Bwana Yesu alisema: Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii,
la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu
na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote
yatimie. (Mt. 5:17-18).
Baadhi ya watu hudhani kuwa maneno haya yanamaanisha kwamba hakuja kubadili yale yaliyokuwako zamani; yaani kwamba yale
ya zamani bado yanatakiwa kutendeka kama ilivyokuwa katika nyakati za zamani.
Lakini maana hasa ya maneno haya ya Bwana Yesu ni nini?
Ulimwengu huu unaenda kwa ratiba. Inaeleweka kwamba, katika uumbaji wote wa
Mungu, macho ya Mungu yameelekea zaidi kwa kiumbe huyu, mwanadamu!
Imeandikwa kwamba: Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata
umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji ya utukufu na
heshima; umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; umevitia vitu vyote chini ya
miguu yake. (Zab. 8:4-6).
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, hiyo ratiba ya Mungu inahusiana zaidi na
mwanadamu. Ndiyo maana hata ardhi inalaaniwa au kubarikiwa kulingana na
mwenendo wa mwanadamu.
Tunaweza kuigawa ratiba hiyo ya uumbaji katika hatua nne, yaani:
- Kwanza ilianza kwa mwanadamu kuumbwa katika utakatifu na ukamilifu. Imeandikwa: Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. (Mwa. 1:31). Hii inaonyesha kuwa mwanadamu naye alikuwa ni mwema, mtakatifu na mkamilifu kabisa.
- Lilifuata anguko la mwanadamu kutokana kuasi sheria ya Mungu na kuingia kwa dhambi na laana ulimwenguni. Kwa mfano, Mungu anamwambia Adamu: Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako... (Mwa. 3:17).
- Kisha ulikuja ukombozi kwa njia ya mauti ya Yesu Kristo. Imeandikwa: Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (Yoh. 3:16).
- Hatimaye, kitafuata kipindi cha kumilikishwa mambo yote katika nchi na mbingu mpya. Maana maandiko yanasema: Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hamjaona vitu vyote kutiwa chini yake, ila twamona yeye Aliyemfanya mdogo punde kuliko kuliko malaika, yaani Yesu...(Ebr. 2:8-9).
Kutokana na anguko katika bustani ya Edeni, mwanadamu alitengwa mbali na
Mungu. Dhambi ni kitu kibaya sana mbele za Mungu aliye mtakatifu. Kwa sababu
hiyo, iliingizwa torati/sheria. ...ili kosa lile liwe kubwa sana... (Rum.
5:20). Maana maandiko yanasema kwamba: ... sheria haimhusu mtu wa haki, bali
waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi... (1 Tim. 1:9). Hii ni
kusema kwamba, sheria huja kwa sababu ya kuwapo kwa waasi.
Torati ina maagizo mengi ndani yake. Lakini yote yalikuwa na athari moja
kubwa: yalileta mauti kwa mwanadamu. Iweje tena torati ilete mauti? Paulo naye anauliza
swali hilihili: Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? (Rum.
7:13).
Mauti hii haikuja kwa sababu torati ni mbaya, hapana! Bali, mauti ilikuja
kutokana na udhaifu wetu wa kibinadamu.
Maandiko yanasema: Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya roho ni
uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana
haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. (Warumi 8:7).
Kupitia torati, Mungu alikuwa anamwambia mwanadamu, “Kwa kuwa umeniasi na
kusababisha dhambi kuingia ulimwenguni, [maana maandiko yanasema katika Warumi
5:12:...kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni.], basi ili uweze kuishi au
kutoka kwenye hali ya umauti, ni lazima utimize sheria (torati) YOTE! Maana imeandikwa:
Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja,
amekosa juu ya yote. (Yak. 2:10).
Hata hivyo, kama tulivyoona hapo juu, tatizo likawa kwamba, hakuna hata
mwanadamu mmoja anayeweza kutimiza matakwa YOTE ya torati. Maana: Wote
wamepotoka, wameoza wote pia; hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. (Rum. 3:12).
Mungu si kigeugeu hata siku moja. Akisema jambo, amesema. Alishasema kwamba
matokeo ya dhambi ni mauti – basi! Mbele zake hakukuwa na uwezekano hata kidogo
wa kuja tena kusema kinyume, labda: “Kwa kuwa mwanadamu ameshindwa kitimiza
torati, basi nitamsamehe tu.” Hapana!
Neno la Mungu linaeleza msimamo wa Mungu juu ya dhambi yoyote ile. Imeandikwa:
... wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe. (Nah. 1:3).
Ilikuwa ni lazima madai au masharti YOTE ya torati yatimizwe. Na hapo ndipo
anapoingia Bwana Yesu na haya maneno yake: Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua
torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin,
nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya
torati haitaondoka, hata yote yatimie. (Mt. 5:17-18).
