Mwanamke mmoja kutoka Bolivia aitwaye Adelaida De
Carrillo alipelekwa Mbinguni na Kuzimu na Yesu Kristo. Kule alionyeshwa ni
Utakatifu gani anaotakiwa mtu kuwa nao ili aweze kuingia kwenye UFALME WA
MUNGU, na pia ni dhambi gani (ambazo wengi wetu tunadhani kuwa ni ndogo),
zinaweza kumfanya mtu aingie Jehanamu.
Tuko kwenye safari ya maisha ya kimwili hapa duniani
tukielekea kwenye maisha ya kiroho kwenye ulimwengu ule ujao. Huo ni ulimwengu
halisi ambao una maisha halisi, utawala halisi na kanuni halisi za kuingia
huko.
Wakati ulimwengu tuaoishi leo una serikali nyigi na
watawala wengi, ulimwengu ule ujao utakuwa na serikali moja tu inayoongozwa na
Yesu Krito. Wakazi wa uliwengu huo ni watakatifu WOTE!!!
Huo ni ulimwengu unaoongozwa na Mungu mwenyewe kwa upendo
na amani. Kule hakuna magonjwa, vita, njaa, na dhambi zingine zote. Tiketi ya
kuingia kule ni moja tu: nayo ni kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi aliyekufa
na kufufuka kwa ajili yetu. Kisha tunaishi hapa duniani kwa kutii maagizo yake.
Hata hivyo, wale wote ambao hawatakuwa wamestahili kuingia
kwenye ulimwengu huo (kutokana na wao kuishi maisha ya dhambi na uasi dhidi ya
sheria za Mungu hapa duniani), watatupwa nje ya mbingu kweny giza na moto,
yaani kwenye jehanamu ya milele.
Katika ushuhuda huu, tunaona kile ambacho Bwana Yesu
anatuagiza ili tuweze kustahili kuingia kwenye ufalme ule ujao na kuishi na
Mungu MILELE!!!
Adelaida De Carrillo anasema:
HATUA YA 1: Ilianzia Kanisani kwenye wakati wa Huduma
Katika
Ezekieli 36:25-26, Biblia inasema:
“Nami nitawanyunyizia
maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago
vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo
mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani
ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.”
Ushuhuda wangu uko namna hii: Siku moja ya Jumapili,
kwenye saa 3 hivi, Kanisa letu lilikuwa na kipindi cha Huduma. Mungu alikuwa
akimimina baraka zake juu yetu. Mchungaji wangu aliniambia, “Adelaida, Bwana ananiambia nikupake
mafuta.”
Aliweka mafuta mengi kwenye viganja vya mikono yake na
akaanza kunipaka mwilini. Alinipaka masikioni, miguuni, tumboni na kwenye mwili
wangu wote. Alipoweka mikono yake kwenye uso wangu, niliona mwanga mkubwa ukija
kutokea juu, ukinielekea mimi. Kuanzia hapo nilipoteza fahamu na sikujua kilichokuwa
kinaendelea kwangu.
HATUA YA 2: Safari Yangu Kwenda Mbinguni
Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao.
Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi.
Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu
kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri
sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake.
Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite.
Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu
kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na
uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!
HATUA YA 3: Kuoshwa na Kubadilishwa Moyo Wangu
Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao.
Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi.
Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu
kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri
sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake.
Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite.
Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu
kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na
uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!
Ghafla, nilisikia sauti ndani yangu, ikisema, “Nataka
ufahamu kuwa nilikupa magoti hayo ili uwe mwanamke wa maombi, na si kwa ajili
ya kuzungukazunguka ukifanya mambo yasiyonipendeza Mimi. Magoti haya ulipewa
ili kufanya maombezi kwa ajili ya Kanisa. Ulitakiwa kulijua hilo.”
Kwa ujumla mimi nilikuwa si mwanamke wa maombi sana.
Maombi yangu yalikuwa na kawaida ya kuwa mafupi sana. Lakini Bwana alitaka niwe
mwombaji zaidi.
Malaika aliendelea kuosha miguu yangu, huku akiiparua, na
mimi nilikuwa namlilia Mungu anihurumie kutokana na maumivu yale. Bwana
akasema: “Miguu hii ulipewa ili uwe unazunguka kwenda kuhubiri Injili yangu,
kueneza Neno langu na si kuzungukazunguka kwa majirani zako kupeleka umbeya, na
kufanya mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Na kwa sababu hii,” Bwana akasema, “ninasafisha
miguu yako.”
Jambo hili liliendelea na lilifanyika kwa maumivu makali
sana. Bwana akasema, “Hii ni muhimu sana ili uweze kuelewa mipango
niliyo nayo kwa ajili yako.”
Baadaye, nilipelekwa kwenye sehemu nyingine ambako
malaika wngine watatu walikuwa wananingojea. Sehemu hii ilikuwa tofauti.
Niliona vitu kama mashine. Malaika wale walianza mchakato mwingine wa kusafisha
macho yangu kwa kutumia aina fulani ya mafuta. Nilihisi kama vile macho
yameng’olewa kutoka kwenye matundu yake. Nikasema: “Tafadhali mnihurumie.
Naomba msaada. Kwa nini mnanifanyia hivi?” Ilikuwa kama vile wanakwangua
macho yangu. Kitu kama samaki kilitolewa kutoka kwenye macho yangu.
Bwana akasema, “Binti yangu, nafanya hivi kwa ajili yako kwa
sababu nataka ubadilike. Mambo uliyokuwa ukifanya duniani hayakuwa
yakinipendeza. Sikuwa nafurahi ukiwa duniani ulipokuwa ukitazama mambo ambayo
hayakunipendeza Mimi. Ulikuwa ukitazama TV” [Soap Operas]
... “Hayo hayajengi maisha yako.”
... “Sifurahii pale wanangu wanapoangalia vitu kama
hivyo; vitu ambavyo havinipi utukufu.”
Nikasema, “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.” Na Bwana akasema, “Katikati ya usiku kwenye saa
sita, mara zote huwa uko macho ukiangalia sinema ambazo hazikujengi wewe; na
nyingi ya sinema hizo zimejazwa mambo mengi yanayohusu mapenzi. Sikukupa macho
hayo kwa ajili ya mambo kama hayo. Nilikupa hayo macho ili utazame mambo yale
tu yanayonipa Mimi utukufu. Na kwa sababu hii ndiyo maana ninasafisha macho
yako.”
Malaika waliendelea kusafisha macho yangu huku mimi nikiendelea
kuomba kuhurumiwa. Baadaye macho yangu yalipakwa mafuta, na kuanzia hapo nikawa
na mtazamo tofauti; macho yangu yalibadilishwa kabisa. Bwana akasema, “Usitamani
waume wa watu wengine tena!” Mimi nilikuwa na
kawaida ya kuvutiwa sana na wanaume wengine, na Bwana alisema kuwa mambo hayo
hayampendezi.
Nitakueleza mimi nilikuwa mtu wa namna gani. Nilikuwa
Mkristo duni wa kilokole ambaye alikuwa hatendi mambo sawasawa na Biblia inavyoagiza.
Kila nilichofanya kilikuwa ni kutokana na matamanio yangu na njia zangu
binafsi, kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Nakueleza haya ili uweze
kurekebisha njia zako; ili roho ziweze kuokolewa. Nakueleza kuwa tamaa NI
dhambi; kuangalia michezo ya kwenye TV [Soap Operas], sinema za kidunia – mambo
yote haya hayampendezi Mungu.
Malaika waliendelea na mchakato wa usafishaji. Walikuwa
na kijifimbo kidogo cha kioo ambacho walikiingiza moja kwa moja masikioni
mwangu. Walipoanza kukwangua masikio yangu, nilihisi maumivu makali sana. Moyo
wangu ulihisi maumivu haya yote. Mara maji meusi yalianza kutoka kwenye masikio
yangu, na baadaye maji ya rangi ya kijivu. Niliendelea kulia.
Bwana akasema, “Binti yangu, ninasafisha masikio yako kwa
sababu ulipenda sana kusikiliza mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Ulipenda
kusikiliza umbeya. Uliyatoa kabisa masikio yako kusikiliza mambo
yasiyonipendeza Mimi. Baadhi ya watu wanakuja kwako kuleta umbeya na wewe
ulipenda kuwasikiliza hata kama walileta umbeya dhidi ya Mchungaji wako
mwenyewe. Ulipenda kuwasikiliza hao. Badala ya kumtetea Mchungaji wako na
kumsahihisha mbeya huyo ili arekebishe njia zake, ulikuwa kama wao, ukifanya
umbeya pamoja nao. Usisikilize umbeya tena. Mtu akija kwako na umbeya wa aina
yoyote, waombe radhi, kisha ondoka mara moja bila kushiriki. Usisikilize tena
mambo yasiyokujenga!”
Nikasema: “Bwana, nisamehe!” Nilijua kuwa nilikuwa
nina hatia. Hakuna jambo lililofichika mbele za Mungu. Hakuna anayeweza
kujificha mbele zake. Kila tunachofanya na kusema hapa duniani kimewekwa
kumbukumbu Mbinguni. Kutokana na maumivu yote yale masikioni mwangu, nikasema: “Bwana,
nisamehe. Naomba rehema zako.” Hatimaye
masikio yangu yalipakwa mafuta na malaika.
Bwana akaniambia: “Kuanzia leo na kuendelea, utasikiliza tu
mambo ambayo nimekuruhusu kusikiliza. Utafanya mambo yale tu ambayo nimekutaka
ufanye; hautakuwa Adelaida wa zamani tena. Hivi sasa wewe ni mtu mpya na ni
lazima uwe ni mwanamke yule ambaye ninataka uwe.”
Baada ya hapo nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako
malaika walianza kusafisha kinywa changu. Ulimi wangu ulitolewa kabisa kinywani
na kuwekwa kwenye aina fulani ya sinia. Malaika alianza kusafisha ulimi wangu,
na hapa tena nilihisi maumivu makali sana. Bwana akasema: “Nataka
kukusafisha. Nataka kukusafisha.”
