Thursday, April 17, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 4Sura ya 3: Utawala mwovu


Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. (Yohana 10:10) 


Baada ya kurudi Lagos, niliendelea na biashara; na baada ya wiki mbili nilirudi tena baharini. Malkia wa Pwani alinipatia kile aambacho alikiita ni “kazi ya kwanza”. Nilitakiwa kwenda kwenye kijiji changu na kumwua mjomba wangu, ambaye alikuwa ni mganga maarufu wa kienyeji, na ambaye huyu malkia  aliniambia kuwa ndiye aliyehusika kuwaua wazazi wangu.

Saturday, April 12, 2014

Mbinguni, peponi, kuzimu na jehanamu
Mpendwa mmoja aliniuliza maswali yafuatayo ambayo nimeona ni muhimu niyajibu kama Makala fupi kwa ajili hata ya faida ya watu wengine wenye maswali kama haya:


Swali la 1: Hivi watu wakifa, roho zao zinakuwa wapi hasa?
Swali la 2: Roho hizo zinakuwa katika hali gani hasa?

Sunday, April 6, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ay 3
Agano Langu na Alice
Mapema asubuhi moja, Alice aliniambia kuwa kulikuwa na sherehe ya muhimu iliyotakiwa kufanywa kwenye nyumba yake. Saa 8 usiku alileta mtoto mchanga wa kike anayetambaa, akiwa hai. Mbele ya macho yangu, Alice alitumia vidole vyake kunyofoa macho ya mtoto yule! Kilio cha mtoto huyo kiliniumiza sana! Kisha alimkatakata vipande na kumimina damu pamoja na nyama kwenye sinia na kuniambia nile. Nilikataa! Alinitazama moja kwa moja usoni na kile kilichotokea machoni mwake siwezi kukielezea kwa kuandika. Kabla sijajua nini kinaendela, nilijikuta si tu natafuna zile nyama, bali pia nilikuwa nalamba damu. Wakati haya yakiendelea alisema, “Hili ni agano kati yetu. Hautasema chochote kamwe utakachoona nikifanya au chochote kuhusiana na mimi kwa mwanadamu yeyote duniani. Siku utakayovunja agano hili, lako litatoweka.” Alimaanisha kuwa siku nitakayovunja agano hilo, nitauawa!

Monday, March 31, 2014

Niliokolewa Toka kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 2

Sura ya 2: Kuingizwa Kundini

Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti.” (Mithali 14:12).


Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka. Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu.” (Isaya 57:20-21).

Tuesday, March 25, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza – Sehemu ya 1

Emmanuel Eni alizaliwa nchini Naijeria. Alipitia mateso na dhiki nyingi chini ya vifungo vizito vya ibilisi. Katika ushuhuda huu, anatusimulia kile kilichotokea maishani mwake, mateso aliyopata na hatiamaye jinsi Bwana alivyompa ushindi.

Sunday, March 16, 2014

Mwanafunzi wa Mchawi - Sehemu ya 5


(Waebrania 11:35-40)


Hii ni sehemu ya mwisho ya ushuhuda wa Jim McCoy aliyekuwa mwanafunzi wa mwanamke mchawi kule Marekani, lakini akaokolewa na Bwana Yesu na kutolewa ndani ya vifungo vya mauti.

Monday, March 10, 2014

Mwanafunzi wa Mchawi - Sehemu ya 4


Kuhubiri Injili kwa kila kiumbe na kila mahali


Matibabu ya kisaikolojia (psychotherapy) ni aina nyingine ya mazoezi ambayo yanaonekana ni ya kisayansi kabisa, kama njia ya kuwasaidia watu. Watalamu wengi wa  ‘psychotherapy’ hutumia taaluma hii kuwasaidia watu sababu hasa ya majonzi yao (depression) au kubadili namna ya tabia au mazoea mabaya waliyo nayo. Lakini ni nini hasa kinachoendelea humo? Wanafungua milango ya ndani na kwa kufanya hivyo, wanafungua njia kwa kazi za mapepo. Hii ni pamoja na aina zote za mapumziko ya kisaikolojia (psychological relaxations).

