Picha ya kubuni kuonyesha jinsi Bikira Maria
alivyowatokea watoto watatu kule Fatima
Duniani humu
yako mambo yanayoendelea chini kwa chini bila wengi wetu kujua. Wengi tuko
kwenye harakati za kuishi na labda hata kustarehe tu bila kujali nini kiko
mbele yetu.
Kuna mahali
katika ratiba ya nyakati ambako tunaelekea hakika. Ni jambo lililo wazi kabisa
kwamba tulikotoka kulikuwa na unafuu mkubwa kuliko tuliko na tunakoelekea.
Misingi mikuu ya kijamii kama vile uaminifu, upendo, kuvumiliana, kushirikiana
na kusaidiana ilikuwa na nguvu sana huko nyuma kuliko sasa, na kuliko huko
mbele tuendako.
Ni rahisi tu
kusema kwamba hiyo inatokana na ugumu wa maisha katika nyakati hizi. Lakini
nikwambia kweli, kuna zaidi ya hapo. Mambo haya yanapangwa katika ulimwengu wa roho na
kusimamiwa kikamilifu na viumbe wa rohoni ambao hawamtakii mema mwanadamu.
Na kama huna
uwezo wa kustahimili hali ya sasa, nakuhakikishia kabisa huko mbele tuendako
ndio kabisa usahau. Hutaweza katu kusimama. Maandiko yanasema:Kwa kuwa wakati huo kutakuwako dhiki kubwa,
ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala
haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu yeyote;
lakini kwa ajili ya wateule, zitafupizwa siku hizo. (Mt. 24:21-22).
Mambo haya,
kama nilivyosema, hayazuki tu. Ni mipango iliyoanza miaka na miaka. Inapangwa
taratibu kiasi kwamba inazoeleka na kuonekana kama sehemu tu ya kawaida ya
maisha. Lakini inakuwa inapanda kiwango kadiri muda unavyoendelea.
Leo ninapenda
tuongelee kuhusu maono au jambo ambalo lilitokea mwaka 1916 na 1917 kule Ureno. Haya yalikuwa ni maono ambayo yanaaminika na
wengi kuwa yalikuwa yanamhusu Mariamu mama wa Yesu.
Mnamo mwaka
1916 watoto watatu wa kijiji cha Fatima kule Ureno, yaani Lucia dos Santos
(miaka 10), Francisco Marto (8) na Jacinta Marto (7) waliokuwa wachunga kondoo,
walitokewa na kile ambacho kinaaminika kwa wengine kwamba ni malaika ambaye
aliwaambia kuwa yeye ni Malaika wa Amani. Aliwaambia waungane naye kuombea
amani; maana hiki kilikuwa ni kipindi cha vita kuu vya kwanza vya dunia.
Ilikuwa ni kama maandalizi ya kukutana na Bikira Maria.
Watoto
Jacinta, Francisco na Lucia
Tarehe 13 Mei 1917
Tarehe 13 Mei 1917 wakiwa machungani tena, waliona
kama mtu akiwa anatoa nuru kali kuliko jua ambaye alikuwa ni mwanamke. Lucia
alimwuliza anatoka wapi na anataka nini. Aliwaambia anatoka mbinguni na anataka
wawe wanaenda pale (ilikuwa ni eneo
liitwalo Cova da Iria) kwa muda wa miezi sita lakini iwe ni kila tarehe ya 13
ya mwezi katika muda uleule. Kisha alisema kuwa baada ya hapo ndipo atawaambia
kusudi lake. Akawaambia wawe wanasali rozari kila siku ili kuleta amani duniani
na kumaliza vita.
Tarehe 13 Juni 1917 walienda tena kwenye eneo lile, na wakati huo
kulikuwa na watu takribani 50 hivi pamoja nao. Watoto wale walimwona tena huyo
Maria (lakini si wale watu wengine) na akawaambia, “Nataka mje tarehe 13 mwezi
ujao na kusali rozari kila siku. Kisha baadaye nitawaambia nitakacho.
Lucia alimwomba awapeleke mbinguni. Maria akasema kuwa angewachukua
Jacinta na Francisco baada ya muda mfupi, lakini Lucia angebaki. Ni kweli
Jacinta na Francisco walikufa wakiwa watoto lakini Lucia aliendelea kuwapo hadi
katika umri mkubwa.
Yule Maria alimwambia Lucia: Jesus
wants to use you to make Me known and loved. He wishes to establish the
devotion to My Immaculate Heart throughout the world. I promise salvation to
whoever embraces it; these souls will be dear to God, like flowers put by Me to
adorn his throne."
Yaani: “Yesu anataka kukutumia wewe kunifanya mimi nijulikane na
kupendwa. Anataka kuanzisha ibada ya moyo wangu safi
duniani kote. Naahidi wokovu kwa yeyote atakayekubali; roho hizi
zitapendwa na Mungu. Kama maua yaliyowekwa name kupamba kiti chake cha enzi.”
Tarehe 13 Julai watoto hao walifika tena Cova na kumwona Maria. Lucia
akamwuliza anachokitaka. Akawajibu tena: "Nataka mje hapa tarehe 13 mwezi
ujao ili kuendelea kusali rozari kila siku kwa heshima
ya Mama yetu wa Rozari; ili kuleta amani na mwisho wa vita duniani, maana ni yeye tu ndiye anayeweza kuwasaidia."
