====
SIKU YA 10 ====
Kim, Joo-Eun:
Wakati
nikiwa nimezama katika kuomba kwa lugha, joka jekundu lilinitokea. Lilikuja
kwangu kwa kasi na kunirukia. Lilikuwa na macho kama ya mamba na makucha
makubwa makali, na likajaribu kunitisha kwa makucha yake. Moshi unaotia kinyaa
ulitoka kwenye pua zake. "Ewe shetani mbaya, ondoka kwangu kwa Jina la
Yesu." Nilikuwa napaza sauti kama mwanamke mwenye wazimu. Ndipo joka
hilo likaelekea upande wa kaka Haak-Sung. Haak-Sung akashtuka. Kuomba
kwake kwa lugha kukawa kwa bidii na kwa sauti zaidi. Alikemea kama nilivyofanya
mimi, "Ewe shetani mbaya, ondoka kwangu kwa Jina la Yesu."
Mara, lile joka likanijia, na kugeuka kuwa joka jeusi. Kwa kicheko kiovu,
likaanza kusema, "Usiombe. Kwa nini unafungua
macho bila kutumia nguvu yako wakati wa kuomba? Kama ni hivyo, basi fungua
macho yako. Kwani ni lazima ufunge macho yako wakati wa kuomba? Fungua macho yako sasa hivi? Kwa nini unaomba
kwa bidii hivyo siku ya leo?" Lilijaribu kuniondolea uzingativu
wangu wakati wa kuomba. Nikapaza sauti tena, "Ewe shetani mbaya, ondoka
kwangu kwa Jina la Yesu." Lakini joka lile halikuondoka kirahisi. Kwa
hiyo, ilibidi nisisitize Jina la Yesu zaidi. Kwa kusema kwa sauti Jina la Yesu,
joka lile lilinigeukia tena kwa macho maovu, likasaga meno yake na kutoweka.
Mara pepo
jingine likanikodolea macho, na kuanza kunijia. Niligundua lilikuwa ni pepo
maarufu la kike linaloonekana kwenye sinema nyingi za Kikorea za mambo ya
kutisha na kwenye TV. Niliogopa, lakini nikatambua kuwa nikiruhusu tu woga,
litapata ujasiri wa kunishambulia. Kwa nguvu zangu zote nilijitahidi
kutoonyesha woga, wakati nikipambana nalo kwa maombi. Lengo la pepo hili ni
kuwaogopesha watu hadi wafe. Damu ilichuruzika toka kwenye kona za midomo yake,
na nywele zake zilikuwa hovyohovyo. Lilitoa sauti mbaya na kicheko cha kutisha.
Kwa nguvu zote nilisema kwa sauti, "Ondoka kwangu kwa Jina la Yesu!"
nalo likatoweka.
Baadaye,
Bwana Yesu alinitokea. Hata hivyo, safari hii nilihisi kulikuwa na jambo lisilo
sawa. Sikujisikia amani, nikaingiwa na hofu kumwona Bwana. Nikakumbuka mchungaji
wangu aliniambia niwe makini, maana shetani huweza kujigeuza malaika wa nuru.
Niliambiwa kama nikishindwa kupambanua roho, ama niombe kwa lugha au niijaribu
roho kwa kutamka Andiko. Nilimjaribu huyu yesu kwa kunena kwa lugha.
Kilichokuwa kimeonekana kama uso wa Yesu, kilianza kumomonyoka na kuwa uso
mweusi tii. Shetani alinijia akiwa amevaa sura kama ya Yesu. Macho ya shetani
lile yaligeuka pande zote na akawa haondoki akijaribu kuniondolea uzingativu
katika kuomba.
Dada Baek, Bong-Nyo:
Leo nikiwa
naomba kwa lugha, Bwana Yesu alinijia. Nililia, "Bwana, Bwana."
Yesu alizungumza akasema, "Acha kulia. Nimekuja kukuchukua hadi Mbinguni. Haya twende."
Kulikuwa na huruma kwenye uso wa Bwana akiwa amenishika mkono. Kila
ninapotembelea Mbinguni, ninajawa na furaha sana kutokana na maajabu yote
ambayo hayana mwisho na ni ya milele. Navutiwa sana na mandhari ya huko. Nahisi
kuwa itatuchukua milele kuona na kutembelea Mbingu yote. Yesu aliniambia niende
nikaangalie Kanisa la Mbinguni. Mara tulipofika pale, nilibakia mdomo wazi
kutokana na uzuri wa jengo hilo. Nikasema kwa mshangao, "Haa!"
Nilikuwa nimeshangaa kwelikweli. Lilikuwa jengo kubwa sana. Lilionekana kama
vile linaweza kugusa anga la Mbinguni.
