Friday, November 29, 2013

Jiandae kwa Kurudi kwa Bwana! - Sehemu ya 1
Dada Barnarda Fernandez alichukuliwa katika Safari ya Mbinguni mara 2 na Bwana Yesu. Alionyeshwa thawabu za mbinguni zilizoandaliwa kwa ajili ya watakatifu wa Bwana, unyakuo, Karamu Kuu na taji za uzima. Pia aliona hali ya Kanisa, hukumu ijayo na roho zilizopotea zilizoko kuzimu. Ufuatao ndio ushuhuda wake:


……………………………….

Safari yangu ya kwanza

Nilikuwa sijisii vizuri asubuhi ile, hivyo mume wangu alikataa kwenda kazini ili abakie na mimi. Nilimwambia kuwa sikuwa peke yangu. Baada ya kuondoka, nilihisi kuwa ninakufa. Kwa hiyo, niliamua kuwapigia simu baadhi ya marafiki zangu, pamoja na mama mkwe wangu. Mama mkwe wangu alijibu: "Bernarda, Mungu atakubariki leo, usiogope." Jibu lilelile lilikuja kutokea kwa kaka mwingine katika Kristo ambaye naye nilimpigia simu. Lakini yeye aliongezea kusema,  "Bernarda amka toka kitandani kwako na umsifu Bwana; mlilie na umtukuze Yeye." 

Licha ya kukosa kwangu nguvu, nilimlilia Bwana na nikisema: "Bwana, Wewe ndiwe nguvu zangu. Njoo unisaidie." Nilijaribu kunyanyuka lakini nguvu ziliniishia. Sauti yangu haikusikika tena. Lakini moyoni mwangu nilikuwa ninamlilia Bwana anisaidie kwa kuwa nilikuwa najisikia kwamba ninakufa. Ghafla, chumba changu kiliangazwa na nuru iliyoonekana kama moto. Mara hofu yangu ikatoweka na nikaona malaika wakishuka na kutembea kwenye chumba changu. Niliwasikia wazi wakiongeleshana. Ghafla tena, alitokea mmoja aliye mzuri sana kuliko wale malaika. Alivaa vazi jeupe huku akiwa na ukanda wa dhahabu. Kifuani mwake kuliandikwa maandishi ya dhahabu:  "MWAMINIFU NA WA KWELI." Uso wake ulionyesha upole na Upendo. Yesu Kristo alikuwa amesimama mbele yangu; Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Jina lake libarikiwe! 

Yesu alinisogelea, akagusa kichwa changu na kuniambia: "Mimi ndimi Yesu niliyekufa kw ajili yako. Tazama alama hizi kwenye mikono yangu. Bado ziko hapa kwa ajili yako. Nimeshuka kutoka kwenye kiti changu cha utukufu ili kuja kuzngumza nawe. Yako mambo mengi maishani mwako yanayotakiwa kuwekwa sawa. Wewe ni mvivu na una hasira za haraka. Mbali na hivyo, sitaki Wakristo 25% wala 95%, bali 100%. Kama unataka kwenda mbinguni, ni lazima uwe mtakatifu kama mimi nilivyo mtakatifu. Nimekuja ili nikuchukue katika safari." 

nikamwuliza, "Bwana, ni safari ya kimishenari?" Akajibu, "Hapana." Kisha akanishika mkono, akaniinua; na kuzungumza nami kwa upole na Upendo. Akanileta hadi kwenye madirisha yangu. Akalitazama jiji la New York.  Niliona huzuni kwenye uso wake. Alilia na kusema, "Neno langu linahubiriwa vizuri, lakini watu hawasikii. Dhambi ya mji huu imeshamfikia Baba Yangu.

Mji ulikuwa umejaa mashoga; na miongoni mwao ni wanasiasa. Bwana akaniambia, "Ni Sodoma nyingine, lakini Mimi ni hai na hukumu za Baba Yangu zitauangukia mji huu muda si mrefu." Kisha nikapiga magoti mbele za Bwana huku nikilia naye akaniambia, "Usiogope. Hukumu itakaposhuka kwenye dunia hii, Kanisa langu halitakuwapo tena duniani." 

