==== SIKU YA 24 ====
Kim Joseph: (2 Timotheo 3:1-5)
Wakati
nikiomba kwa kunena kwa lugha, ghafla nilianza kulia machozi ya toba. Nilikuwa
nimeshangoja kwa muda mrefu ili kuihisi hasa kwa machozi toba yangu. Mwili
wangu ulishakuwa moto. Kwa hiyo, pepo mchafu mwenye umbo la nyoka alipotokea,
nilimkamata na kumzungusha hewani.
Lee Yoo
Kyung:
Nilipokuwa
naomba kwa bidii, pepo ovu baya sana lilitokea huku likipaa juu yangu. Liliruka
mbele yangu kwa mbawa zake kama za popo. Lilikuwa na macho kama ya chura, pua
nyekundu na ulimi mrefu. Nilikerwa na jinsi lilivyokuwa likinitolea sauti kama
ya nyoka. Kwa hiyo, nililikamata na kuchana mabawa yake na nikalitupa hewani.
Damu nyekundu ilivuja kutoka kwenye sehemu zake zilizojeruhiwa.
Wakati
huohuo, joka baya jeusi lilinijia. Mimi naogopa sana nyoka. Ni viumbe ambao ni wa
kuchukiza mno. Aliponikaribia, sikuwa na uwezo wa kufanya chochote zaidi
ya kupiga kele, “Bwana! Naogopa! Kuna joka hapa!” Mara moja Yesu
alitokea, akalikamata na kulitupa mbali.
Bwana
akauliza, “Yoo Kyung, uko vizuri? Usiogope!
Hebu twende tukatembelee Mbinguni.” Nilimshika mkono na
tukaondoka kwenda Mbinguni. Yesu aliniambia niimbe wimbo wa sifa wakati tukipaa
kupita galaksi. Tuliimba, ‘Sifu ee! Moyo wangu!’ mara kadhaa. Baada
ya kutembelea mbinguni, tulirudi kwenye Kanisa la Bwana na nikaendelea kuomba.
Yesu
akaenda karibu na Mchungaji Kim na akasikiliza kwa makini akiomba. Yesu
alisikiliza kwa muda mrefu na akamgusa eneo ambalo mchungaji alikuwa na
maumivu. Maumivu yalikuwa kwenye mgongo wake ambako pepo ovu lilimng’ata. Yesu
akamkaribia Joseph na kusema kwa sauti, “Tubu
zaidi! Zaidi, zaidi, zaidi! Omboleza! Ni pale tu utakapolia ndipo mlango wa
Mbinguni utafunguka!” Joseph aliomboleza sana leo. Alikuwa
anabubujika machozi ya toba.
Yesu
alirudi kwangu na baadhi ya malaika walitokea. Bwana akasema kwa ujasiri, “Yoo Kyung, usiugue; kila wakati uwe na afya. Changamka!” Malaika
nao hata wakapiga kelele, “Mtakatifu Yoo Kyung! Usiugue!” Bwana akasema,
“Changamka!” Kisha tukaagana.
Lee
Haak Sung: *Tabaka la ulinzi lililofanywa na malaika
Wakati
ninaomba, malaika wengi walikuja kupitia mlangoni. Malaika wale walinizunguka,
huku wakifanyika tabaka la ulinzi. Niliwauliza malaika kile walichokuwa
wakikifanya. Wakaniambia kuwa walikuwa wakinizunguka kwa tabaka la ulinzi.
Malaika waliponizunguka kwa tabaka la ulinzi, moto mtakatifu uwakao
ulinichemsha. Nikaona pepo ovu likiwa limesimama nje ya tabaka la ulinzi. Pepo
lile ovu lilikuwa limeshikilia kisu na likanikumbusha kuhusu Chucky toka kwenye
sinema za kutisha. Lilimkaribia mmoja wa malaika na kumchoma, lakini mara
moja kisu kiliyeyuka na mkono wake ukawaka moto. Niliona pepo jingine ovu
lilija. Lilionekana kama mti uliozeeka sana. Wakati lilipokuwa likinijia
taratibu, lilitoa mikono yake na kugusa tabaka la ulinzi. Liliwaka moto na mti
wote ukawa unateketea. Mti ule ulipiga kelele huku ukikimbia.