Baadaye Maria aliwaonyesha maono ya kuzimu
ambako roho nyingi zinateseka. Baada ya hapo, akawaambia kwamba:
"You have seen hell where the souls of poor sinners go. To save
them, God wishes to establish in the world devotion to my Immaculate Heart. If
what I say to you is done, many souls will be saved and there will be peace
...”
Yaani: “Mmeona kuzimu zinakoteseka roho za wenye dhambi. Ili kuwaokoa, Mungu anataka kuanzisha duniani ibada kwa moyo wangu safi.
Kama mkifanya kile nitakachowaambia, roho nyingi zitaokolewa na kutakuwa
na amani ...”
Tarehe 13 Agosti ilipokaribia, habari hizi zilishafikia vyombo vya
habari ambavyo haviungi mkono mambo ya kidini. Hiyo ilifanya habari hizi
zisambae kwa watu wengi sehemu mbalimbali. Asubuhi ya tarehe 13, watoto wale
walitekwa na meya wa Vila Nova de Ourem, Arturo Santos. Walihojiwa juu ya siri
walizokuwa wanazijua lakini waligoma kabisa kusema. Watekaji walijaribu
kiuwahonga fedha na hata kuwatishia kifo, lakini hawakusema kabisa.
Agosti 19, Lucia, Francisco na Jacinta walikuwa pamoja kwenye eneo
linaloitwa Valinhos, karibu na Fatima wakati wa mchana. Walimwona tena Maria
ambaye aliwaambia: "Nendeni tena Cova da Iria tarehe 13 na kuendelea
kusali rozari kila siku." Maria akasema kuwa angefanya muujiza ili watu
waamini, na kama watoto wale wasingekuwa wametekwa, basi huo muujiza ungekuwa
mkubwa zaidi.
Tarehe 13 Septemba 1917
Tarehe 13 Septemba kundi kubwa la watu
lilikusanyika Fatima. Mchana hao watoto walifika na waliweza kumwona huyo Maria
(lakini si watu wengine). Alimwambia Lucia:
"Endeleeni kusali rozari ili kukomesha vita. Mwezi wa Oktoba Bwana wetu atakuja
pamoja na Mama yetu wa huzuni na Mama yetu wa Karmeli (Our Lady of Dolours and
Our Lady of Carmel). Mtakatifu Yohana atatokea pamoja na mtoto Yesu ili
kuibariki dunia ....”
Tarehe 13 Oktoba 1917 watu wengi sana walikusanyika Cova. Wengi walienda
wakiwa hawajavaa viatu huku wakisali rozari kama namna ya kuonyesha unyenyekevu
kwa Maria. Mchana watoto wale walimwona Maria.
Kwa mara nyingine tena Lucia alimwuliza swali lilelile la siku zote:
Unataka nini? Akasema: Nataka kukuambia kwamba kanisa
lijengwe hapa kwa heshima yangu. Mimi ndimi Mama wa Rozari. Endeleeni
kila wakati kusali rozari kila siku. Vita vitakwisha, na askari watarudi hivi
karibuni nyumbani kwao.” Baadaye alianza kupaa kwenda juu kuelekea kwenye jua.
Wakati huo ndipo umati mkubwa wa watu uliweza kuona kile kinachotajwa
kama mwujiza. Kwa vile kulikuwa na mawingi, mawingu yale yaliachana na jua
likaonekana kama duara jeusi ambalo mtu aliweza kulitazama bila kuumia macho. Mashuhuda
wanasema kuwa waliona jua likitetemeka na kuchezacheza na kugeukageuka rangi.
Wengine wakasema waliona uso wa Maria, nk.
Sehemu ya umati wa watu uliojitokeza kuja
kumshuhudia Bikira Maria
Kanisa lilikaa kimya kuhusu maono ya Fatima hadi ilipofika Mei 1922
ndipo Askofu Correia alitoa barua ya kichungaji juu ya jambo hili; akisema
kwamba angeunda tume ya kuchunguza suala hili. Mwaka 1930 alitoa barua nyingine
ambayo, pamoja na mambo mengine, ilisema:
"In virtue of considerations made known, and others which for
reasons of brevity we omit; humbly invoking the Divine Spirit and placing
ourselves under the protection of the most Holy Virgin, and after hearing the
opinions of our Rev. Advisors in this diocese, we hereby:
- Declare worthy of belief, the visions of the shepherd children in the Cova da Iria, parish of Fatima, in this diocese, from the 13th May to 13th October, 1917.
- Permit officially the cult of Our Lady of Fatima."
Yaani: “Kulingana na masuala ambayo yamewekwa wazi, pamoja na mengine
ambayo hatutayataja kwa lengo la kufupisha taarifa hii; huku tukimsihi Roho wa
Kiungu na kujiweka chini ya ulinzi wa Bikira Mtakatifu sana, na baada ya
kusikiliza maoni ya mapadri Washauri katika jimbo hili:
- Tunatangaza kuwa maono ya watoto wachunga kondoo kule Cova de Iria, parokia ya Fatima, katika jimbo hili, yaliyoanza tarehe 13 Mei hadi tarehe 13 Oktoba 1917 yanastahili kuaminiwa.
