kuwa hakuna sehemu yoyote ulimwenguni ambayo ni mbaya kama ile!
Sehemu ile ilikuwa ni kubwa sana na nilipata hisia kuwa inaendelea kupanuka
muda wote. Ilikuwa ni sehemu ya giza totoro na joto lake halipimiki; ilikuwa ni
joto kuliko moto ulio mkali kabisa. Sikuona miali yoyote ya moto au chanzo cha
joto lile lakini kulikuwa ni JOTO! Kulikuwa na wadudu wa kila ukubwa; wa
kijani, weusi, na wa kijivu - ila aina ya wadudu unaoweza kuwafikiria. Zaidi ya
hapo, kulikuwapo pia kila mahali funza wafupi, wanene, weusi, ambao wanapanda
juu ya kila kitu. Walianza kupanda juu yetu na wadudu nao walikuwa
wametuzunguka kila upande. Mahali pale kulikuwa na harufu mbaya mno; hakuna
maneno ya kutosha kuelezea harufu ile. Harufu ilikuwa kama nyama iliyooza
lakini ilikuwa ni mbaya mara mia zaidi ya nyama iliyooza niliyowahi kunusa maishani mwangu mwote!
Kulikuwa na kelele za vilio na kusaga meno, pamoja na vicheko vibaya vya
mapepo.
Kibaya kabisa kwenye sehemu hii ni kuwa pamejaa watu. Walikuwa ni wengi
sana kiasi kwamba hawahesabiki. Walikuwa ni mifupa tu. Ninaweza kusema kwa
ujasiri na uhakika kabisa kwamba mifupa hii ilikuwa ni wanadamu kwa vile
niliweza kuwatambua baadhi ya ndugu zangu wa karibu na watu kutoka kijijini
kwangu. Mifupa yao ilikuwa ya kijivu cheusi na mikavu sana. Walikuwa na meno
marefu makali kama wanyama wa porini. Midomo yao ilikuwa mikubwa na mipana na
ndimi zao zilikuwa ndefu na nyekundu sana. Mikono na miguu yao ilikuwa na
vidole vyembamba virefu, na kucha kali, ndefu. Baadhi yao walikuwa na mikia na
pembe.
Kulikuwa na mapepo yakichanganyika na watu: mapepo
yalionekana kama mamba na yalitembelea miguu minne. Yalionekana yanajisikia
vizuri tu kwenye mazingira yale na mara zote yalikuwa yakiwachokoza na kuwatesa
wanadamu. Kelele kutoka kwa yale mapepo zilikuwa ni kama vile yako kwenye
sherehe; maana yalionekana yana furaha. Yalikuwa pia yakicheza na kurukaruka
muda wote. Wanadamu kwa upande wao, walionekana wana mateso na fadhaa; walikuwa
katika hali ya kukosa msaada. Kelele za wanadamu zilisababishwa na maumivu.
Walikuwa wakilia, wakipaza sauti na kusaga meno yao; na walikuwa katika hali ya
mateso makali yasiyo na mfano.
Watu katika sehemu ile, walikuwa ni wengi mno, lakini niliweza kuona kuwa
wengi wao walikuwa wanawake. Waligawanyika katika makundi mbalimbali. Japokuwa
walikuwa katika makundi, ilikuwa haiwezekani kukadiria idadi yao katika kundi
lolote maana makundi yenyewe yalikuwa ni makubwa kupita kiasi!
Mwanamume yule alinipeleka hadi kwenye kundi mojawapo upande wa mashariki
wa sehemu ile. Kisha alinitazama na kusema: “Victoria, hili ni kundi la watu ambao walikataa kuwasamehe wengine.
Niliwaambia mara nyingi na kwa njia nyingi kuwa wawasamehe wengine lakini
walinikataa; Mimi nimewasamehe wao dhambi zao zote lakini wao walikataa
kuwasamehe wengine. Muda wao uliisha na wakajikuta wako hapa. Watabakia hapa
milele yote; wanakula matunda ya kazi yao milele na milele. Hata hivyo,
inaniuma sana kuwaona kwenye sehemu hii mbaya na katika sehemu hii ya milele –
maana ninawapenda.”
Nilipelekwa kwenye kundi linalofuata, na mwanamume yule aIiniambia kuwa watu
wa kundi lile la pili walikuwa ni wale waliokuwa na madeni: walikuwa na uwezo
wa kulipa madeni yao lakini waliendelea kuahirisha. Walikuwa wakisema kuwa
tutalipa kesho, wiki ijayo, mwaka ujao, hadi muda ukawaishia. Hapa ndipo
watakaa milele; wanakula matunda ya kazi yao.
Aina ya pili ilikuwa ni ya wale ambao walikuwa na madeni na walikuwa na
uwezo wa kuyalipa; na walikuwa tayari kuyalipa, lakini walikuwa wakiogopa
matokeo maana, labda, kama wangesema kweli, wangeishia kukataliwa, au
wangefungwa, au labda kile ambacho walitenda kingejulikana duniani kote nao
wangeaibika. Yule mwanamume akasema: “Hakuna kati yao ambaye alinijia
kuniomba njia ya kufanya. Kama wangeniomba, ningewaonyesha njia rahisi kabisa
ya kutoka kwenye hali zilizowakabili. Muda wao uliisha na wakajikuta wako hapa
ambako ndiko watakuwako milele. Wanakula matunda ya kazi zao.”