Baadaye,
tukiwa tunatembelea Mbingu, Yesu alisema, "Bong-Nyo,
hebu twende tukatembelee kilele kirefu kabisa Mbinguni." Tulipofika
juu, niliweza kuona sehemu mbalimbali za Mbinguni. Niliona malaika wengi na
bustani pana zenye maua aina mbalimbali. Ilikuwa haiwezekani kwangu kuhesabu
aina zote za mimea na maua niliyoona. Niliweza kuona bahari isiyo na mwisho,
ikiwa na maji angavu kabisa. Kulikuwa na meli nzuri zikiwa juu ya maji.
Baadaye,
niliporudi duniani, japokuwa ndio nilitoka tu kutembelea Mbinguni,
niliwakumbuka tena wazazi wangu na kaka yangu walioko kuzimu. Nililia kwa saa
nyingi, na sikujua cha kufanya. Mara, kikundi cha malaika kumi na tano kilinitokea.
"Bwana Mungu ametuamuru kwenda duniani kumfariji Dada Baek,
Bong-Nyo. Hii ndiyo sababu tuko hapa." Walinizunguka na kuanza
kunihudumia kwa maneno ya faraja. Mara niliweza kutulia na machozi yangu
yalifutwa.
Baadaye
tena, niliendelea kuomba. Ghafla, niliona Mbingu zimefunguka, na Mungu Baba
alikuwa amekaa kwenye kiti chake cha enzi Mbinguni. Alizungumza na kuniambia
nisilie. Roho Mtakatifu alikuja na kuniambia, "Nitakupa wewe na Dada Kang, Hyun-Ja karama ya
uponyaji na moto wa Roho Mtakatifu. Lakini ni lazima muwe na shauku kubwa ya
karama hiyo na kuitaka kwa bidii." Yesu akiwa amesimama mkono
wa kuume wa Baba, aliniambia, "Bong-Nyo, ukichoka na kuwa dhaifu wakati wa kuomba, nitakupaka mafuta kwa
nguvu ya Roho Mtakatifu."
Baada ya
kitambo kidogo, Yesu alianza kuongea kwa sauti yenye ukali. Alisema kuwa
makanisa na wachungaji wanamwabudu Yeye bure. Wanafuata mapokeo na mafundisho
ya wanadamu. Ibada nyingi ni fupi na hazina ujumbe. Kiasi cha muda unaotumika
kuabudu na kusifu kimekuwa hakikubaliki. Wanawaza zaidi ni lini ibada itaisha.
Muda wa mahubiri umefupishwa. Yesu alikuwa anaeleza huzuni yake. Kwa ujumla,
ibada ni za kama saa moja tu. Hata hivyo, ibada nyingi zimekuwa chini ya saa
moja. Wana haraka ya kumaliza. Yesu angependa kujidhihirisha kwenye miili ya
wahubiri wake, lakini wachungaji wanahubiri kimwili na sio kiroho. Wanaangalia
zaidi muda kuliko kuhubiri katika Roho kwa muda kidogo wa kuabudu na wa ibada.
Wahubiri wengi wanatumia muda unaobaki kwa mambo binafsi, kwa mfano kwenda
kula, kusafiri na waumini, na kupoteza muda kwa mambo yasiyo na maana. Baadhi
ya wachungaji wanadanganyika kwa wadada warembo, na wanajali zaidi uzuri wao.
Zaidi ya
hapo, baadhi ya wachungaji hawawajali waumini kwa kiwango sawa. Waumini wenye
fedha wanaheshimiwa na kupewa muda zaidi kuliko wasio na fedha. Aina hii ya
wachungaji hawatumii muda wa kutosha kwa maombi kwa utukufu wa Mungu, bali
wanaomba kidogo tu, jambo ambalo linamkosesha raha Bwana wetu. Ujumbe
hauongozwi na Roho Mtakatifu. Ujumbe unatokana na nguvu ya uelewa wa mchungaji
na mwili wake. Ujumbe usiotokana na Roho Mtakatifu utaishia kwenye mahubiri
mafupi yasiyo na nguvu. Wachungaji hawachagui kuongozwa na Roho Mtakatifu bali
na waumini. Yesu anatamani sana kuwaongoza wachungaji kwa uweza mkuu kwa ajili
ya utukufu wa Mungu. Lakini wachungaji wao wenyewe walishaacha kutafuta upako
wa Bwana. Sasa hivi akili zao za kimwili zinatawala roho zao. Wahubiri wengi
hawahisi tena moyo wala shauku ya Mungu. Mungu anahuzunika sana. Wakati wakipanua au
kujenga makanisa, baadhi ya wachungaji hufanya hivyo kwa ajili ya utukufu wao
wenyewe na kujikweza. Mioyoni mwao,
jengo ni mnara wa kumbukumbu yao. Aina hii ya wachungaji hutumia muda kidogo sana
kwa maombi na wanahangaika zaidi na mali na mambo ya kidunia.
