Huu
ni ushuhuda unaotokana na kitabu kinachojulikana kama Baptized by Blazing Fire,
Devine Expose of Heaven and Hell kilichoandikwa na Mchungaji Yong-Doo Kim wa
Korea. Ni ushuhuda mrefu ambao utakupa mafundisho, maonyo, utakutia moyo na
kukuimarisha katika safari yetu ya kuelekea kwa Baba, Mbinguni.
…………………………………………………………
KITABU CHA 1 – SEHEMU YA PILI
==== SIKU YA 6 ====
Baek, Bong-Nyo:
Saa 4 zilishapita
tangu mchungaji aanze mahubiri yake. Hakuna kati yetu ambaye hata alifunga
macho. Hata Meena mwenye miaka 5 naye alikuwa akisikiliza kwa makini.
Nilipokaza macho yangu kwa mchungaji, Yesu alitokea na kundi la malaika. Yesu
alikuwa akiongoza kondoo tisa. Nikagundua kuwa idadi ya kondoo ilifanana na
idadi ya mashujaa wa maombi waliokuwapo! Alisema, "Ninyi wote ni kondoo wangu.
Ninawachunga wakati wote, kwa hiyo msiogope."
Mahubiri ya
mchungaji Kim yalikuwa yanawaka, aliongea kwa moto wa Roho Mtakatifu. Yesu
alihusika sana kwenye mahubiri hayo ya mchungaji, na alipaza sauti akisema, "Safi sana Mchungaji Kim. Unafanya vizuri sana."
Yesu alikuwa akitembeatembea pembeni ya Mchungaji Kim, huku akitabasamu kila
wakati. Mchungaji akienda kushoto, Yesu naye anaenda kushoto; akienda kulia,
Yesu naye anaenda kulia. Kisha walitokea malaika kumi. Mmoja alisimama akiwa na
kitabu kilichofunguliwa huku akirekodi mambo fulani kwa haraka. Malaika wengine
walimzunguka mchungaji huku wakiwa na vyombo, wakikusanya mahubiri yale. Chombo
kimoja kikijaa, malaika mwingine anakuja na chombo kingine. Waliendelea hivi
huku wakiondoka na mahubiri yale hadi Mbinguni. Yesu alifurahia na malaika nao
walifurahia.
Baada ya
mahubiri, ulifika wakati wa kuomba kwa pamoja. Tukiwa tunaomba, washirika tisa
wa ile timu ya maombi walionekana kama wanapigana vita. Tukiwa tunamlilia Bwana
kwa toba, machozi na jasho vilikuwa vikitiririka.
Kisha Yesu
alinisogelea, huku akiniita jina langu. Bwana aliongea kwa kulinganisha
Makanisa kadhaa. "Bong-Nyo,
makanisa mengi yamelala huku misalaba yao myekundu ikiwa inawaka usiku, lakini
washirika wa Kanisa la Bwana wanaomba
kwa bidii. Nina furaha sana sasa." Kisha malaika walishuka wakiwa watatuwatatu. Moja, mbili, tatu,
nne, tano... Nilihesabu kwa muda lakini sikuona mwisho wa mstari wao, kwa hiyo
nikaacha kuhesabu. Waliendelea kushuka bila mwisho na kusimama mbele ya
madhabahu ambako sisi tisa tulikuwa tukiomba. Walikusanya maombi yetu kwenye
vyombo vya dhahabu na kwenda nayo Mbinguni na kurudi tena. Malaika hupelekea
maombi yetu kwa Mungu. Lakini hivi karibuni, wakati washirika wa Kanisa la
Bwana wakiabudu usiku kucha huku tukijitupa kwenye maombi, malaika
walitushukuru kwa kuwapatia kazi ya kutosha ya kufanya.
Yesu alisema,
"Kwa juhudi yenu
ya kumwita Bwana na kuabudu usiku na mchana, Baba wa Mbinguni, Mimi na Roho
Mtakatifu tumeshangazwa na kujitoa kwenu. Ni nadra kuona Kanisa kama lenu
duniani." Baba wa Mbinguni alituuliza sisi, "Je, niwape kitu gani?"
Kisha Baba alimwuliza Yesu, "Mwanangu, unafikiri nifanye nini?" Yesu akajibu, "Baba, fanya kama upendavyo Wewe." Roho Mtakatifu
alitupa upako wa moto mtakatifu, mafuta na vipawa vya Mbinguni. Baba
akasema, "Kwa mke
wa mchungaji, Kang, Hyun-Ja, yeye hasa nataka kumpa upako wa moto uwakao wa
Roho Mtakatifu na uwezo wa kuponya wagonjwa, na nataka aweze kucheza uchezaji
wa kiroho kwa ujasiri."