Akanirudisha tena kitandani kisha akaniambia nimpigie simu kaka mmoja wa kanisani kwetu. Aliniambia nimwambie kuwa roho yangu itatoka kwenye mwili wangu; na kwamba wasipeleke mwili wangu hospitalini au kwenye maandalizi yoyote ya mazishi. Badala yake wamwambie mume wangu amwamini Yeye aliye Ufufuo na Uzima. (Yohana 11:25). Bwana akaniambia tena, "Mimi nitoaye uzima, nitaichukua roho yako; lakini utarudi kuja kuwaambia watu waniamini kikamilifu. Yeye aniaminiye Mimi hatakufa kamwe." (Yohana 11:26). Alinyoosha mikono yake na nikaona mwili wa kiroho ukitoka kwenye mwili wangu wa nyama. Nilikuwa nimevaa vazi jeupe na nilikuwa ninang’aa kama Bwana. Akaniambia, "Tazamak! Huu ndio mwili ambao Wakristo wanaotii Neno langu watakuwa nao muda mfupi ujao." 

Nilitambua kuwa nilikuwa na uwezo wa kupenya ukutani. Bwana ambaye alikuwa amenishika mkono alisema,  "Tazama!" Nilipogeuka, niliuona mwili wangu ukwa hauna roho. Alinieleza kuwa mwili wangu wa nyama hauna thamani yoyote; ni mavumbi tu; na kwamba, baada ya kufa unarudi kuwa mavumbi tena kama mwili mwingine wowote wa nyama. Akaongeza kwamba, ule mwili mpya niliokuwa nao ulikuwa na utukufu ambao ni roho aliyompa mwanadamu. Nilidhani angenipeleka moja kwa moja mbinguni, lakini haikuwa hivyo. 

Tulishuka kupitia shimo chini ya dunia, na tulipokaribia sehemu
fulani, nilianza kuhisi harufu mbaya sana. Nikasema, "Bwana, sitaki kwenda sehemu hiyo." Lakini tuliingia ndani. Kulikuwa na giza sana. Niliwasikia watu wakiteseka, wakilia na kupiga kelele. Tulipofika mwisho wa shimo, tulikaa kwenye jiwe na Bwana akaniambia, "Tazama!" Niliona watu wakiteseka. Kuzimu, watu wanalia muda wao wote, na hakuna anayemjali mwingine.

Wapendwa kaka na dada zangu, nilitambua kwamba KUZIMU NI HALISI. Nililia na kulia. Na nilipomtazama Bwana, aliniambia, "Yashikilie hayo uliyoyaona na usiyasahau."  Watu walikuwa wakilia, "Ooh! O0h! Ni milele! Ni milele! Maumivu na chuki milele na milele!"

I turned toward the Lord and asked Him: "Is there anyone from my family in hell?" He answered me "I will not allow you to see a member of your family."  So I asked Him, "is there anyone that I know here?" "Yes and I will allow you to see him." Suddenly I saw a young man coming from the depths of the hell: It was Alexander. 

Nilimfahamu kijana mmoja kwenye krusedi ambayo mimi na mume wangu tulihudhuria kule Jamuhuri ya Dominika. Wakati wa krusedi
ile, nilisikia sauti ikiniambia, "Inuka ukutane na Alexander ambaye anapita hapo. Mwambie asikatae ujumbe huu, maana ninampa nafasi ya mwisho." Hii ilikuwa ni sauti ya Bwana, japokuwa sikumwona Bwana wakati ule. Nilimwambia Alexander kile ambacho Bwana aliniambia; na hivi ndivyo alivyojibu: "Nyie Wakristo wote ni wapumbavu. Mnadanganya watu kwa kuwaambia kwamba Yesu Kristo anarudi. Mimi, Alexander, siamini kuwa hilo ni kweli." Nikamwambia, "Alexander, Mungu hutoa uhai na kuuchukua pale atakapo. Alexander, utakufa muda si mrefu." Akajibu, "Siwezi kufa na ujana wote huu. Bado nina miaka mingi ya kula raha kwenye dunia hii."

