Sunday, April 21, 2013

Yesu ni Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni





Yohana 19:1  Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi.

Yohana 19:2  Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau.

Yohana 19:3  Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi.

Yohana 19:4  Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake.

Yohana 19:5  Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu!

Yohana 19:6  Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake.

Yohana 19:7  Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.

Yohana 19:8  Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa.

Yohana 19:9  Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote.

Yohana 19:10  Basi Pilato akamwambia, Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha?

Yohana 19:11  Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.

Yohana 19:12  Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari.

Yohana 19:13  Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.

Yohana 19:14  Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!

Yohana 19:15  Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.

Yohana 19:16  Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.

Yohana 19:17  Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.

Yohana 19:18  Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.

9 comments:

  1. Ni kweli kwamba,Yesu ni njia ya kwenda mbinguni, lakini si ya pekee na si ya watu wote, bali ni njia ya kwenda mbinguni ya wana waisraeli...''MUNGU AMEWALETEA WAISRAELI MWOKOZI...''kwa maana hiyo, waisraeli wa enzi ya yesu,ili waende mbinguni walitakiwa wamsikilize Yesu, alietumwa na mungu kwao. Na waisraeli wa enzi za Musa, walitakiwa wamsikilize Musa ili waweze kupata uzima wa milele, kwahiyo Musa vilevile ni njia. Wale waisraeli wa enzi ya daudi, walitakiwa wamsikilize Daudi ili wapate uzima wa milele, Daudi pia ni njia mwisho kabisa, tupo katika enzi za kisasa, ambazo enzi hizi, Unatawala ujumbe wa Muhammad kutoka kwa mungu, kwa ajili ya watu wote. Sio waisraeli pekee yao''...WATAPEWA TAIFA JINGINE, LENYE KUZAA MATUNDA...'' Kwa hiyo, Muhammad ni njia ya kwelekea mbinguni kwa watu wote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ibra, jibu ni HAPANA! NO! NO! NO!

      Delete
    2. Mhh ila ndugu zetu waislam uwa mnajua kuigeuza Bible kwerikweri sijui mambo mengine huwa mnayatoa wapi??!!.. kwa hiyo Mungu naye ana mambo ya kisasa na ya kizamani??!! basi ndo maana hii inatupelekea Wakristo tuamini kuwa huyu mnaemuita alaah na Mungu muumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo si mmoja allah ni mwingine na Mungu ni mwingine kabisa maana Mungu si mwanadamu kumlinganisha na pia Mungu si kama unavyomfikiria yeye ni mwanzo na mwisho hivyo hana usasa wala uzamani bali yeye ni mwendelzo (yaani hana mwanzo wala mwisho)

      Delete
  2. Huyo mchangiaji No. 1 amekosea kabisa kabisa, si kweli YESU ndio Kila Kitu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika kabisa rafiki. Yesu ni kila kitu. Ulimwengu wote ni mali yake; wanadamu wote ni mali yake; na kanuni za uzima zinatoka kwake.

      Delete
  3. Replies
    1. Ubarikiwe brother Thomas. Japo mimi si mchungaji. Labda kuna siku nitakuwa mchungaji nini?

      Delete
  4. Nami nichangie kidogo hapa kwa Mara ya kwanza..kuna tofaut kubwa sana na kutokuingiliana kwa Ukristo na uislam..haijalishi ni vipi kuna makengeusho ya namna gani..Yesu alisema kuwa Yeye ndie njia ya kweli na uzima waliotangulia ni wezi na kondoo ni wapi mtume muhamad kasema mimi ndiye njia ya uzima zaidi ya kuwaforce watu kuwa waislam kwa kuwaua vibaya..hivi Allah ana upendo kweli!!!Yesu alisema kila amwaminie atampa ahadi ya kujawa na Roho mtakatifu atakayemshuhudia Yeye na kutuongoza katika kweli yote..waislam hudai kuwa ni mtumee muhammad..acha kupotoka..muhamad anaweza kukaa ndani yangu,kuniongoza,kunipa amani..kuniombea nk wakati yeye alikufa na kwa bahati mbaya hakutubu na kuuposha ulimwengu wote..kuna tofauti za allah na Jehovah hata kama ni kweli inawezekana kwa kiarabu Jehovah ndo allah lakini mungu wa waislam na Mungu wa wakristo kuna tofauti mf.Jehovah hufanya kazi katika nafsi tatu allah hapana..Jehovah ana wana na Yesu ndie mwana pekee wake allah hazai..allah atawasamehe dhambi wenye dhambi kidogo..Jehovah no mapka uwe mtakatifu kama Yeye alivyomtakatifu..allah anakubali kuabudiwa na mapepo mna majini lkn sio Jehovah..Jehovah alimtuma Yesu allah akamtuma muhammad..allah atawapa watu wake wanawake baada ya kufa wazini nao haera tena wengi wenye macho kama vikombe(nadhani hayo ni mapepo)mbingini hakuna kuoa na kuolewa..ukifuatilia zaidi utagundua utofauti mkbwa sana..asiyemwamini Yesu na kuishi maisha matakatifu haijailishai anajiita mkristo au nano makao yake ni jehanam baada ta kufa..waislam achena kupotosha..ahsante

    ReplyDelete