- Tunaruhusu rasmi imani ya Mama Yetu wa Fatima.
...............................
Hadi hapa tumeshaona kile hasa kilichotokea kule Fatima. Sasa, yafuatayo ni
mambo matano tunayoweza kujiuliza kutokana na hicho tulichokiona:
Moja: Biblia inasema kwamba: Wapenzi, msiiamini kila roho,
bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa
uongo wengi wametokea duniani. (1 Yohana 4:1).
Unawezaje kuijaribu roho? Ona jinsi Paulo anavyosema: Lakini ijapokuwa sisi
au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo
tuliyowahubiri, na alaaniwe. (Gal. 1:8).
Maana yake ni kwamba, injili au neno la kweli ni lile linaloendana na kile
kilicho kwenye Biblia tu! Hata kama malaika atakuja na jambo ambalo liko
kinyume na maandiko, hapaswi kuaminiwa hata kidogo ingawaje yeye ni malaika.
Sasa, Petro anamwongelea Bwana Yesu na jina lake akisema: Wala hakuna
wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya
mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. (Mdo. 4:12).
Lakini hebu angalia huyu ‘bikira Maria’ alivyosema tarehe 13 Julai: "Nataka mje hapa tarehe
13 mwezi ujao ili kuendelea kusali rozari kila siku kwa heshima ya Mama yetu wa
Rozari, ili kuleta amani na mwisho wa vita duniani, maana
ni yeye tu ndiye anayeweza kuwasaidia."
Je, Mungu anaweza kutoa maagizo yanayojipinga? Je, maneno ya Mungu kupitia
Paulo na Petro hapo juu yanamhusu nani? Je, hayamhusu hata huyu ambaye alijiita
ni ‘bikira Maria’?
Yanapotokea maneno yanayopingana juu ya jambo lilelile, ni wakati wetu wa
kuchambua lipi la kweli na lipi sio; na sio kuyachukua yote mawili kuwa ni
kweli. Na ukweli hautokani na maoni na mapenzi yetu, bali unatokana na Neno la
Mungu lililo katika Biblia.
Mbili: Vilevile ‘Maria’ anawaambia hao watoto: “Mmeona kuzimu zinakoteseka
roho za wenye dhambi. Ili kuwaokoa, Mungu anataka
kuanzisha duniani ibada kwa moyo wangu safi. Kama mkifanya kile
nitakachowaambia, roho nyingi zitaokolewa na kutakuwa na amani ...”
Tumeona hapo juu kwamba Maandiko yanasema:
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina
jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
(Mdo. 4:12).
Tangu zamani katika Agano la Kale, inajulikana wazi kwamba msamaha wa
dhambi ulifanyika tu baada ya kumwagika damu. Hebu angalia jinsi Mungu
anavyowaambia Israeli:
Kisha mtu awaye yote ... atakayekula damu, ya aina
yoyote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia
mabali na watu wake. Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa
ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho juu ya nafsi zenu;
kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa ajili ya nafsi. (Mambo ya Walawi
17:10-11).
Utoaji sadaka ya wanyama ili kumwaga damu kwa ajili ya ondoleo la dhambi
yalikuwa ni maandalizi ya ujio wa sadaka kuu na ya mwisho ya Mwanakondoo wa
Mungu, Yesu Kristo.
Na maandiko yako wazi kabisa: Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa
kwa damu, na pasipo kumwaga damu HAKUNA ondoleo. (Ebr. 9:22).
Wenye dhambi wote sehemu yao ni katika jehanamu ya moto. Dhambi inaondoka
kwa njia MOJA TU, nayo ni kwa kusafishwa kwa damu ya Yesu!
Sasa hebu niambie ndugu msomaji, huyu Maria anasema: Mungu anataka
kuanzisha duniani ibada kwa moyo wangu safi. Kama mkifanya kile
nitakachowaambia, roho nyingi zitaokolewa na kutakuwa na amani ...” Je, roho hii
inakubaliana na Maandiko? Kama anachokisema ni kweli, je, Yesu alikufa kwa
mateso kiasi hicho ili iwe nini? Je, kifo chake ni batili?
Tatu: Huyu mama Maria akasema: Nataka
kukuambia kwamba kanisa lijengwe hapa kwa heshima yangu.
Bwana Yesu alipofukuza wafanyabiashara katika
hekalu alisema maneno haya: Imeandikwa, Nyumba
yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la
wanyang’anyi. (Mt. 21:13).
Pia akamwambia Petro: Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya
mwamba huu nitalijenga kanisa langu;
wala milango ya kuzimu haitalishinda. (Mt. 16:18).
Ndugu, kanisa ni kanisa la Kristo Yesu mwenyewe.
Hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kumiliki kanisa aliloanzisha Kristo.
Sasa, ni kwa vipi maneno ya ‘Maria’ hapo juu hayapingani na maneno ya Yesu?
Tunawezaje kutekeleza maneno yake bila kupingana na Maandiko?
