Baba yangu mmoja wa kiroho
alipenda kusema, “Jiachie tu kwa Mungu naye atafanya.”
Neno hilo lilinisumbua kwa muda
mrefu sana kujua maana yake. Nilikuwa najiuliza, “Jiachie maana yake nini? Mbona
mimi najaribu kuishi maisha matakatifu lakini nashindwa? Ina maana mimi
sijaokoka?”
Kila tunaposikia au kusoma Neno la
Mungu, hapo ndipo tunapojiona jinsi ambavyo tumepunguka; tuko chini ya viwango
vya utakatifu wa Mungu!
Lakini wakati huohuo Biblia
inasema: Tafuteni
kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hakuna mtu atakayemwona
Mungu asipokuwa nao. (Waebrania 12:14).
Yaani nisipokuwa mtakatifu siwezi
kabisa kumwona Mungu? Utakatifu ni nini? Je, ni kuishi maisha ambayo hayana
dhambi nyingi na kubwakubwa? Hapana! Utakatifu ni kutokuwa na dhambi kabisa –
iwe kubwa au iwe ndogo.
Mungu ni mkamilifu na anasema wazi
kwamba mbinguni hakitaingia chochote kilicho kinyonge. (Ufunuo 21:27).
Sasa je, tunaweza kweli kuishi humu
duniani bila dhambi?
Sheria ya Mungu ina maagizo mengi.
Mungu anasema: Ombeni bila kukoma; mpende adui yako na umwombee; usitamani vitu
vya wengine; usiseme uongo; usiwaze mabaya; usichukie wengine; ishi kwa imani, chochote
kisichotokana na imani ni dhambi, n.k., n.k. Je, ni kweli yupo mtu anayeweza
kusema, “Mimi sina dhambi?”
Labda mara kwa mara umekuwa
ukijaribu kusimama lakini kila baada ya muda mfupi unaanguka tena. Matokeo yake
unaingiwa na hatia moyoni na hata hofu ya kuachwa siku ya mwisho au endapo
utakufa. Wengine pia wamekata tamaa kabisa na kusema tu, “Haiwezekani kuishi
maisha ya wokovu!” Wameamua kurudi nyuma kwenye dhambi kama zamani.
Lakini ni nini hasa ambacho Mungu
anategemea kutoka kwetu? Bwana anasema, Je, Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui
madoa-doa yake? Kama aweza ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea
kutenda mabaya. (Yeremia 13:23).
Ngozi nyeusi ya Mkushi na madoa ya
chui ni asili yao. Dhambi ni asili yetu. Biblia inasema wazi, Tazama, mimi
naliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu alinichukua mimba hatiani.
(Zaburi 51:5).
Ukianza kujitahiditahidi,
kujizuia, na kujilazimisha kuishi sawasawa na sheria ya Mungu, utapoteza muda
wako na utaishia kwenye kukata tamaa. Tukifanya hivyo, Mungu anasema kuwa hapo ni
kutaka kuithibitisha haki yetu wenyewe (Rum. 10:3). Yaani ni kama tunataka kuja
kusema, “Ah, nimepigana hadi nikashinda!” Isaya naye anasema, Kwa maana sisi
sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama
nguo iliyotiwa unajisi. (Isaya 64:6).
Juhudi zetu zote ni kupoteza tu
muda kwa jambo ambalo halina faida bali hasara tupu. Bwana Yesu anasema, ... pasipo mimi
ninyi hamwezi kufanya neno lolote. (Yohana 15:5).
Ukianza kujitahidi kwa nguvu zako
mwenyewe, hicho ni kiburi. Huko ni kukataa kushuka chini ili usaidiwe.
Ukiona kwamba kuna dhambi fulani
inakusumbua maishani mwako, acha kujitahidi kuiacha. Ndiyo maana ni muhimu sana
kuishi kwa kufanya toba mbele za Mungu kila tunapokosa.
Kwa hiyo, acha kujitahidi
kumpendeza Mungu kwa juhudi zako, badala yake fanya mambo yafuatayo:
- Kiri kwamba kuna dhambi maishani mwako.
- Kusudia kuacha kutenda dhambi hiyo tena.
- Tubu dhambi hiyo mbele za Bwana.
- Piga magoti mbele za Bwana umwambie Roho Mtakatifu, “Siwezi peke yangu Bwana. Nisaidie kushinda dhambi hii.” Hakuna dhambi isiyosalimu amri chini ya neema ya Bwana – iwe ni ulevi, uasherati, dawa za kulevya, uchawi, n.k.
- Endelea kuomba rehema na neema za Bwana ili azidi kukutia nguvu hatimaye utatoka nje kabisa ya shimo hilo.
Huu ni unyenyekevu mbele za Bwana.