Mke wa
mchungaji alianza kucheza uchezaji wa kiroho, kila mmoja alitazama kwa heshima
kubwa. Uso wake ulianza kuwa mwekundu kadiri alivyocheza kwa uongozi wa Roho
Mtakatifu.
Ghafla Mungu
alinisukuma mahali ambapo palionekana kama vile niko ndani ya maji; na kana
kwamba mwili na miguu yangu vilikuwa vikienda kwa akili zake vyenyewe. Baadaye
kidogo nilisikia sauti ya Bwana ikisema,
"Nitawabatiza
kwa moto uwakao." Nilihisi kama vile nimetupwa kwenye mafuta,
na mwili wangu mara moja ulikuwa kama una moto.
Baadaye Yesu
alianza kuongelea kuhusu makanisa ya Korea. Kwa sauti yenye ghadhabu, alisema, "Kuna faida gani kwa kanisa kuwa
tu kubwa na tupu ndani huku likiwa na msalaba unaowaka? Niliwachagua viongozi
wa kichungaji ili kuokoa roho zilizopotea, lakini hawana maombi, na moyo Wangu
unaumia."
Baadaye,
nikawa nacheza uchezaji mtakatifu huku nikiomba kwa lugha pale Yesu
aliponishika mkono, huku akisema, "Bong-Nyo, twende Mbinguni." Mara
niliposhika mkono wa Yesu, nikajikuta nimevaa vazi jeupe, na nilikuwa napaa na
Yesu hewani. Nilipofika juu zaidi, dunia ikaendelea kuwa ndogo zaidi na zaidi.
Ulimwengu ulikuwa mzuri sana. Tulipaa kwa muda, kisha tukafika kwenye galaksi.
Tulipovuka galaksi, kukawa giza tena, nami niliona barabara mbili. Tulipita
kwenye barabara ya kulia. Kwa hiyo, nikauliza, "Bwana, hii barabara ya kushoto
inaelekea wapi?" Aliniambia kuwa ilikuwa inaenda hadi jehanamu.
Ilionekana kuwa tulikuwa kwenye barabara kwa muda mfupi, ndipo ulionekana
mwanga ghafla ambao ulikuwa mkali sana, kiasi kwamba sikuweza kufungua macho
yangu.
Mbingu
ilikuwa imejaa nyota. Duniani mara nyingi watu hutumia neno paradiso, lakini
kile nilichokiona hakiwezi kuelezwa kwa maneno ya kibinadamu. "Inawezekanaje?
Inawezekanaje?" niliuliza. Wanadamu hawawezi kuelewa kikamilifu vile
Mbingu ilivyo. Malaika wengi walinisalimia na kunikaribisha. Yesu akasema, "Umeamua na kujitoa mwenyewe
kuhudhuria kanisani kwa bidii, kwa hiyo nataka nikuonyeshe nyumba yako ya
Mbinguni. Twende nifuate.." Niliona malaika wengi wakijenga
kitu fulani. Yesu akaniambia, "Hii ni nyumba yako." Niliangalia lakini kulikuwa hakuna
nyumba! Niliona tu msingi mrefu. Malaika walikuwa wakitumia dhahabu kufanya
kazi yao. Yesu akasema, "Ndani ya siku chache, nyumba yako itainuka. Usikate tamaa, bali omba kwa
bidii na ishi kwa uaminifu. Ulimwabudu shetani na umewapeleka watu wengi kwenye
udanganyifu. Lakini ulifanya uamuzi wa kuniamini Mimi na kuhudhuria kanisani
kwa bidii." Yesu akasema, "Kuna mahali nataka nikuonyeshe,
kwa hiyo nifuate," na akanipeleka mahali pengine. "Mpendwa wangu Bong-Nyo, nitakuonyesha
stoo ya hazina na nyumba ya watu wanaohusika na kuwaletea Injili ninyi,
mchungaji wa kanisa lako, Kim, Yong-Doo, na mke wake, Kang, Hyun-Ja. Angalia
kwa makini. Nyumba ya ghorofa elfu moja duniani ni sawa na nyumba ya ghorofa
moja Mbinguni, na kila kitu Mbinguni hakiwezi kuelezewa kwa msamiati wa
kibinadamu maana haujitoshelezi."
