Friday, November 17, 2017

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 10==== SIKU YA 19 ====    (Waebrania 10:35-39)
Shin Sung-Kyung: * Shemasi Shin Sung-Kyung alicheza uchezaji wa kiroho
Nilikuwa naomba kwa kunena kwa lugha na mwili wangu ukajisikia kama moto unaowaka. Nje baridi ilikuwa kali sana na ilifikia hadi nyuzi hasi 10 na tulizima mitambo yote ya kupasha joto. Ndani ya kanisa kulikuwa baridi. Lakini Roho Mtakatifu alikuwa juu yetu kiasi kwamba baridi ile kali hata haikutusumbua kwa kuwa Bwana aligeuza miili yetu kuwa kama moto unaowaka. Ilitubidi kuvua makoti yetu mazito ambayo huwa ni kwa ajili ya kipindi cha baridi kali na tukabaki tu nguo za mikono mifupi.


Nilipigwa na moto wa maombi, kana kwamba jua kali lilikuwa linaniangazia. Tulikuwa tumelowa jasho kama vile tuko juani. Kwa kawaida, ningekuwa natetemeka kwa baridi, na kushindwa hata kumaliza mkesha wote nikiomba. Nilihisi maombi yangu yakizama ndani zaidi na zaidi. Baada ya kama saa moja hivi, mikono yangu ilianza kutembea bila mimi kuisogeza. Mtembeo huo ulikuwa wa aina tofauti na ilisogea kwa ulaini.

Hadi wakati huo, nilikuwa nikiweza kuona tu uchezaji wa mke wa mchungaji na Dada Bong-Nyo nami nilikuwa na shauku kubwa ya kupokea kipawa hicho. Niliomba, “Bwana, nisaidie na mimi niweze kucheza uchezaji wa kiroho! Ninatamani sana kipawa hiki cha kiroho. Bwana, natamani kwa dhati kabisa. Nisaidie nami nijue huu ni uchezaji wa namna gani.”

Kwenye maisha yangu yote ya Ukristo, sikuwahi kujazwa Roho. Nilikuwa mwenye dhambi sana na mara zote nilikuwa najisikia aibu mbele za Bwana. Kwa kipindi hiki, nikawa naziona nguvu za Roho Mtakatifu zaidi wakati wa maombi ya mkesha siku za katikati ya wiki kuliko hata wakati wa ibada ya Jumapili. Ibada ya Jumapili ni ya saa mbili tu ambazo ni za kumsifu Mungu, kuomba na mahubiri na pia matangazo. Zinaniacha nikiwa bado nina njaa ya kupokea zaidi.

Lee, Yoo-Kyung: * Kuingia mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu (Ufunuo 4:2-4)
Mara tu maombi yangu yalipoanza, pepo lenye mapembe matatu lilitokea. Nikapaza sauti, “Ewe pepo, kwa Jina la Yesu, toweka!” Na likatoweka. Nikasema kwa sauti, “Baba, ninakumisi!” Mara Yesu akaja huku akiita, “Mpendwa wangu Yoo-Kyung, je, umemwita Baba yako?” Nikajibu kwa ujasiri, “Ndiyo.” Bwana akauliza, “Ulipenda kumwita Baba yako?” Nikajibu, “Ndiyo, ninapenda sana.” Kisha akaniambia, “Haya ita!” Nikapaza sauti mfululizo, “Baba! Baba!”

Yesu akanichukua hadi Mbinguni. Napenda kupaa mawinguni kote kwenye Mbingu, huku nikiimba sifa kwa Yesu na kukanyaga maji ufukweni. Yesu akaniuliza, “Yoo-Kyung, unakumbuka ahadi niliyokupa jana?” Nikajibu, “Ndiyo, Yesu. Uliahidi kunionyesha Mungu Baba.” Yesu kwa uaminifu alitimiza ahadi yake na akanichukua kwenda kumwona Baba yake. Baba yetu ni mkubwa kuliko unavyoweza kufikiri! Anafika hadi juu kabisa ya mbingu za mbingu na anang’aa kuliko jua. Alikaa kwenye kiti kikubwa sana cha enzi.

Nilijawa na furaha, nikaimba sifa mbele za Mungu. Nikaimba, ‘Mbariki Bwana, moyo wangu’ na Mungu Baba akanisikiliza nikiimba. Alicheza kwa furaha na kila aliposogea, miali ya rangi zinazong’aa isiyoweza kuelezeka ilitoka kwake. Mbele ya Mungu Baba kulikuwa na kitabu kikubwa sana – kikubwa kuliko mlima – na alikuwa akiangalia humo.