Nne: Jambo jingine kubwa linalotakiwa kumshtua kabisa mtu ni
tarehe ya matukio haya. Ni jambo lililo wazi kwa wasomaji wa Biblia kwamba
Mungu hutumia sana namba kwenye maandiko katika kufikisha ujumbe wake
mbalimbali. Namba za Mungu zinafahamika, kwa mfano 3, 7 na 12.
Mathalani, tunasoma kuhusu Utatu Mtakatifu wa Mungu, Kristo alifufuka siku
ya 3, katika Ufunuo kuna baragumu 7, mapigo 7, mihuri 7, malaika 7, makanisa 7;
kabila 12 za Israeli, mitume 12, nk.
Lakini katika namba za Mungu, 13 haipo kabisa! Hebu angalia andiko hili
ambalo linaongelea wafalme fulani katika agano la kale: Hawa wote wakakutana
panapo bonde la Sidimu, kwenye Bahari ya Chumvi. Miaka kumi na miwili
walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu wakaasi. (Mwa. 14:3-4).
Kumi na tatu ni namba ya uasi. Ni namba ya kishetani, sio ya kiungu. Hata
hivyo, mstari huu hauwezi kuonyesha kwa wazi sana kuwa hii ni namba ya uasi.
Lakini tunapokuja kwenye maisha ya kawaida, hapo ndipo tunapoona mambo haya
kwa uwazi kabisa.
Namba 11, 13 na 33, ni namba zinazoheshimika na kutumika sana na waabudu
shetani, kwa mfano freemason na illuminati. Kwa mfano, namba hii inaonekana
wazi kwenye muhuri mkuu wa Marekani (the Great Seal of America). Tazama picha
hapa chini:
Muhuri Mkuu wa Marekani
Huu ni muhuri mkuu wa Marekani kwa mbele na nyuma. Ukiangalia upande wa
mbele utaona yafuatayo: kuna majani 13, matunda 13, mistari myeupe na myekundu
13 kwenye ngao, mishale 13, maneno "E
Pluribus Unum" yenye herufi 13, nyota 13!
Kwa upande wa nyuma, utaona ngazi za matofali ziko 13, maneno “Annuit Coeptis” yenye herufi 13.
Lakini swali la haraka atakalojiuliza mtu ni kuwa, je, iweje jambo hili
liwe la kiserikali? Ndugu, kuna nchi moja tu hapa duniani iliyoanza na msingi
wa kweli wa Mungu aliye hai, yaani Israeli.
Marekani nayo ni nchi ambayo waasisi wake wa mwanzo walianza vema kabisa,
lakini baadaye mambo yaliharibika. Nchi nyingi zimeanza na mazindiko na mikataba
ya kishetani. Zimewekwa wakfu kwa shetani. Viongozi wake wameingia madarakani
kwa msaada wa joka wa zamani, yaani Lusifa.
Wachunguzi mbalimbali walishagundua kuwa muhuri huu ulitengenezwa na watu
ambao walikuwa ni freemason, hivyo ukaingizwa serikalini bila wengi kujua. Haya
ni maagano ya kishetani ambayo Marekani na watu wake waliingizwa bila wao
kujua. Unaweza kusoma zaidi juu ya hili kwa kubofya hapa.
Sasa, tukirudi kwa bikira Maria wa Fatima, bila shaka utaona wazi sasa
kwamba kuna jambo ambalo limejificha hapa. Kwa nini asisitize kuwa watoto hao
ni lazima waje tarehe 13 na katika muda uleule? Tangu lini Mungu wa mbinguni
alitumia namba 13 kwa mambo yake? Ulimwengu Na kwa lugha nyepesi ni kuwa, swala
la Fatima halina Mungu aliye hai ndani yake.
Tano: Mwisho nimalizie kwa kuuliza swali kuhusu uamuzi wa
kanisa kupitia uamuzi uliofanywa na tume ya Askofu Correia. Kanisa liliamua
kuwa ni sahihi kufanya ibada zinazomhusu huyu ‘Maria’ na kwamba jambo hili
linastahili kuaminiwa.
Wasomaji wa Biblia wanafahamu kuwa Mungu anasema kuwa tusiongeze wala
kupunguza katika Neno lake (Ufunuo 22:19). Sasa je, wewe msomaji, unadhani
katika haya kanisa liliongeza au halikuongeza. Kama unadhani halikuongeza, je, unafikiri
ni hadi mtu afanye nini ndipo ionekane kuwa ameongeza katika Neno la Mungu?
Rafiki, Yesu anakuita uingie ndani ya safina kabla gharika haijamwagwa. Saa
ya wokovu ni sasa. Kama ninavyosema kila mara, usiendekeze dini bila Yesu. Dini
zimemwacha Yesu nje na kufundisha mambo yao ya kibinadamu ambayo Bwana anasema:
Watu hawa huiheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu
bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. (Mt. 15:8-9).
Hatuendi mbinguni kwa sababu tuna dini. Tunaenda mbinguni kwa sababu tuna
Yesu kila siku; kila saa; kila wakati. Maana unaweza kujua hata Biblia yote na
mbinguni usiende kwa sababu unaweza kujaza maandiko moyoni kichwani lakini usiwe na Yesu.
Imeandikwa: Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake;
na hayo ndiyo yanayonishuhudia. (John 5:39).