Kulingana na kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI, neno ‘tangua’ maana yake
ni vunja kanuni au maafikiano; batilisha.
Anachomaanisha Bwana Yesu hapa ni kwamba: Sikuja kubatilisha hata nukta
moja ya torati; yote ni lazima itimizwe kama inavyotakiwa, maana uasi
ulishafanyika kwa hiyo hukumu inayotolewa na torati ni lazima itimizwe
kikamilifu! Kwa sababu dhambi imeshaingia ulimwenguni, na torati inasema kwamba
mshahara wa dhambi ni mauti, basi ni LAZIMA hilo litimizwe. Si hivyo tu, lakini
pia na madai mengine yote mahsusi kwa dhambi mahsusi nayo ni lazima yatimizwe.
Si rahisi kutaja madai na hukumu zote za torati katika makala haya mafupi,
lakini inaeleweka kwamba dhambi ilipoingia ulimwenguni ilifungulia mlango wa
kila jambo baya kutoka kuzimu. Mambo hayo ni pamoja na magonjwa, umaskini,
chuki, dharau, uasi, hasira, n.k. Ha haya yote mwisho wake ulikuwa ni mauti.
Kimsingi sisi wanadamu ndio tuliotakiwa kulipa kila hukumu ambayo torati
inaitamka juu ya kila anayetenda dhambi. Lakini Mungu kwa huruma zake akamtuma
Mwanawe Yesu Kristo ili aje alipe hukumu hizo.
Hebu tuangalie vitu vichache vilivyoingia ulimwenguni kutokana na uasi na
jinsi ambavyo Bwana Yesu alitimiza madai ya torati ili kurejesha kile
kilichokuwa kimepotea:
- Huzuni
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu. (Isa. 53:4).
- Amani
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake. (Isa. 53:5).
- Magonjwa
... kwa kupigwa kwake sisi tumepona. (Isa. 53:5).
- Umaskini
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa
ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa
umaskini wake. (2 Kor. 8:9).
- Dhambi
Lakini BWANA aliridhika kumchubua;
amemhuzunisha; utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi. (Isa. 53:10). Tazama,
Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu. (Yoh. 1:29).
- Mauti
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa
milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Rum. 6:23).
Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, kutokana na ukweli kwamba
Bwana Yesu alitimiza sheria yote, ndio maana sisi leo tunapokea wokovu kwa njia
ya imani na si kwa kujaribu kutekeleza masharti ya torati.
Imeandikwa kwamba: Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo
mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. Na
ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu, .... aliwafanya hai pamoja
naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena,
akaigongomea msalabani. (Kol. 2:12-15). Haleluya kwa Bwana!
Ni kweli maandiko yanasema kuwa imani pasipo matendo imekufa, lakini
hatutendi matendo mema kwa lengo la kupata wokovu. Wokovu wetu tunapokea bure
kwa kuamini kazi aliyofanya Bwana Yesu ya kulipa deni na hukumu nzima ya
torati. Kisha baada ya hapo ndipo tunaanza kutenda matendo mema ili kuonyesha
utii kwa Mwokozi wetu na pia kufaidiana sisi kwa sisi wanadamu.
Ashukuriwe Mungu wetu ambaye alitimiza masharti yote ya torati nasi
hatudaiwi tena. Tunapokea wokovu kwa imani. Si tena kama zamani ambapo torati
iliagiza kwamba: ...mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu
akizitumia ataishi kwa hizo. (Law. 18:5) – jambo ambalo, kutokana na udhaifu wa
mwili, HALIWEZEKANI!
Asante kwa somo hili.
ReplyDeleteAsante pia kwa kusoma somo hili. Mungu akubariki.
ReplyDeleteKaribuni Kwa Kristo [waadventista wasabato]
ReplyDeleteKaribuni Kwa Kristo [waadventista wasabato]
ReplyDeleteAsante kwa neno lenye uzima, MUNGU akubariki na akupe nguvu na maarifa ili uzidi kuyachambua maandiko.
ReplyDeleteha ha ha mungu anakuona ..biblia imesema hakuja kutangua torati sasa wew ingiza maneno yako wakati biblia imesema ole atakae ongeza ata neno katika maneno ya mungu... jiandae cha kujibu mbele za mungu.. ujizaniae umesimama angalia usianguke lakin pia angalia umesimama wapi maana unaweza ukawa umesimama pabaya.
ReplyDeleteUmenena vyema mtumishi.
ReplyDeleteUbarikiwe mtumishi, nikuelewa vizuri nimejifunza kitu hapo
ReplyDeleteEh natambua sasa uko juu kwa uchambuzi wako
ReplyDeleteBarikiwa Jonas Sume
DeleteNaomba kuuliza mtumishi, pale yesu aliposema" anipendae mmi atazishika amri zangu" Naomba kufaham ni amri zipi
ReplyDeleteAsante kwa uchambuzi mzuri
ReplyDelete