Mikono mikubwa sana ya Mungu ilinyooshwa na akanigusa kichwa changu kwa upole. Ukubwa wa mikono yake hata hauelezeki. Upande wa juu wa mwili wa Mungu ulifunikwa kwa wingu lililoonekana kama ukungu. Yesu aliomba niendelee kuimba sifa, kwa hiyo nikaendelea. Mungu alifurahia sifa zile kwa kupiga makofi kwa mikono yake na kushika mikono yangu huku akiijongeza huku na huku. Nilijawa na furaha sana nikawa najongeza mikono yangu kwa kuizungusha. Yesu akanitahadharisha kwamba, “Kwenye uwepo wa Mungu Baba yetu usitupe mikono yako kiasi cha kushindwa kuitawala!” Alinifundisha kuinua mikono yangu juu huku kichwa changu kimeinamishwa kwa heshima. Baadaye, Yesu akanirudisha tena kanisani.

Lee, Haak-Sung: * Yapige mapepo kwa mikono yako!
Mchungaji wetu alikuwa bado anasumbuliwa na maumivu kutokana na mashambulizi ya mapepo yaliyopita. Alituambia kuwa tungeweza kabisa kuyakamata mapepo kwa mikono yetu usiku ule na akatuomba tuwe tayari kuyalipiza kisasi. Kwa umoja, tukapaza sauti, “Amen!” Ulikuwa ni muda wa ibada ya maombi, kwa hiyo niliomba kwa kunena kwa bidii.

Yesu alikuja kimyakimya. Alikaa mbele ya mke wa mchungaji na kusikiliza maombi yake kwa muda mrefu. Kisha akasogea karibu na mchungaji na kumwongelesha, “Mchungaji Kim, ni sehemu gani unajisikia maumivu?” Mchungaji akaonyesha maeneo ambako mapepo yalimuuma na kumparua. Yesu akajielekeza zaidi kwenye shingo ya mchungaji na mgongoni. Akawa anaendelea kupapasa maeneo hayo.

Baada ya Yesu kuondoka, niliendelea kuomba kwa kunena. Mapepo matano yakashambulia kwa pamoja. Nikakumbuka ujumbe wa mchungaji kuhusiana na kupambana na mapepo moja kwa moja. Nikanyoosha mkono wangu na kushika kitu. Nilipotazama kwa macho yangu ya rohoni, nikaona lilikuwa ni pepo la kike, limevaa gauni jeupe. Nilikuwa nimeikamata miguu yake na likawa halina nguvu zozote.  (Marko 3:15). Nikalizungusha kama pangaboi la helikopta. Ilikuwa ni ajabu kweli. Nikalizungusha na kulitupa kwenye kona. Shingo yake ikavunjika kwa sauti na likalia, “Aaa! Unaniua!” Nikakumbuka ujumbe wa mchungaji aliposema, “Ukiyaona mapepo, yapondeponde bila huruma! Ng’oa macho yao na uyakanyagekanyage!” Niliyapiga ngumi na mateke. Yalipiga kelele, “Oooh,! Aaa! Tuokoeni!” Yakakimbia. Ilikuwa inashangaza kweli. Mimi siogopi tena. Pamoja na kwamba mapepo hushambulia kwa makundi, niko tayari kupambana nayo.

Nililizungusha pepo jingine na kulitupa kule. Pepo ambalo Joo-Eun alilitaja, lilinisogelea, huku likizungusha macho yake meupe. Nililisubiri pepo hili hadi likanikaribia kabisa. Lilipojaribu tu kuingilia maombi yangu, nikang’oa macho yake bila huruma na kulipondelea sakafuni. Lilipokosa macho, likawa linatambaa sakafuni likitafuta na kulia, “Oh, hapana! Macho yangu! Macho yangu yako wapi? Nisaidieni kuyatafuta.” Hatimaye liliyapata, lakini lilipojaribu kuyarudishia kwenye mashimo yake, yalikuwa yamejaa uchafu. Liliyaweka vibaya na likakimbia.

Pepo la kiume lililovaa singleti iliyochanika, lilinijia taratibu kana kwamba linaangalia ishara kutoka kwangu. Nikawaza niliviringe kama mpira. Lilipokaribia kiasi cha kutosha, nilinyosha mkono wangu na kutia vidole vyangu viwili kwenye macho yake na kimoja kwenye pua yake. Nikalitupa kama mpira, na kulibamiza. Likateleza na kutoweka.