Karibi kwa Yesu sasa. Acha
kuahirisha kuokoka. Acha kuendelea kutumainia dini. Mpate Yesu ndipo na dini itakuwa na maana. Maana ya kusema hivi kuwa, haitoshi tu kusema kwa mdomo kuwa mimi ni Mkristo. Mfanye Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako. Ni kwa njia hiyo tu ndipo hata utaweza kuogopa kutenda dhambi kwa sababu yake. Lakini kama mtu huwa anatenda dhambi watu wengine wanapokuwa hawamwoni, ina maana kuwa kwake Yesu hana nafasi. Kama akiwa na nafasi kwako, utamwogopa Yeye na si wanadamu. Mungu akubariki.
Hi, i think that i saw you visited my weblog thus i came to
ReplyDelete“return the favor”.I am attempting to find things to enhance my site!
I suppose its ok to use a few of your ideas!!
Here is my page; http://www.het-vakantiehuis-frankrijk.nl/duitsland.htm
Hi, thanks for visiting my little blog. Mine is a gospel spreading blog, so the ideas in here can be used completely freely. Be blessed.
Deletehata wewe usipotoshe watu, kupanga tarehe ni mipango ya mtu inamana hata hizo tarehe zifutwe kwenye kalenda?? tusiziishi kwa mawazo yako??kanisa linamueshimu Maria kama mama wa mkombozi, ungeijua rozari usingeongea mana ndani yake ni Yesu mwenyewe. mambo yamchukizayo Mungu twayatambua na hatuoni dosari ktk hilo. Tafuta sadaka za watu kwa njia nyingine si kwakupotosha.
ReplyDeleteAsante ndugu kwa kutembelea blog hii na kuandika kile kilichomo moyoni mwako. Ni kweli tarehe haina shida; na tarehe kama tarehe kusema kweli haifanyi suala la Bikira Maria kuwa dhambi. Vilevile, ni kweli kabisa Mariamu ni mama wa Mkombozi wetu, Yesu Kristo na anastahili kuheshimiwa kabisa.
DeleteTatizo linapokuja ni pale tunapounganisha kila kitu ndani ya mafundisho yanayomzunguka mama Maria.
Hivi ni kweli kwa mfano kuwa huyu mama anaweza kutuombea sisi?
Hivi ni kweli watu sasa hawasamehewi dhambi kwa damu na kifo cha Yesu badala yake wanasamehewa kutokana na kumwomba Maria? Huko si kubatilisha msalaba wa Kristo?
Kutoona dosari juu ya jambo hakulihalalishi. Haujasikia hata msemo tu wa kawaida kwamba: The path to hell is paved with good intentions?
Hatuwezi kusimamia mambo kutokana na hisia zetu. Kanisa limejengwa juu ya Neno la Kristo; si vinginevyo. Uthabiti wetu katika imani unatokana na kusimama kwenye kile kilichoandikwa kwenye Biblia?
Mbona kuna 'makanisa'ambayo yanadai kuwa Yesu si Mungu, na kwamba hakuna mahali panapoitwa jehanamu ya moto. Hakika kabisa na hawa nao hawaoni dosari katika mafundisho haya! Je, kutokuona kwao dosari kunahalalisha imani hii waliyo nayo?
Kwani ukitaka kuamini utamuuliza yule anayetuhubiria: "Hivi unaona dosari yoyote katika haya unayonihubiria?"
Au utauliza: "Ni wapi ambako Biblia inasema hayo unayonihubiria?"
Mimi nitauliza hili swali la pili.
Mpendwa, mimi sina tatizo na wewe kuwa na msimamo huo kulingana na haya unayoyasema, ila sikukubalii hadi uthibitishe kimaandiko.
Bwana akubariki.
Ulichokiongea ndicho kilichopo, watu hawajui lipi ni neno la Mungu na yepi ni maagizo ya shetani ila kwakuwa dini wamezaliwa wamezikuta hata kama mtu angeambiwa vipi, haweziamini maana kazaliwa kakuta imni ndiyo ipo hivyo na anaona anayemwelekeza jambo tofauti na alivyokaririshwa. Nin.Mungu pekee ndiye atakayewezambadilisha mtu huyu kutokana na fikra potofu alizopewa
DeleteSema msemayo,watu wa kizazi hiki mlishaambiwa kuwa hamtaona muujiza isipokuwa wa Yona,mnajidai kuijua kweli ya Mungu wakati dunia ndiyo inazidi kuangamia,Mungu anahitaji wanyenyekevu wapeleke sala kwake dunia ipate kuokolewa, je wako wapi? sana tunaona ushuhuda wa mapepo na watu wa kuzimu,ivyo tunarudi kwa mwanadamu mwenzetu ambaye yeye Mungu mwenyewe alituhakikishia kuwa ni msafi,mbarikiwa na myenyekevu,mama wa Kristu apeleke sala zutu kwa mwanawe ili tupate kuokolewa Mungu anasema "SALA ZA WATAKATIFU NI MANUKATO KWAKE" Nakushauri tuma sala zako kwa mama naye atazifikisha kwa mwanawe wewe na mimi sala zetu hazifiki tunayo MAWAA, Lakini yawezekana wewe mwenzetu ni mkingiwa pia soms Warumi 8:28-30 na pia biblia inasema yeye anayejiona hana dhambi anajidanganya na kweli haipo ndani yake.