Malaika walivyokuwa wanakwangua ulimi wangu, maji meusi
yalikuwa yanatoka humo, na baadaye yalitoka maji meupe. Mwishowe malaika
walitumia maji matamu sana kuoshea ulimi wangu. Yalikuwa matamu mno. Hakuna
kitu duniani kinachoweza kulinganishwa na utamu wa maji yale. Kisha ulimi wangu
ulipakwa mafuta. Kinywa changu nacho kilipitia mchakato huohuo. Maji meusi
yalitoka kwenye kinywa changu.
Bwana akasema, “Binti yangu, ninafanya hivi kwa ajili yako
ili usifanye umbeya tena; ili uache kufanya mambo yasiyonipendeza; maana ulimi
wako ulishiriki katika mambo mengi sana ambayo hayanipi utukufu Mimi. Ulisema
uongo mwingi sana. Acha kusema uongo! Kusema uongo hakutoki kwangu. Waongo
hawanipendezi Mimi. Waongo wote hawataniona Mimi. Hakuna mwongo atakayeingia
kwenye Ufalme wa Mbinguni.”
Nikasema: “Bwana, nihurumie. Najua kuwa nilifanya
mambo hayo yote. Nilisema uongo mara nyingi, lakini tafadhali nisamehe.”
Nilisema yote haya kwa sababu ya maumivu niliyokuwa nayahisi.
Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ninakupenda.
Ukiendelea na hali uliyokuwa nayo, nitakupoteza. Kama nisingefanya yote haya,
usingebadilika kamwe. Ni lazima niokoe moyo wako na hii ndiyo sababu ya kufanya
yote haya. Nakupenda, na kwa sababu nakupenda, sitaki kukupoteza.”
Bwana akasema tena: “Kama ulivyo wewe, wengi
kati ya watu wangu wako namna hiyohiyo.Wanasema uongo, wanaishi maisha ya aina
mbilimbili, na wanaonekana wako safi mbele ya watu wengine. Unapomwinulia mumeo
sauti ulimi wako unakuwa unatumiwa pia.” Kinywa changu
kilitakaswa kabisa. Halafu Bwana akaniambia nimeze maji hayo. Nami nikafanya
hivyo.
Ulimi wangu na kinywa changu vilipakwa mafuta ya thamani
sana ya mbinguni. Mafuta hayo yalikuwa maalum sana, yakiwa na harufu ya thamani
sana. Hayawezi kulinganishwa na mafuta yoyote ya hapa duniani. Ulimi wangu
ulirudishwa tena kinywani mwangu. Malaika mmoja alikuja na kuweka hatamu kwenye
koo langu. Na Bwana akaniambia: “Hii ni sawa na vile farasi anavyowekewa
hatamu.”
Nikwambie tu kwamba, hii ndiyo njia pekee tunayoweza
kubadilishwa. Acha kuongea maneno machafu na kushiriki katika mambo ambayo
hayatujengi. Mambo haya hayampendezi Mungu kamwe.
Acha kutamka maneno machafu na yasiyo na maana. Wako
Wakristo wengi – akina kaka, dada, Wainjilisti, Wamisionari, n.k., ambao
wanapenda kusema maneno machafu na yasiyo na maana. Niko hapa kukuhakikishia
juu ya kile ambacho Bwana alinionyesha ili maisha yako yabadilishwe. Ushuhuda
huu ni kwa ajili ya wewe kubadilika. Upendo wa Mungu na wa kwangu kwako ndio
ulioleta ushuhuda huu.
Ulimi wangu ulirudishiwa tena mahali pake na malaika na
ukawa umebadilishwa kabisa. Naweza kukuambia sasa, hakuna mtu anayeweza
kunikasirisha tena. Sasa naweza kufanya yale tu yanayompendeza Mungu.
Kisha, pua yangu nayo ilipitia mchakato huohuo. Maji meusi
yalitoka puani mwangu wakati wa kusafishwa na baadaye maji meupe. Pua yangu
ilipakwa mafuta na nilihisi maumivu makali sana wakati wa mchakato wa
kusafishwa. Nilisema: “Bwana, tafadhali niambie mambo niliyofanya kwa
kutumia pua yangu ambayo hayakukupendeza.”
Bwana akaniambia: “Baadhi ya wateja wako huvuta sigara na wewe
unavuta ule moshi kupitia pua zako maana
uliwahi kuwa mvutaji sigara na sasa wewe unajisikia vizuri kukaa nao wakati
wanapovuta.” Nikasema: “Bwana, najua. Nisamehe. Naomba
unirehemu.”
Bwana akaniambia: “Uko sawa tu na wale wote wanaovuta sigara na
wote wanaokunywa pombe pale unapokaa nao na kuvuta harufu ya sigara na pombe.”
Bwana akasema tena: “Hii ndiyo sababu yangu
ya kukusafisha wewe. Kwa hiyo, kuanzia leo kila utakapomwona mtu anavuta sigara
au anakunywa pombe, hautajisikia vizuri kukaa nao tena. Utajisikia kinyaa.”
Hakuna cha kujitetea mbele za Bwana. Mungu anafahamu fika
wewe ni nani na mimi ni nani. Libarikiwe Jina Takatifu la Bwana, Amina.
Niliendelea kumwomba Bwana rehema na nilipelekwa sehemu
nyingine. Pale, malaika walianza kuosha mwili wangu uliobakia kwa kutumia
sabuni nyeupe. Maji ya kijivu yalitoka kwenye mwili wangu.
Nikasema: “Bwana, nisaidie. Tafadhali, nisaidie.” Malaika
walikuwa wanasugua mwili wangu na ngozi ya juu iliondoka. Damu ilikuwa
inachuruzika kutoka kwenye ngozi yangu na nikamwuliza Bwana: “Kwa nini
unanifanyia hivi?”
Bwana akaniambia: “Ninakusafisha. Ni lazima uwe safi mwili wako
wote, nafsi yako, na roho yako. Roho yako, nafsi na mwili ni lazima viwe safi,
asema Bwana.”
Sabuni ilisuuzwa kutoka kwenye ngozi yangu kwa kutumia
maji ya thamani sana. Kisha malaika walipaka mafuta kila sehemu ya mwili wangu;
kila sehemu ya mwili wangu. Sehemu zote za mwili wangu zilipakwa mafuta.
Bwana akaniambia: “Usirudi tena kwenye njia zako za zamani, binti
yangu. Hivi sasa wewe ni Mtakatifu wangu aliyepakwa mafuta.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe kwa mambo yote niliyokuwa
nikifanya zamani hata mbele za uwepo wako. Nisamehe Bwana kwa kuwa kila kitu
ambacho Mchungaji wangu alijaribu kunisahihisha mimi nilikuwa nikipingana naye.
Nilisema mambo mengi kwake ambayo sikutakiwa kusema.”
Mchungaji wangu mara nyingi alikuwa akiniambia kuwa
mavazi yangu kama Mkristo hayakuwa sawa. Nilishindana naye sana. Aliwahi
kuniambia kuwa nilisema uongo na mimi nikahuzunika. Pale mtu anapopotoka na
Mchungaji wake akamsahihisha, mtu huyo huhuzunika. Siku zote mimi nilikuwa
kinyume na Mchungaji wangu.
Kisha nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako
nilipokelewa na malaika watatu. Malaika wale walitumia nguo nyeupe kufuta maji
kwenye mwili wangu. Kwenye nyuso za malaika wale, niliona kuwa walikuwa
wanajisikia huruma sana kwa ajili yangu kutokana na yote niliyopitia lakini
hawakusema kitu chochote, hata neno moja. Sikuweza kumwona Bwana kwenye sehemu
hizi. Nilikuwa nasikia tu sauti yake.
Malaika wengine watatu walinipokea kwenye idara nyingine.
Malaika hawa walinivika nguo nyeupe ya juu na sketi ndefu. Sketi ilikuwa ndefu
sana kiasi kwamba miguu yangu ilikuwa haionekani.
HATUA YA 4: Niliwaona Watakatifu Wengine Mbinguni
Nilipelekwa kwenye sehemu nyingine na mlango
ulifunguliwa. Niliona mwanga mkubwa ukimulika kupitia mlango ule. Ulikuwa ni
mwanga wa kuvutia sana. Bwana aliniambia nipite ndani. Nikasema, “Bwana,
naogopa.”
Nilijua kuwa Mungu alikuwa ananiandaa kwa sababu anataka
niokoke. Upendo haupendi mtu yeyote apotee. Nilisema: “Bwana, unirehemu.” Moyo
wangu ulikumbuka vizuri sana kila kitu nilichoacha nyuma kule duniani; wanangu.
Nikasema: “Bwana, naikabidhi familia yangu mikononi mwako.”
Kwenye sehemu ile niliweza kuona vitu kama miji mikubwa
na watu wengi sana ambao walikuwa wananingojea. Walikuwa wananipungia mikono.
Walikuwa wanataka niende kwenye sehemu ile walikokuwa.
Bwana akaniambia: “Mtakatifu wangu, muda umeshafika. Muda
umefika wa kuwaona wote walio hapa ambao wanakungojea.” Watu wengi sana
walikuwa wananingojea. Nami nilimwuliza Bwana: “Kitu gani kinaendelea hapa?”
Bwana akaniambia: “Ni wakati wa wewe kwenda na kuwahubiria watu
wote. Ni wakati wa wewe kwenda na kuhubiria mataifa yote. Ni wakati umefika.
Yote ambayo nimekuambia, nenda kawaambie Kanisa langu maana nitalifanya Kanisa
langu kuwa kamilifu. Nitaifanya nyumba yangu kuwa kamilifu. Kisha Neno langu
litapelekwa sehemu zote duniani zilizobakia, asema Bwana. Lakini kwanza ni
Kanisa langu.”
Hatua Ya 5: Safari Yangu Kuzimu na Yote Niliyoyaona Kule
Malaika walinitoa pale na tukawa tunaelekea chini.
Nikawauliza malaika wale: “Mnanipeleka wapi?” Niliingiwa na hofu kubwa
sana na ghafla ardhi ilifunguka.
Nikauliza tena: “Mnanipeleka wapi? Kitu gani
kinachoendelea kwangu?” Tuliingia moja kwa moja kwenye ardhi. Ilikuwa
inatisha sana. Kila upande kulikuwa na giza, nami sikuelewa malaika wale
walikuwa wananipeleka wapi.