Malaika
walikuwa wakiweka pia tabaka la ulinzi kumzunguka shemasi Shin, ambaye alikuwa
anaomba. Malaika walikuwa takribani 200. Wote walikuwa wanafanya kazi kuweka
tabaka la ulinzi kwa washirika wa kanisa. Niliona pepo ovu lililofanana na ‘buff
man’ nje tu ya tabaka la ulinzi. Lilikuwa linanijia mimi. Pepo hilo ovu
lilijaribu kupenya tabaka la ulinzi, lakini tabaka likawa la moto mno kama moto
uwakao. Likakata tamaa ya kuingia. Kisha pepo hilo likamwendea shemasi Shin.
Bahati nzuri, alikuwa amefunikwa kwa tabaka la ulinzi na moto. Lilishindwa
kupenya kwenye matabaka yake. Pepo hilo likaruka kuelekea kwa mama yangu.
Lilipomkaribia mama yangu, liliwaka moto na kutoweka.
Ghafla,
mwanga mkubwa unaong’aa ulimulika kutokea Mbinguni. Niliona malaika mkubwa
mrefu akija kuelekea kanisani huku amepanda farasi mweupe. Ilikuwa ni hali ya
kustaajabisha sana. Moyo wangu ulikuwa unadunda kwa kasi. Malaika alikuja kwangu na kujitambulisha, “Habari,
Mimi ni Malaika Mkuu Mikaeli.” Malaika
mwingine anayeng’aa alikuwa anafuata nyuma ya Mikaeli, aliyeitwa Malaika Mkuu
Gabrieli. Gabrieli alishikilia bendera kubwa iliyofungwa kwenye mti wake.
Walinieleza kuwa Malaika mkuu Mikaeli anapoyashinda mapepo, Malaika Mkuu
Gabrieli anaiyumbisha bendera ya ushindi upande hadi upande nyuma ya Mikaeli.
Malaika
wakuu Mikaeli na Gabrieli walikuwa na urefu karibu sawa. Walisimama kimya
wakimwangalia mchungaji akiomba. Nilipotazama jambo hili la kushangaza,
niliduwaa kabisa. Ilikuwa vigumu kwangu kutofautisha kama nilikuwa naota au
nilikuwa naona jambo halisi.
Kim
Joo Eun:
* Mapepo mengi yalikuwa yanakuja mbio kwa
makundi lakini imani yetu iliongezeka
Mara ya mwisho nilipoomba, pepo ovu
lenye jicho moja na umbo la nusu mwezi lilitokea, likiwa linabiringika kuja
kwangu. Pepo lile liliponikaribia, nililichoma jichoni na kuling’oa jicho hilo.
Nilizungusha kidole changu ndani ya shimo la jicho. Pepo lililipuka huku damu
ikisambaa kote nilipolishambulia. Baada ya muda mfupi, pepo ovu lililojifanya
msichana mdogo lilitokea huku likijizungusha kwa kichwa chake kama pia.
Nilikamata baadhi ya nywele zake, nikalitikisa, nikalizungusha mara kadhaa, na
kulitupa mbali. Yesu alinijia na kunipongeza kwa kitendo changu, akisema, “Madoa (Freckles), kazi nzuri!”
Yesu akaendelea kusema, “Madoa, unaonekana mrembo sana leo! Nani amekusuka nywele
zako?” Nikajibu, “Ni shemasi Shin!” Bwana akapongeza, “Kweli eh? Amefanya kazi nzuri sana!” Kwa
kuwa shemasi Shin alikuwa bado hajaamshwa kiroho, hakujua kuwa Yesu alikuja
karibu yake. Malaika wengi walimsindikiza Yesu. Mara nyingi huwa nawaona
malaika wakimsindikiza Yesu lakini safari hii walikuwa wengi zaidi. Miongoni
mwa malaika, baadhi yao walikaa wawiliwawili na kukaa karibu na washirika wa
kanisa waliokuwa wakiomba. Malaika wale walitumia mikono yao kufunga vyombo vya
dhahabu vilivyokuwa na midomo mipana juu na kwa bidii walivijaza kwa maombi ya
watakatifu.