Wednesday, February 26, 2014

Mwanafunzi wa mchawi - Sehemu ya 3
Katika Sehemu ya 1 na ya 2 tuliona jinsi ambavyo Jim McCoy aliingizwa kwenye vifungo vya kipepo na mwanamke mchawi (lakini kwa ridhaa ya McCoy mwenyewe); lakini akajikuta kwenye mateso mengi. Hatimaye Bwana Yesu alimhurumia na kumtoa kwenye vifungo hivyo.

Katika sehemu hii, McCoy anaendelea kueleza mbinu na hila zinazotumika leo duniani; ambazo shetani na maajenti wake wanafanya juhudi za kuzieneza kote duniani ili, sit u watu wanaomkataa Yesu, bali hata Wakristo waweze kunaswa katika mtego na kuishia jehanamu.

Friday, February 21, 2014

Mwanafunzi wa mchawi - Sehemu ya 2


Yale makucha yalijaribu kunizuia tena lakini yakashindwa. Kwa hiyo, niliikamata ile Biblia na kuiweka kifuani pangu. Biblia ilijifunua yenyewe! Nilitaka kuinyanyua hadi kwenye mwanga wa mshumaa ambao nilikuwa tayari nimeshauwasha. Lakini shetani aliuzima ule mshumaa. Kwa hiyo, sasa kulikuwa na giza kabisa kwenye chumba kile. Na hivyo, sikuweza kusoma chochote kutoka kwenye kitabu hicho na sikuona kilichokuwa kimeandikwa kwenye ukurasa ule ambako Biblia ilijifunua yenyewe kimiujiza. Kulikuwa na giza totoro.

Sunday, February 2, 2014

Mwanafunzi wa mchawi - Sehemu ya 1Jim McCoy alikuwa ni mwanafunzi wa mchawi mkubwa wa Kimarekani. Ufuatao ni ushuhuda wake ambao aliutoa kwenye mkutano kuhusiana na  
New Age, kule Jamhuri ya Cheki kwenye mwaka 1995, miaka michache baada ya kuanguka kwa ukomunisti.
  
Bwana alimwambia, “Nenda kawaambie na wengine kile ambacho nimekutendea wewe, ili kwamba waweze kuamini kuwa ninakuja tena hivi karibuni.”

Sunday, December 15, 2013

Asili hasa ya Uislamu ni nini?
Je, wewe ni Mkristo? Je, wewe ni Mwislamu? Sote tuko kwenye safari ya kuelekea mbinguni huku tukiamini kuwa njia ile tuliyomo ndiyo sahihi; na njia ile waliyomo walio kinyume nasi haiko sahihi.

Ukristo na Uislamu ni dini kubwa ambazo zinadai kuwa zinaabudu Mungu mmoja aliyeumba mbingu na nchi tofauti na dini zingine ambazo zinaabudu miungu mingi. Hata hivyo, zipo tofauti za msingi sana kati ya Uislamu na Ukristo ambazo KATU haziwezi kufanya pande hizi mbili ziwe zote sahihi. Kwa mfano:

Friday, December 13, 2013

Saa 8 mbinguni - Sehemu ya 2
Mchungaji Ricardo Cid


Ndugu msomaji wa blog hii, katika sehemu ya kwanza ya ushuhuda huu tuliona jinsi ambavyo Ricardo amechukuliwa na malaika wa Bwana kupelekwa mbinguni kukutana na Bwana Yesu. Walikuwa wamepita mbingu ya kwanza na wako kwenye mbingu ya pili. Wakati akiwa anaangalia shughuli mbalimbali za mapepo kwenye mbingu hiyo, kwa mbali aliona nyota yenye mwanga mkali ikiwajia pale. Je, hiyo ilikuwa ni nyota ya namna gani? Na je, nini kiliendelea baada ya hapo? Tafadhali karibu kwenye sehemu ya 2 na ya mwisho ya ushuhuda huu wenye ujumbe muhimu kwa Kanisa.

Wednesday, December 11, 2013

Saa 8 mbinguni - Sehemu ya 1

Mchungaji Ricardo CidMchungaji Ricardo alipata mafunuo mbalimbali kutoka kwa Bwana Yesu kuhusiana na hali ya kanisa, haja ya kuwa waombaji wenye bidii, haja ya kujiandaa kwa ujio wa Bwana, unyakuo na kadhalika. Karibu kwenye Sehemu ya 1 ya ushuhuda huu wenye nguvu ambao, kupitia humu, Bwana atasema na moyo wako na kukupatia msukumo mwingine wa kusonga mbele zaidi katika safari hii ya kiroho katika maisha haya ya kimwili.