Tulifika mahali ambako niliweza kuona mwanga mkali.
Kulikuwa na mlango chini ya ardhi. Mlango ule ulikuwa mbaya sana. Hakuna kitu
kwenye dunia hii kinachoweza kufananishwa na mlango ule.
Bwana akaniambia: “Huu ni mlango wa kuzimu.”
Nilifikiri labda ndio nilikuwa nimehukumiwa kutupwa
kuzimu kwa yale yote niliyotenda zamani. Kulikuwa na mtu akiningoja pale. Bwana
wetu Yesu Kristo ni mzuri sana. Bwana wetu Yesu Kristo alinyosha mkono wake
kwangu. Alikuwa akiningoja kwenye mlango wa kuzimu huku akiwa na ufunguo. Na
niliweza kuona wanyama wengi wa kutisha wakitokea kuzimu.
Nikasema: “Bwana, ni kitu gani kinachotokea kwangu?
Tafadhali Bwana, nihurumie.”
Bwana akaniambia: “Nitakuonyesha kuzimu na kila kitu kilichomo
ndani yake, ili uweze kuogopa na pia, kupitia wewe, watu wengine waweze kujua
kuwa kuzimu kweli kupo.”
Nikasema: “Bwana, hapana. Sitaki kwenda humo!”
Bwana akasema: “Binti yangu, fuatana nami. Njoo.”
Tulipofika pale, baadhi ya mapepo yalinyosha mikono yao
kujaribu kunikamata. Nikasema, “Bwana,
siwezi kuona, tafadhali.” Nilijaribu
kufunika uso wangu kwa mikono yangu, lakini bado nilikuwa naona kila kitu
waziwazi. Ukiwa pale, unasikia kila kitu, unaona kila kitu na unagusa kila
kitu, kama ilivyo kwa roho zingine zilizoko humo kuzimu. Bwana aliwazuia mapepo
kunikamata. Nilikuwa niko na Bwana. Niliweza kuona jinsi roho zilizoko kuzimu
zinavyoteseka.
KUNDI LA KWANZA LA ROHO
NILILOONA KUZIMU: MASHOGA NA WASAGAJI
Bwana alinipeleka mahali fulani. Watu waliokuwa pale
walikuwa ni Wakristo. Walimtumikia Bwana walipokuwa duniani lakini wakati
huohuo walikuwa wakitenda mambo yasiyompendeza Mungu. Walikufa na sasa wako
kuzimu.
Bwana alinionyesha mchungaji ambaye alikuwa akitumia
vibaya Neno la Mungu. Mchungaji huyu alikuwa anafanya mapenzi na wanaume
wenzake. Hakuwa mwana wa Mungu kwa sababu wana wa Mungu hawatendi mambo kama
hayo. Hapohapo, niliweza kuona jinsi mapepo yalivyokuwa yanamtesa mchungaji
yule ambaye alilinajisi Neno la Mungu. Mapepo yalimwingiza kwenye tyubu fulani,
na tyubu hiyo ikaanza kumzungusha na kumzungusha! Alikuwa anateseka kweli! Alipokuwa
duniani, alikuwa akinajisi watoto wadogo. Alinajisi hata wanaume wenzake.
Kama ambavyo unasoma ushuhuda huu, huenda haya ndiyo
unayofanya. Kuzimu ni halisi na pia kuna adhabu inayowangoja wote wasiotii Neno
la Mungu.
Mungu alikuumba wewe mwanamume. Pia, alimuumba mwanamke.
Niliona jinsi mwanamume huyo alivyokuwa anateswa kuzimu. Roho yake ililipuka
kisha ikajikusanya tena na kuendelea na mateso yale.
Bwana alimwambia: “Mwanangu, ulikuwa na muda wa kutosha duniani
wa kutubu na kurekebisha njia zako.”
Bwana alimwonyesha skrini na kwenye skrini hiyo
yalionekana maisha yake alipokuwa duniani. Alionekana mzee ambaye alikuwa akimwambia
asifuate njia mbaya; akimwambia atii Neno la Mungu. Kila neno ambalo Bwana
alimwambia kwa njia mbalimbali alionyeshwa kwenye skrini ile. Alikataa kutubu
na kurekebisha njia zake.
Na siku moja, alipata ajali na akafa. Hivi sasa yuko
kuzimu. Alijifanya kuwa yeye ni mchungaji kumbe hakuwa mchungaji.
Bwana alimgeuzia mgongo na yule mtu akaanza kutukana.
Hakuna upendo kuzimu. Hakuna kitu kabisa zaidi ya uchungu, huzuni, na maumivu
ya kutisha ambayo hakuna mtu anayeweza kustahimili.
Wakati niko pale, nilijihisi kama nataka kufa. Nilisema: “Bwana,
nataka kufa.”
Bwana akaniambia: “Binti yangu umeshakufa. Ona kile ambacho roho
zinateseka kuzimu binti yangu.”
Nikasema: “Bwana, siwezi kuvumilia zaidi. Roho yangu
inaungua. Joto ni kali sana. Bwana, siwezi!”
KUNDI LA PILI LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: MAKAHABA
Bwana alinipeleka sehemu nyingine. Niliona jinsi mapepo yanavyoitesa
roho ya mwanamke mmoja kuzimu. Mwanamke huyu alikuwa ni kahaba wakati akiwa
duniani. Aliwahi kuokoka. Bwana alimtoa kwenye ukahaba. Lakini alianguka tena
na kurudia ukahaba ule na akawa katika hali mbaya kuliko mwanzo. Alikufa kwa
kuuawa na sasa yuko kuzimu.
Niliona jinsi mapepo yalivyokuwa yanamtesa kuzimu. Badala
ya kuolewa na kufanya mapenzi na mume mmoja tu, aliamua kufanya kinyume. Mungu
anachukia mambo hayo yote. Hayo ni machukizo mbele za Mungu. Mwanamke yule
alikuwa uchi. Alilazwa chini na mapepo walikuwa wanamteza. Nikasema: “Bwana,
mhurumie.”
Bwana akasema: “Hapanaaa binti yangu. Alikuwa na muda wa
kutosha duniani wa kutubu.” Bwana alimwonyesha skrini na
wakaonekana Wainjilisti mbalimbali walioenda kumweleza juu ya kuyatoa maisha
yake kwa Yesu. Lakini hakutii sauti ya Mungu. Hivi sasa yuko kuzimu.
Ujumbe huu ni kwa wanawake wote wanaojiuza miili yao.
Labda unafanya hivyo kwa ajili ya kupata fedha za kulisha wanao; labda huna
mume. Mungu anakuambia leo urudi kwake. Mungu atakuhudumia wewe na familia
yako. Kwa wanawake wote wanaouza miili yao, nawaambia kwamba, tubuni leo na
kumrudia Mungu kupitia ushuhuda huu. Mungu ameleta ushuhuda huu kwa ajili ya
wokovu wa roho zenu ili kwamba msije kuishia kwenye sehemu ile ya mateso.
KUNDI LA TATU LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WAONGO NA WASENGENYAJI
Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine waliko waongo na
wasengenyaji. Niliona jinsi walivyokuwa wanateseka kuzimu. Ni hali ngumu mno.
Ni vigumu mno kuongelea kuhusu kuzimu.
Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako.
Kuwasengenya majirani zako kunaweza kukupotezea wokovu. Kumsengenya mchungaji
wako kuwaweza kukupotezea wokovu wako. Tubu leo kupitia ushuhuda huu na umrudie
Mungu, na Mungu naye atakurudia wewe, asema Bwana.
Niliuliza: “Bwana, yaani hii ni kwa sababu ya
usengenyaji tu?”
Bwana akasema: “Ndiyo, ni kwa usengenyaji tu.”
Nikauliza: “Bwana, lakini si huwa tunaomba rehema
tunapokutenda dhambi?”
Bwana akasema: “Hapana. Watu hawa hawakuomba rehema; na sasa
wanalipia dhambi zao.”
Kwa sababu hiyo, tunatakiwa kupatanishwa na Mungu kila
siku kwa sababu hakuna ajuaye ni lini atakufa. Usiondoke uweponi mwa Mungu.
Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako.
KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WAABUDU SANAMU
Mateso mahali pale yalikuwa makali sana. Kwa wanawake
wote wanaomtumikia Maria Lionza, je, mnamjua ni nani huyo? Huyo ni pepo. Bwana
alinionyesha Maria Lionza ni nani. Ni
pepo ambaye wachawi wengi wanapiga magoti kumwabudu kule kuzimu. Mapepo yaliwatesa
kupita kiasi. [Maelezo ya blogger: Maria Lionza ni
mzimu unaoabudiwa hasa kule Venezuela. Unaweza kusoma zaidi kwa kubofya HAPA.]
Miali ya moto wa kuzimu huwa haizimiki. Inawaka usiku na
mchana. Inawaka milele. Tafadhali ningependa utambue hili: waabudu sanamu
hawawezi kuuona uso wa Bwana.
Mungu anataka kubadili maisha yako. Mungu anataka uache
kuabudu sanamu. Mungu anataka umwabudu Yeye tu. Kuna Mungu mmoja tu na zaidi
yake hapana mwingine.
Roho za watu walio pale wanalazimishwa kumwabudu pepo
huyo hata kama hawataki. Wanateswa sana. Wanalazimishwa kuvuta sigara kuzimu
pale wanapomwabudu huyo pepo.
Shetani ni mwongo. Amekuja kuua na kuharibu. Lakini ni
lazima nikuambie hili: Yesu Kristo alikuja kuleta uzima na uzima tele. Mungu
Mwenyezi anakuita leo kupitia ushuhuda huu. Natamani uweze kuelewa ujumbe huu
na mipango aliyo nayo Mungu kwa ajili yako. Mungu ni halisi.
Nilikuwa kuzimu kwa saa 16 ili kuelewa makusudi ya ujumbe
huu; ili niweze kuuhubiri; ili niweze kusambaza ujumbe wa wokovu kwa kila mmoja
kwa moyo wote.
Nilimwona Barbara. Nilimwona Shango. Ninyi mnaomwabudu
Barbara, mtupeni nje ya nyumba zenu. Bwana anasema huyo ni pepola ukahaba.