Kisha akasema: “Kundi la
tatu walikuwa na madeni ambayo hawakuwa na uwezo wa kuyalipa, lakini pia, nao
hakuna hata mmoja ambaye aliniambia kuwa ana deni asiloweza kulipa. Kama
wangefanya hivyo, ningewalipia madeni yao. Pia, walijaribu kutumia ufahamu wao
na hekima yao, kitu ambacho hakikuwasaidia kwa njia yoyote. Hivi sasa
wamejikuta mahali hapa ambako ndiko watakakoku. Wanakula matunda ya kazi yao.
Moyo wangu unauma kwa ajili ya watu hawa wote maana ninawapenda sana.”
Katika kundi la kwanza, niliwaona ndugu zangu wawili wa kike wa karibu sana
pamoja na mtoto wa miaka kumi na mbili, naye pia akiwa ndugu yangu. Nilijua
alikuwa na miaka kumi na mbili maana huo ndio ulikuwa umri wake wakati anakufa.
Katika kundi la pili nako pia niliwaona baadhi ya ndugu zangu, pamoja na
Mchungaji ambaye nilimfahamu vizuri sana. Rafiki yangu wa kiume, Jakes, ambaye
alijiua kwa sababu mimi niliamua kumpa Kristo maisha yangu, naye alikuwa kwenye
kundi la pili. Niliwaona baadhi ya majirani zangu kwenye makundi yote pia.
Niliwatambua watu niliowajua kabla ya kufa kwao; nao pia walinitambua.
Ndugu zangu walijawa na hasira sana waliponiona na wakaanza kunitukana.
Walikuwa wakitumia lugha chafu kabisa wakati wakinitukana. Mmoja wao alisema
kuwa sikustahili kumfuata mwanamume yule ambaye nilikuwa naongozana naye;
walikuwa wakiongelea mambo ambayo nilikuwa nikiyafanya kabla ya kutoa maisha yangu
kwa Kristo. Hawakuwa wakisema uongo. Mambo waliyokuwa wakinituhumu nayo
yalikuwa ya kweli. Jakes alikuwa akisema kuwa mimi nilikuwa wa kwake na kwamba
nilitakiwa kwenda pale alipokuwa maana nilitenda dhambi zilezile kama alizotenda
yeye. Mara ya kwanza, yule mchungaji alionekana amefurahi kuniona na akasema
nimefanya vema kuja, lakini alibadilika ghafla pale alipomwona yule niliyekuwa
nimeongozana naye; kisha naye akajiunga na wale waliokuwa wakinilaani kwa
matusi. Mwanamume yule aliyekuwa nami akaniambia nisiwajali maana hawajui
walitendalo.
Nilipigwa na bumbuazi na kujawa na huzuni kubwa sana. Mwili wangu ulikuwa
ukitetemeka na sikuweza kusimama. Nilikuwa nikilia bila kuweza kujizuia.
Mwanamume yule alinigeukia, akanikumbatia, na kusema: “Amani iwe nawe, Victoria.” Nguvu zangu
zilinirejea na nikajisikia salama mikononi mwake. Kisha akaniambia kuwa
tulitakiwa kuondoka pale na kurudi. Alinitazama na kusema: “Victoria, nimeshakuonyesha. Sasa
inabidi uchague ni kundi lipi unataka kuingia; uchaguzi umo mikononi mwako. Ni
lazima uwaeleze watu kila kitu ulichokiona lakini usiongeze au kupunguza
chochote.”
Nakumbuka kuwa tuliondoka pamoja kwenye ile sehemu ya kutisha lakini
sikujua nimemwacha wapi maana fahamu zangu za kawaida zilinirudia. Nilifungua
macho yangu na kujikuta kwenye mwili wangu wa nyama, huku nikiwa nimelazwa
kwenye Hospitali ya Oshakati. Nilikuwa nimetundikiwa dripu kwenye mkono wangu
wa kushoto; na nilimwona mama yangu na ndugu zangu wengine wa kijijini kwenye
kona moja ya chumba, ambako walikuwa wakiniangalia kwa mshangao. Niliona kwenye
uso wa mama yangu kwamba alikuwa analia. Nilimwuliza nesi mmojawapo kama
alikuwa anafahamu tatizo langu lilikuwa nini lakini alinifanyia tu mzaha na
kusema: “Umerudishwa. Labda ulifanya kosa fulani na unatakiwa kutubu.” Nesi
alikuwa anajaribu kuelezea kwa lugha nyepesi namna hali yangu ilivyokuwa,
lakini nilibaini kuwa alikuwa anaogopa kunikaribia. Nilimwomba aniitie daktari
aliyenihudumia.
Daktari alipofika, alisema kuwa hakujua kulikuwa na tatizo gani kwangu.
Mwanzoni, alidhani kuwa nilikuwa na malaria lakini vipimo vilionyesha kuwa
sikuwa nayo. Aliendelea kunieleza kuwa joto langu, mapigo ya moyo, na shinikizo
la damu vilikuwa chini sana kwa viwango vya hatari lakini hakuweza kujua sababu
yake. Alisema kuwa hakuwa na cha kufanya tena kwa ajili yangu. Hakuweza hata
kuniandikia kulazwa maana sikuwa na ugonjwa. Dripu waliyoniwekea ilikuwa
haifanyi kazi mwanzoni, lakini nilipofungua tu macho yangu, ikaanza kufanya
kazi. Alipendekeza kuwa nesi aniwekee dripu nyingine mara ile ya kwanza
itakapoisha ili niweze kupata nguvu za kutosha kwenda nyumbani.