Kweli kabisa hiyo ilikuwa ni nafasi ya mwisho kwa Alexander.  Wiki tatu baadaye, Alexander alikufa akiwa amelewa. Aliishia kuja kwenye sehemu hii ya mateso nilikomwona (kuzimu). Biblia inasema wazi kwamba walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (Wagalatia 5:21). 

Nilipowaangalia watu kuzimu, nilimwona Alexander anashambuliwa minyoo mikubwa miwili. Alikuwa akipiga kelele, "Uwii! Uwii! Uwii!" Alikuwa anateswa. Alinitambua na kuniambia, "Nilidharau nafasi yangu ya mwisho. Niko hapa leo, nikiteseka. Tafadhali, utakaporudi duniani, nenda nyumbani kwetu uwaambie wamwamini Yesu Kristo na kutii Neno lake, ili wasije kuja kwenye sehemu hii ya mateso."
Bwana alinionyesha maelfu ya watu waliokuwa wakiteseka kuzimu, na akasema, "Unaona, baadhi ya hawa watu walinijua Mimi walipokuwa duniani. Na bado wako watu wengi duniani ambao wanatembea mitaani bila kujua watakwenda wapi. Tambueni kwamba njia ya kuingia mbinguni ni nyembamba, na bado itakuwa nyembamba hata zaidi. Kutakuwapo na majaribu duniani ili kwamba muweze kuwa safi kama dhahabu, lakini msiogope maana Mimi ninawatangulia kama shujaa mwenye nguvu." 

Nikamwuliza, "JE, KUNA WAKRISTO HUMU KUZIMU?" Akajibu, "Ndiyo. Unajua ni kwa nini? Waliniamini lakini hawakuenenda kulingana na Neno langu. Wako Wakristo wengi na aina hiyo ambao hujifanya wanyenyekevu wawapo TU kanisani, mbele za wachungaji na familia zao. Lakini wanajidanganya sana. Macho ya Baba Yangu yanaona kila kitu na anaelewa kila neno, kokote uliko. Waambie watu Wangu ni wakati wa kuishi maisha matakatifu mbele za Baba Yangu, mbele za ibilisi na mbele za ulimwengu. Shetani asipate haki ya kushitaki watu Wangu; na pia ulimwengu usinyooshe vidole kwa watu Wangu." (1 Petro 1:14-16). 

Kisha tulienda kwenye ziwa la moto. Lilikuwa linanuka sana, na Bwana akasema, "Unachoona pale ni ziwa la moto, ambalo liko tayari kwa ajili ya ibilisi, nabii wa uongo na Mpinga Kristo. Sikuandaa sehemu hii kwa ajili ya wanadamu, lakini wale wasioniamini Mimi kama Mwokozi wao na wale wasioishi sawasawa na Neno langu wataenda pale." (Ufunuo 20:14). 

Hapo nilimwona Yesu akilia na akaniambia tena, "Wale waliopotea ni wengi zaidi ya wale watakaoingia Mbinguni." Alinionyesha idadi ya watu waliokuwa wakifa kila dakika na kusema,  "Tazama! Ni wangapi wanaopotea! Kanisa langu limelala licha ya ukweli kwamba limepokea nguvu Zangu; lina Neno langu na Roho Mtakatifu, lakini limelala. Duniani wako watu ambao wanafundisha kwamba kuzimu hakupo. Nenda kawaambie kuwa mahali hapa ni halisi.

Niliweza kuhisi joto kali. Tuliondoka kwenye sehemu ile na kwenda Mbinguni. Tulipaa juu zaidi na zaidi na kupita mbingu ya pili. Alinionyesha jua na nyota na kusema,  "Angalia nyota hizi. Kila moja nimeipa jina lake. Unaona jua hili? Ni kwa uweza wangu linatoa nuru yake kwa wema na waovu. Lakini siku inakuja ambapo jua halitatoa tena nuru. Kila kitu kitakuwa giza." (Matendo 2:20).