Kwa
mara nyingine tena, kundi la mapepo wachafu lilitokea kwenye kona ya chumba na
kuja kuelekea kwangu. Waliponikaribia, Dada Yoo Kyung aliyakamata,
akayazungusha juu, na kuyatupa mbali. Kaka
Haak Sung na Kaka Joseph nao pia walikuwa wakipambana na mapepo wachafu.
Waliyakamata mapepo machafu, wakayazungusha juu na kuyatupa kule. Sote
tulirudiarudia mbinu hii mara nyingi.
Niliweza
kusikia sauti za mapepo wachafu yakijibamiza yanapoanguka ukutani au chini.
Kulikuwa na kelele sana. Karibu na mwisho wa kipindi chetu cha maombi,
tuligundua kuwa kulikuwa na mashambulizi mengi mbalimbali kwetu. Hata hivyo,
kila shambulizi lilisababisha imani yetu kuwa na nguvu zaidi na zaidi.
Dada
Baek Bong Nyu:
* Mchungaji Kim alisababisha Yesu acheke
Nimeshashuhudia
na kuona mambo mengi ya rohoni. Kwa upendeleo huu, pia nimevumilia maumivu
mengi. Yesu alinishangaza kwa kunipeleka kwenye bustani ya maua Mbinguni.
Aliniruhusu kuwa na muda wa kurejezwa upya kwa kujiburudisha kwenye bustani
ile. Niliweza kutumia muda mwingi kwenye bustani ile kadiri nilivyopenda.
Kwenye bustani, nilijibiringisha, niliruka na kucheza na malaika kama mtoto.
Bustani ya maua ya mbinguni ni kubwa na nzuri kwa namna ambavyo ni vigumu hata
kufikiria. Harufu nzuri ya maua ilikuwa ya thamani sana. Nisingekubali hata
kupewa dunia yote. Kwa kuwa mwili wangu ulikuwa dhaifu na umechoka, nilipumzika
na kujilaza baada ya kuwa nimesharudi kwenye Kanisa la Bwana. Wakati wa ibada
ya asubuhi, mchungaji alipokuwa akihubiri, alitembea toka upande mmoja hadi
mwingine, huku akifuatwa kwa karibu na Yesu.
Mchungaji
wetu ana vichekesho sana kiasi kwamba ninapomfikiria, natabasamu na kucheka
papo hapo. Kwa udadisi tu, nilimwuliza mchungaji swali, “Mchungaji,
hivi wewe ulikuwa na vichekesho hivi hata kabla sijajiunga na kanisa hili?” Mchungaji
akajibu, “Kanisa letu si la zamani sana. Hakuna jambo ambalo naweza
kukumbuka ambalo linaweza kuwa la kuchekesha. Sikumbuki jambo lolote ambalo
limekuwa la kuchekesha wakati wa kusanyiko letu hili la maombi. Mara zote
nilikuwa nimevunjika moyo. Nilijisikia mzito na wa kutia huruma.” Nikauliza, “Kwa nini basi umebadilika
kiasi hicho?” Mchungaji akasema, “Hata sijui kwa kweli. Nimebadilika
wakati wa maombi haya! Sijui hasa ni nini kinaendelea. Ukiniuliza kwa vipi
nimekuwa hivi na ni nani au nini kimenikuta, itanibidi niseme tu ni Bwana ndio
ameumba mazingira ya furaha.”
