Friday, April 5, 2013

Injili ya BarnabaJe, umewahi kusikia juu ya ile inayoitwa Injili ya Barnaba? Hii ni injili ya namna gani?

Injili ya Barnaba ni kitabu kikubwa karibu sawa na Injili zote za kwenye Biblia zikichanganywa pamoja. Injili hii inapendwa na kusambazwa sana kwenye ulimwengu wa Kiislamu, wakidai kwamba ndiyo injili sahihi kabisa.

Injili hii inadai kwamba iliandikwa na mmojawapo wa mitume wa Yesu Kristo aliyeitwa Barnaba.

Sababu za injili hii kuwa maarufu kwenye ulimwengu wa Kiislamu ni kwamba injili hii:

  1. inasema kuwa Yesu si Mungu. 
  2. inasema kuwa Yesu si Masihi.
  3. inasema kuwa Muhammad ndiye mtume ambaye angekuja siku za mwisho; na kwamba Yesu alisema kuwa hastahili kumlegezea kamba za viatu vyake!

Lakini pamoja na kwamba kwa Mkristo ni suala lililo wazi kabisa kuwa injili hii ni ya uongo, kwa mamilioni ya Waislamu ni kitabu cha muhimu sana kwa kuwa wanadhani kinathibitisha ujio, uhalali na utume wa Muhammad.

Kwa nini basi injili hii ni ya uongo? Tafadhali bofya HAPA ili kupata majibu ya swali hili.

1 comment:

  1. Nimeyapenda masomo yako nimejalibu kutafuta namba yako nimekosa sijui nitaipataje mtumishi

    ReplyDelete