Sunday, December 21, 2014

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 7




Bwana alizungumza waziwazi. Wakati huu, shughuli za kiroho za makanisa zinapingana na kile ambazo niliwakusudia. Viongozi na waumini wananiabudu kimazoea tu na wananijua kwa nadharia tu za vitabuni. Iweni na shauku kubwa kisha mnijie Mimi.


Bwana wetu ana shauku ya kutuonyesha uhalisia wa kuingia kwenye mapambano ya kiroho dhidi ya mapepo wabaya na kufungua macho yetu ya kiroho ili kwamba tuweze kuona moja kwa moja Mbinguni, kuzimu, malaika na shetani. 

Saturday, December 13, 2014

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 6







====  SIKU YA 13  ==== 

Kim, Joo-Eun 

Leo yalikuwapo mashambulizi makubwa kutoka kwa mapepo. Wakati ninaomba, nilipelekwa hadi kwenye sehemu yenye giza, ambayo nilijua kuwa ni kuzimu. Niliona mapepo mengi ambayo yalikuwa yamezunguka kiumbe kikubwa kiovu. Kiumbe hiki kikubwa kilionekana kina hamaki pamoja na hofu. Kilipiga kelele na kuhaha huku na huku, na kuonekana kimechanganyikiwa na kisichokuwa na utulivu.


Wednesday, December 10, 2014

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 5






====  SIKU YA 11  ====

Kim, Joo-Eun

Kadiri nilivyoomba kwa bidii, nuru kali ilitokea mbele yangu, na mbele ya hiyo nuru alisimama Yesu. "Joo-Eun, nakupenda. Omba bila kukoma; omba kwa bidii; omba kwa moyo wako wote. Usiache kuomba." Nilihisi ujotojoto na niliweza kumwona Yesu kwa wazi zaidi. Ndipo nikatambua ni kwa nini Yesu aliniambia niinue mikono yangu juu zaidi. Niliweza kumwona wazi zaidi nilipofanya hivyo. Nikamwambia, "Haa! Nakuona waziwazi, Bwana. Ni vizuri sana, Yesu. Nakushukuru." Kutokana na kule kujisikia vizuri sana, nilijikuta ninaacha kuomba kwa muda kidogo. Mara lilitokea pepo chafu. Lilikuwa jeusi tii kuliko giza. Nikalifukuza kwa Jina la Yesu, na nikaendelea kuomba kwa kunena kwa lugha.