Barbara hana upendo. Amejaa uharibifu. Ziko nyumba nyingi
ambazo hazina amani. Yeye ndiye anayehusika na hilo. Pia, unaweza kuwa
unashangaa ni nini kinachoendelea kwenye maisha yako – labda una sanamu yake
kwenye nyumba yako. Natamani sana ungeelewa ujumbe huu na mpango wa Mungu kwa
ajili yako. Pepo huyu alikuwa anawalazimisha watu kuzimu wamwabudu yeye. Watu
pale wanateseka sana. Ni moto tu kila mahali.
Nilimwuliza Bwana: “Je, hukuwapa watu hawa nafasi ya
kurekebisha njia zao?”
Bwana akasema: “Niliwapa. Nilituma watakatifu wangu kwao.”
Palepale kuzimu skrini inawekwa mbele yao nao
wanaonyeshwa kila kitu. Roho zilizo kuzimu hazina cha kujitetea mbele za Bwana.
Bwana anawaonyesha kila fursa waliyopewa walipokuwa duniani.
Kama hutatubu na kurekebisha njia zako leo, utaona jinsi
kifo kitakavyokushangaza nawe utaishia kuzimu.
KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WALEVI
Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine. Ilikuwa ni kama
klabu kubwa. Nilisikia watu humo wakipiga kelele, huku wakiomba kuhurumiwa na
kusaidiwa. Nikauliza: “Ni nini kinachoendelea humu?”
Bwana akasema: “Peleka ujumbe huu
kwa wote wanaotumia vileo usiku na mchana; kwa wote wale wanaoingiza miilini
mwao vitu ambavyo haviwajengi; kwa wote ambao wanatumia hata fedha za watoto
wao kwa ajili ya kulewea; peleka ujumbe huu kwa wanawake wale wote wanaolewa –
waambie warekebishe njia zao kupitia ujumbe huu.”
Pale kuzimu niliona meza imewekwa mbele yao ili wanywe.
Walilazimishwa kunywa bila kupenda. Wote walikuwa katikati ya moto. Kile
walichokuwa wakinywa ni asidi nami niliona jinsi roho zao zinavyolipuka baada
ya kunywa.
Nikasema: “Bwana, hapana. Siwezi kuvumilia zaidi ya
hapa, tafadhali Bwana.”
Kuna mwanamume kuzimu ambaye, wakati angali duniani,
Bwana alimpelekea Mwinjilisti baa akiwa analewa. Mwinjilisti yule alimwambia
atoe maisha yake kwa Bwana wetu Yesu Kristo, maana Mwinjilisti yule alihisi
kuwa mtu yule asingechukua muda mrefu kabla ya kufa. Mtu yule alimtukana
Mwinjilisti huyo. Alimwita kuwa ni mwanamke mwenye wazimu, jambo ambalo watu
wengi duniani wanawaambia Wakristo duniani. Siku ileile, mtu yule alitoka baa
akiwa amelewa. Alipata ajali na sasa yuko kuzimu.
Alikuwa analazimishwa kunywa vinywaji vya kule kuzimu.
Alijaribu kukimbia mateso lakini mapepo hayakumwachia. Anateswa pale kuzimu
milele.
WAVUTA SIGARA
Wavuta sigara nao wana idara yao kule kuzimu. Wale wote
wanaovuta bangi na wao pia wana idara yao kuzimu. Wanateswa milele.
KUABUDU AU KUHESHIMU SANAMU
Huenda unajiita Mkristo au vinginevyo, lakini bado
unaheshimu au kuabudu sanamu. Ni lazima utubu leo na kuyatoa maisha yako kwa
Yesu Kristo.
Kule kuzimu kuna wanaume na wanawake. Unaweza ukawa
tajiri sana hapa duniani kama ukitaka. Utaenda kuzimu usipotaka kuyatoa maisha
yako kwa Yesu Kristo. Fedha zako haziwezi kukununulia wokovu. Wokovu wako
ulishanunuliwa na Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.
Alikuwapo mwanamume mwingine ambaye naye alikuwa
analazimishwa kunywa kinywaji cha kuzimu. Nikamwuliza Bwana kwamba yule alikuwa
nani.
Bwana akasema: “Mtu huyu alikuwa ni Mtakatifu wangu. Aliniacha
na kuziendea njia zake na hatimaye alikufa katika dhambi.”
Kila kitu ambacho Bwana alikisema kuhusiana na mtu yule
kilikuwa kinaonyeshwa kwenye skrini – ujumbe, siku na saa ambayo Bwana
alimpelekea ujumbe. Mtu huyo yuko kuzimu sasa kutokana na uasi wake.
Unaweza kuwa unasema kwamba hii si kweli. Lakini niko
hapa kukueleza kwamba Bwana wetu Yesu Kristo ni halisi.
KUNDI LA SITA LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WANAWAKE WA MUNGU [WAHUBIRI]
Hawa ni wanawake waliomtumikia Mungu wakati wakiwa
duniani. Lakini hawakutaka kubadilika na kukubaliana na mafundisho ya Mungu.
Badala yake wao walipendelea kumtumikia Mungu kwa namna zao wenyewe. Mateso
niliyoyaona hapa yalikuwa mabaya zaidi ya yale niliyoyaona kabla.
Nilisikia huzuni kubwa sana kwa ajili ya hawa wanawake wa
Mungu walio kuzimu, maana walimtumikia Mungu wangali duniani.
Bwana aliniambia: “Kila wakati niliongea nao. Nilijaribu
kuwarekebisha kupitia baadhi ya Watakatifu wangu lakini hawakutaka kuelewa
makusudi.”
Bwana alinionyesha mmojawapo wa wanawake hawa. Alikuwa
amekaa kwenye kiti na kiti kile kilikuwa kimezungukwa na moto. Ghafla pepo lilitokea
na kummiminia maji fulani kichwani.
Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa
analia; Bwana wetu alikuwa analia.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini unalia?”
Bwana akaniambia: “Niliteseka sana kwa ajili ya roho zilizoko
kuzimu. Alikuwa ni Mtakatifu wangu. Nilimrekebisha ili asiipende dunia wala
mambo ya dunia.” Bwana alikuwa anamsahihisha aache kupaka
nywele zake rangi.
Bwana aliniambia: “Alikuwa anaonea aibu mvi nilizompa. Alikuwa
anajaribu kujionyesha kwa mwonekano ambao si wa kwake.”
Nywele zangu zilikuwa nyeusi na mimi nilitaka ziwe
nyeusi. Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupatia.” Pepo
liliendelea kumtesa. Alimlilia Bwana amsaidie. Bwana alimwambia kwamba
alishachelewa. Akaanza kutukana.
Hatuwezi kuishi kwa kujificha uhalisia wetu. Siku moja
sote tutakuwa na mvi.
Kadiri mapepo yalivyoendelea kummimina yale maji kichwani
mwake, shingo yake ilipinda upande mmoja. Nywele zake zilikuwa zinadondoka.
Alinyosha mikono yake ili kujaribu kuomba msaada.
Nikasema: “Siwezi kuvumilia zaidi.”
Nilijaribu kufunika uso wangu maana hata mimi nilikuwa
ninabadili rangi ya nywele zangu lakini sikuweza kuufunika uso wangu.
Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupa.”
Mwanamke yule alikuwa na nywele ndefu sana. Alikuwa ni
mwanamke mrembo lakini alitaka kuwa mrembo zaidi ya alivyokuwa. Lakini aliishia
kutenda kosa kubwa sana. Kama Mungu ametupa mvi, ni lazima tuzikubali maana
zinatoka kwa Mungu. Jambo hilo ni lazima litimie kwenye maisha yetu.
Nikasema: “Bwana, sikujua kuwa kubadili rangi ya
nywele ni dhambi.” Kisha nikasema: “Bwana, msaidie. Mrehemu.”
Bwana alipeleka Mchungaji kwa mwanamke huyu wakati
alipokuwa duniani. Alikuwa ni Mwinjilisti. Mwanamke huyu alikuwa akihubiri na
kufundisha. Kama ilivyo kwa baadhi, pale wanapohubiri, wanajaribu kujionyesha
wao kwanza kwenye kusanyiko ili wakubalike kwa jinsi walivyo, ili waweze
kuhubiri na kufundisha kile wakitakacho.
Mwanamke huyu hakuwahi kutaka kuelewa makusudi ya Mungu.
Hatimaye alikufa na sasa yuko kuzimu. Huyu alikuwa ni mwanamke aliyemtumikia
Bwana.
Bwana akasema: “Binti yangu, naenda kukuonyesha wanawake
wanaotumia vipodozi kwenye nyuso zao.”
Nikasema: “Bwana, hata mimi natumia vipodozi pia.
Natumia poda kwenye uso wangu ili nionekane mrembo zaidi, ili kuziba mabakabaka
kwenye uso wangu.”
Bwana akasema: “Vitu hivyo havinipendezi
mimi. Nafurahishwa na mwonekano wa asili wa Watakatifu wangu. Mwanamke
anatakiwa anifurahishe mimi na mume wake. Kwa hiyo, hahitaji vipodozi ili
kuonekana mrembo kwa mtu mwingine yeyote.”
Wakati huo ndipo nilipomwona mwanamke ambaye alikuwa
ameshikilia kioo mikononi mwake na mapepo yalikuwa yanamlazimisha kupaka vitu
fulani usoni mwake. Alipaka majimaji fulani usoni kisha ngozi ya uso wake
ikabanduka na kuanguka.
Huenda unasoma ushuhuda huu na unasema kwamba vipodozi si
dhambi. Nikwambie sasa – Mungu anaposema jambo, sote ni lazima tutii! Mwanamke
yule alikosa kutii alipokuwa duniani. Alikuwa akitumia vipodozi hapa duniani na
sasa yuko kuzimu. Kule analazimishwa kupodoa uso wake usiku na mchana.
Bwana akasema: “Vitu hivyo havinipendezi mimi. Unakumbuka
niliposema kuwa yule atakayeupenda ulimwengu ni adui wa Mungu?”
Ni lazima tutii mstari huo wa kwenye Biblia: Msiipende duni, wala mambo yaliyoko katika
dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. (1 Yohana 2:15).
