
Mzee Nikodemo aliwahi kumwendea Yesu usiku akamwuliza maswali mbalimbali akihitaji kujua namna ya kufika kwenye ufalme wa Mungu.
Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia,
Mtu asipozaliwa KWA MAJI na KWA ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. (Yohana
3:5)
Nini maana ya kuzaliwa kwa maji?
Nini maana ya kuzaliwa kwa roho?
Kuzaliwa kwa roho ni rahisi kueleza. Lakini huku kuzaliwa kwa maji maana yake ni nini hasa?
Kile ninachoamini ni hiki:
Yohana alihubiri ubatizo wa toba.
Kutubu maana yake hasa sio kusema:
Nimesema uongo, nisamehe.
Nimeiba, nisamehe.
Kutubu maana yake ni kusema: Nimekuwa mwongo; nimekuwa mwizi; kuanzia sasa naacha kabisa mambo hayo.
Tena sio kusema kwa
maana ya kumwambia mtu (japo kufanya hivyo hakuna ubaya), lakini ni kule
kufanya uamuzi binafsi moyoni kwamba sitaki tena maisha mabaya; nataka kuanza
kuishi maisha mema. Kutubu ni "kugeuka" kutoka kwenye mwenendo mbaya
na kuingia kwenye mwenendo sahihi wa kimungu.
Kwa hiyo, ubatizo wa toba maana yake ilikuwa kama kuzaliwa upya KIMTAZAMO
Mtu alipomsikia
Yohana akihubiri, aliguswa na kusema kwamba, kuanzia sasa naacha mambo maovu na
kufuata mambo mema. Na jambo hilo likaambatana na kuzamishwa kwenye maji.
Unazika ile tabia ya kale; unafufuka katika upya uliouchagua.
Ukishafufuka sasa, unahitaji fikra, mitazamo, mawazo na mfumo mpya wa maisha.
Sasa unaupata wapi?
Jibu ni kuwa unaupata kwenye NENO la Kristo.
Ndio maana ya maneno ya Yesu kuwa:
Maneno haya ninayowaambia ni Roho tena ni uzima (Yoh 6:63).
Ukishafufuka sasa, unahitaji fikra, mitazamo, mawazo na mfumo mpya wa maisha.
Sasa unaupata wapi?
Jibu ni kuwa unaupata kwenye NENO la Kristo.
Ndio maana ya maneno ya Yesu kuwa:
Maneno haya ninayowaambia ni Roho tena ni uzima (Yoh 6:63).
Kama ulikuwa mwizi,
mwongo, mzinzi, muuaji, nk, Neno linakwambia:
Usiibe,
Usiseme uongo,
Usizini,
Usiue,
Usisengenye,
Usiogope,
Amini,
Mwambie Baba wa
mbinguni,
Mpende jirani yako,
Heshimu mamlaka,
nk, nk, nk
Kadiri unavyoliingiza ndani yako Neno hili,
Unabadilika na kuwa kiumbe kipya. Tofauti kabisa na ulivyokuwa mwanzo, kabla hujaamua kugeuka.
Sasa unakuwa:
Unaona kama Yesu.
Unawaza kama Yesu.
Unaamua kama Yesu.
Unaona kama Yesu.
Unawaza kama Yesu.
Unaamua kama Yesu.
Unatenda kama Yesu.
Kimsingi, hata ndoto
zako za usiku zinabadilika.
Huko kubadilika ndio kuwa kiumbe kipya
Huko kubadilika ndio kuwa kiumbe kipya
Barikiwa na Bwana Yesu.
ni kweli kabisa na kwa kazi ya mungu inatustahili tukawe watu wa kujitolea jinsi mungu alivyo mtoa mwanawe wa pekee yesu kristo (yohana 3:16)nawe utaona makubwa ya mungu.imeandikwa katika kitabu cha wafilipi (4:6)msijisumbue kwa neno lolote;bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru;haja zenu na zijulikane na mungu.
ReplyDeleteAmen Sebastiane. Mungu akubariki ndugu.
DeleteAmen Ndugu, asante kwa Neno hili na Mungu wetu katika Yesu Kristu azidi kukubariki.
DeleteAsante kwa ujumbe huu mzuri barikiwa
ReplyDeleteSija ona maana yakuzaliwa Mara yapili
ReplyDeleteUshuhuda Wangu wa Kutoka Moyoni 💖
ReplyDeleteBaada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba mirefu, nilikuwa nimevunjika moyo kabisa. Alinizuia kwenye mitandao yote ya kijamii, akaondoka, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Karibu nikate tamaa, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitendea.
Siku moja, bosi wangu kazini aligundua jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dkt. Dawn. Dkt. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu angerudi kwangu ndani ya siku tatu. Kwa kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao wangu mkubwa, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa na nguvu na uzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akipenda na kunijali mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa katika miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dkt. Dawn, ambaye kwa kweli alifanya jambo lisilowezekana liwezekane. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya uhusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Matatizo ya utasa au bahati nasibu
Kesi za mahakamani au urejeshaji wa mali
Dkt. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurudisha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com