Niliogepeshwa na kile nilichoona mahali pale na sikuweza kujizuia kulia. Harufu
mbaya ya pale iliendelea kuwa halisi kama nilipokuwapo hapo. Taswira za pale
ziliendelea kunijia wakati wote. Nilishindwa kulala na mwili wangu wote ulihisi
maumivu makubwa. Nilijihisi kana kwamba miguu na mikono yangu ilinyofolewa na
kurudishiwa tena. Ah, nilijisikia vibaya sana. Nilikuwa na tumbo la kuendesha
na kichwa kiligonga kwa wiki nzima.
Niliamua moyoni mwangu kwamba nisingemweleza mtu yeyote juu ya kile
nilichoona maana ni nani kwanza angeniamini? Watu watanielewaje? Niliendelea
kujiambia kuwa sitamweleza kamwe mtu yeyote juu ya mambo hayo. Mmoja wa
washauri wangu alinipigia simu siku tatu baadaye kuulizia kuhusu hali yangu
maana nilikuwa nimemtumia meseji aniombee. Bila kujitambua, nilijikuta
nikimsimulia kuhusu yaliyonikuta. Niliposhtuka, tayari nilishamweleza karibu
kila kitu. Nilitamani kujipiga mateke. Nilikuwa nalia kwa kuwa niliamini kuwa
nimefanya kosa kubwa kabisa maishani mwangu. Sasa hadithi nzima ilikuwa wazi;
hakukuwa na uwezekano wa kuificha tena. Sasa najua kuwa kama Mungu akitaka
jambo fulani lielezwe, lazima litaelezwa. Maana yeye si ni Mungu?
***********
Agosti 19, niliamka huku nikijisikia hali ya upako kwenye mwili wangu wa
nyama. Nilikuwa dhaifu na kutetemeka, huku mawimbi ya umeme yakipita kwenye
mwili wangu. Jioni, niliona mwanga mkali ukija chumbani kwangu, na katikati
yake, alikuwa yuleyule mwanamume. Safari hii alikaa chini kwenye kiti karibu na
kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki kilitoka wapi lakini kilikuwa pale mara
tu alipokuwa tayari kukaa. Kilikuwa ni kiti kizuri cha dhahabu tupu. Umbo lake
lilikuwa la kiti cha kawaida, kikiwa na sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila
mguu kulikuwa na nyota ya madini ya fedha iliyopachikwa kwenye dhahabu ile;
nyota ileile ilikuwa pia katikati ya sehemu ya nyuma ya kuegemeza mgongo.
Kulikuwa na magurudumu kwenye kila mguu.
Baada ya kunisalimia, aliniambia kuwa alijua kuwa nina maswali mengi kuhusu
yeye ni nani; hivyo alikuja kujitambulisha kwangu na kufafanua mambo kadhaa
ambayo tayari nilikuwa nimeyapitia. Alisema: “Mimi ni Yesu Kristo, Mwokozi wako. Kama una mashaka yoyote, tazama
mikono yangu. Mahali pale ambako tulienda, ni Kuzimu.” Nilipoangalia mikono yake, niliona makovu ambamo misumari
ilimtoboa.
Rafiki, napenda nikueleze kuwa kuzimu si sehemu ya kufikirika tu mawazoni;
lakini ni mahali halisi na si kuzuri hata kidogo. Ni mahali ambako hakukutengenezwa
kwa ajili ya wanadamu bali kwa ajili ya shetani na mapepo yake. Sehemu
inayotustahili ni Mbinguni pamoja na Yesu lakini inatubidi tumchague Yesu kabla
hatujachelewa. Leo, unapoisikia sauti yake, usifanye moyo wako kuwa mgumu;
mkubali Yesu awe Mwokozi wako binafsi kisha uishi kwa ajili yake. Kuzimu ni
kubaya mno: ni sehemu ya hofu na huzuni; ni sehemu ya mateso na vilio vya
milele na kusaga meno. Shetani anataka awachukue watu wengi kadiri iwezekanavyo
ili aende kule pamoja nao. Usishirikiane naye; shirikiana na Yesu nawe, badala
ya kufa, utaishi.
Sikuelewa kwa nini Bwana aliniambia nichague kati ya makundi mawili
aliyonionyesha kule kuzimu ilhali mimi tayari nilikuwa Mkristo niliyeokoka.
Nimeshamkubali maishani mwangu lakini bado alikuwa akiniambia nichague kama
nataka kwenda kuzimu au la! Sikuweza kuelewa. Nilianza kuomba na kumwuliza
Mungu anipatie ufunuo juu ya kile alichomaanisha na ni nini anataka nifanye. Bwana
alinifunulia kuwa nilikuwa nimeficha roho ya kutosamehe na chuki moyoni mwangu kwa
sababu ya dada yangu mmoja, pamoja na binamu yangu mmoja. Nilimwomba Bwana
anisamehe kutokana na kutosamehe kwangu. Pia nilimwomba dada yangu anisamehe
kwa kuweka hasira na uchungu moyoni mwangu kwa ajili yake. Bwana alinielekeza
niende pia nikamwombe msamaha binamu yangu.