Sote tutahukumiwa kwa neno hili. Aina zote za vipodozi
unazotumia hapa duniani, utavitumia na kuzimu pia. Nilikuwa nikitumia “wet-lips”
ili kufanya midomo yangu ing’ae na kuwafanya watu wengine wanione.
Nikasema: “Bwana, unisamehe maana nilikuwa na hatia ya
jambo hili.”
Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ya upendo nilionao
kwa roho yako. Ili kuleta hofu ya uzito wake ndani yako; ili uweze kuelewa
uzito wa matokeo; ili kwamba uweze kuwaeleza na wengine waache kutumia
vipodozi.”
Mwanamke yule alikuwa katikati ya moto huku akiendelea
kulazimishwa kujipodoa uso wake. Matokeo yake uso wake na midomo yake vilikuwa
vinadondoka chini.
Enyi wanawake wa Mungu; wanawake wa Mungu msiwatazame
majirani zenu. Yatazamani maisha yenu binafsi leo na kumwomba Mungu. Sema: “Bwana,
ni mambo gani ninayotenda ambayo hayakupendezi?” Muulize
Bwana naye atakujibu. Mungu huwa anajibu.
KUNDI LA SABA LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WANAWAKE WANAOVAA MAPAMBO YA VITO
Bwana aliniambia: “Sasa nitaenda kukuonyesha waliko wanawake
wanaovaa mapambo ya vito.”
Hapo nilimwona mwanamke ambaye alikuwa akilazimishwa na
mapepo kuvaa hereni kwenye masikio yake. Joka kubwa lilikuja kwake naye alivaa
hereni masikioni mwake. Kisha lile joka lilijiviringisha kwenye shingo yake.
Bwana yuko kinyume kabisa na wanawake wanaotumia mapambo
ya vito. Nikasema: “Bwana, lakini mbona hili ni pambo la kawaida tu?”
Bwana akasema: “Binti yangu, vitu hivyo havinipendezi Mimi.”
KUNDI LA NANE LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: FAMILIA NA WAPENDWA
Bwana alinipeleka mahali ambako nilimwona mwanamke
akilia; akipiga kelele sana kuzimu. Nilimwuliza Bwana: “Bwana, mwanamke huyu
ni nani?” na Bwana akasema: “Nitakuonyesha huyu ni nani.”
Alikuwa ni mwanamke niliyemfahamu miaka mingi iliyopita.
Tangu nilipoyatoa maisha yangu kwa Bwana, sikuwahi kuhubiri ujumbe wa wokovu
kwa mwanamke huyu.
Bwana aliniambia: “Yuko hapa kuzimu kwa sababu yako. Nilitaka
kuiokoa roho yake kupitia wewe lakini hukuwahi kwenda kumweleza habari zangu.”
Nikasema: “Bwana, naomba unihurumie!”
Mwanamke yule aliomba rehema kwa Bwana nami nikasema: “Bwana,
mhurumie.”
Mwanamke huyu alikuwa mlevi wakati alipokuwa angali
duniani. Bwana alimwonyesha kupitia skrini fursa zote alizokuwa nazo wakati
angali duniani za kuyatoa maisha yake kwa Bwana lakini alikataa. Siku ambayo
nilisukumwa kuongea na mwanamke huyu, sikusema naye kwa sababu aliniambia kuwa
angeniua kama ningemweleza habari za Bwana. Niliogopa na sikuweza kumhubiria.
Hivi sasa yuko kuzimu akiteseka. Jina lake ni Augustina.
KUNDI LA TISA LA ROHO NILILOONA
KUZIMU: WATUMIA DAWA ZA KULEVYA
Nilimwona mwanamume ambaye alikuwa akilazimishwa na
mapepo kutumia dawa za kulevya kuzimu. Alipewa kitu kama sigara ikiwa imejaa
miali ya moto ili aivute. Nikasema: “Bwana,
mwanamume huyu ni nani?”
Bwana akaniambia: “Njoo umwone ni nani.”
Nilimkaribia na nikashangaa kuona kuwa kumbe ni kaka
yangu Esau yuko kuzimu! Nilijawa na huzuni sana kumwona kaka yangu akiteseka
kuzimu. Nikasema: “Bwana, mhurume kaka yangu.”
Kaka yangu alinyoosha mkono wake ukiwa umejaa miali ya
moto na kuanza kumwomba Bwana rehema. Bwana akamwambia kaka yangu: “Mwanangu,
unakumbuka kuwa uliyatoa maisha yako kwangu wakati ulipokuwa gerezani na
ukaniomba nikutoe gerezani; na ukaahidi kwamba ungenitumikia katika maisha yako
yote?”
Kaka yangu akasema: “Bwana najua; nakumbuka. Lakini
tafadhali nisamehe. Nipe tu fursa ya kutoka mahali hapa.”
Bwana alimwonyesha skrini na tukaweza kuona wakati akiwa
gerezani miaka mingi iliyopita. Bwana alimwonyesha siku hiyo pamoja na ahadi
zote alizoahidi kumtumikia Bwana.
Bwana alimtoa gerezani kwa ili aweze kumtumikia lakini
alipotoka, alikataa kutimiza ahadi yake ya kumtumikia Bwana. Na miaka miwili
baadaye aliuawa mikononi mwa mama yangu. Kaka yangu alikufa kifo kibaya kwa
sababu ya kutokutii kwake.
Huyu ni kaka yangu ambaye ninakuambia habari zake. Kaka
yangu mwenyewe yuko kuzimu! Inatisha! Sikutaka kulisema hili waziwazi lakini Bwana
aliniambia kuwa ni lazima niliseme. Nililia sana nilipomwona kaka yangu akiwa
kuzimu.
Huwezi kupata picha jinsi Bwana
wetu anavyolia kwa ajili ya roho zilizoko kuzimu, Bwana aliniambia.
Bwana alinionyesha mwanamke aliyekuwa Mchungaji wakati
alipokuwa duniani. Alikuwa amekalia kiti kilichozungukwa na miali ya moto.
Alikuwa anavalishwa wigi (nywele za bandia) kuzimu na jingine tena juu
yake.
Bwana aliniambia: “Alikuwa ni Mtakatifu wangu wakati fulani
uliopita. Alikuwa ni Mchungaji wangu. Alikuwa ni mwanamke mkubwa wa Mungu.
Nilimtumia kwa kiwango cha juu sana, lakini aliasi Neno langu.”
Nikasema,
“Bwana, mhurumie.”
Alinyoosha
mkono wake kwa Bwana kuomba msaada. Najua kuwa hadithi ya mwanamke huyu
itasababisha maumivu makubwa sana ya kihisia.
Alikuwa
ni mwanamke aliyemtumikia Bwana. Alibadili mafundisho ya Bwana. Alimwacha Bwana
kwa ajili ya vitu vya dunia. Alikuwa akifanya vitu ambavyo vilikuwa
havimpendezi Bwana. Alikuwa akisema maneno yasiyo na maana kila wakati. Bwana
alimwonyesha kwenye skrini mambo yote aliyofanya wakati akiwa duniani.
Bwana alimwuliza: “Binti
yangu, unaweza kukumbuka pale nilipokuletea Neno langu kupitia Mtakatifu wangu,
Elma?”
Dada yangu, Elma alizungumza na mwanamke huyu wakati
akiwa duniani lakini yeye alimtukana dada yangu. Alikataa kutii na Bwana
akasema: “Hiyo ilikuwa ni fursa yako ya kurekebisha njia zako na kunirudia mimi
lakini ulikataa na hii ndiyo adhabu yako. Je, unakumbuka jinsi ambavyo binti
yako alikukumbatia na kusema, Mama rudi lakini hukutaka kusikiliza?”
Bwana alimgeuzia mgongo na mwanamke yule akaanza
kutukana.
Bwana wetu Yesu Kristo
alimgeuzia mgongo na kuanza kulia sana.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini unalia?”
Bwana akasema: “Huwezi kujua jinsi ninavyojisikia kuona roho
zikiwa hapa.”
NILIONA KITI CHA ENZI CHA
SHETANI KUZIMU
Bwana aliniambia: “Naenda kukuonyesha kitu binti yangu. Sikuwa
nimemwonyesha mtu yeyote kitu hiki kabla. Nataka ukione ili uweze kuelewa kuwa
shetani ni mwongo. Shetani huiga mambo.”
Nikasema: “Bwana, tafadhali naomba unitoe mahali hapa.
Siwezi tena kuvumilia zaidi.”
Bwana akanionyesha kiti cha enzi kuzimu. Niliona kiti cha
enzi cha shetani kuzimu! Shetani anamwiga Mungu Mwenyezi huko kuzimu. Nilimwona
akiwa amekaa kwenye hicho kiti chake cha enzi. Shetani ni mbaya sana. Naye anajifanya
ana ngazi za madaraka.
Niliweza kuona malaika wamemzunguka lakini wote ni
mapepo. Alikuwa amevaa joho jeupe likiwa limejaa madoadoa na ni chafu sana. Niliona
wazee ishirini na wanne wakimwabudu shetani kuzimu. Walidondosha taji zao na
kumwabudu. Niliweza kuona kuwa wote walikuwa ni mapepo.
Kiti cha enzi cha shetani kimejaa mambo yaliyoigwa kutoka
Mbinguni. Kila kitu kilionekana kibaya sana.
Nikauliza: “Bwana, hii ni nini?”
Wakati huohuo, shetani aliita mojawapo ya mapepo yake na
akalituma kwenda kumleta mtu fulani kutoka kuzimu. Mapepo yanafanya kila kitu
ambacho shetani anayaambia yafanye. Kila wakati huwa anayatuma duniani ili
kufanya uharibifu.
KITABU CHA KUZIMU
Bwana akasema: “Nataka ufahamu kuwa shetani huiga mambo ya
mbinguni. Nataka ufahamu kuwa shetani ni halisi. Shetani anataka kuuharibu
ulimwengu.”
Mahali pale niliweza kuliona pepo katika umbo la malaika
wa kishetani likiwa na makucha marefu sana na limeshikilia kitabu mkononi
mwake. Pepo hili lilikuwa linaandika kitabuni majina ya watu ambao wataenda
motoni.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini wanafanya hivi?”