ReplyDeleteNdugu mpendwa, muujiza wa Yona unaozungumzwa unahusianaje na bikira Maria kuwa mwmbezi? Nadhani unahusiana zaidi na kufa kwa Yesu na kufufuka kwake - Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo NDIVYO MWANA WA ADAMU ATAKAVYOKUWA SIKU TATU MCHANA NA USIKU KATIKA MOYO WA NCHI. (Mat 12:40)
DeleteWatu walio wasafi si bikira Maria peke yake. Mungu anasema: WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI NDIO WALIO BORA, HAO NDIO NILIOPENDEZWA NAO. (Zab 16:3)
Yako mambo mengi ambayo kanisa Katoliki linafundisha ambayo hayana ukweli wa kibiblia ndugu yangu. Mungu anasema watakatifu wako duniani hapahapa; tena hawa ndio BORA ZAIDI YA WALE WALIOKO MBINGUNI.
Sasa utasemaje kuwa bikira Maria anasikiwa kwa sababu yeye ni msafi.
Kwanza NI UONGO MTUPU kusema kwamba: [yeye Mungu mwenyewe alituhakikishia kuwa ni msafi].
Huu ni uongo wa kanisa Katoliki. Hakuna POPOTE kwenye Biblia Mungu analosema kuwa bikira Maria hakuwa na dhambi; badala yake Biblia inasema:
“Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, HAKUNA MWENYE HAKI HATA MMOJA. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. WOTE WAMEPOTOKA, WAMEOZA WOTE PIA; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawakuijua. (Romans 3:10-17).
Asiye na dhambi ni MMOJA TU:
(2Kor 5:21) YEYE ASIYEJUA DHAMBI alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Huyu ni Yesu Kristo.
Naomba unionyeshe KOKOTE kwenye Biblia ambako kumeandikwa kuwa bikira Maria hakuwa na dhambi ya asili (kama kanisa Katoliki) linavyofundisha – NI UONGO!
Umeongelea kuhusu Waumi 8:28-30
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza. (Rm 8:28-30).
Wala hakuna uhusiano hapa na bikira Maria. Hapa inaongelea kuhusu wote walio katika Kristo Yesu – akiwamo na bikira Maria mwenyewe; ambao wamehesabiwa haki na Mungu KATIKA KRISTO.
JE, SI KWELI KWAMBA JAPO TUKO DUNIANI SASA, LAKINI PIA TUKO MBINGUNI KAMA TU NDANI YA KRISTO?
Bwana anasema:
hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. (Efe 2:5-7).
Mpendwa wangu, hatuko hapa kushindana na dini yoyote. Bwana Yesu hakuja kuleta dini duniani bali wokovu. Yeyote anayekubali wokovu wake na – awe ni Mkatoliki, Mlutheri, au mwingine – anakubaliwa na Baba wa mbinguni. Lakini kung’ang’ania mafundisho ambayo ni wazi kabisa kwamba NI UONGO na kuona kwamba wale wanaoyapinga kuwa ama WANAJIDAI, WANAJIKWEZA, WANAHUKUMU, WANAJIHESABIA HAKI, n.k. hakumsaidii yeyote.
Hatutaogopa kusema iliyo kweli kwa kuogopa kwamba tutaitwa majina. Ni lazima INJILI SAHIHI YA YESU ihubiriwe ili watu WAOKOLEWE.
Mungu akubariki sana.
Asante sana nimekuelewa vizuri sana na huko sahihi 100%
DeleteYesu mwenyewe alisema hakuna jina lingine litupasalo/tulilopewa wanadamu kuokolewa kwalo bali ni jina moja tu ''YESU'' ambalo kila goti litapigwa kuanzia wanadamu mpaka lusifer achilia mbali mapepo yanatetemeka mara wasikiapo jina tu YESU.
na pia alisema huwezi kufika/kuingia mbinguni bila kupitia kwake. akiwa na maana umkiri umjue na umfuate maana yeye ndiye njia na lango la kukufikisha mbinguni, bila yeye hufiki mbinguni. (kama ni hivyo hapa angekupa na option number 2 kama alijua na mama yake ni njia ya kutufikisha kwake. lazima angesema tu.)
Maria yeye alikufa kama watu/wanaadamu wengine na aliweka alipopaswa kuwekwa mara baada ya kufa. yeye asikii wala hajui kinachoendela duniani bali ni Yesu. na msaidizi ambaye tumeachiwa atusaidie na kutuongoza kufikia/kufuata ile kweri yaani Roho Mtakatifu.
kumbe kwa vile wewe si mkatoliki ndio unaamua kupotosha watu....hivi wewe hapo unamuheshimu mama yako humuheshimu? kwa nini na sisi wenye Adabu tusimuheshimu mama aliyemzaa Mungu?
Deletekama unamuheshimu mama yako definitely utamuheshimu mama wa Yesu....
Najua vijana siku hizi mnaona dili kujifunza bible na kuomba watu michango fanya kazi kijana.....Bila bikira Maria usingemjua Emmanuel
Mh!!