Wednesday, December 4, 2013

Jiandae kwa kurudi kwa Bwana! Sehemu ya 2
Mpendwa msomaji wa blog hii na mwana wa Mungu aliye hai, hii ni Sehemu ya 2 ya ushuhuda huu. Katika Sehemu ya 1, tuliona safari ya kwanza mbinguni ya dada Bernarda. Katika sehemu hii, anatueleza kile kilichotokea pale Bwana Yesu alipomchukua kwa mara ya pili na kwenda naye mbinguni kisha akamrudisha.

Friday, November 29, 2013

Jiandae kwa Kurudi kwa Bwana! - Sehemu ya 1
Dada Barnarda Fernandez alichukuliwa katika Safari ya Mbinguni mara 2 na Bwana Yesu. Alionyeshwa thawabu za mbinguni zilizoandaliwa kwa ajili ya watakatifu wa Bwana, unyakuo, Karamu Kuu na taji za uzima. Pia aliona hali ya Kanisa, hukumu ijayo na roho zilizopotea zilizoko kuzimu. Ufuatao ndio ushuhuda wake:

Saturday, November 23, 2013

Wakristo walio kwenye giza la nje
Dada Liyan ni mwenyeji wa China. Bwana alisema naye kwa njia ya maono na hata kumpeleka mbinguni na kuzimu. Anayo mafunuo mengi ya muhimu sana ambayo tunayahitaji mno, hasa katika nyakati hizi za mwisho. Tafadhali fuatana naye katika ushuhuda huu muhimu na Bwana atasema na moyo wako kwa namna ya ajabu sana.

Sunday, November 17, 2013

Yesu - nitoe humu kuzimu!(Hii ni picha tu ya mtandaoni - si ya Linda)


Ndugu msomaji, wako watu wengi sana wanaopita kwenye lindi la huzuni ambazo zimesababishwa na aina ya maisha au familia walimojikuta kiasi kwamba inaonekana kama kila kitu kimekwama. Haijalishi tunapita kwenye hali ngumu kiasi gani. Wito wa Bwana wa mabwana, Yesu Kristo bado uko palepale: Njoni kwangu ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha (Mt 11:28). Bwana Yesu yuko kazini saa ishirini na nne. Karibu utiwe moyo na ushuhuda huu wa dada ambaye alishakata tamaa kabisa na kuamini kabisa kuwa tayari alikuwa kuzimu. Lakini Yesu anapoingia, kila kitu kinabadilika.

Sunday, September 29, 2013

Siri Inayohusu Moyo wa Mwanadamu - Sehemu ya 3
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu,
kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini,
na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia,
na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
(Mwanzo 1:26).


Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge,
na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru. (Luka 10:19).

‘Kutawala’ ni kuwa na mamlaka, amri au usemi wa mwisho juu ya jambo au hali. Hii ina maana kwamba chochote kilicho chini ya mamlaka hayo hakiwezi kufanya kilicho juu ya mamlaka hayo iwapo mamlaka yenyewe yamesimama sawasawa.

Monday, August 26, 2013

Kanisa Litanyakuliwa Wakati Wowote!
Yapo mambo mengi sana ambayo Wakristo tunapishana na kutofautiana katika mitazamo na tafsiri zake kuhusiana na Maandiko. Jambo mojawapo ni kuhusu unyakuo wa Kanisa. Baadhi ya watu husema kuwa  unyakuo utatokea kabla ya dhiki kuu; na wengine wanasema kuwa unyakuo utatokea baada ya dhiki kuu.

Saturday, August 17, 2013

Wachawi Wapigwa Kisha Waumbuliwa Waziwazi na Bwana Yesu! 
[Picha kutoka mtandaoni. Walioumbuliwa si hawa]

Mungu anatenda kazi. Kazi ya kueneza Injili ya Yesu Kristo si kazi nyepesi kwa sababu ushindani wake hautoki kwa wanadamu bali ni kutoka kwenye falme za giza zinazoongozwa na mapindikizi ya mapepo yanayoongoza majeshi kwa majeshi ya pepo wachafu.