Bwana akasema: “Nenda ukaiambie dunia kwamba watu wasio na
Yesu Kristo maishani mwao, shetani ameshaandika majina yao kwenye kitabu cha
kuzimu.”
Bwana akaniambia tena: “Angalia, pepo hili
limetumwa kwenye barabara ili kusababisha ajali. Kuna ajali nyingi zinazotokea kwenye
maeneo mbalimbali. Shetani na mapepo yake ndio wanaohusika na mambo haya.”
Nikasema: “Bwana, hali hii ni mbaya sana.”
Bwana akasema: “Ni muhimu uone mambo haya yote ili uwe na
uwezo wa kuielezea dunia jinsi kuzimu kulivyo, ili dunia iweze kujua na kuamini
kuwa kuzimu kweli kupo.”
NILITESWA NA BAADHI YA MAPEPO
KUZIMU
Kisha Bwana alikuwa akinipeleka kwenye sehemu nyingine.
Nikasema: “Niondoe mahali hapa. Hapa ni kubaya sana, tafadhali.”
Bwana alinishikilia mkono wakati tukiwa bado tunaenda.
Ghafla lilitokea pepo la kutisha, kubwa lenye makucha marefu.
Pepo lile lilikamata nywele zangu na likaruka na mimi.
Wakati huu sikuweza kumwona Bwana. Bwana alipotea na kuniacha peke yangu. Pepo
lile lilinikokota hadi kwenye sehemu nyingine, kisha mapepo mengine yalikuja na
kuanza kunitesa kwa namna mbalimbali.
Sauti ikawa inaongea kwenye ufahamu wangu ikisema: “Utabakia
hapa kuzimu milele na utateswa, na utahisi maumivu na majonzi yote ambayo yako
hapa kuzimu.”
Nikasema: “Bwana, siwezi kustahimili haya. Siwezi
kustahimili haya!”
Pepo jingine lilikuja kwangu likiwa na mdomo mrefu sana,
likapanda juu yangu. Nilijaribu kulisukuma lakini sikuweza. Liliingiza domo lake
kwa nguvu kinywani mwangu na nilihisi
mate yake kwenye kinywa changu chote. Nikapiga kelele: “Bwana, kwa nini
unaruhusu haya yote yanipate?”
Bwana akasema: “Ni muhimu; ni muhimu kwa wewe kuwaambia watu
duniani jinsi kuzimu kulivyo hasa ili waweze kuelewa makusudi.”
Bwana akasema: “MIMI NI MUNGU MTAKATIFU, wako watu kanisani
ambao wanafanya kila aina ya mambo machafu kwa vinywa vyao.”
Nikauliza: “Bwana, nitawezaje kusema mambo haya yote?”
Bwana akaniambia: “Sema kila kitu nilichokuonyesha.”
Bwana alinionyesha skrini na nikaweza kuona uchafu
mwingi. Wako watu wengi kanisani leo ambao wanatenda aina mbalimbali za dhambi
za siri.
Nikauliza: “Bwana, hii ni nini?”
Bwana akasema: “Waambie wabadilike. Waambie kuwa MIMI NI
MUNGU MTAKATIFU. Waambie kuwa vinywa vyao ni kwa ajili ya kunitukuza mimi na si
kwa ajili ya uchafu.”
Nikasema: “Bwana, ondoa pepo hili mwilini mwangu” maana
lile pepo lilikuwa linanyonya mwili wangu wote. Mate yake yalikuwa meusi sana
na yamefunika mwili wangu wote. Hali ilikuwa inatisha. Harufu ya kuzimu ni
mbaya mno kuliko hata mbwa aliyeoza. Sina maneno ya kuweza kuielezea. Nikasema:
“Bwana, nisaidie. Siwezi kustahimili zaidi.”
Bwana akaniambia: “Binti yangu, tulia. Ni muhimu sana kwa wewe
kupitia mambo yote haya.”
Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha peke yangu?”
Mara pepo jingine lilikuja. Likanichukua hadi kwenye
sehemu nyingine. Kule niliona roho zingine zikicheza. Nikauliza: “Bwana,
nini kinachofuata cha mimi kufanya sasa?”
Niliwekwa ili nicheze katikati ya moto. Kulikuwa na vitu
humo ndani vikinilazimisha kucheza. Nikauliza: “Bwana, kwa nini haya
yananipata?”
Bwana akasema: “Kwa sababu wewe ni mchezaji. Huwa unacheza
unaposikia kila muziki wa Kikristo na miziki mingine inayokupendeza wewe.”
Bwana akaniambia tena: “Mambo hayo hayanipendezi
mimi.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe. Sitarudia tena.”
Bwana akasema: “Kama ulivyo wewe, wako watu wengi miongoni
mwa watu wangu ambao hucheza kama watu wa dunia. Wanachezesha viuno vyao kama
watu wa kidunia. Mambo hayo hayanipendezi mimi.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe. Naomba unihurumie,” kwa
sababu roho yangu ilikuwa inaungua. Nilikuwa katikati ya miali ya moto.
Ninaweza kukuambia jinsi kuzimu kunavyotisha kwa sababu roho yangu ilikuwa
pale. Sisemi uongo hata kidogo. Nawaambia kweli tupu. Kuzimu ni halisi!
Nilikuwa pale!!
Mapepo yalinitoa mahali pale na kunipeleka sehemu
nyingine tena. Kulikuwa na minyoo mingi sana hapo. Minyoo ile iliingia sehemu
mbalimbali za mwili wangu – kupitia masikioni, machoni.
Nikasema: “Bwana, tafadhali nihurumie. Nitafanya kila
ulichoniambia nifanye, lakini tafadhali naomba unitoe hapa.”
Bwana akasema: “Hii ni muhimu sana ili kila mtu aweze kuelewa
kuwa kuzimu ni mahali halisi. Watu wengi husema kuwa kuzimu hakupo. Nenda
ukawaambie kuwa kuzimu kupo.”
Palepale
nilikumbuka kitabu cha Luka 16:19-31 kinachoongelea juu ya tajiri na Lazaro.
Pale kaka yangu aliponyoosha mkono alisema: “Bwana, peleka ujumbe huu kwa
familia yangu ili wasije kuja huku kuzimu.”
Bwana aliniambia: “Kumbuka hadithi ya Tajiri na Lazaro. Tajiri
alipoomba kwamba Lazaro atumwe duniani kuiambia familia ya tajiri kwamba kuzimu
kweli kupo.”
Niliondolewa kwenye sehemu ambako nilikuwa nateswa na
minyoo. Bwana akaniambia: “Ni muhimu sana ukaseme mambo yote uliyoona ili
roho ziokolewe. Ninafanya yote haya kwa sababu ya upendo nilio nao kwa
wanadamu. Kama nisingekuleta hapa,
ningekupoteza.”
Bwana akasema tena: “Roho nyingi zitaokolewa
kutokana na ushuhuda huu.”
Nikasema: “Tafadhali Bwana. Niondoe huku kuzimu.
Siwezi kuendelea kuwa hapa!”
Nilipitia mateso mengi sana kuzimu huku moto ukiwa
umefunika mwili wangu wote.
Hatimaye, ghafla nuru kali ilitokea na Bwana akanitokea.
Nilimkimbilia Bwana na kumkumbatia. Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha
peke yangu? Kwa nini uliniacha peke yangu? Kwa nini???”
Bwana akasema: “Ndiyo binti yangu. Binti, ilikuwa ni muhimu
sana uone maumivu ambayo roho zinayapata hapa kuzimu ili uwe na uwezo wa
kuuelezea ulimwengu uliobakia.”
Kisha Bwana alinitoa pale. Bwana alinionyesha vitu
vingine ambavyo sitaweza kuvisema kwa sasa. Mungu ataniambia ni lini niviseme
vitu hivyo. Hivi sasa nitakueleza tu vitu vile ambavyo Bwana aliniambia
niviseme.
SAFARI YANGU YA PILI KWENDA
MBINGUNI – KILA KITU KIKO TAYARI MBINGUNI
Bwana akasema: “Nitakuonyesha mahali ambako niliwaambia
mitume wangu kwamba naenda kuwaandalia mahali, ili mimi niliko na wao watakuwa
hapo pia, ili ukamwambie kila mtu kwamba mambo haya ni halisi.”
Bwana alikuwa ananipeleka moja kwa moja hadi mbinguni.
Kisha niliona mlango mkubwa ukiwa wazi.
Nikasema: “Bwana, kuzimu ni kubaya sana. Lakini mahali
hapa [mbinguni] ni kuzuri.”
Bwana akaniambia: “Binti yangu, nitakuonyesha Mbinguni.”
Na niliona sehemu kama jiji kubwa mbinguni. Ndiyo,
napaita mahali pale jiji kubwa kwa sababu hicho ndicho hasa nilichoona. Bwana
alinipeleka kwenye mtaa mmoja mbinguni. Mitaa ya mbinguni ni ya dhahabu tupu.
Ni dhahabu halisi kabisa! Niliona maua mazuri
pembeni ya mitaa ya mbinguni. Ni maua mazuri mno kiasi kwamba hakuna
maua hapa duniani yanayoweza kulinganishwa nayo!
Bwana alinipeleka mahali fulani na akaniambia: “Ninaenda
kukuonyesha mto. Nitakuingiza humo.”
Kulikuwa na mawemawe kwenye mto huo. Mto wenyewe ni kama
kioo. Mawe ya kwenye mto ule yanang’aa. Kulikuwa na samaki kwenye mto huo pia.
Bwana alimtoa samaki mmoja kwenye mto ule na kumshika mkononi; na samaki yule
alikuwa na furaha, huku akichezacheza mikononi mwa Bwana.
Nikasema: “Bwana, mrudishe samaki majini, atakufa.”
Bwana akasema: “Hakuna anayekufa hapa. Mauti haipo hapa.
Mahali hapa kumejaa uzima tu. Kila kitu hapa ni uzima.”
Nikasema: “Bwana, kuna watu wengi sana kule
wanaoteswa. Kwa nini hukuwapatia fursa ya kurekebisha njia zao ili waje hapa
Mbinguni?”
Bwana akasema: “Wako pale kutokana na uasi wao.”