Kisha tena, pepo lenye nywele ndefu lililovaa gauni, likatokea. Lilinifanya nisisimuke kwa sababu lilikuwa likitoka damu kwenye macho na midomo. Nikalikimbilia na kulikamata. Nikalizaba vibao usoni na kulivamia. Nilijisikia mshindi kwelikweli! Nikaliambia, “Mkome kuja hapa! Mnasumbua enyi mapepo!” Baada ya kulipiga mfululizo, lilikimbia huku likilia kwa sauti. Hii ilikuwa inashangaza mno. Nilikuwa najisikia raha mno kuyapiga mapepo yale!

Nikaendelea kuomba kwa kunena kwa lugha ndipo pepo kubwa la kiume na lenye nguvu, ambalo lilivaa kinyago cha chuma lilinijia. Jicho moja tu ndio lilionekana kupitia kwenye kile kinyago na jicho lile lilijaa funza. Sikutaka kabisa kuligusa. Kwa hiyo nikasema kwa sauti, “Kwa Jina la Yesu, toweka kwangu!” Lakini halikuondoka badala yake likaanza kucheza kwa kujinyonganyonga. Likawa linapotea na kuonekana tena na tena, huku likicheza. Nikangoja hadi lilipotokeza na nikalikamata. Nikaanza kulizungusha, kisha nikalitupa kuelekea upande wa nyuma wa kanisa, na likatoweka. Wakati huo, Yesu alikuja na kunipongeza, huku akisema, “Mpendwa wangu Haa-Sung, hatimaye umeongeza kiwango chako cha kuyatesa mapepo haya. Najivunia wewe; najivunia sana.”

Muda fulani wakati wa ibada, niliona malaika wakimimina namna fulani ya mafuta juu ya kichwa cha mchungaji na mahubiri yake yakawa na nguvu sana. Pale mahubiri yalipohusu aina ya mapepo fulani,  mapepo yale yalijificha kwa siri kwenye kona mojawapo na kutetemeka huku sura zao zimejaa hofu.

Kim, Joo-Eun
Nilikuwa nikiimba, ‘Utukufu, utukufu, haleluya’ na mwili wangu ukajisikia kama moto. Kulikuwa na baridi kali sana kwenye chumba, lakini nilikuwa natoka sana jasho. Pepo lilelile ambalo Haak-Sung alipambana nalo, ambalo lilijirudishia macho yake vibaya, lilikuwa likilalamika, “Aah, bwana ee, ninateseka kwa sababu ya hili jinga, Haak-Sung. Ndiye aliyenisababishia haya.” Nikajibu, “Hiyo ni safi sana. Nafurahi sana kusikia hivyo.” Likaanza kulia na kusema, “Acha! Tafadhali acha kusema hivyo.” Nikasema kwa sauti, “Ewe pepo mchafu. Kwa Jina la Yesu, ondoka kwangu!” Likatoweka.

Kitu fulani kikaanza kuvuta nguo zangu, lakini sikuweza kuona chochote. Pia nikahisi nywele zangu zikivutwa kwa nguvu, na ninachomwa na kitu ubavuni. Nikaona kitu cha ajabuajabu kikibiringika hapo. Nikaliambia pepo hili jinsi nilivyojawa na hasira dhidi yake, na lenyewe likajibu, “Kweli? Safi, endelea kunichukia. Tafadhali, ninajaribu kukupeleka Kuzimu. Kwa nini unaomba kiasi hiki, ewe kijitu kisumbufu? Acha kuomba. Kwani unapata chochote cha kula unapoomba? Kwa nini unaomba?” Kwa haraka nikajibu, “Wewe! Ninapoomba, miujiza inatokea na ninajikusanyia thawabu. Ewe pepo, toweka kwangu!” Mara moja likajibiringa kuondoka kwangu.

Baadaye, nilishituliwa na joka kubwa lenye vichwa viwili. Niliogopa, nikatetemeka kwa hofu, maana lilikuwa kubwa kuliko hata nyoka aina ya anakonda na likaanza kuja kwangu. Nikapiga kelele, “Yesu, nisaidie! Tafadhali niondolee joka hili baya!” Yesu alikuja papo hapo na kulikamata joka lile. Akaanza kulizungusha kwa nguvu kisha akalitupilia mbali. Nikamshukuru Yesu naye akasema, “Mpendwa wangu Ufuta, kila unapoita Jina langu, nitakuja mara moja na kukusaidia, kwa hiyo usiogope. Cha kufanya tu ni kuomba kwa bidii.”