Imeandikwa:
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. (Waefeso 6:12).

Sunday, August 4, 2013

Nilipokuwa Nje ya Mwili Wangu Nilimwona Mungu, na Wafu Walio Hai!

Huu ni ushuhuda wa mtumishi wa Mungu, Dr. Roger Mills, ambaye anaishi North Carolina kule Marekani. Hii ni sehemu tu ya ushuhuda huo ambao ameuandika kwenye kitabu. Lakini nimeona niulete viyo hivyo katika ufupi wake, maana naamini kuwa kuna mambo ya muhimu mengi ya kujifunza katika sehemu hii kwa ajili ya uzima wetu wa milele katika Kristo Yesu.

Tafadhali karibu uendelee kupokea kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kile ambacho alimfunulia mtumishi wake kwa ajili yangu na yako.

Friday, July 12, 2013

Ushuhuda wa Rodolfo Acevedo Juu ya Mbinguni, Kuzimu na Hali ya Kanisa la Leo

Ufuatao ni ushuhuda wa Mwinjilisti Rodolfo kutoka Jamuhuri ya Domonika, ambao Bwana alimwonyesha kuhusiana na kuzimu, mbinguni pamoja na mambo yanayoendelea katika Kanisa la siku za leo.


Utangulizi
Mimi ni Mwinjilisti Rodolfo Acevedo Hernandez kutoka Jamuhuri ya Dominika. Koo langu limeathirika kutokana na usimuliaji wa ushuhuda huu lakini bado nitafanya hivyo tena leo hata kama kuna upinzani. Utukufu ni kwa Mungu! Tupo hapa kuhubiri Neno la Bwana Yesu Kristo na ninaenda kutoa ushuhuda ambao ulibadili maisha yangu na maisha ya maelfu kwa maelfu ya watu wengine!!

Monday, June 3, 2013

Akef Tayem, Mwislamu Kutoka Palestina Akutana na Bwana Yesu na Kuokoka - Sehemu ya 2

Hii ni sehemu ya 2 ya ushuhuda wa Akef Tayem, Mwislamu wa kutoka Palestina ambaye alikutana na Bwana Yesu, kisha akawa Mkristo. Ili kupata picha kamili, tafadhali anza kusoma sehemu ya 1 HAPA.

…………………….


Baada ya Akef Tayem kukataliwa na familia yake kwa sababu amekubali kumpokea Yesu Kristo maishani mwake, alijikuta akikosa kabisa hamu ya kula kwa siku zaidi ya 40 akiwa porini. Mwili wake ulidhoofika sana na kuishiwa maji. Yafuatayo ni mahojiano kati ya mtangazaji, Sid Roth and Akef Tayem:

Saturday, May 11, 2013

Siri Inayohusu Moyo wa Mwanadamu - Sehemu ya 2
Mwanadamu alivyoumbwa

Tukisoma Biblia kuhusiana na uumbaji wa mwanadamu, imeandikwa hivi:

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo 2:7).

Kulingana na andiko hili, tunajifunza yafuatayo:
(a) Mwanadamu ana sehemu kuu mbili.
(b) Sehemu ya kwanza ni mavumbi, yaani mwili unaoonekana 
     kwa  nje na tunaweza kuugusa.
(c) Sehemu ya pili ni pumzi ya uhai ambayo iko ndani na hatuwezi
     kuiona wala kuigusa.
(d) Mavumbi pamoja na pumzi ya uhai yanaunda nafsi hai.

Thursday, May 9, 2013

Siri Inayohusu Moyo wa Mwanadamu – Sehemu ya 1
Mungu anasema mengi sana kuhusiana na moyo. Lakini moyo ni nini? Na umuhimu wa moyo ni nini katika maisha yetu ya kiroho na ya kimwili?

Hebu angalia maandiko machache yafuatayo na uone kile ambacho Bwana anasema kuhusiana na moyo.

Sunday, April 21, 2013

Yesu ni Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni

Yohana 19:1  Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi.

Yohana 19:2  Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau.

Yohana 19:3  Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi.

Yohana 19:4  Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake.