Maandiko yanasema, Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa
wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye
hujishughulisha sana na mambo yenu. (1Petro 5:6-7).
Utakatifu katika dunia hii
unawezekana, si kwa sababu ya juhudi zetu, bali kwa sababu iko damu ya Yesu
inayotusafisha na udhalimu wote (1Yoh.1:9) na yupo Roho Mtakatifu anayetupa
kushinda na zaidi ya kushinda!
mtumishi mungu akubariki usikate tamaa.songa mbele kufundisha neno la bwana katika mtandao
ReplyDeleteAmen ndugu yangu. Mungu akubariki kwa kunitia moyo. Songa mbele pia kujitakasa kila kukicha.
DeleteKAZI UNAYOIFANYA MALIPO YAKE NI MUNGU PEKEE ATAKAYEKULIPA. HONGERA NA MUNGU AENDELEE KUKUTIA NGUVU
ReplyDeleteasante sana Noel. Mungu akubariki na kuendelea kukupa nguvu katika safari yetu ya kiroho.
Deletekuna kitu furani nahisi kuwa kinapatikana katika huduma yako! na kitu hicho kinanifanya nisichoke kutembelea blog yako! kwa ufupi unanitiamoyo sana katika safari ndefu hii tuliyonayo.....ambayo kadri tunavyomkaribia inakuwa ni fupi kuliko tulivyodhani!
ReplyDeleteNakushukuru vilevile emback kwa maoni ya kutia moyo. namshukuru pia Roho Mtakatifu kwa kutumia mafundisho haya kusema nawe. Ubarikiwe na Bwana tunapokuwa tunamalizia safari hii tuliyo nayo.
ReplyDeleteMtushi James MUngu pekee yake Akubariki hadi ushangaee kwani umenigusa sanaa na umenitiaa moyo katika wakovu,pia umeniapa kitu sasa nina kitu moyoni......naamu MUngu anasema imani huja kwa kusikia au kusoma nami nimesoma neno la MUngu JAMES, almight God bless you.
ReplyDeletenaomba roho mtakatifu azidi kunena nawe zaidi,...
PIA NAKUOMBA
UTUFUNDISHE VIJA TULIO WENGI MAHUSIANO SAHIHI YA KIMUNGU KATIKA MAANDALIZI YA UCHUMBA NA KUOA.
Ubarikiwe sanaa.
Franco asante kwa maoni na kwa kunitia moyo. Ashukuriwe Mungu wetu kwa kusema nawe kupitia masomo haya. Kuhusu masuala ya uchumba kama ulivyosema, nitafanya hivyo. unarikiwe.
ReplyDeleteBarikiwa James, nilikuwa naomba ufundishe kuhusu kusikia sauti ya Mungu, jamani hili swala linanitatiza sana wapendwa, hasa jinsi ya kupambanua hii ni sauti ya Mungu, shetani au mawazo binafsi hasa wakati mtu unaomba
ReplyDeleteNingeshukuru sana kama una mafundisho kama hayo unitumie hata kwa email nahitaji sana kujua
Barikiwa sana mtumishi hata kuliko Abraham
Star, nitaangalia kuhusu hilo suala la kusikia sauti ya Mungu, kisha nitajibu.
ReplyDeleteAsante mtumishi umenitia moyo sana barikiwa sana
ReplyDeleteubarikiwe na Bwana ndugu.
DeleteUbarikiwe mtumishi wa mungu
ReplyDeleteAmen ndugu. Bwana Yesu akubariki sana nawe pia.
DeleteUbarikiwe sana. Tafadhali endelea kutufunza.Asante Yesu
ReplyDeleteamen Joseph. Endelea kusonga mbele na Bwana Yesu. ukudaha. utarave unyuma. kukaku lakini ukudaha! mu muntu ukukiriywa u u njia ni nkaku ila ni ukwatia kwa nguu yong'e.
Deleteubarikiwe james na facebook upo.
ReplyDeleteAmen. Ubarikiwe nawe pia. Facebook nipo japo zaidi najihusisha na mijadala kati wa Wakristo na Waislamu kwa hiyo kwenye account yenyewe unaweza usione kitu sana. lakini inaitwa Jimmy John. Alama yake ni picha iliyochorwa kuashiria kupimana nguvu kati ya Yesu na shetani na pia kuna picha ya aliyeigiza Yesu akiwa msalabani.
ReplyDeleteUbarikiwe sana Mtumishi wa Mungu kwa neno la uzima
ReplyDeleteAmina. Nawe barikiwa pia.
DeleteBarikiwa sana mtumishi wa Mungu kwa neno lako la uzima
ReplyDeleteNawe pia Peter
DeleteAmina Mtumishi James
ReplyDeleteAmen
Delete