Bwana alinichukua kama mtoto mdogo kutoka kwenye mto hadi
mahali pengine. Mto huo ni mzuri sana. Kila kitu kinachotungoja Mbinguni ni
kizuri sana!
Kisha niliomba jambo kwa Bwana. Nilimwambia Bwana: “Ziko
wapi roho ulizoziokoa? Wako wapi hapa mbinguni?”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha.”
Bwana alinipeleka mahali ambako alinionyesha mmojawapo wa
dada zangu katika Kristo ambaye alishakufa. Jina lake ni Aurora Esperanza.
Bwana alinionyesha dada mwingine. Alikuwa ni binti wa mmoja wa dada zangu, dada
Grace. Alionekana akiwa mdogo na mzuri sana.
Bwana akasema: “HAWA NI WATAKATIFU WANGU.”
Ana amani sana Mbinguni. Watakatifu walioko Mbinguni ni
kama malaika. Niliwaona Watakatifu wachanga Mbinguni. Mavazi yao ni tofauti. Mahali
ambako Bwana alinionyesha pamejaa maua mazuri. Ni mahali pazuri sana penye
harufu nzuri sana. Nilikuwa Mbinguni! Nilipaona Mbinguni! Nilipagusa Mbinguni!
Bwana aliniambia: “Sasa nitakuonyesha yaliko mavazi ya
Watakatifu wangu.”
Nikamwuliza Bwana: “Je, utanionyesha vazi langu?”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha mavazi ya Watakatifu Wangu.”
Bwana alionyesha baadhi ya mavazi, mavazi meupe ambayo
yamepambwa kwa dhahabu. Mavazi hayo yana mikanda ya dhahabu na yote yameandikwa
majina juu yake. Bwana alinionyesha pia mavazi mengine. Mavazi haya ni ya
baadhi ya watu ambao bado wako duniani ambao bado hawajampokea Bwana wetu Yesu
Kristo.
Bwana akaniambia: “Haya ndiyo mavazi ya Watakatifu Wangu na haya
ndiyo mavazi ya watu wengine ambao bado wako duniani, ambao bado hawajanipokea
mimi.”
Nikasema: “Bwana, nataka kuona mataji. Nataka
unionyeshe taji ya Mchungaji wangu, na taji yangu mwenyewe. Bwana, nataka kuona
taji yangu.”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha.” Bwana
alinionyesha mataji hayo, ni mazuri sana. Nitakueleza juu ya taji ya Mchungaji
wangu. Nilimwomba Bwana anionyeshe taji yake maana nilitaka kumletea Mchungaji
wangu habari njema.
Bwana alinionyesha taji yangu. Taji yangu haikuwa na vito.
Haikuwa kama taji zingine ambazo zilinivutia sana kama ile ya Mchungaji wangu.
Nikamwuliza Bwana: “Kwa nini taji yangu haina vito?”
Bwana akasema: “Huwezi kuelewa mambo aliyopitia hadi kufikia
kuwa na taji yenye vito vingi kama hii.”
Malaika alichaguliwa kuweka mataji na pia vito kwenye
mataji. Watu wanapotubu na kuja kwa Yesu Kristo, unapoleta roho kwenye
Ufalme wa Mbinguni, malaika ataweka
kito kwenye taji yako. Unapowasaidia wenye shida, malaika
ataongeza kito kingine kwenye taji yako.
Unapowasaidia maskini na wasio na mahali pa kuishi, malaika
ataongeza vito zaidi kwenye taji yako.
Bwana alikuwa anaongea nami kuhusu Mchungaji wangu.
Alisema kuwa ameshateseka sana kwa ajili ya Ufalme wa Mungu; na kwamba alipitia
magumu mengi hadi kupata taji kama hiyo. Ana moyo sana wa kuleta roho za watu
kwa Kristo.
Bwana akasema: “Mwambie ashikilie kwa nguvu kile alicho nacho
ili mtu mwingine asije akachukua taji yake.”
Nilimweleza Mchungaji wangu yale yote ambayo Bwana
aliniambia.
Halafu Bwana alinionyesha mataji ya Watakatifu Wake wote.
Alinionyesha mataji ya watu ambao hawajayatoa maisha yao
kwake lakini bado wako duniani.
NILIONA KITI CHA ENZI CHA MUNGU
MBINGUNI
Bwana alisema: “Binti yangu, nitakuonyesha kitu.”
Kutokea mbali, niliona kiti cha enzi kikubwa sana; cha thamani
sana.
Bwana akasema: “Hiki ni kiti cha enzi cha Baba yangu.”
Bwana alikuwa amekaa pale. Nuru kali ya kiti cha enzi
ilinifanya nisiweze kuona mengi. Niliona baadhi ya wazee wakitupa taji zao
chini na kuinama ili kumwabudu Bwana. Hawaachi kumwabudu Bwana Mbinguni.
Niliona malaika wengi sana wakiwa wamesimama kuzunguka
kiti cha enzi cha Mungu. Kitabu cha Ufunuo kinaongelea kuhusu sehemu hii.
Mbingu ni halisi. Niliona mbingu kwa sababu nilifika pale.
Bwana akasema: “Binti, kaiambie dunia kwamba mbingu ni halisi.
Zungumza binti yangu.”
Nikauliza: “Bwana, unadhani wataniamini?”
Bwana akasema: “NDIYO.”
Nilikuwa nazungumza na Bwana kama ambavyo naweza
kuzungumza na kaka yangu au na Mchungaji wangu.
Niliona malaika wengi sana Mbinguni; na kila walipomwona
Bwana, walivua mataji yao na kuinama na kumwabudu Bwana. Nilijawa na furaha
sana kuona mambo haya.
Bwana akasema: “Binti yangu, UTUKUFU WOTE NI MALI YANGU.
UTUKUFU WOTE NI WANGU.”
Hapa nilielewa kwamba Mungu hashirikiani utukufu wake na
yeyote. Malaika walikuwa wakiimba, wakimwabudu Bwana muda wote. Hawaachi hata
kidogo kumwabudu Bwana. Niliona jinsi kanisa lenye wachungaji wazuri
linavyomwabudu Bwana. Dada yangu, Yasmine, alikuwa akiwaongoza.
Bwana akasema: “Waambie kwaya ya kanisa la wachungaji wazuri
waniabudu Mimi na waache kufanya mambo yasiyonipendeza. Waambie kuwa kila
wanaponiabudu, malaika Mbinguni huabudu pamoja nao.”
Ujumbe huu ni kwa wote wanaoabudu. Bwana anataka mmwabudu
zaidi.
“Waambie waniabudu Mimi,” Bwana alisema.
Malaika walikuwa wakipiga vyombo mbalimbali katika
kumwabudu Bwana.
MUNGU WETU NI BABA MTAKATIFU, AMINA
Malaika ni wazuri sana. Wanapomwabudu Bwana. Niliona
amani kubwa sana kati yao. Waliabudu kutoka moyoni.
Bwana alinipeleka sehemu nyingine. Niliwaona malaika saba
wameshikilia tarumbeta saba. Na karibu yao, kulikuwa na malaika wengine saba wameshikilia
vikombe mikononi mwao. Walikuwa ni malaika wakubwa na warefu sana. Walivaa
mavazi meupe sana; weupe ambao hata hauelezeki!
Nikauliza: “Bwana, malaika hawa ni akina nani?”
Bwana akasema: “Malaika hawa wanasubiri kutumwa duniani ili
kuiharibu dunia.”
Malaika wale tayari wana tarumbeta mikononi mwao.
Wanasubiri tu Bwana awaambie waanze kuzipiga.
Nikauliza: “Bwana, mbona ni warefu hivyo?”
Bwana akasema: “Kwa kuwa wao ni wana wa Mfalme.”
Nilikuwa nimekusudia kuuliza maswali zaidi. Lakini Bwana
akaniambia: “Usiwe mdadisi sana. Usiulizeulize maswali mengi mno. Wewe onyesha tu
yale ambayo nimekuonyesha; mambo ambayo nimekwambia useme. Waambie kuwa kuna
Mbingu moja tu na wala hakuna nyingine. Waambie kuwa Mimi ni halisi, maana watu
wengi hawazungumzi kuhusiana na Mimi. Waambie kuwa Mungu yuko pale juu
akiwangoja.”
Kisha Bwana akasema: “Sasa nitakuonyesha kile
kinachoendelea miongoni mwa watu wangu.”
Bwana alinionyesha sehemu moja. Sehemu ile ilikuwa na
pazia. Halafu akasema: “Ona kile kinachoendelea kwenye Kanisa langu. Ndani
ya Kanisa langu yapo mambo mengi ambayo hayanipendezi. Nitaleta kwa Baba yangu
taifa Takatifu tu. Kanisa langu haliko tayari. Nenda kawaambie wajiweke tayari
kwa sababu tarumbeta karibu italia.”
NILIONA MEZA YA BWANA
IMESHAANDALIWA TAYARI
Bwana akasema: “Sasa nitakuonyesha mahali ambako Watakatifu wangu
watakula pamoja na Mimi.”
Akanionyesha meza kubwa sana, imepambwa vizuri kwa
vitambaa vyeupe, vikombe vya dhahabu, huku kukiwa na viti kila mahali, na viti
vyote vina majina ya Watakatifu yameandikwa juu yake. Sikuweza kuelewa majina
yale. Nilimwomba Bwana anionyeshe kiti changu.
Bwana alinionyesha kiti changu na kusema: “Liambie
Kanisa langu lijiandae. Waambie watu wangu kwamba meza imeshaandaliwa.”
Nikasema: “Bwana, hapa ni pazuri sana.” Nilitaka kukaa kwenye kiti kimojawapo.
Bwana akasema: “Usikae kwenye kiti. Bado muda haujafika.”
Kisha niliona malaika wakienda na kurudi, na mmoja wao
alikuja na kuzungumza na Bwana moja kwa moja masikioni mwake.
Nikamwuliza
Bwana: “Amesema nini?”
Bwana akasema: “Usiwe mdadisi sana.”
Kisha malaika alikuja tena na kuzungumza masikioni mwa
Bwana. Bwana akasema: “Binti yangu, muda umeshafika wa wewe kurudi. Kaliambie
Kanisa langu wajiandae. Kawaambie kila kitu nilichokuonyesha.”