ReplyDeleteAcha kupotosha watu. nashangaa watu kung'ang'ana na kanisa katoliki. kuna wapagani wangapi na waislamu ambao hawamjui Yesu Kristo. Watafute hao uongeze sadaka. maana siku hizi dini mmeifanya mtaji eti mmekuwa wajasiriamali kwa kudanganya watu kwa mgongo wa kuokoka wakati matendo yenu ni ya aibu.
ReplyDeleteImani bila matendo ni bure. Mmekaa kusengenyana na kusema uongo. kutapanya siri za watu wanaowaamini na kuwaeleza matatizo yao. kutumia vifungu vya biblia kudai sadaka. ni aibu tupu. tuacheni sisi wakatoliki tusali rozali, tuombe kupitia Mama Maria. Yawauma nini nyie? Kwamba nyie mliookoka mtaenda mbinguni? jidanganyeni sana. Imani bila matendo ni bure.
ReplyDeleteYesu ndo njia ya kweli, wala sio bikira maria
DeleteInaonyesha ulivyo na ufinyu wa mawazo
ReplyDeletewele wote unaowaona katika madhehebu mengine hpo mwanzo walikuwa wakatoliki, baada ya kuijua kweli ukatoliki hauna nafasi kwao tena, kuhesabu rozali, kuombewa na wafu,kutubu kwa padre,kukariri sala ndefu zilizotungwa na wazungu, kufuata liturgia,misa,sacramenti saba, upapa badala ya roho mt. wanaoweza kuijua vizuri ukatoliki na katoliki ni waliokuwemo wakatoka si wewe uliyemo ndani.
ReplyDeleteamen. mimi pia mmojawapo wa waliokuwa wakatoliki. ubatizo, komunio na kipaimara vyote nilipata.
Deletekwa akili za kushikiwa ukatoka....umepotea sana
Deletehaya unapa shilingi ngapi kwa siku kwa kujifanya na wewe unakanisa,,,,,,eti mama Maria aruhusiwi kuwa na kanis alke mbona gwajima analo na kila siku unaenda kuhesabu nae sadaka
Inaoneka wazi wewe ni Muislamu usipotoshe Jamii hasa wakristu....Je yesu aliposema yeyote mtakao waondolea dhambi wameondolewa na mtakao wafungia wamefungiwa hata mbinguni aliwaambia akina nani? alimaanisha nini? somo hilo linawahusu nani? "wewe ni mtumwa wa shetani"
DeleteDuh!!!!!!!!!!!!!!!!! Barikiwa Mtumishi James
ReplyDeleteAmen. nawe pia Harrison.
Deletehicho usemacho ni kweli kabisa mungu alinifanyia muujiza kwa namba 12 akutie nguvu sana Ndugu kwa huduma yako inasaidia wengi
ReplyDeleteKWELI KABISA NDUGU ZANGU WAKATOLIKI HIKI KINACHOELEZWA NI KWELI KABISA KUMBUKENI MTUME PAUL ALISEMA HATA MALAIKA WA GIZA WATAJIGEUZA KUWA MALAIKA WA NURU ILI KUPOTOSHA UKWELI 2WAKORINTHO 11:14 BIKIRA MARIA HANA SEHEMU YOYOTE KUHUSU WOKOVU WA MWANADAMU YESU ANASEMA MIMI NDIYO NJIA KWELI NA UZIMA MTU HAJI KWA BA ILA KWA NJIA YA MIMI Yoh. 14:6
ReplyDeleteWewe na James ambae ni msadukayo ni mmoja wa wasiojua dini unafata mkumbo..unajua maandiko matakatifu ? Ufunuo 12:1 unaijua? Muujiza wa kwanza wa Yesu alifanya kwa kuambia na nani?....Yesu wakati anakufa msalabani unajua alimwambia nini Mama yake...na alimwambia nini Yohane? Jifunze biblia utaishia kuwa body guard wa wachungaji wenu feki
DeleteKatika ulimwengu wa leo kuna njia nyingi za kutumaini. Furaha ya milele na Mbinguni vina hubiriwa kila mahali. Hata hivyo kuna dini nyingi tofauti, filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo (furaha ya milele) vinatofautiana. Na kila mmoja katika tofauti hizo za dini na filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo; anaamini ya kuwa amesimama katika ukweli.
ReplyDeleteNa maisha ya mwanadamu yamefikia mawazo ya hali ya juu. Wengi wetu wanapenda kuishi katika dunia hii kwa muda mrefu iwezekanavyo. Baadhi yao wanategemeo la kuishi milele katika dunia hii.
Lakini kuna njia moja tu ya kumuingiza mtu katika furaha ya kweli ya milele. Kuna ukweli mmoja tu, umfanyao mtu kuwa huru. Kuna namna moja ya maisha itakayomfikisha mtu katika uzima wa milele. Yesu Kristo Mwana wa Mungu, ndiyo “Njia, na Kweli na Uzima.” Kumbuka Yesu mwenyewe alisema, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi,” Yoh. 14:6.