Bwana pia alinikumbusha kuwa kulikuwa na wakati ambapo nilipata kazi ya
ualimu kwa kutumia cheti cha diploma cha uongo na alihesabu hilo kuwa ni deni
na wizi. Nilikusudia kutenda kilicho sahihi na nilimwomba anisaidie kutoka
kwenye tatizo hili na anionyeshe njia rahisi ya kutoka humo maana hili lilikuwa
ni kosa kubwa na lingeweza kunifannya nifungwe. Alinielekeza niende kwenye
Idara ya Elimu nikakiri kosa nililofanya. Nilikuwa tayari kwenda jela kama
ingebidi. Nilipata upendeleo wa Bwana kwa kiasi kikubwa sana. Nilipofika kule,
mhusika kwenye Idara ya Elimu aliniambia niamue kile ninachotaka kufanya: ama
kulipa mshahara ambao nilipokea kutoka serikalini au la. Waliahidi kuwa
hawatanishtaki maana walishangazwa na kitendo changu cha kwenda kukiri kosa
lile. Mungu wetu ni Mungu mwaminifu ambaye analiheshimu Neno lake.
Kama uko kwenye hali inayofanana na niliyokuwa nayo, napenda nikutie moyo kuwa
utende kile kilicho sahihi, bila kujali matokeo. Unaweza kufungwa kwenye jela
ya kidunia lakini hiyo ni ya muda tu. Hakuna maumivu au aibu inaweza kulinganishwa
na kutengwa na Mungu milele. Kuzimu si mahali pazuri: ni bora kumruhusu Mungu
akuhukumu sasa kabla hujachelewa. Hatutakiwi kuogopa hukumu ya Mungu tungali bado
kwenye kipindi cha Neema; ni lazima tumruhusu afunue chochote kisicho sawa
kwenye maisha yetu tungali bado na muda wa kuweka mambo sawa naye, maana hakuna
msamaha upande wa pili wa kaburi.
Safari ya pili kuzimu
Oktoba 18, 2005, niliamka saa 11:30 asubuhi lakini sikuweza kwenda kazini.
Nilijisikia hali ya udhaifu sana na kulewa;
sikuweza kusogea au kugeuka kitandani kwangu; na uwepo wa Bwana ulikuwa mzito
sana chumbani. Nilikuwa natetemeka na nikahisi kama umeme ukipita mwilini
mwangu. Bwana alinijia kabla tu ya saa 2:00 maana kwa mara ya mwisho
nilipotazama saa ilikuwa ni saa 1:48; na Yeye alifika muda mfupi tu baada ya
hapo. Alinisalimia na kusema kuwa tunatakiwa kwenda tena maana muda unaisha
haraka sana. Nilisimama na tulianza kutembea. Utembeaji wa safari hii ulikuwa
tofauti kabisa na safari zingine zote. Japokuwa miguu yetu ilikuwa inafanya
kitendo cha kutembea, tulikuwa kama vile tunaelea zaidi kuliko kutembea. Wakati
tukiwa njiani, Yesu aliniambia kuwa dhambi zote ni
mbaya na hakuna kitu kama dhambi ndogo au dhambi kubwa. Dhambi zote mwisho wake
ni mauti - ziwe kubwa au ndogo. Bwana aliniambia kwamba tunaenda kutembelea
kuzimu tena na akaniuliza iwapo nilikuwa nina hofu. Nilimjibu kuwa nilikuwa nayo.
Alisema, “Roho
ya woga haitoki kwa Baba yangu au kwangu; inatoka kwa Ibilisi. Woga
utakusababisha utende mambo ambayo yatakupeleka kuzimu.”
Bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu na hofu ni kinyume kabisa cha
imani. Ni wazi kuwa hofu haimpendezi Mungu kwa kuwa inaharibu imani yetu. Muda
wote tulipokuwa njiani, tulikuwa tunatembea kila mmoja peke yake. Lakini mara
tu tulipofika kwenye lango la kuzimu, alinishika mkono wangu kwa mkono wake wa
kulia kwa muda wote tuliokuwa kuzimu. Nilifurahi sana kwa Bwana kunishika mkono
maana kwa namna alivyokuwa amenishikilia kwa nguvu, hofu yote ilitoweka. Sehemu
ile ilikuwa bado iko vilevile: hakukuwa na tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Kulikuwa na wadudu, funza, joto kali sana, harufu, mifupa, kelele: kila kitu
kilikuwa kama mwanzo nilipoenda pale. Tulipita tena kwenye geti lilelile baya
na Bwana akanipeleka kwenye kundi moja la watu. Kulikuwa na watu wengi
niliowafahamu wakati wangali duniani. Maskini, walikuwa kwenye hali mbaya sana.
Walionekana ni wenye taabu na maumivu makubwa; lakini baya zaidi ilikuwa ni
nyuso zao zisizo na matumaini kabisa.
Bwana alimwonyesha mwanamke mmoja wa makamo ambaye nilimfahamu kabla
hajafa. Alikufa kwa ajali ya gari mwanzoni mwa mwaka 2005. Nilipigwa na butwaa
kumwona pale maana sote tulimjua kuwa ni mtu aliyekuwa na hofu ya Mungu na
aliyempenda Mungu. Bwana aliniambia kuwa mwanamke yule
alimpenda na Yeye Bwana naye alimpenda; alimwokoa angali akiwa duniani;
aliwashuhudia wengi ambao walimwijia Bwana na alifahamu Neno vizuri sana.
Alikuwa mkarimmu kwa maskini na wahitaji; aliwapatia walichohitaji, na
kuwasaidia kwa njia nyingi. Alikuwa ni mtumishi mzuri wa Bwana kwa namna
nyingi.
