Mpendwa msomaji wa blog hii na mwana wa Mungu aliye hai, hii ni Sehemu ya 2 ya ushuhuda huu. Katika Sehemu ya 1, tuliona safari ya kwanza mbinguni ya dada Bernarda. Katika sehemu hii, anatueleza kile kilichotokea pale Bwana Yesu alipomchukua kwa mara ya pili na kwenda naye mbinguni kisha akamrudisha.
Safari
Yangu ya Pili
Siku moja tulikuwa sote
kwenye maombi; tulikuwa watu takribani ishirini. Kama kawaida, tulianza kwa
kumsifu na kumtukuza Bwana.
Ghafla, tulihisi uwepo wa Mungu.
Ulikuwa na nguvu sana kana kwamba ilikuwa ni siku ya Pentekoste. Nakumbuka mama
mkwe wangu, bibi mzee ambaye alijitoa kwa Mungu, aliniambia, “Bernarda, hebu tupunguze kelele wakati wa
kusifu. Tunapaza mno sauti.”
Alikuwa sahihi, maana
kusifu kulikuwa ni kama sauti ya mafuriko ya maji. Wakati nikiwa tayari
kuwaambia kaka zangu wapunguze sauti, nikamsikia Bwana akiniambia: “Usiseme
chochote! Duniani, watu wanapopaza sauti, hakuna anayejali. Sasa, kwa nini
usimamishe sifa?” Kwa hiyo tuliendelea kumsifu na kumwabudu Bwana.
Nilihisi kuwa kuna kitu kikubwa kilikuwa kinaenda kutokea. Ghafla, nilikumbuka
kile ambacho Bwana aliniambia wakati wa safari yangu ya kwanza. Alisema, “Nitarudi kwako
tena.”
Mara moja niliona nuru
kali ikijaza nyumba yangu. Kaka zangu nao waliiona nuru ile. Wote walipiga
magoti mbele za Mungu. Sikujua cha kufanya; nilibaki tu nimesimama pale. Nuru
ile ilizidi mng’ao zaidi, na mara ikawa umbo la mwanadamu. Mbele yangu, akawa
ni Bwana Yesu Kristo; mzuri na aliyejaa upendo. Sijawahi kuona uzuri kama ule
kwenye uso wa mtu yeyote duniani. Alikuja karibu na kila mmoja wa kaka zangu.
Lakini nikiwa najiandaa kusema kwamba Bwana alikuwa amekuja kwa ajili yangu,
nilianza kunena kwa lugha. (1 Wakor 14:39-40).
Kwa kule kunitazama tu,
roho yangu ilitoka kwenye mwili na tayari nikawa hewani. Yesu alinishika mkono
na tukaelekea welekeo wa Jamuhuri ya Dominika. Tulipofika kwenye jiji, Bwana
akaniambia, “Kuna
dhambi mbili kubwa ambazo nchi hii inatenda mbele za Baba Yangu; uchawi na
kuabudu sanamu.” Niliwaona watu
wa nchi ile wakiwakimbilia wachawi na miungu sanamu.
Baada ya hapo, Bwana
alinileta hadi Venezuela. Nilikuwa niko hewani kisha Meksiko. Kule Venezuela,
nilikuwa niko hewani na Bwana Yesu, lakini niliona watu wakigeukia uganga,
mingu na uchawi. Kule Meksiko, niliona watu wakikusanyika na kuabudu mapepo.
Bwana akaniambia, “Machukizo ya dhambi hii yamefika mbele za Baba Yangu. Ishara ya
kwanza ninayotoa kama onyo ni kwamba kutakuwa na tetemeko Meksiko endapo wakazi
wa nchi hii hawatatubu na kunirudia Mimi.” (Baadaye niliporudi
duniani, nilienda Meksiko na kuhubiri ujumbe huu. Watu hawakusikiliza, na hivi
karibuni, kulikuwa na tetemeko baya sana Meksiko).