Nikasema: “Bwana, hapanaaaa! Sitaki kurudi.”
Bwana akasema: “Ndiyo, ni lazima urudi ukawaambie kila kitu
ulichoona. Waambie kuwa meza iko tayari, inawangoja. Ni lazima mjiweke tayari.”
Wakati tukiwa tunaondoka, Bwana akasema: “Kanisa
langu liko namna hii: baadhi ya watu ni wa nia mbilimbili, baadhi ni wanafiki,
wengine hawako tayari, wengine hawanipendi Mimi kwa moyo wote, baadhi wanafanya
mambo kwenye nyumba yangu kwa sababu wanalazimika tu kufanya, wengine wanataka
waonwe na kusifiwa na wachungaji wao.”
Bwana alianza kulia!
WATOTO WASIO WATII, WANAOPOKEA
SIMU WAKIWA KANISANI
Bwana alinionyesha Kanisa. Nilimwona mhubiri akihubiri
madhabahuni na ghafla simu yake iliita. Mhubiri huyu aliacha kuhubiri. Alitoka
nje ili kwenda kusikiliza simu yake.
Bwana akasema: “Unaona jinsi wanavyopuuza uwepo wangu; ona
jinsi wanavyopuuza uwepo wangu. Mtu anapohubiri, anakuwa anahubiri Neno langu.
Wanaona bora kwenda kusikiliza simu kuliko kushughulika na Mimi.”
Kisha Bwana akaniambia: “Sema, sema na Wachungaji
waachane na mafundisho yao. Wanaweza kukuchukia kama wakitaka, lakini watu
wengi wataelewa makusudi ya Mimi kukuleta hapa na wengi watatubu.”
Ujumbe kwenu wachungaji. Watu wanaweza kuwachukia pale
mnapoamua kuyafanya mapenzi ya Mungu. Haijalishi kama watawachukia. Sahauni
mafundisho yenu wenyewe. Fuateni kile ambacho Mungu amewapa. Msijaribu
kumfurahisha kila mtu. Msikubali kuridhia mambo asiyopenda Mungu.
Bwana akasema: “Nitaenda kuliunganisha Kanisa langu pamoja.
Mimi nina Kanisa moja tu. Sina Kanisa jingine duniani zaidi ya Kanisa moja tu.
Hili ndilo Kanisa nitakalolipeleka mbinguni. Hili ndilo Kanisa
nitakalolikabidhi kwa Baba yangu.”
Sisi tulio wa Huduma ya Kiinjilisti ndio Kanisa la Mungu.
Wale ambao wameyatoa maisha yao yote kwa Yesu Kristo. Wale ambao hawatendi
dhambi tena. Wale ambao wameziacha njia zao za zamani ili kuyafanya mapenzi ya
Mungu. Wale waliozaliwa upya. Hawa ndio watu watakaouona uso wa Mungu.
HITIMISHO
Ushuhuda wangu unakaribia mwishoni. Nimewaeleza kila kitu
ambacho Bwana aliniambia niseme, kwa utukufu wa Mungu. Utukufu wote, utukufu
wote ni wa Mungu.
Niko hapa kwa rehema za Mungu. Ni kwa rehema za Mungu tu
ninawaambia mambo haya ambayo Bwana alinitaka niyaseme. Ujumbe huu utakwenda
moyoni mwako na kubadili maisha yako ili kwamba uweze kutubu.
Mwulize Bwana: “Bwana, ni eneo gani la maisha yangu
ambako ninashindwa?” Bwana atakujibu.
Napenda kukuambia kwamba Yesu Kristo anakupenda wewe;
Yesu Kristo anakupenda wewe! Anataka kuyabadili maisha yako. Yesu Kristo hataki
uende jehanamu bali anataka uende Mbinguni. Mbingu ni halisi, na kuzimu nako ni
halisi pia. Tubu sasa na uyatoe maisha yako kwa Yesu Kristo. Wokovu unapatikana
kwa Yesu Kristo tu!
Yesu Kristo anagonga kwenye mlango wa moyo wako kupitia
ujumbe huu. Mtafute Bwana kwa moyo wako wote, naye atafanya mambo makubwa
kupitia wewe.
Bwana akasema: “Mambo yote haya niliyokuonyesha
yalishatabiriwa kwenye Kitabu cha Ezekieli, Kitabu cha Danieli na Kitabu cha Ufunuo.
Mafunuo yote haya yamo kwenye Biblia.”
Ninaomba kwamba ushuhuda huu ukabadilishe maisha yako kwa
ajili ya utukufu wa Mungu. AMINA.
MUNGU awabariki nyote.
**********
Ushuhuda huu nimeutafsiri
kutoka kwenye toleo lake la Kiingereza ambalo linaweza kupatikana kwa kubofya kwenye
kiungo kifuatacho: http://www.divinerevelations.info/Adelaida/index.htm
naca testimon
ReplyDeleteasante mwandishi kwa kutuwekea mungu akuzidishie kila wakati.
ReplyDeleteila mie ndo nakwenda kuisoma kwa sasa.
nitakuja kutoa maoni yangu tena nikisha kusoma.
ila ingependeza zaidi kama kungekuwa na uwezekano mgetuwekea ya audio ili nasi tukaipakua na kwenda kwatangazia wale ambao hawamini.
shalom Jeremia. Asante kwa maoni yako. Nitaangalia kama kuna audio yake kisha nitawasiliana nawe. Ubarikiwe na Bwana Yesu.
Deletedaa nimefurah sana kwa kutuletea habari nzur.
ReplyDeletejapo sijafaham kuwa alikujaje duniani.
hakika habar imeniingia moyoni mwangu na kunifunulia kuwa ni mwenye dhambi.hivyo yanipasa kutubu haraka.
mie kinanisibu zaidi ni kutawalwa na shetani kwa kunitumia kwa kupiga punto mala kwa mala kwani sili! sifichi nataka kila mtu ajue kuwa kinanisibu kitu gani...!na kingine kinanisibu ni kuto watembelea wagonjwa na kuwaeshimu wakubwa zangu.haya ndo mambo nais kuwa yatanifikisha kuzimu au jehanamu.ila leo nasema nimekoma na sita ludia na shetani amekwama iwe kwa viboko iwe kwa mateso iwe kwa uchungu gani,nitaakisha sifa na utukufu nampa mungu.
kaka yangu mpendwa kuna sitoria ya nyikasi wa uyole nae alichukuliwa na mungu. yy nilibahatika kusikiliza anavyo ongea mpendwa ni her kusikia au kusoma lakiliza ni hatar.
kanifanya nibadilishe mwenendo wangu japo namba yake siijui.na wala mawasiliano hakutaja waweza ww ukawa ni mwandishi waweza kunipatia masiliano.namba yangu 0786302811.
email
jeremia.juma@yahoo.com.asante mpendwa.
it' real that hell exist
ReplyDeleteShalom Huruma. Does your comment intend to question or to support the idea of the existence of 'hell'?
DeleteAmen. Mungu na atusaidie ktk kutimiza mapenzi yake.
ReplyDeleteAmen. Ni kweli kabisa bila Bwana Yesu hatuwezi chochote. Ni neema yake pekee inayoweza kutusaidia kumfuata Yeye.
DeleteHay a mambo ya kujipodoa name urembo yatapeleka walokole weng kuzimu isee.. ombeeni mabinti waamama.. ktk hili.. NashukuruMungu naendelea kupona hapo amen..maana nimehakikishiwa nine kweli baada ya kusoma shuhuda kamhizo zaidi ya 5..
ReplyDeleteAmen dada Jessica. Asante kwa maneno yako na Bwana Yesu azidi kukupa ushindi kwenye kila eneo la maisha yako.
DeleteTunaangushwa na ile roho ya "kutaka kuwa kama wengine" (conformity) badala ya kutaka kuwa kama Yesu.
Endelea kusonga mbele katika Jina la Yesu.
Dada Jessica Honore mbona bado unavaa mawigi au ndo umeshasahau ulichokisoma mwaka 2014? tubadilike jamani,,,...
DeleteKwa kweli imenigusa sana ila na hapo kwenye mvi wamama wengi wanapend sna kuweka nywele zao kuwa nyeusi na vipodozi navyo ni issue. Mungu atusaidie manake kuingia huko ni kwa Neema ya mungu tu peke yetu hatutaweza!!!
ReplyDeleteNi kweli Eliza unachosema; hatuwezi bila msaada wa Bwana mwenyewe. Ndiyo maana anasema kuwa "Pasipo mimi ninyi hamuwezi lolote."
DeleteTunahitaji neema yake kila saa; kila dakika.
Mungu akubariki ukiyetafsiri ujumbe huu, ili uwafikie wengi Ni Mungu atakulipa kwa utumishi huu. Ushuhuda huu umenifanya nianze kutizama mengi na jicho la tofauti na naumbika hofu ya Mungu, Mungu atusaidie maana wengi wataishia kuzimu kama hawatabadilika, inatisha!!!!!
ReplyDeleteamina. ubarikiwe nawe pia.
DeleteMungu atutie nguvu maana kweli Yesu yu malangoni
ReplyDeleteamen. uzidi kubarikiwa na Bwana akushike mkono hadi mwisho wa safari hii.
DeleteKwa kweli Mungu asimame mwenyewe tu, nimepata majibu ya vitu vingi nilivyokuwa nikijiuliza kama ni dhambi au la. Ninaomba tu reheme Ya Bwana ituokoe maana tumeoza na kupotoka. EE Mungu uishiye na kumiliki naomba unirehemu na wengine wote waliokuwa kama mimi. Amen.
ReplyDeleteAsaƱte Mungu kwa neema ya mafunuo kupiia watumishi wako,tuwezeshe kushinda ,
ReplyDeleteAisee Mungu ametufumbua macho pia ushuhuda wa Margaret O.Amure,Rachel Mushala,Emmanuel Senayon na Linda Rika Ngaujah umegusia mapodozi na mavazi
ReplyDeleteNelson Yandilo
ReplyDeleteAsante kwa bwana for this message thank to dada apo kwa kujitowa kuu sender kwenye net tunafurahi na MUNGU atubari
ReplyDelete