Maneno hayo ya Bwana yalinishitua hata zaidi; nami nikamwuliza kwa nini
amwache mtu kama huyo aliyemtumikia kwa kiasi kikubwa hivyo aingie kuzimu? Bwana
alinitazama na kusema kuwa mwanamke yule aliamini uongo wa Ibilisi. Japokuwa
aliyajua Maandiko vizuri, aliamini uongo wa ibilisi kwamba kuna dhambi ndogo na
kubwa. Alidhani kuwa dhambi ‘ndogo’ zisingempeleka kuzimu, maana alikuwa
Mkristo hata hivyo.
Bwana aliendelea kusema, “Nilimwendea
mara nyingi na kumwambia aache kile alichokuwa anakifanya lakini mara nyingi
alijenga hoja akilini mwake kuwa kile alichokuwa anakifanya kilikuwa ni kidogo
sana na alichukulia kuwa yale maonyo yangu yalikuwa ni hisia zake tu za hatia.
Kulikuwa na muda ambapo aliacha kwa muda lakini baadaye alijishawishi tena kuwa
maonyo yale hayakuwa yanatoka kwangu, bali ni sauti yake tu kwa kuwa aliona
kuwa dhambi ile ilikuwa ni ndogo sana kuweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu.”
Nilimwuliza tena Bwana ili aniambie ni dhambi gani basi mwanamke yule alitenda.
Alinijibu kwamba, “Mwanamke
huyu alikuwa na rafiki ambaye alikuwa nesi kwenye Hospitali ya Oshakati. Kila
mwanamke huyu alipoumwa, hakwenda hospitali na kulipa kwa ajili kadi yake kama
inavyotakiwa kwenye taratibu za kawaida; badala yake yeyé alipiga tu simu na
kumwambia rafiki yake amfanyie mipango ya dawa kutoka kwenye Zahanati ya Hospitali. Na mara zote rafiki
yake yule alikubali na kumwambia kuwa apite pale muda fulani kuchukua dawa. Kwanza,
aliamua kukubali uongo wa ibilisi juu ya kuwapo kwa dhambi kubwa na ndogo na
kuikataa kweli yangu; alimsababisha mtu mwingine atende dhambi na kuiba kwa
niaba yake, lakini kibaya zaidi, ALIMHUZUNISHA ROHO MTAKATIFU. Hicho ndicho
kilichomfanya afike kuzimu. Haijalishi kwamba utaleta mamilioni ya roho kwa
Bwana; bado upo uwezekano wa kuingia kuzimu kutokana na kumhuzumisha Roho
Mtakatifu. Si tu kwamba ni lazima ujali wokovu wa wengine lakini pia ni lazima
uwe mwangalifu usije ukasahau roho yako. Kuwa makini na Roho Mtakatifu wakati
wote.” Baada ya maneno hayo, Bwana alisema ni
wakati wa kurudi.
************
Wakristo wengi waliosikia hadithi yangu hii huiona kama ina matatizo. Mara
nyingi huwa wanniuliza, “Vipi kuhusu kuhesabiwa haki, rehema, na neema?” na pia
“Inawezekana kweli kupoteza Wokovu wako baada ya kuwa umeupokea?”
“Huko si kuvuka kiwango?”
“Mungu anaweza kuwa mkatili kiasi hicho?”
Kama nilivyosema kwingineko kwenye kitabu hiki, mimi siongei theolojia
yangu hapa. Ninasema tu kile ambacho Bwana alinionyesha na kunifundisha – na
kile alichoniruhusu kukishuhudia. Tafadhali someni Biblia zenu ili kupata
majibu. Tazama aya zifuatazo, kisha uhukumu mwenyewe.
“…bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe,
nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” (1Wakorintho 9:27)
“Tuseme nini basi?
Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
Hasha! Sisi tulioifia
dhambi tutaishije tena katika dhambi?” (Warumi
6:1-2)
“Basi, dhambi isitawale
ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.” (Warumi 6:12)
“Maana, kama tukifanya
dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa
ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto
ulio tayari kuwala wao wapingao.” (Waebrania 10:26 –27)
Unasema, “Je, naweza kwenda kuzimu baada ya kuwa nimemtumikia Bwana na
kuwaleta wengi kwa Kristo?” Hukumu mwenyewe!
Kutokutii
Jumatatu ya tarehe 6 Machi 2006, niliamshwa na saa ya kengele saa 11:30. Nilianza
kuomba na nikatambua kulikuwa na upako mzito juu yangu. Mwili wangu ulikuwa
dhaifu na nilikuwa nikitetemeka; mawimbi ya umeme yalikuwa yanapita kwenye
mwili wangu.
Wakati wa mchana, nikiwa nimelala kitandani, niliona nuru nyeupe ikijaza
chumba changu. Niliona shanga ndogondogo, nyeupe, za duara, zenye ukubwa wa
kichwa cha pini. Shanga hizi zilikuwa zikianguka kama mvua inavyonyesha na
zilipogusa ngozi yangu, zilizama ndani. Zaidi ya hapo, niliona kama wingu
linalofanana na ukungu mweupe likija kutokea juu. Nalo pia lilikijaza chumba na
likawa likizama kwenye ngozi yangu kila liliponigusa. Baada ya hapo, nilimwona
Yesu akitembea katikati ya lile wingu la ukungu kuelekea pale nilipokuwa.
Alikaa kwenye kiti chake pembeni mwa kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki
kinatokea wapi; huwa kinatokea tu mara anapokuwa tayari kukaa. Ni kiti kizuri kilichotengenezwa kwa dhahabu.