Wakati tulipokuwa bado
tuko hewani, Bwana aliniambia kuwa Mikono ya Baba Yake imeshanyoshwa juu ya
watu wa dunia. Niliona bahari ikiwa na mawimbi makubwa sana, kama mazimwi. Pia
niliona tufani zikitokea dunia. Nikamwuliza Bwana, “Bwana, itakuwaje kuhusiana na Wakristo wakati haya yote
yatakapotokea?” Akanijibu, “Nenda na ukawaambie kwamba, kwa wale walio waaminifu
Kwangu, hakuna hata unywele wao mmoja utakaoguswa.”
Baada ya hapo, Bwana
alinileta sehemu nyingine. Niliona mahali ambapo dunia ilipasuka. Bwana
akaniambia, “Muda
si mrefu ujao, nchi nyingi zitatoweka kwenye uso wa dunia.”
Kisha tuliondoka hapo na
kwenda sehemu nyingine ambako niliona maji yakiwa katika mwendo. Tuliingia kwenye
shimo la chini kwa chini hadi ndani kabisa ya dunia. Niliona milango mikubwa. Haikuwa
inafanana na ile niliyoiona kwenye safari yangu ya mara ya kwanza. Kwenye milango
hii kulikuwa na minyororo mikubwa. Bwana alienda kwenye ile milango. Aliondoa minyororo
na kuniruhusu niingie ndani ya shimo.
Niliona maelfu ya watu
wakiwa vichwa chini huku wamevaa mavazi machakavu. Walifungwa minyororo
mikubwa. Nikasema, “Bwana, hii maana yake
nini?” Akajibu, “Wanaume na wanawake hawa wote wanaelekea Kuzimu.” Miongoni
mwao nilimwona kaka mkubwa wa mume wangu, Adolfo. Alikuwa ni mtu mwenye
matatizo. Alikuwa akioa na kuacha kadiri apendavyo na alikuwa akimlaani Mungu. Kisha
nilianza kumwomba Bwana nirudi duniani kwenda kumwonya Adolfo kwamba alikuwa
anaelekea kuzimu; lakini Bwana hakunijibu. Nilimwona tena Adolfo na mke wake
wakitembea kwenye lile shimo. Walikuwa ukingoni kabisa mwa shimo. Nilimwomba tena
Bwana nirudi duniani ili nikawaambie watu kile nilichokiona. Bwana aliinua
mkono wake na kusema, “Nenda kawaambie kuwa muda ni kama umekwisha … maelfu kwa
maelfu ya watu wataenda kuzimu. Muda wa Adolfo umekwisha. Atakufa.”
(Niliporudi duniani,
shemeji yangu Adolfo hakutaka kubadili maisha yake. Siku moja alirudi ghafla
kutoka kazini na kumwambia mke wake, “Sitaki
kufanya tena kazi. Kuna kitu kinaniambia kuwa nitakufa.” Mke wake akajibu, “Ni kwa sababu umelewa kama kawaida yako
ndiyo maana unasema hayo.” Wote walienda kulala. Dakika chache baadaye, mke
aliona maono. Alijiona yeye na mume wake wakiwa kwenye shimo, wamevaa nguo
chakavu, na wanaekea kuzimu. Alimsikia Bwana akimwambia, “Muda wenu nyie wawili umekwisha.”)
Wakati nilipokuwa bado
angani, Bwana aliniambia, “Unajua ni kwa nini nimekuleta hapa kwa mara ya pili? Ilikuwa
ni kukuonyesha kwamba katika ziara yako ya mara ya kwanza idadi ya watu
waliopotea ilikuwa ndogo kuliko sasa.” Hivi sasa kulikuwa na roho
nyingi zaidi zilizopotea kuliko kwanza.
Kisha Yesu na mimi
tuliondoka mahali pale na kupaa tukapita mbingu ya pili. Tulipofika kwenye
mbingu ya tatu, Ufalme wa Mungu, niliona malaika wakienda mbiombio kutoka
upande mmoja hadi mwingine. Nikamwuliza Bwana, “Kwa nini malaika hawa wako katika mwendo hivi?” Yesu akanijibu, “Ni kweli
malaika zangu wako kwenye mwendo hapa. Lakini nitakuonyesha jinsi ambavyo dunia
nayo iko katika mwendo. Kuwa mwangalifu kwa sababu mapepo mengi yameshavamia
dunia. Ibilisi ana hasira sana dhidi ya Wakristo kwa sababu amebakiwa na muda
kidogo tu.”