Mwanamke wa Kiislamu Aokoka Baada ya Yesu Kumjia Ndotoni

Katika kukua kwangu, mara zote nilimwona Mungu kama yuko mbali sana. Nilikuwa nikimuogopa sana. Na nilikuwa nikijaribu kumpendeza kwa matendo yangu yote, huku nikijitahidi kubakia safi kulingana na mafundisho niliyopokea, nikiwa kama mwislamu wa kishia.

Nilikuwa nikijitahidi kufanya zile swala 5 kwa siku, huku nikigeukia kwenye Ka’aba, Makka. Pamoja na matendo yangu haya mazuri, nilikuwa sina uhakika ni wapi nitakwenda baada ya maisha haya.

Na tena, kwa sababu ya vita na hali ilivyokuwa nchini, nikiwa nimezaliwa wakati wa mapinduzi na kuona vijana hawa wote waliouawa, nilianza kumhoji Mungu. “Hivi wewe kweli upo ilhali haya yote yanatokea?” Na mara zote mama yangu alikuwa akiniambia, “Nyamaza. Utakwenda motoni. Hutakiwi kumhoji Mungu!”

Je, Mtume Muhammad Yuko Wapi Hivi Leo?
Mungu hutufunulia mambo mbalimbali kupitia watumishi wake mbalimbali anaowachagua ili kutujulisha yale yaliyopo na hata yajayo; yaliyo katika ulimwengu huu na pia ule ujao. Wapo watu wengi ambao Mungu amewatumia kutufahamisha juu ya mbingu na hata juu ya kuzimu.


Bo Ra Choi ni mchungaji kutoka Korea ya Kusini. Mchungaji huyu amekuwa akionyeshwa maono mbalimbali na Mungu kuhusu mambo ya ulimwengu wa roho. Mojawapo ya maono aliyoonyeshwa yanamhusu Muhammad, mtume wa Uislamu.


Je, Muhammad yuko wapi hivi leo? Tafadhali bofya HAPA ili kupata jibu.

Tuesday, April 9, 2013

Kuna Nguvu Katika Mawazo Yetu – Sehemu ya 3
MPANGO WA MUNGU KUHUSU MAWAZO YETU

Bila mimi hamuwezi

Mawazo yetu ni muhimu sana kwa maisha yetu ya sasa na yale yajayo. Kwa hiyo, Mungu anayo mengi ya kusema kuyahusu. Ametuwekea utaratibu na mwongozo wa kuweza kuvuna baraka zake kwa kupitia kwenye mawazo yetu. Hata hivyo ni muhimu kukumbuka wakati wote kuwa msaada wetu unatoka kwa Bwana. (Zaburi 124:8). Pia Yeye anasema: “Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.” (Yohana 15:5).

Friday, April 5, 2013

Kuna Nguvu Katika Mawazo Yetu – Sehemu ya 2Mawazo ni kama sumaku

Sumaku ina nguvu za aina mbili - nguvu ya kuvuta vitu vije kwake na nguvu ya kusukuma vitu viende mbali nayo. Sumaku huvuta au kusukuma vitu vinavyofanana nayo, kwa mfano vipande vya chuma. Haiwezi kuvuta au kusukuma kipande cha mti, maana hakifanani nayo. Mawazo, hali kadhalika, huvuta au kusukuma mambo yanayofanana nayo. Hili ni jambo la kweli kabisa! Kwa mfano, kuna watu wengi ambao utawasikia wakisema, “Najisikia kama nataka kuumwa. Nadhani nitakuwa na malaria.”


Ukiwa na mawazo ya kuumwaumwa, mawazo hayo yatavuta magonjwa na udhaifu vije kwako. Iwapo una mawazo ya kuweza na kufanikiwa, vivyo hivyo, mawazo hayo ni lazima yatavuta mafanikio yaje kwako.

Injili ya BarnabaJe, umewahi kusikia juu ya ile inayoitwa Injili ya Barnaba? Hii ni injili ya namna gani?

Injili ya Barnaba ni kitabu kikubwa karibu sawa na Injili zote za kwenye Biblia zikichanganywa pamoja. Injili hii inapendwa na kusambazwa sana kwenye ulimwengu wa Kiislamu, wakidai kwamba ndiyo injili sahihi kabisa.