Na Yesu Kristo ni “Njia na Kweli na Uzima.” Kwa sababu Yeye alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Wote wametenda dhambi kwa kuiasi Sheria ya Mungu (Rum 3:23; 1 Yoh 3:4). “Na mshahara wa dhambi ni mauti,” Rum 6:23. Hii ndiyo mauti ya pili au Jehanamu (Ufu. 21:8; Mat. 10:28). Kwa sababu ya dhambi zetu tulistahili adhabu ya milele katika Jehanamu, lakini kwa sababu ya upendo mkuu wa Mungu na rehema zake alimtoa mwanawe Yesu Kristo akafa msalabani akalipa deni letu la dhambi zetu (Yoh. 3:16-17; Rum. 5:5-10; 6:17-23). Yesu ni “Njia na Kweli na Uzima.” Kwa sababu Yeye alifufuka kutoka kaburini. Kabla hajaja Yesu Kristo, kaburi la giza la mauti lilikuwa likitungojea mwisho wa safari yetu pasipo tumaini. Lakini Yesu alishinda kifo akafufuka toka kaburini. Yesu alishinda mauti. Yeye atatupa ushindi juu ya mauti wale tunaompokea na kumtii (1 Kor 15:2023; Ufu. 1:17-18). Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima: yeye aniaminie mimi, ajapokufa atakuwa anaishi,” Yoh 11:25.
Yesu ni “Njia, Ukweli na Uzima,” kwa sababu Yeye atawahukumu watu wote siku ya mwisho (Mdo. 17:30-31). Kila mtu atasimama mbele ya Yesu Kristo na atatoa hesabu ya matendo yake aliyoyafanya wakati wa maisha ya hapa duniani. Mtume Paulo kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu aliandika hivi: “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda kwamba ni mema au mabaya,” 2 Kor. 5:10.
Yesu ndiye njia pekee ya kwenda mbinguni. Yesu peke yake ndiye kweli. Hakuna atakayepata uzima wa milele isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo. Ili mtu apokee baraka zitolewazo na yesu mwenyewe, ni sharti awe amuamini Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu
aliye hai. Kumbuka Yesu alisema “....Msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu,” Yoh. 8:24. Pia inampasa kutubia dhambi zake, Yesu alisema nawaambia; “Sivyo msipotubu ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo,” Lk. 13:3. Mtu hawezi kupokea baraka zitolewazo na Yesu Kristo iwapo atamuonea haya. Maana Yesu alisema,
“Yeye atakayenikiri mbele za watu nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye Mbinguni, bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye Mbinguni,” Mat. 10:32-33. Pia inampasa mtu abatizwe katika kristo ili apokee msamaha wa dhambi na baraka. Kumbuka Yesu alisema, “Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiye amini atahukumiwa,” Marko 16:16.
Yesu Kristo Mwana wa Mungu hakika ndiye, “Njia na Kweli na Uzima.” Hakuna atakaye okoka isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo. Kama ukimwamini Yesu leo na kumtii ujue ya kuwa furaha na amani na uzima vita kuwa vyako; sio katika ulimwengu huu tu, bali na katika ulimwengu ule ujao.
SIYO MALAIKA WATAKATIFU WALA BIKIRA MARIA!!!
Nilitaka kukwambia kuwa ukisemacho kinauzito sababu sisi ni wanadamu na hatujakamilika sababu biblia ni ngoa na upanga una waza ni ambia maana ya neno hilo katika biblia ukitaka kuonana na baba yangu pitia kwanza kwangu na ukitaka kuniona pitia kwa baba yangu
ReplyDeleteNilitaka kukwambia kuwa ukisemacho kinauzito sababu sisi ni wanadamu na hatujakamilika sababu biblia ni ngoa na upanga una waza ni ambia maana ya neno hilo katika biblia ukitaka kuonana na baba yangu pitia kwanza kwangu na ukitaka kuniona pitia kwa baba yangu
ReplyDeleteYESU NI BWANA
ReplyDeleteYESU NI ALFA NA OMEGA [Ufunuo1:8,Ufunuo1:17 ISAYA 41:4]
ReplyDeleteYESU NI ALFA NA OMEGA [Ufunuo1:8,Ufunuo1:17 ISAYA 41:4]
ReplyDeleteYESU NI BWANA
ReplyDeleteusipotubu utahangamia na hapa hapa Duniani utapata bakora zako kwa kumzarau mama wa Mungu....rubbish
ReplyDeletewewe ni mmoja wa wapinga kriso.chuki za kidini zimekufanya utumie akiri nyingi na vifungu vya biblia kumpinga mama wa Mungu.kumbuka shetani pia alitumia biblia kumshawishi Yesu amsikilize.Dunia nzima inajua kuwa Bikira Maria aliwatokea hao watoto.shahidi wa kwanza ni sista lucia mwenyewe aliyekufa waka 97.tafiti zimefanywa kwa miaka zaidi ya 100 na utabiri wa kupigwa risasi papa mwaka 81 aliutoa mama,na mama mwenyewe ndiye alimwinua papa.angalieni nyie wapinga kristo shetani anajitukuza ndani mwenu
ReplyDeleteUnaweza kujadili kwa kutumia maandiko? Kama ni kutokewa tu na viumbe, wapo waliotokewa na viumbe mapangoni na leo wana wafuasi mamilioni. Ongea kwa kutumia maandiko.
Delete