Bwana aliniruhusu kuona
mapepo yakiwa yenye hasira mno, na akaniambia, “Mapepo hayo unayoyaona ni mapepo ya
uzinzi. Yatashambulia maelfu ya watumishi Wangu na wengi wataanguka kwenye
dhambi hiyo. Unajua ni kwa nini ibilisi anafanikiwa kuwaangusha watumishi
wangu? Ni kwa sababu watumishi Wangu hawanipi utukufu wote. Wanaiba utukufu
wangu na kuwa na kiburi. Zaidi ya hayo, wake zao wanaishi katika mvurugiko wa
kiroho. Hawakujenga nyumba zao kwa hekima.”
(1 Tim 2:11-14).
Niliona maelfu ya malaika
ambao sikuweza kuwahesabu wakiwa
tayari kwa vita. Kisha Yesu aliniambia, “Sasa nawatuma
maelfu kwa maelfu ya hawa malaika duniani ili kuwalinda watu Wangu. Katika siku
hizi za mwisho, ulinzi utakuwa mara dufu. Shetani naye pia atazidisha
mashambulizi yake mara dufu, lakini msisahau kuwa Mungu wenu ni Mkuu na Mwenye
Nguvu. Kama umejiungamanisha naye, hakuna kitu kitakachotokea kwako.”
Karamu
Kisha Bwana alinileta
kwenye sehemu nyingine. Niliona meza kubwa imezungukwa na viti vya dhahabu. Kwenye
kila kiti liliandikwa jina; na joho la kitani liliwekwa hapo. Mbele ya kila
kiti, juu ya meza, niliona mataji. Kisha
niliona kuwa kulikuwa na kiti kikubwa kuliko vingine. Mbele ya kiti kile
kulikuwa na kikombe kikubwa cha dhahabu. Yesu aliniambia nikachungulie nione
kilichomo kwenye kikombe kile. Kilikuwa kimejaa mvinyo, tayari kwa kugawiwa. Yesu
akaniambia, “Unajua
ni kwa nini mvinyo uko tayari kugawiwa? Nenda kawaambie watu Wangu kwamba Mimi
ndimi mlango. Ninakuja hivi karibuni.”
Bwana alinipa joho la
kitani safi na taji. Nilivaa joho na taji lile na kwenda kwenye sehemu ambako
kulikuwa na namna ya kioo. Yesu akaniambia, “Hakuna doa wala mkunjo kwenye joho lako, si ndiyo? Hakuna
mtu atakayepita kwenye mlango huu wala kushiriki meza hii ambaye hajavaa kwa
namna hiyo. Baadhi miongoni mwa watu Wangu duniani wameshachafua mavazi yao. Wengine
wana mavazi yenye mikunjo, na bado kuna ambao wameyaweka pembeni ya kwao na
kuyasahau. Waambie watu wangu kuwa ni wakati wa kuosha mavazi yao, kuyanyoosha
na kuyachukua tena. Wakristo wanatakiwa kumwambia Roho Mtakatifu awasaidie
kuyaweka mavazi yao katika hali nzuri, maana si muda mrefu Mfalme atasherehekea
Karamu ya Harusi kwenye ufalme wa Baba Yake.” (Mathayo 22:1-14).
Familia
yangu
Ninatokea kwenye familia
iliyotalikiana na nimekulia kwa baba yangu. Mama yangu alikuwa ni muumini sana
wa dini. Lakini baba yangu alikuwa haamini chochote. Nina dada yangu ambaye
yuko kwenye nyumba ya utawa, lakini ninajua kuwa Yesu atamtoa huko hivi
karibuni naye atahubiri Injili pamoja nami. Huwa ninaomba sana kwa ajili yake. Nilipokuwa
ninatafakari juu ya maisha ya mama yangu kwenye dini hiyo ya ajabuajabu
(mystic), wakati wa safari yangu ya kwanza paradiso, nililia mbele za Bwana na
kumwambia, “Bwana, mama yangu amepotea,
lakini nimeshahubiri Injili kwake naye hataki kusikia. Anaendelea tu kung’ang’ania
zaidi na zaidi dini hiyo ya kipagani.” Bwana akaniambia, “Nitamwokoa mama
yako, lakini nitamleta nyumbani mara moja, vinginevyo ataanguka tena dhambini
na kwenda Kuzimu. Kwa sababu hiyo, mara baada ya kuokoka, atakufa muda mfupi
baadaye na kuja hapa paradiso.”