* Maombi yanayoweza kukufikisha Mbinguni
Leo niliona malaika wawili wazuri wakishuka taratibu. Walikuwa warefu zaidi kuliko binadamu, na kwa heshima wakasema, “Salamu dada Joo-Eun.” Mikononi mwao kulikuwa na vazi zuri linalong’aa, na lenye mabawa upande wa mgogoni. “Dada Joo-Eun, vazi hili ni zuri sana, si ndio?”
Nikajibu, “Nataka kulijaribu sasa hivi.” Wakanivalisha kwa upole. Malaika wale walisimama mmoja upande huu na mwingine huu na kunishika mikono. Nilijawa na nguvu na nikapaa kuelekea Mbinguni. Mara, tulivuka angahewa na dunia ikawa mbali sana. Tuliruka hadi kwenye mahali ambako nyota za galaksi ya ‘njia ya maziwa’ (milky way) zimetawanyika kila upande. Kulikuwa kunapendeza mno. Mikono yangu ikapumzika na nikaona mabawa ya kwenye vazi langu yakijaribu kupigapiga. Kwa namna fulani, tukawa tunashindwa kuendelea. Nikawaza, “Nilitaka kwenda hadi Mbinguni, sasa nini kimetokea tena hapa?” Malaika wakanieleza, “Sababu ni kuwa hukuomba kwa nguvu kiasi cha kutosha. Kwa hiyo hapa tu ndio tutaishia.” Nilivunjika sana moyo na tukaanza kurudi duniani.

Dunia ilionekana nzuri sana kutokea angani, lakini sikuamini kuwa ni sayari ndogo kiasi hicho. Leo ilikuwa siku niliyokosa fursa, lakini nilijifunza jambo muhimu kuhusu maombi. Ili kusafiri hadi Mbinguni kwa maombi, inanibidi kukusanya nguvu nyingi kwa ajili hiyo.

Dada Baek, Bong-Nyo: * Kwenda matembezini na Yesu
Wakati ninaomba, Yesu alinichukua kwenda kutembelea Kuzimu. Mara nguzo kubwa sana ilitokea na nikawa naona kama kuna vitu vinatembea kwenye nguzo hiyo. Nilipotazama kwa makini zaidi, niliona maelfu ya watu yasiyo na idadi wamenaswa kwenye nguzo ile. Walikuwa uchi na wamefungwa kwa nguvu sana kiasi kwamba hata kusogea hawawezi. Wadudu weupe walikuwa wanakula nyama za miili yao, huku wao wakipiga kelele kwa maumivu makali. Mara nyama yote inapoliwa, mifupa tu inabakia. Kisha nyama inarudi tena na mzunguko ule unajirudia tena.

Nilimwuliza Bwana kuhusu dhambi ambazo watu hawa walitenda na Yeye akanijibu, “Hawa ni watu ambao huhudhuria ibada ya asubuhi kwa muda mfupi, kisha wanatoa sababu ya kuondoka na kwenda kujifurahisha na dunia, kisha wanaishia kufa kwa ajali za magari. Pia, kuna watu ambao huhudhuria ibada, lakini wanapokuwa peke yao wanakunywa pombe na wakati mwingine wanatembelea baa, na vilevile wale ambao wanahudhuria ibada tu kama kutimiza wajibu, bila hasa kukutana na Bwana.”

Sikuweza kuvumilia hali ile ya kutisha, kwa hiyo nikamwomba Yesu aniondoe pale. “Sawa, basi twende Mbinguni sasa,” alisema. Alinishika mkono tukaanza kupaa kwenye anga, hadi tukafika kwenye Bustani ya Edeni. Yesu na mimi tulishikana mikono kwenye bustani na tulifurahia sana kutembelea pale. Alivyoona jinsi nilivyokuwa na furaha, Yesu akaniambia kwa upole, “Mpendwa wangu Bong-Nyo, afya yako si nzuri sana. Kwa hivi sasa mambo ni magumu sana kwako, lakini inabidi uvumilie.” Mara zote maneno yake hunifariji na kunifanya nitokwe machozi. (2 Wakorintho 1:5).