Umbo lake ni kama la viti vingi tunavyovifahamu lakini kina sehemu ya kuegemeza
mgongo. Kwenye kila mguu kuna nyota ya fedha; na nyota nyingine ya aina ileile,
japo ni kubwa zaidi, iko kwenye sehemu ya kuegemea. Kuna magurudumu kwenye kila
mguu.
Yesu alinisalimia na akaninyooshea mkono wake na
kuniambia niamke maana muda unakimbia haraka sana. Alinivuta mkono wangu nami
nikainuka na kukaa kitandani kwangu.
Kisha akaniambia, “Victoria, tuombe.” Aliomba kwa lugha ambayo
siielewi; nilielewa neno moja tu ‘Amen’. Kisha aliendelea kwa kuniuliza nilikuwa naona nini nami nilimwambia kuwa nilikuwa
naona kundi la watu wakienda kazini kwao na wengine wakirudi kutoka kazini
kwao. Nilikuwa pia naona vile vishanga vyeupe vikiwaangukia wale waliofika
mwanzo kazini kwao. Baada ya kundi la kwanza, kundi jingine nalo lilifika
baadaye. Wakati huo, ile mvua ya vile
vishanga iliacha kunyesha.
Niliona pia makundi mbalimbali ya watu, wakiwasili kwenye makanisa mbalimbali
Jumapili asubuhi. Mvua ile ingeanza kunyesha mara tu watu wa mwanzo wanapoingia
kwenye uwanja wa kanisa. Iliendelea kunyesha kwa muda kisha ikasimama. Wale
wanaochelewa hawakuti chochote.
Yesu aliniuliza iwapo nilikuwa naelewa maana ya maono yale, nami
nilimwambia kuwa sikuelewa. Ndipo alinifafanulia kwa kusema kwamba: “Maono haya yanamaanisha kuwa kila
mahali ambako unatakiwa kuwako kwa muda fulani na wewe unajua ni wakati gani
unatakiwa kuwa pale, mara zote huwa kuna malaika wanagawa baraka kwa ajili ya
muda huo. Kama ukifika mapema, utapokea baraka zako, lakini ukichelewa, unakosa
baraka zako kwa siku ile maana malaika hugawa baraka kwa muda ule tu. Victoria,
nataka kukuonya kwa sababu huwa unaenda kazini kwa kuchelewa, na hasa huwa
unaenda kanisani kwa kuchelewa. Ni lazima ujue kuwa kwa nyakati zile huwa unachelewa
bila kuwa na sababu za msingi; umekuwa ukikosa baraka zako kwa siku zile;
hazitakurudia tena. Victoria, ni lazima
uache jambo hili na usilitende tena, isipokuwa pale unapokuwa na sababu ya
msingi ya kuchelewa.”
Bwana alipomaliza kusema maneno yale, kwa kweli nilitamani kutoweka au
angalau nimpatie sababu inayokubalika kutokana na kukosa kwangu nidhamu.
Nilimwambia kuwa wakati mwingine napitiliza kulala lakini alinitazama moja kwa
moja machoni na kusema kuwa nilikuwa nasema uongo na kwamba nilikuwa nina tabia
mbaya ya kurudi kitandani baada ya kuwa nimeamka, ili kutimiza ile shauku ya
kusema ‘ngoja nilale kidogo tu.’
Baada ya Yesu kuwa amenionya. alisema, “Simama. Tuondoke sasa. Muda unakimbia haraka sana. Kuna mambo ambayo
ni lazima tuyafanye.”
Safari hii Bwana alinipeleka mahali ambako sikuwahi kufika kabla. Ilikuwa
pia ni mara ya kwanza kufuata barabara tuliyotembea siku ile. Tulifika kwenye
bustani iliyojaa maua mazuri na miti mizuri ya kijani. Hakuna kitu duniani
kinachoweza kulingana na mahali pale. Maua yalikuwa ya kila aina ya rangi za
kung’aa. Tulikaa kwenye benchi zuri la
bustanini, ambalo lilitengenezwa kwa dhahabu safi huku likiwa na nyota ndogo za
madini ya fedha ya kung’aa.
Tulipokaa, alionyesha kidole mbele na kusema, “Victoria, tazama, unaweza kuona mji ule?” Nilipotazama, niliona jiji kubwa sana. Lilikuwa
zuri kuliko maelezo. Jiji lile lilikuwa na geti la dhahabu inayong’aa, na
kwenye geti lile kulikuwa na mwanamume amekaa, mwenye umri mkubwa. Alikuwa na
ndevu ndefu nyeupe na nywele nyeupe. Nilishamwona mwanamume huyo kabla; na
nilipomwuliza Yesu kuwa mwanamume yule ni nani, aliniambia
kuwa alikuwa ni Ibrahimu, baba wa imani.
Niliona barabara nyingi kwenye mji ule, ambazo nazo ni za dhahabu. Kuna majengo
marefu, ambayo nayo yalikuwa ya dhahabu inayong’aa. Mng’ao wa mji ule hata
hauelezeki!
Yesu alinigeukia na kuniuliza, “Unawaza nini juu ya jiji lile?”