Bwana
aliponiambia mambo haya, niliona uso wake ukionyesha huzuni. Japokuwa wahubiri
wengi wanaweza kujitapa kuhusiana na majengo mazuri, Mbingu zinaona mambo hayo
kuwa ni madogo sana. Njia za Mbingu ni za juu sana kuliko njia za dunia. Kitu
ambacho duniani kinaonekana ni kikubwa sana, Mbinguni kinaweza kuonekana kidogo
sana. Yesu aliniambia: "Si wachungaji wote ni waovu. Hata hivyo, wasio watii ni lazima
waadabishwe. Kama wasipotubu, nitawatupa jehanamu. Kule watateswa. Baada ya
muda mfupi nitakupeleka kule ukawaone baadhi yao ambao walishatangulia huko."
Baadaye siku
hiyo, nilihitaji msaada toka kwa Bwana ili kuelewa baadhi ya vitu. Baadhi ya
waumini, ambao walishakuwa Wakristo kwa miaka na miaka, waliniambia kuwa mtu
akifa, anaingia Mbinguni au kuzimu. Walisema kuwa mtu aliye hai hawezi
kutembelea Mbinguni wala kuzimu. Walisema ni upuuzi tu kuamini kitu kama hicho.
Walibeza mikutano yetu ya maombi na kuomba kwetu kwa muda mrefu. Pia walisema
kuwa Mchungaji Kim na kanisa lake wanaweza kuwa ni kikundi cha imani za
kishetani (cult). Kwa hiyo, niliomba,
"Tafadhali Bwana, vipi kama kanisa letu ni cult? Nini kitatokea kwa familia
yangu?" Bwana akasema, "‘Cult’ ni nini? Watu wanalaumiana na kuhukumiana kwa sababu ya tofauti
zao, madhehebu na mafundisho yao. Wanatenda dhambi. Hata hivyo, mimi
nafurahishwa na kanisa lenu. Wewe na waumini wa kanisani kwenu mnaomba bila
kukoma usiku kucha. Wale waliowatesa na kuwaita imani ya kishetani watajua kuwa
Mimi ni hai na ni Bwana. Mmepokea karama ya uponyaji wa wagonjwa na uwezo wa
kutoa pepo. Pia mnaishi kwa kumfuata Roho Mtakatifu." Yesu
akaendelea kusema, "Watu wanaohukumiana na kulaumiana watapata hukumu ya kutisha sana.
Usikubali wakupoteze. Ninaguswa sana na maombi yenu. Msiogope. Nitakulinda wewe
na kanisa lenu. Japokuwa ni shauku yangu kujidhihirisha kwa watu wangu wote na
kuwapatia karama za rohoni, lakini hawanitafuti. Wengi hawaombi sawasawa na
mapenzi yangu." Nikamwuliza, "Yesu, nini
kitatokea kwa kanisa?" Yesu akasema, "Mna bahati kujazwa na Roho Mtakatifu na kupokea
kipawa cha kunena kwa lugha haraka hivi. Moto mtakatifu utaenea na kupokewa na
kusanyiko lote."
Wakati wa
ibada ndefu, Mchungaji Kim alitoa mahubiri yenye nguvu kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu. Baadhi ya watu wanaweza kuwaza kuwa tutasinzia kwa kuwa ibada ni
ndefu. Hata hivyo, mahubiri, sifa, kuimba na kuabudu vinafanyika kwa moyo sana
kiasi kwamba tunakuwa tumejaa nguvu zinazotuwezesha kuendelea usiku kucha hadi
siku inayofuata. Siku moja, mchungaji wetu alihubiri kwa nguvu sana kiasi
kwamba uso wake uligeuka na kuwa mwekundu. Wakati wa mahubiri, niliona maono ya
kiti cha enzi cha utukufu cha Mungu. Mungu Baba alikuwa akimimina mafuta ya
upako. Ilionekana kuwa Roho Mtakatifu anampaka mafuta mchungaji kwa moto. Niliweza
kumwona Mungu Baba akimimina mfululizo moto na mafuta ya upako juu ya
mchungaji. Mahubiri yakawa na nguvu na ya kuvutia zaidi. Nilimwona Bwana Yesu
akicheka kwa furaha. Bwana alimwambia malaika mmoja arekodi kwa bidii matukio
ya ibada ile. Malaika aliitikia na kutii.
Nikamwuliza Yesu
juu ya kanisa liiloenea duniani kote, likiwa na matawi mengi, hata Korea. Wengine
husema kuwa idadi yao ni kubwa kwa sababu ya historia na utamaduni wao.