Mchungaji Kim, Yong-Doo: * Kama shoti ya umeme
Nilikuwa bado nina maumivu makali kutokana na mashambulizi ya mapepo, lakini Mungu kwa neema yake aliniwezesha kutoa mahubiri na kuimba sifa huku nikiwa na kiwango cha maumivu ambacho niliweza kukistahimili. Kwa nguvu zangu zote, niliomba huku mikono yangu ikiwa imeinuliwa juu. Nilianza kuhisi kama shoti za umeme zikipita kwenye mikono yote. Umeme ule ulikuwa wenye nguvu na uliendelea kupenya kila sehemu ya mwili wangu.

Mungu alimimina mafuta ya upako kwangu, lakini maumivu yangu ya mwili hayakupungua. Kuomba huku mikono yangu ikiwa imeinuliwa juu ilikuwa ni vigumu sana. Kulikuwa na nyakati ambapo nilisikia maumivu kama vile nimechomwa na sindano. Kisha ninashusha mikono yangu. Maumivu yakipungua, nainua tena mikono kuomba na nilirudia hivi mfululizo.

Niliazimia kuomba huku mikono yangu imeinuliwa juu. Ghafla, kiganja changu cha kushoto kilijongea kuelekea nje. Kisha kikashuka na ndani ya saa moja, mkono wangu wa kushoto ukageuka kabisa kutoka kuangalia ndani hadi kuangalia nje. Ilichukua kama saa tatu kwa mkono wangu wa kulia nao kuhama kutoka kuelekea ndani hadi kugeukia nje. Nilibaki kwenye hali hii kwa muda. Mikono yote miwili ikawa imepooza na nikawa naomba katika hali ile kwa zaidi ya saa nne. Yalikuwa ni mateso makali.

* Kutubu kila dhambi
Sikujua kama jambo hili lilitoka hasa kwa Bwana. Kwa hiyo, nikasema kwa sauti, “Shetani, ondoka kwangu! Niache!” Yesu hakusema neno. Badala yake aliendelea kumimina furaha, amani na moto wa Roho Mtakatifu kwenye mwili wangu uliokuwa ukitetemeka. Nikaanza kukumbuka dhambi za nyuma kwenye maisha yangu, hivyo nikaanza kutubu. Nikatubu kuhusu maisha yangu yasiyostahili ya kiuchungaji na kupenda kwangu sana kucheza michezo. Dhambi ile ilinifanya nisimtumikie Bwana kikamilifu. Nilijaribu kutubia kila dhambi. Huku mikono yangu yote ikiwa imepinda, niliendelea kuomba kwa kutumia kila kitu nilichokuwa nacho, hadi nikaanguka kutokana na maumivu.     

Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu.” (Warumi 2:5)

Kwa kweli ninapenda michezo, na ninapocheza, nakuwa makini nayo kweli, kiasi cha kumsahau Bwana. Jambo hili lilimuumiza. Ulevi wangu ulikuwa juu ya michezo mingi, ikiwa ni pamoja na kuviringisha tufe (bowling), soka, na hasa mpira wa vinyoya. Kwa kweli nilipenda kwa dhati kujiweka sawa kimwili, lakini nilipoteza muda mwingi mno kwenye michezo. Mara nyingi ningetokana kwenda kwenye uwanja wa mpira wa vinyoya, karibu na “mineral spring water resort”. Pale, niliondoa uchovu wangu wote. Kucheza michezo si jambo baya, lakini mambo mengi tunayofanya yanaweza kuteka kabisa akili zetu. Kadiri ninavyozidi kuzama kwenye ulimwengu wa roho, ndivyo ninavyotambua kwamba mapenzi yangu kwenye michezo yalininasa na kunifanya niwe na ulevi wa michezo. Vikwazo hivi viliendelea kurundikana na kuathiri ukuaji wangu wa kiroho. Nililia na kutubia kila kitu.

Wakati mmoja kwenye maisha yangu, washirika wangu waliacha kuhudhuria kanisani na kwenda kwenye makanisa mengine nikabakiwa na mzee mmoja tu. Kanisa lilikuwa halikui kabisa. Kwa bahati nzuri, mchungaji mmoja kutoka Seoul, ambaye namjua vema, alinipa nafasi ya kuwa mchungaji kiongozi wa kanisa lenye waumini mia kadhaa. Niliwaza, “Naam, hii ni nzuri!” Nikajiandaa kukubali jambo hilo. Siku moja kabla ya kuondoka, wakati nikiomba, Yesu alinitokea huku ameshikilia kiboko kirefu kilichoanzia mbinguni hadi duniani. Yesu akaniamuru nipige magoti na kuinama. Nikatii. Yesu alinipiga kwa kiboko kile kwa nguvu sana. Lakini hakikuniletea maumivu badala yake nilisikia upendo wa Bwana kwangu. Lakini uso wake ulijaa huzuni na alitoa machozi. Yesu akasema, “Mtumishi wangu mpendwa, ungependa kufanya nini washirika wako wakiongezeka? Mchungaji Kim Yong-doo! Mchungaji Kim, utatoa sadaka aina gani kwa ajili ya madhabahu?” Sikuwa na jibu la kumpa Bwana. Nilijua jibu langu lingedhihirisha ukweli wa aibu ya moyo wangu.