Nilimjibu kuwa lilikuwa ni zuri sana na nilikuwa natamani kwenda pale. Yesu
alisema: “Nitakupeleka pale
kama ukiendelea kuwa mtii maana hapo pia ndiko nyumba yako itakakokuwako. Uendelee
tu kuwa mtii – maana ukikosa utii, Victoria, kunguru wataruka kwenye nyumba
yako. Nyumba yako itakuwa makao ya bundi na viwanja vya kuchezea vya mizimu. Hata
hivyo, usiogope, maana mimi niko pamoja nawe. Wewe uwe mtii tu. Kwa kila mmoja
ambaye si mtii, nyumba yake itakuwa na kunguru wakiruka pale; itakuwa ni makao
ya bundi na mahali pa mizimu pa kuchezea.”
Yesu ni halisi
na anatupenda kwa pendo lisiloweza kuelezeka. Shauku yake kubwa ni sisi
tuchague uzima na kuishi milele naye. Moyo wake unauma kwa ajili ya wale watu
ambao wanakufa na kuenda kuzimu kwa vile tu wanachagua kukataa Wokovu aliowapa
na badala yake wanachagua mauti.
Uwe ni Mkristo
uliyeokoka au la, tafadhali siku zote kumbuka jambo hili: Muda unakimbia haraka!
Mpendwa msomaji wa blog hii, kama ungependa kusoma au kusikiliza ushuhuda huu kwa Kiingereza, bofya HAPA. Mungu wa mbinguni akubariki na kukutia nguvu.
**********************
Mpendwa msomaji wa blog hii, kama ungependa kusoma au kusikiliza ushuhuda huu kwa Kiingereza, bofya HAPA. Mungu wa mbinguni akubariki na kukutia nguvu.
It took me time to learn all the comments, but I honestly loved the blog. It proved to be very advantageous to me and I'm positive to all of the followers here!
ReplyDeleteWelcome to my site [url=http://www.about-dogs.zoomshare.com/]www.about-dogs.zoomshare.com[/url].
Hello, thank you for visiting my blog and thank you for inviting me into yours. God bless you.
ReplyDeleteThat is great thanks for it
ReplyDeleteHi Maliva,
ReplyDeleteThanks for visiting this blog.
God bless you.
thanks for good massege i like and god bless you and also i like to stay in grory of jesus but icant so why
ReplyDeletecan help me my name is dorothea
Shalom Dorothea.
DeleteNakupongeza kwa shauku yako ya kutaka kumpendeza Bwana Yesu. Hiyo peke yake ni mtaji tosha wa kiroho na mahali pa kuanzia. Kuna watu wengi sana ambao hata ile shauku haipo kabisa.
Dorothea, wokovu ni mapambano kamili kabisa. tunashindana na majeshi ya mapepo ambayo yapo yanamfuatilia kila mtu kibinafsi. Shetani amempangia kila mtu mapepo ya kumfuatilia na kujaribu kumrudisha nyuma. Yako kazini saa 24.
Lakini jambo la muhimu ni kutambua kwamba na sisi tunao malaika wanaopigana upande wetu. Pia tunazo silaha nyingi zenye nguvu - ikiwa ni pamoja na Damu ya Yesu, Neno la Kristo na Jina la Bwana wetu Yesu.
Nguvu yetu hata hivyo, inatokana na kusoma Neno, kuamini na kuomba kila siku. Kuna nyakati kadhaa utahisi kama vile Bwana yuko kimya sana na hakusikii. Hayo ni mawazo anayopandikiza shetani na mapepo yake. Usimwamini. Wewe shikilia Neno la Bwana.
Kumbuka kwamba, unapoomba au kukemea, mambo HALISI KABISA yanatendeka katika ulimwengu wa roho.
Unaweza kwa neema ya Bwana, Dorothea.
Waweza pia kuniandikia kwenye e-mail yangu: ijuekweli77@yahoo.co.uk
Bwana Yesu akubariki.
Dada Victoria nimeupoke ushuhuda wako wema kabisa tena umenijenga sana.Lakini nilikuwa na swali Vipi kuhusu nywele zako ana heleni masikioni yesu hakukwambia kuwa ni machukizo mbele za Mungu.Maana hilo ni eneo muhimu sana au ni picha tu ya zamani kabla haujatokewa na Yesu?Bwana azidi kukutia nguvu na uendelee na maisha ya wokovu.Maana kuvumilia mpaka mwisho ndiyo wokovu.Kweli Muda unakimbia.
ReplyDeleteShalom mpendwa. Asante kwa kutembelea blog hii. Bahati mbaya Victoria hawezi kukujibu maswali yako maana si yeye aliyeweka ushuhuda wake hapa. Na sina uhakika hata kama anajua kuwa ushuhuda wake uko hapa ukiwabariki watu mbalimbali. Hii ni tafsiri kutoka kwenye ushuhuda wake ambao aliuandika kwa Kiingereza. Mungu akubariki.
DeleteBwana Yesu asifiwe wapendwa mimi kabla sijaokoka nilitenda zambi moja ofisini kwngu ilitokea short ya milion moja nilitakiwa kuilipa sijui ilitokea vipi sijui nilipewa pesa pungufu ama la ile short iliniumiza sana kwani nalipa kitu sikijui siku moja niliingia kwenye store ya pesa ilikuwa imezidi laki nne nilichukua lakitano pale store moja kwamoja niliziweka kwenye mfuko wangu kuzifidia pesa hizo nimesoma hapa ushuhuda wa dada Victoria wapendwa nimejisikia vibaya sana juu ya ile zambi naomba Mungu anirehemu juu ya dhambi hiyo.
ReplyDeleteKusema kweli kabla ya kuokoka tulifanya mambo mengi yasiyompendeza Mungu. Tunapookolewa, yote yanakuwa mapya; ya kale yanapita. Bwana akubariki kwa Jina Yesu.