Injili hii inadai kwamba iliandikwa na mmojawapo wa mitume wa Yesu Kristo aliyeitwa Barnaba.

Thursday, April 4, 2013

Kuna Nguvu Katika Mawazo Yetu – Sehemu ya 1Je, mawazo yana athari au mchango katika uhusiano wetu na Mungu? Je, yanaweza kutumika kuboresha uhusiano huo?

Kila mmoja wetu huwa anawaza mambo mbalimbali kila wakati, maadamu tuko macho. Wakati mwingine huwa tunawaza kwa kuamua na wakati mwingine huonekana kana kwamba mawazo fulani yanavamia tu akili zetu; na kila tukijitahidi kuyaondoa inakuwa ni vigumu.

Thursday, March 28, 2013

Msamaha! Msamaha!
Kibinadamu ni vigumu na haiwezekani kufanya mambo ya kimungu. Upendo na msamaha ni jambo la kimungu. Lakini mwanadamu yumo ndani ya anguko; ndani ya dhambi. Je, anawezaje kutenda jambo la kimungu?


Bila shaka inahitajika nguvu tofauti na uwezo wetu wa kibinadamu. Sisi ni kama magari ambayo yanahitaji kupitia kituo cha mafuta ili kupewa nguvu ya kufanya safari ndefu. Kwa uwezo wake lenyewe gari haliwezi kufanya hivyo bila nguvu hiyo.

Wednesday, March 27, 2013

Dhambi Isikupeleke Kwenye Hatia Bali Kwenye Msamaha


Karen

Kama ilivyo kwa wanadamu wote, Karen naye alikuwa na dhambi yake imzingayo kwa upesi. Dhambi hiyo ilimfanya ajisikie hatia (ambalo si jambo baya), lakini sasa alijikuta akikwamia humohumo. Matokeo yake akawa na matatizo mawili, kwanza ni hiyo dhambi yenyewe; na pili ni hatia kutokana na dhambi hiyo.

Alijua kuwa Bwana Yesu ni lazima atakuwa ana hasira sana naye. Lakini kwa neema ya Bwana, Karen aliweza kumwona Bwana Yesu. Matarajio yake yote yalibadilika pale alipogundua kuwa, kumbe Bwana hakuja kuuhukumu ulimwengu bali kuuokoa. 

Si tu kwamba dhambi yake iliisha, bali na hatia nayo. Hivi sasa Karen anasema, "Siwezi kuacha kumpenda Yesu!"

Ufuatao ni ushuhuda wake alioupa jina: Nilimwona Yesu.

Thursday, March 21, 2013

Aliyekuwa Ustaadhi na Hakimu wa Mahakama ya Kadhi Akutana na Injili ya Yesu Kristo na Kuokoka – Sehemu ya 1Ahmed alikuwa ni injinia. Baadaye alishawishiwa na Ulama mmoja na kupandikiziwa chuki dhidi ya Wakristo na Wayahudi kiasi kwamba aliamua kuacha kazi yake na kwenda kusomea masomo ya dini ya Kiislamu (licha ya mama yake kupinga sana).

Masomo hayo yalimwezesha kuwa hakimu wa mahakama ya sharia. Kutokana na ukandamizaji mkubwa aliouona kwenye mahakama hizo na kukosekana kwa haki na pia kukosekana kwa msimamo juu ya tafsiri sahihi ya sheria za kiislamu, moyo wake ulikosa kabisa amani.

Kwa neema za Yesu Kristo, Ahmed alifunguliwa macho yake na sasa anajiuliza ilikuwaje akaamini Uislamu?

Ufuatao ni ushuhuda wake kwa maneno yake mwenyewe ambao ameupa kichwa cha habari: “Njia ya Allah Kuelekea Jehanamu au Njia ya Yesu Kuelekea Mbinguni.”

Tuesday, March 19, 2013

Je, Tuache Kula Nyama Zilizochinjwa na Waislamu?Kumekuwapo na migogoro hivi karibuni inayohusiana na suala la uchinjaji wa wanyama.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa Wakristo tunatakiwa tuache kulala, badala yake tudai serikali itupe uhuru au ‘haki’ ya kuwa na bucha zetu wenyewe. Baadhi ya viongozi wa dini hata walifikia kuwaambia waumini wao (Wakristo) wasinunue nyama kutoka kwenye bucha za Waislamu. Tazama hapa

Sababu mojawapo inayotolewa ni kuwa tunalishwa nyama zilizoombewa dua zisizohusiana na Mungu wetu. Je, tuache sasa kununua nyama kutoka kwenye bucha za Waislamu? Je, tuwe na bucha zetu?