"Je, na wao ni waumini kama sisi?" nilimwuliza Yesu. Yesu akasema,
"Kama wananiamini
Mimi, basi wataokolewa. Lakini kanisa hilo linashusha hadhi ya Neno la Mungu
kwa kulishirikisha na dunia."
Tukiwa tunajadili
kanisa hili, katika maono, nilionyeshwa mfalme wa mapepo. Pepo hili ovu
lilionekana lina wasiwasi juu ya mipango yake kuhusiana hasa na kanisa hilo. Yesu
akasema, "Watu wa
Mungu wengi sana hawana ufahamu juu ya ibilisi na mapepo waovu. Watu wangu
wanaishi kwa uaminifu maisha yao bila kutafakari sana juu ya adui. Hata hivyo,
ibilisi atajaribu kuzuia kazi yenu. Iweni na ujasiri."
Baadaye,
wakati naomba pembeni ya mchungaji, pepo kubwa sana jekundu lilitokea. Jitu hilo
lilingilia mlango wa mbele. Lilionekana kuwa refu hadi mawinguni. Sura yake
ilijaa ghadhabu. Lilikuwa linachezeshachezesha pua yake. Joka lile liliongea, "Ninajaribu kuingia ndani ya mwili wako. Unawezaje kupingana
na mimi! Mimi ni mfalme wa kuzimu! Wote kule kuzimu wananitii mimi na kwa hofu.
Wewe ni nani hasa? Wewe si lolote si chochote! Huna haki ya kuweka wazi uwepo
wangu. Aha. Sasa najua wewe ni nani. Mmoja wa watumishi wangu ameshaniambia
wewe ni nani. Mwanzoni nilishamwagiza huyo mtumishi wangu awadanganye wengi na
kuwapeleka kuzimu. Lakini alirudi bila mafanikio. Nilipomwuliza kwa nini
alishindwa, alisema, ‘Mfalme wangu, inabidi uje mwenyewe uone kwa nini ni
vigumu. Nilidhani nitawashawishi kirahisi watu wajiue. Lakini maombi ya
Wakristo yana nguvu sana.’ ‘Ndio unasema nini?’ nilimkemea mtumishi wangu. Ilibidi
nije kuthibitisha maneno ya mtumishi wangu. Yalikuwa ya kweli. Karibu ilikuwa
haiwezekani kushindana na maombi haya."
Japokuwa
joka lile lilitutisha na kutukemea, tuko salama kwa sababu Yesu anatulinda. Joka
lile lilitoa lugha chafu, kisha likasema, "Nimeshazuiliwa."
Yesu akamjibu yule joka, "Unadhani uko wapi hapa? Usilete fujo na ghasia. Ukimgusa hata mtu mmoja
kwenye Kanisa la Bwana (The Lord's Church), utaadhibiwa, na Baba yangu
atakupiga." Joka lile lilijaa huzuni na ghafla likatoweka. Yesu
akasema, "Joka
lile kule kuzimu lilijaribu kuwadanganya ninyi kama mfalme wa mapepo. Hii ni
mara ya kwanza ya udhihirisho wa hilo joka. Mara zote limekuwa likituma walio
chini yake duniani kutekeleza maagizo yake. Ombeni kwa bidii na bila kukoma. Mara
zote iweni waangalifu na msiwe na hofu, maana Utatu Mtakatifu wa Mungu utawalinda."
Mchungaji Kim, Yong-Doo:
Ilikuwa ni
Jumanne, na nje barafu ilikuwa ikidondoka, huku halijoto ikiwa nyuzi 15 chini
ya sifuri. Licha ya hali ya hewa kuwa hivyo, washirika wetu wanne walitoka
kwenda kushuhudia. Lakini kabla ya kufanya hivyo, walikuwa wakijiandaa kwa
bidii kwa maombi na nguvu za Roho Mtakatifu. Na Bwana alikuwa akiwapa upako wa
moto mtakatifu. Hao wanne walijadiliana mchezo wa kutumia ili waweze kushuhudia
kwa mafaniko zaidi. Walijua kuwa malipo mazuri sana yanawangojea kwa kufanya
kazi ya Bwana bila kuchoka. Wote walirudi wamechelewa sana, na walikuwa
wamejawa na furaha. "Mchungaji, hatukujua kuwa kushuhudia ni jambo la
kuburudisha kiasi hiki," walisema.
Jina la BWANA YESU libarikiwe! James umetumika vema ktk kutenda kusudi la MUNGU, ubarikiwe. Umekuwa kimya ni kitambo kirefu sasa, tushirikishe ulipo.
ReplyDeleteTafadhali Ndugu James ,tunabarikiwa na post zako -Ongeza nyingine tafadhali
ReplyDelete