DeleteNimefunguka Upya jamani mimi nina cheti feki Mungu kupitia ushuhuda huu sitakitumia tenaaaa Naomba Rehema Mungu wangu kweli nimekuwa mkosaji mimi
ReplyDeleteAmen. Bwana akufungulie mlango wako katika Jina la Yesu ili uamuzi wako uwe ni kwa faida yako kwa Jina la Yesu.
DeleteAmen, nashukuru sana kwa kuweka ushuhuda huu, Mungu akubarki kwani umeniongezea kitu kikubwa ndani yangu. Mungu akubariki sana.
ReplyDeletePia tunaweza kupata shuhuda nyingine kwenye tovuti ya http://heavenvisit.com
Nilisoma ushuhuda wa dada anaitwa Angelica Zambrano ambao umeandikwa katika lugha nyingi sana, pia ameeleza mambo ambayo ni vema watu wakafahamu (uko hata kwa kiswahili). Unaweza kuusoma katika http://www.divinerevelations.info/documents/prepare_to_meet_your_god/
Mbarikiwe.
Amen Dickson. Na pia ukienda kwenye hiihii blog sehemu ya FREE EBOOKS, (http://injiliyakweli.blogspot.com/p/free-e-books_3.html) utaukuta hapo na unaweza ku-download kwa ajili yako na wapendwa wako wote. Ubarikiwe.
DeleteUshuhuda wa victoria umenigusa na kunitia hofu ya kuogopa dhambi, hata hivyo nimejifunza mengi kutoka kwake. na Mungu ambariki sana! na BWANA aendelee kumpa ufunuo zaidi! AMEN!
DeleteShalom Sebastian. Ni vizuri kuwa na hofu ya Mungu, maana hiyo ndiyo kinga na usalama wetu. Na ndiyo maana hata Biblia ikasema: Kumcha Bwana (yaani kumhofu) ni chanzo cha maarifa. Kwa hiyo, mtu anayekuwa na hofu ya Bwana yuko kwenye njia ya usalama. Bwana akubariki.
DeleteNAITWA ANOSISYE MWAIPOPO WA TANZANIA!
ReplyDeleteNAMPENDA YESU NA NIMECHAGUA KUMFWATA ILA VITA NI NYINGI NA VISHAWISHI KUNA KIPINDI VINANISHINDA NA KUNIINGIZA DHAMBINI NAOMBA DADANGU MPENDWA NIOMBEE PIA NAMI NIWEZE ISHINDA VITA HII, BWANA MUNGU AKUBARIKI SANA!
Bwana asifiwe Anosisye. Huu ni ushuhuda ambao nimeutafsiri na kuuweka hapa, lakini mhusika mwenyewe (yaani Victoria) hayuko Tanzania na wala sidhani kama anajua kuwa ushuhuda wake uko hapa. Yeye aliutoa kwa Kiingereza na mimi nikatafsiri na kuuweka hapa kwa faida ya wengine wengi.
DeleteNi kweli kabisa tunakutana na vishwishi vingi mbalimbali maishani mwetu, lakini usikate tamaa. Tubu na endelea kumwambia Roho Mtakatifu akusaidie na Yeye atafanya hivyo hakika.
Bwana Yesu Asifiwe.Naitwa Amos ni mfanyakazi,nimeokoka ninampenda Yesu nina kuna wakati ninafanya udanganyifu ili nipate fedha,je nifanyaje ili niondokane na maisha haya.Maana kwa ushuhua huu hakuna wokovu je ninatakiwa kuomba toba nitasamehewa?Nisaidie mtuishi
ReplyDeleteSijafungua blog yangu siku nyingi. Lakini Amos, msamaha ukiomba unasamehewa, ila tunatakiwa kuomba KWA LENGO LA KUACHA DHAMBI sio kuomba ili usamehewe kisha uendelee tena. Ukiamua kuacha na kumtumaini Roho Mtakatifu, inawezekana kusonga mbele. Hata hivyo, hii haina maana kuwa utaacha kujaribiwa. Majaribu LAZIMA yaje lkn tunatakiwa kuendelea kushikilia upindo wa Yesu kwa nguvu kila siku --- ndio kuubeba msalaba na kumfuata huko. Kisha hatua kwa hatua, anatupa ushindi na tunavuka kabisa.
DeleteBwana Yesu Asifiwe, Naitwa Frediana Mushi nipo Dar, ushuhuda huu umenifundisha mambo mengi na mengine ninayo kama hofu, hasira, kuchelewa kwenye sehemu mbalimbali. Naomba Mungu anirehemu na anifungue ktk maeneo hayo ili niweze kufika kwenye ule mji mzuri nikutane na Bw. Yesu uso kwa uso siku moja.
ReplyDeleteAmen Frediana
DeleteBarikiwa.
Hi there James. Nina issue moja ndogo kuhusiana na ushuhuda wa dada Victoria. Tunapookoka dhambi zetu ZOTE husamehewa; the plate is wiped clean so to speak. However dada Cictoria alipopelekwa kuzimu kutembelea aliambiwa kwamba yumo hatarini kubakia huko kwa sababu ya udanganyifu alioufanya ili kupata kazi ya ualimu. Sasa huyu dada alikuwa ameokoka ... inakuwaje possible yeye kwenda huko kwa dhambi ile ya 1. kudanganya na 2. kupata fedha kwa udanganyifu huo?
ReplyDelete