Mbele ya
macho yangu kulikuwa na jumba kubwa sana sana, na nuru liliyokuwa likiitoa
ilikuwa kali sana kiasi kwamba sikuweza kuinua kichwa changu. "Hii ni nyumba ya Mchungaji Kim,
Yong-Doo," Yesu alisema. Yesu aliinua mkono wake na ghafla
niliweza kuona waziwazi nyumba mpya ya mchungaji kule Mbinguni. Kisha Bwana
akasema, "Sasa
hebu tuone stoo ya hazina ya Mchungaji Kim." Umbali toka
kwenye stoo ya hazina ulikuwa kama wa vituo vitatu hivi vya mabasi, kwa
kulinganisha. Stoo ya hazina ya mchungaji ilikuwa ina ulinzi mkali sana wa
mamia ya malaika, ili tusiweze kuingia. Yesu alipotokea, malaika walinzi
walishusha mabawa yao na kusimama wima na kuinamisha vichwa mbele zake. Kila
nyumba ya hazina Mbinguni ilihitaji ruhusa ya Yesu ili kuingia ndani. Rangi
zinazong’aa toka ndani yake zilikuwa zinashangaza sana. "Haa!
Mchungaji Kim atafurahi sana," nilisema. Ndani ya stoo ya hazina kulikuwa
na malaika wasio na idadi wakishughulika kukusanya vitu vya mchungaji kutoka
duniani. Hazina ya mchungaji inaendelea kuongezeka. Nikamwuliza Yesu, "Kwa
nini nyumba ya Mchungaji Kim ni kubwa kiasi hiki, na kwa nini ana hazina nyingi
namna hii?" Bwana akanijibu, "Mchungaji Kim, Yong-Doo alianza kazi yake ya
uaminifu mapema, na kila wakati amekuwa akiniomba na kunitumikia kwa bidii."
Hatimaye Yesu akasema, "Kwa leo hayo yanatosha. Tutaona mengi zaidi wakati mwingine utakapokuwa
hapa." Akanirudisha kanisani. Yesu alisema jambo moja la mwisho
kabla hajaniacha: "Nilipokufa
msalabani, wengi waliamini kuwa sitaishi tena. Hao waliacha kuniamini; wakaacha
kwenda kanisani, na sasa wanafanya mambo mengine ya kidunia."
==== SIKU YA 7 ====
Kim, Joo-Eun:
Niliomba kwa
lugha kwa takribani saa moja, ndipo ghafla mwanga mkali uliangaza. Kisha Yesu,
akiwa amevaa vazi jeupe alitokea mbele yangu. Alikuwa na nywele za kahawia na
alikuwa amevaa vazi kama mgolole jeupe linalometameta. Aliniita kwa jina. "Joo-Eun, mpendwa wangu Joo-Eun, nakupenda."
Yesu alinisogelea na akawa anaongea nami. Nilishangaa na kusema, "Hivi
wewe kweli ni Yesu? Haa! Hakika nakupenda. Wewe ni mwema sana." Nilijawa
na msisimuko kwa sababu sikujua cha kufanya. Yesu alikaa mbele yangu huku
akisema kuwa ananipenda. Nilisema kwa msisimuko, "Yesu, hakika
nakupenda," naye akajibu, "Ndiyo, nakupenda nawe pia sana." Yesu
akaniambia, "Omba
kwa bidii, nami nitajionyesha kwako. Nitakupeleka Mbinguni na kukuonyesha jinsi
kulivyo. Kwa hiyo, omba kwa bidii,"; baada ya hapo akatoweka.
Nilipoona
haonekani, nilianza kwa kuomba kwa lugha kwa nguvu zangu zote. Ghafla, mbele
yangu kulitokea kitu cha ajabu. Kilikuwa kinakimbia kunijia. Kona zote za macho
yake zilikuwa kama zimechanika, na jicho la kulia lilikuwa na sura ya X.
shetani hili lilikuwa limejaa makovu. Nikapaza sauti, "Kwa Jina la
Yesu, ondoka kwangu!" Lile shetani likapotea. Nikaendelea kuomba,
ndipo kitu chenye macho membamba kuliko ya paka kilitokea mbele yangu. Kilikuwa
na mabawa kama ya popo, na meno makali yaliyotokeza nje. Kilikimbia kuja kwangu
ili kunitisha, lakini nilikishinda kwa Jina la Yesu.
Hatimaye pepo
lenye sura isiyo ngeni lilitokea, na nikawa najiuliza niliiona wapi. Niligundua kuwa nililiona
kwenye michezo ya kompyuta (computer
game Starcraft). Pepo
hili la kike lilinikimbilia. Lilijaribu kunitisha kwa kunikodolea macho.
Tofauti na mapepo mengine maovu ambayo yalikimbia mara nilipoita Jina la Yesu,
hili halikuondoka kirahisi. Hata baada ya kutaja Jina la Yesu mara kadhaa,
halikushtuka, na nikaanza kuingiwa na hofu. Nilikimbia kwa Mchungaji Kim
pembeni ya madhabahu na kuendelea kuomba. Mchungaji alishika mkono wangu na
kuuinua, akaanza kuomba na mimi. Hapo ndipo pepo lile lilipoondoka.
ITAENDELEA ….
No comments:
Post a Comment