Tulipaa juu Zaidi na kufika kwenye Ufalme wa Mungu. Niliona
nyumba nzuri sana. Kuta za nyumba zile zilikuwa ndefu sana, za dhahabu tupu na vito vya thamani. Kulikuwa na malango kumi na mbili. Sikujua kama niingie au la, lakini Bwana alinitazama na kusema, "Unapenda kuingia ndani?" "Ndiyo Bwana! Nataka sana kuingia."  "Basi ingia, maana Mimi mwenyewe ndiye mlango" (Yohana 10:9).

Wakati huo niliingia kupitia mlango wa thamani sana na nikaona bustani yenye maua mazuri sana. "Ungependa kwenda kwenye bustani? Basi ingia, maana nimeandaa haya kwa ajili yako na watu Wangu." Nilipoingia, nilianza kupanga baadhi ya maua katika mafungu. Nilikimbia bustanini kama kasichana kadogo. Maua niliyoshikilia yalikuwa na rangi nyingi na harufu nzuri mno. Bwana alimwita mmoja. Alikuwa ni malaika, mwenye nguvu na mzuri kiasi kwamba siwezi kumwelezea. Bwana aliniambia, "Unamwona huyu? Huyu ni malaika mkuu, Mikaeli. Yeye ndiye anayeongoza jeshi langu. Tazama tena!" Niliona jeshi lenye nguvu juu ya farasi na Bwana akaniambia, "Hili si jeshi la wanadamu, bali ni Jeshi la Baba Yangu. Jeshi hili liko kwa ajili ya Wakristo ambao KWELI wamezaliwa upya. Msiogope, maana lina nguvu zaidi ya lile lililoko duniani.

Kisha akanionyesha malaika mwingine. "Huyu ni mjumbe wa Wakristo wanaotii Neno langu." Nilifurahi kusikia hivyo. Yesu akaniambia, "Sikiliza kwa makini! Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Musa, Mungu wa Eliya, Yeye aliyesababisha moto kushuka kutoka mbinguni; sijabadilika. Nitakuonyesha hali ya maisha ya watu wangu katika siku hizi za mwisho zilizobakia." Bwana akaniambia, "Uwe makini na mambo ninayoenda kukuonyesha." 

Nikaona Wakristo ambao walikuwa dhaifu na wamechoka. Bwana akaniuliza swali hili:  "Unaamini kuwa naweza kulichukua Kanisa katika hali yake ya namna hii?" Akaniambia, "Wakristo nitakaowachukua watakuwa na utukufu, washindi, hawana
mawaa, hawalaumiwi. Miongoni mwa watu wangu kuna uongo, hakuna upendo, watu wangu wamegawanyika. Nimekuonyesha hali ya Wakristo katika siku hizi za mwisho. Sasa nitakuonyesha jinsi kanisa la kwanza lilivyoishi. Wale akina kaka na akina dada walikuwa wamejawa na utukufu wa Mungu. Walifunga na kuomba mara kwa mara; walihubiri Neno Langu bila woga. Lakini Wakristo wa sasa wanafikiri Mimi nimebadilika. Pia wanadhani Roho Mtakatifu amebadilika. Kosa kubwa la Wakristo wa leo ni kwamba wanaishi maisha ya mazoea, yaliyopangwa na wanadamu. Hivyo, wamesahau kwamba
ujumbe unatoka kwa Roho Mtakatifu na kutoka juu. Waambie watumishi wangu, wachungaji, muda umeshafika wa kuachana na program zile za kimazoea. Wakifanya hivyo, mtaziona nguvu za Mungu katikati yao, Roho Mtakatifu ambaye alidhihirishwa kwenye Kanisa la kwanza. Atatenda ishara, miujiza na maajabu mengi sana; na kusababisha wafu kufufuka. Roho Mtakatifu bado ni yuleyule. Ni ninyi ndio mliobadilika."