Wachungaji wanapokusanyika pamoja, kila mmoja wetu huongea kuhusu ‘ongezeko la haraka la kanisa’, ‘ni watu wangapi wanakusanyika’, ‘imechukua miaka mingapi kujenga kanisa’, na ‘ni mchungaji yupi ndio anasifika zaidi ya wengine.’ Nilijua kuwa haya ndio majibu yaleyale ambayo ningetoa. Huku nimepiga magoti na kichwa changu kimeinama mbele ya Bwana, sikuweza kusimama na nilijawa na fedheha. Sikuweza kufanya lolote. Kwa hiyo, nililia tu. Kwa upole, Yesu alipapasa mgongo wangu na kunifariji  kwa wema wake. “Mtumishi wangu mpendwa, nimewahi kutaka sadaka ya ujenzi wa jengo? Nimewahi kutaka uamsho kuhusiana na idadi ya washirika? Usiyaweke mambo haya kwenye moyo wako, lakini nataka ufuate yale ninayoyataka. Nataka wewe uwatafute na kuwaleta kondoo wangu waliopotea, na haijalishi ni idadi gani, iwe ni mmoja au mia moja. Nataka uwatunze kwa bidii. Uwe mwaminifu kwa mambo madogo. Usivutwe na mambo makubwa yanayokuzunguka, lakini omba kwa bidii na subiri muda wangu. Mwisho, usikate tamaa.”

Mke wa mchungaji, Kang, Hyun-Ja: * Maombi ya moyo uliopondeka
Leo, mikono yangu nayo ilikuwa inapindishwa, kama ya mchungaji wetu. Yesu alitufafanulia kupitia kipawa cha unabii cha Joo-Eun, akisema kuwa  kwa mchungaji na mke wake, itakuwa vigumu zaidi kufunguliwa macho ya kiroho. Itakuwa ni mchakato wenye maumivu sana. Kuna aina nyingi tofauti za maombi, lakini yenye nguvu zaidi itakayoharakisha mchakato huo ni ya kuomba toba kwa machozi.

Kulinganisha na wengine, mimi huwa sitoi machozi mara nyingi. Inaweza kuwa ni kwa sababu ya vile nilivyo kitabia. Hata kama nikiomba sana na kumwita Bwana, siwezi kulia, japo nimeshajaribu mara nyingi. Nilimwomba mchungaji anisaidie naye akasema sina moyo uliopondeka. Alinitia moyo nimwombe Bwana anipe moyo uliopondeka.

Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. (Zaburi 34:18)

Mchana wote niliomba kwa moyo uliopondeka na wenye toba na Bwana akamimina kwangu machozi ya toba. Roho Mtakatifu alinifunika kwa machozi na jasho. Nilikabwa kwa kulia kwa machozi wakati nikilia kwa nguvu. Huku akiongea kupitia Joo-Eun, Mungu aliniambia kuwa toba yangu ya machozi imekubalika mbele zake.

Kutokana na kazi yote ile tuliyokuwa tunafanya, adui mara zote alikuwa akitafuta mwanya wa kushambulia. Tusingeweza kujisahau. Kwa vile aina za mapepo zilikuwa zikidhihirika kupitia washirika vijana waliokuwa na kipawa cha macho ya rohoni, ilibidi kujivika silaha kikamilifu kwa njia ya maombi. Hatujui ni kwa nini Yesu alituchagua sisi kupigana vita hivi vya kufa na kupona, maana sisi tu wadhaifu tu. Yesu alituambia, “Ninyi wanakondoo wadogo wa Kanisa la Bwana mnaweza kuendeleza imani yenu kupitia tu kupambana na mapepo waovu. Niaminini. Nishikeni mkono na msonge mbele. Daima nitakuwa nanyi, msiogope.”
………..

UNAENDELEA…

No comments:

Post a Comment