Mchungaji wetu ana kipaji cha kuigiza
aina zote za watu. Kimsingi, si watu tu; anaweza kuigiza vitu vya aina zote,
ikiwa ni pamoja na wanyama na vitu visivyo na uhai. Yesu alikuwa anamuigiza
mchungaji huku akicheka kwa nguvu. Wakati wa ibada, malaika wawili walikuwa
wakirekodi kila neno ambalo mchungaji alikuwa akisema. Hata hivyo, mara kadhaa
walikuwa wakichungulia kuona mchungaji anavyotumia ishara mbalimbali. Malaika
walikuwa wakicheka kwa nguvu kiasi kwamba walikuwa wanapitwa na maneno ya
mchungaji. Malaika walipopitwa na maneno ya mchungaji, Yesu aliwakemea. “Msimwangalie mchungaji; nyie andikeni tu kwa bidii!”
Yesu
anapotabasamu au kucheka, malaika wote huungana naye katika wakati huo wa
furaha. Hata hivyo, Yesu akihuzunika, malaika wanabaki kimya. Katikati ya
ibada, mchungaji aliniuliza swali, “Dada, Yesu yuko wapi hivi sasa?”
Nikasema, “Amesimama hapohapo nyuma yako.” Mchungaji akakenua na kusema,
“Oh, nifanyeje sasa? Nilijamba na kulinuka vibaya sana. Ingekuwa vigumu kwa
mtu yeyote kuvumilia. Namhurumia Bwana kama yuko nyuma yangu, ambako atanusa
gesi yangu. Nifanyeje sasa?”
Bwana
akaongea huku akicheka, “Haina uhusiano
wowote kwa kuw amimi ni roho. Ni sawa tu.” Akashikashika kichwa
na mgongo wa mchungaji.
Mchungaji Kim Yong Doo:
Washirika
wa kanisa walishamaliza nguvu zao za kimwili karibu zote wakati wakati wa
maombi. Badala ya kuacha, waliendelea kwa bidii kuomba kwa kujitoa kabisa huku
wameuma meno yao. Bwana alipoona tunaomba kwa kujitoa kiasi hicho, alifurahi.
Mimi nilikuwa katika maumivu yasiyovumilika. Maumivu yalisababishwa na
mashambulizi ya mara kadhaa ya mapepo wachafu. Aina hii ya majeraha inapona
polepole sana. Maumivu yasiyokoma yalinitesa sana. Ikawa vigumu mimi kuomba kwa
muda mrefu nikiwa nimeinua mikono yangu. Hata hivyo, katikati ya hayo maumivu,
Roho Mtakatifu alisogeza mikono yangu kwa namna mbalimbali. Mijongeo ya mikono
yangu iliendeshwa vizuri sana.
Mikono
yangu yote ilisogea kwa uthabiti. Iliachiana zamu. Ghafla, mikono yangu ilianza
kutetemeka kwa fujo. Nilikuwa na joto kali sana vilevile. Nilimwona Yesu akiwa
amevaa joho jeupe akitembea toka upande hadi upande mbele yangu. Uso wangu
ulihisi upepo wa vuguvugu wa kipindi cha joto. Nilihisi uwepo wake kwa nguvu.
Cha kusikitisha ni kuwa, macho yangu ya rohoni yalikuwa bado hayajafunguka.
Inaonekana kana kwamba Bwana anaangalia hali zetu na mwitikio wetu. Alikuwa
akitutathmini.
Shalom ndugu,
ReplyDeleteUmekaa kimya sana, tafadhali update kubatizwa kwa moto uwakao sehemu zinazofuata,Bwana akutie nguvu.
Ni kweli ndugu nimekaa kimya muda mrefu sana. Mungu mwingi nimekuwa facebook. Amina Bwana anisaidie niendeleze.
ReplyDeleteFacebook unatumia jina gani, je unajua usipomuamini nabii kacou philippe utaenda jehanamu baada ya kifo chako kama hujui najulisha hapa download app ya nabii Kacou kwa masomo zaidi kwa kiswahili nabiikacouphilippe.blogspot.com
Deletetapeli mkubwa wewe
DeleteKazi nzuri ndugu ninafrahia sana
ReplyDeleteKiongozi mbona umeitelekeza blog?
ReplyDelete