Thursday, November 2, 2017

Kuzaliwa kwa Maji na kwa Roho maana yake nini?


Image may contain: one or more people, ocean, outdoor and water

Mzee Nikodemo aliwahi kumwendea Yesu usiku akamwuliza maswali mbalimbali akihitaji kujua namna ya kufika kwenye ufalme wa Mungu.

Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa KWA MAJI na KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. (Yohana 3:5)

Nini maana ya kuzaliwa kwa maji?
Nini maana ya kuzaliwa kwa roho?


Kuzaliwa kwa roho ni rahisi kueleza. Lakini huku kuzaliwa kwa maji maana yake ni nini hasa?

Kile ninachoamini ni hiki:
Yohana alihubiri ubatizo wa toba.
Kutubu maana yake hasa sio kusema:
Nimesema uongo, nisamehe.
Nimeiba, nisamehe.

Kutubu maana yake ni kusema: Nimekuwa mwongo; nimekuwa mwizi; kuanzia sasa naacha kabisa mambo hayo.

Tena sio kusema kwa maana ya kumwambia mtu (japo kufanya hivyo hakuna ubaya), lakini ni kule kufanya uamuzi binafsi moyoni kwamba sitaki tena maisha mabaya; nataka kuanza kuishi maisha mema. Kutubu ni "kugeuka" kutoka kwenye mwenendo mbaya na kuingia kwenye mwenendo sahihi wa kimungu.


Kwa hiyo, ubatizo wa toba maana yake ilikuwa kama kuzaliwa upya KIMTAZAMO

Mtu alipomsikia Yohana akihubiri, aliguswa na kusema kwamba, kuanzia sasa naacha mambo maovu na kufuata mambo mema. Na jambo hilo likaambatana na kuzamishwa kwenye maji. Unazika ile tabia ya kale; unafufuka katika upya uliouchagua.

Ukishafufuka sasa, unahitaji fikra, mitazamo, mawazo na mfumo mpya wa maisha.
Sasa unaupata wapi?
Jibu ni kuwa unaupata kwenye NENO la Kristo.

Ndio maana ya maneno ya Yesu kuwa:
Maneno haya ninayowaambia ni Roho tena ni uzima (Yoh 6:63).

Kama ulikuwa mwizi, mwongo, mzinzi, muuaji, nk, Neno linakwambia:
Usiibe,
Usiseme uongo,
Usizini,
Usiue,
Usisengenye,
Usiogope,
Amini,
Mwambie Baba wa mbinguni,
Mpende jirani yako,
Heshimu mamlaka,
nk, nk, nk

Kadiri unavyoliingiza ndani yako Neno hili,
Unabadilika na kuwa kiumbe kipya. Tofauti kabisa na ulivyokuwa mwanzo, kabla hujaamua kugeuka.

Sasa unakuwa:
Unaona kama Yesu.
Unawaza kama Yesu.
Unaamua kama Yesu.
Unatenda kama Yesu.

Kimsingi, hata ndoto zako za usiku zinabadilika.

Huko kubadilika ndio kuwa kiumbe kipya

Barikiwa na Bwana Yesu.

5 comments:

  1. ni kweli kabisa na kwa kazi ya mungu inatustahili tukawe watu wa kujitolea jinsi mungu alivyo mtoa mwanawe wa pekee yesu kristo (yohana 3:16)nawe utaona makubwa ya mungu.imeandikwa katika kitabu cha wafilipi (4:6)msijisumbue kwa neno lolote;bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru;haja zenu na zijulikane na mungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen Sebastiane. Mungu akubariki ndugu.

      Delete
    2. Amen Ndugu, asante kwa Neno hili na Mungu wetu katika Yesu Kristu azidi kukubariki.

      Delete
  2. Asante kwa ujumbe huu mzuri barikiwa

    ReplyDelete
  3. Sija ona maana yakuzaliwa Mara yapili

    ReplyDelete