Wakristo, ni wakati wa kurudi kwenye maisha ya Kanisa la kwanza. Niliondoka kwenye bustani hii nzuri na kwenda kwenye mtaa mzuri sana wa dhahabu na Bwana akasema, "Gusa! Ndiyo. Ni dhahabu tupu. Nenda kawaambie wanangu kwamba HIVI KARIBUNI SANA wataenda kutembea kwenye mitaa hii ya dhahabu kwa mkono wa Yeye atoaye uzima." (Ufunuo 21:10-15).

Ah! Inafurahisha sana kutembea kwenye zile barabara za dhahabu! Baada ya hapo niliona Kiti cha Enzi cha fahari kubwa kikiwa kimezungukwa na malaika wengi, Malaika wakuu na Maserafi. Wakati wote walikuwa wakimsifu Mungu, ambaye alikuwa amekaa kwenye hicho Kiti cha Enzi, wakisema, "Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu; mbingu nan chi zimejaa utukufu wake. Amen!" "Muda umefika wa kuinua mikono mitakatifu kwangu na kunisifu Mimi."  

Niliona mto wa maji ya uzima ukitiririka kutoka kwenye Kiti cha Enzi. Niliona mti wa uzima na upande wa pili niliona upinde wa mvua na bahari kama kioo. Nikamwuliza Bwana, "Ni nani yuko kwenye Kiti cha Enzi?" Akanijibu, "Ni Baba Yangu, Bwana wa Majeshi." Nikamwambia, "Naweza kumwona Baba?" "Hapana. Muda haujafika bado," Bwana akanijibu. 

Japokuwa sikumwona Baba, yule aliyekuwa kwenye Kiti cha Enzi alikuwa Mwenye Nguvu. Niliona radi na mwanga kama radi ukitoka kwenye Kiti cha Enzi na nikasikia sifa. Yesu akaniambia, "Unazisikia sifa hizo? Hizi ni sifa za wale waliokombolewa." Niliona malaika saba. Kila mmoja wao alikuwa ameshikilia chombo cha dhahabu. Na
malaika saba wengine walikuwa wameshikilia tarumbeta. Nikauliza, "Bwana, hawa malaika ni nani?" Bwana akajibu, "Vyombo hivyo saba ambavyo malaika wameshikilia vimejazwa hasira ya Mungu. Si muda mrefu itamiminwa mara tarumbeta zitakapopigwa. Kanisa langu, (wale Wakristo wanaoishi kulingana na mapenzi ya Baba Yangu) watanyakuliwa. Hawatakuwa duniani tena wakati wa dhiki kuu. Kabla Mpinga Kristo hajajidhihirisha, huyu mtu wa dhambi, Kanisa langu litasikia tarumbeta ya mwisho, nao watanilaki mawinguni.” (1 Wathesalonike 4:16).

Nilikuwa pale, mpendwa rafiki yangu, mbele ya Kiti Kuu cha Enzi, na sikuwaza kabisa kuhusiana na muda. Yesu alinionyesha jinsi Kanisa lake (waamini wa kweli) watakavyonyakuliwa! Niliona katika maono, maelfu ya watu wakipotea. Hili lilitokea duniani kote; na TV na redio zilitangaza kupotea huko kwa watu. Magazeti, yakiwa vichwa vikubwa vya habari kwa rangi nyekundu, nayo, nayo yalitangaza habari hizo. Bwana akaniambia, "Habari hizi zitatokea hivi karibuni. Kama hukumu za Baba Yangu hazijaja ulimwenguni, ni kwa sababu ya Wakristo waaminifu; wale wanaonipenda Mimi kwelikweli.