Tuesday, March 5, 2013

Mpiganaji wa Hezbollah Akutana na Yesu na Kuokoka – Sehemu ya I
Afshin Javid alikuwa ni askari wa Hezbollah ambaye aliyatoa maisha yake kikamilifu kwa ajili ya Allah. Katika maisha yake yote, alijifunza kumtii Allah na alikuwa tayari kufanya lolote, ikiwa ni pamoja na kufa kwa ajili ya Allah.


Lakini baada ya kukutana uso kwa uso na Bwana Yesu, kila kitu kilibadilika. Sikiliza ushuhuda wake huu wenye nguvu sana, ambao si  tu kwamba utakutoa machozi, kama yeye mwenyewe anavyoeleza kwa machozi mengi, bali pia utajua jinsi Bwana Yesu alivyo Mungu Mkuu na wa kweli ambaye, kila anayemtafuta kwa moyo wa kweli, anamwona.


Ufuatao ndio ushuhuda wenyewe:

Wednesday, February 20, 2013

Manyanyaso na Ukandamizaji Mkubwa wa Wanawake Katika Nchi za Kiislamu
Kati ya mambo ya kusikitisha sana ni jinsi wanawake katika nchi za Kiislamu wanavyonyanyaswa na kukandamizwa. Ni wanadamu ambao Bwana Yesu amewaumba na kuwapa heshima kubwa lakini maskini wamejikuta katika nchi ambazo Mungu anayeabudiwa huko amewapokonya ile heshima na kuwatwika mateso makali ambayo hata ni vigumu kueleza. Mungu huyo amewapa wanaume mamlaka ya kuwafanyia chochote watakacho, lakini bahati mbaya sana, kile wanaume hawa wanachofanya ni masikitiko matupu.

Tuesday, February 19, 2013

Bahasha za Zaka Makanisani Zinatoka Wapi?Je, ni huduma kwanza au ni roho kwanza?
Wapendwa nawasalimu katika jina la Bwana wetu, Yesu Kristo.

Katika safari yetu ya kiroho tunakutana na mitihani na changamoto mbalimbali ambazo, ama zinatujenga au, kwa bahati mbaya, wakati mwingine zinatubomoa.

Lakini tunapokutana na changamoto kutoka kwa watu wasiomjua Mungu, hilo halitusumbui sana, maana tunajua kuwa kwa hao hilo ni jambo la kawaida. Mtihani mkubwa unakuja pale tunapopambana nazo kutokea kwa wale wanaomjua Mungu, na hasa kama ni vongozi wetu wa kiroho.

Nimekuwa nikijiuliza juu ya suala moja ambalo, nafikiri, limekuwa likifanyika kimazoea zaidi kuliko kimaandiko. Hili ni suala la ulipaji wa zaka.

Friday, January 11, 2013

Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia? – Sehemu ya II
Katika makala yaliyopita tuliona hoja za ndugu wa Kiislamu wanavyojaribu kwa juhudi nyingi kuonyesha kwamba Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia.

Katika makala hayo niliahidi kuwa nitaeleza jinsi ambavyo hoja zao hazina ukweli wowote. Licha ya kwamba Mungu wanayemwamini amewahakikishia kwamba Muhammad ametajwa kwenye Biblia, ukweli ni kwamba hajatajwa hata kidogo!

Tafadhali bofya HAPA ili kusoma makala haya.

Monday, January 7, 2013

Je, Muhammad Ametabiriwa Kwenye Biblia? – Sehemu ya I Marehemu Ahmed Deedat

Waislamu wanashikilia kwamba Muhammad alitabiriwa kwenye Biblia. Andiko lao kuu wanalotumia kutetea hoja hii ni Kumbukumbu la Torati 18:18. Andiko hilo linasema:

Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.


Haya ni maneno ambayo aliambiwa Musa na Yehova.