Baada ya hapo, niliona kutokea kwa mtu wa kuasi (2 The 2:3). Alikuwa akiwaambia wakaao duniani, "Nawaletea amani na usalama," na mara watu wakasahau mambo yaliyokuwa yametokea. Yesu aliniambia, "Tazama kwa makini!" Niliona katika maono, malaika saba wenye vyombo saba. Rafiki mpendwa, kilichokuwa kinatokea ni vigumu kukielezea. Niliona malaika wale wakimimina hasira ya Mungu duniani kutoka kwenye vile vyombo saba. Tarumbeta zilianza kupigwa. Mungu alikuwa akimimina hukumu yake juu ya wakaao duniani, na nchi nzimanzima zikatoweka! Bwana akaniambia,  "Ona! Watu wote hawa walikuwa sehemu ya Kanisa Langu; na baadhi yao walikuwa wachungaji." Kwa sababu sikuelewa hili kikamilifu, nikamwuliza Bwana, "Inakuwaje watu wako wengi kiasi hiki wakawa kwenye dhiki kuu? Kwa nini kuwepo na wachungaji miongoni mwao; wale waliohubiri Neno lako? " Yesu akajibu, "Ndiyo. Walifundisha Neno Langu, lakini walikuwa hawaishi sawasawa na Neno hilo." Kisha Bwana akaniruhusu kuona kundi jingine la wachungaji. Akaniambia, "Wale wachungaji walikuwa hawafundishi Neno Langu kama lilivyoandikwa. Walidhani kwamba Neno Langu liko nyuma ya karne yao. Walikuwa wanawapendelea sana wale waliokuwa wanatoa sana zaka, maana shauku yao kubwa ilikuwa ni kupata tu vitu. Nenda kawaambie watumishi Wangu kwamba Mimi ndiye niliyewaita, na kwamba fedha na dhahabu ni mali yangu; nami ninawapa kwa kadiri ya ukuu na utukufu Wangu. Waambie wafundishe Neno langu kama lilivyoandikwa. Wako wengi wanaolipa Neno langu maana nyingine. Neno langu ni Neno langu na hakuna anayeweza kulibadili. Ni lazima lifundishwe kama lilivyoandikwa. Wako wengi miongoni mwa watu Wangu wanaopotosha Neno Langu kwa faida yao." 

Baada ya hapo, tuliingia ndani ya Yerusalemu Mpya na Bwana akaniambia, "Unachokiona ni paradiso." Niliwaona mitume na nikamwuliza Bwana, "Bwana, Ibrahimu yuko wapi?" Nilitarajia kuona mzee, lakini ghafla nikamwona kijana wa miaka kama 25 hivi akituja. Yesu akaniambia,  "Huyu ndiye Ibrahimu, baba wa Imani."

Bwana alimwita mwanamke mrembo sana, mwenye uzuri usioelezeka; kama wale wengine niliowaona pale. Bwana
akaniambia, "Huyu ni Mariamu. Nenda kamweleze kila mmoja kwamba Mariamu SIO Malkia wa Mbinguni. Mfalme wa mbinguni ni Mimi, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana; Yeye asemaye, ‘MIMI NDIMI NJIA, NA KWELI, NA UZIMA’ (Yohana 14:6-7). Nenda kawaambie hawa wanadamu waliopofushwa kwamba HAKUNA toharani; maana kama ingekuwapo, ningekuonyesha. Badala yake, kuna Kuzimu, ziwa la moto, Yerusalemu ya thamani, na paradise ambavyo nimekuonyesha. Lakini waambie kuwa hakuna toharani. Waambie kuwa NI UONGO KUTOKA KWA IBILISI; HAKUNA TOHARANI!"

Kisha Bwana alinipeleka kwenye ghala la mataji. "Haya ni mataji
ya uzima… Unaona nini?" Niliona Kanisa la mahali, waumini wa mahali pale, kuimba na kuhubiri. Kisha nikamwuliza Yesu, "Kwa nini majina ya waamini wa kwenye jumuiya yangu hayajaandikwa kwenye kitabu hiki?" Naye akaniambia,  "Kwa sababu ya makosa yao wayatendayo duniani." (Ufunuo 3:11).

Baada ya haya yote, Bwana aliniruhusu kurudi duniani; kwenye mwili wangu. Safari ikawa imekwisha.

………………………………………..

Mpendwa msomaji, karibu ujumuike nami kwenye sehemu ya pili na ya mwisho ya ushuhuda huu muhimu. Bwana akubariki hadi tutakapokutana tena kwenye sehemu hiyo.

No comments:

Post a Comment