Niliporudi duniani,
niliomba, nililia, nilishusha pumzi na kumkumbusha Bwana juu ya ahadi
aliyonipa, lakini nilimwona mama yangu akizama tu kwenye ibada ya sanamu ya
dini yake. Siku moja Bwana alimtumia mwanangu wa kiume kumbadili mama yangu. Siku
tatu tu baada ya kuokoka, alikufa!
Katika safari yangu ya
pili paradiso Bwana aliniambia, “Tazama! Kile ambacho kinywa Changu kinasema, mikono
Yangu inakitimiza.” Nilimwona mama yangu kwenye ile paradiso nzuri. Alikuwa
miongoni mwa wanawake wengine. Tulienda mahali ambako niliona maelfu ya watoto
wamevaa mavazi meupe wakimsifu na kumtukuza Bwana. Yesu akaniambia, “Watoto hawa ni
wale ambao mimba zilitolewa na wazazi wao na madaktari wahalifu. Watoto ambao
watu waliwaua wangali kwenye matumbo ya mama zao, na ambao wanakutwa kwenye
mapipa ya taka na kwenye mito, wote wako hapa mbinguni.”
Wapendwa kaka na dada
zangu, tofauti na vile ambavyo mnaweza kufikiri, kwa Bwana, mimba ikitungwa tu inakuwa
ni binadamu tangu siku ya kwanza.
Yesu aliniambia tena, “Bernarda, fanya
kazi maana Mimi ni nguvu zako. Ujumbe huu ni lazima uende duniani kote. Ni ujumbe
kwa ajili ya Wakristo, wachungaji, na watu wote wakaao duniani, ikiwa ni pamoja
na wewe. Yeye aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakatifu.”
Wakati huo malango ya
mbinguni yalifunguliwa. Kulikuwa na ngazi inayopanda yenyewe (eskaleta) nzuri
sana. Yesu aliwaita maelfu ya malaika waje, kisha Bwana alinisindikiza kurudi
nyumbani.
Tulipofika nyumbani, nilimwona
mume wangu na ndugu zangu wa Kikristo wakiwa wanangoja roho yangu irudi. Niliutazama
mwili wangu wa nyama, na nikamwambia Bwana kuwa sikuwa nauhitaji tena mwili
ule. Bwana akaniambia, “Huwezi kurusi mbinguni pamoja nami, maana muda wako
haujafika bado. Unatakiwa ukawaambie watu Wangu kwanza kile ulichokiona, ili
kwamba wajiweke tayari.” Kwa sauti
yenye nguvu, aliniambia, “Ingia na upokee uzima. Mimi ndimi ufufuo na uzima. Yule aniaminiye Mimi, hata ajapokufa,
atakuwa hai.” (Yohana 11:25-26).
Mwisho wa ushuhuda.
………………………………..
Mpendwa msomaji wa blog
hii kama ungependa kusoma ushuhuda huu kwa Kiingereza, bofya HAPA.
Mungu akubariki kwa kazi nzuri. Ni ushuhuda mzuri sana unaotuonya siku hizi za mwisho, wakristo tumejisahau sana ni wahubiri wachache sana wanowakumbusha waumini zao juu ya kujiandaa kurudi kwa mwokozi wetu Yesu. Ki ukweli muda umeisha sana lakini wahubiri wengi wamejikita kuhubiri utajiri na kusahau misingi ya injili ya kuwaokoa watu wasiende jehanmu. Brother John kuna yale maswali uliulizaga ndugu zetu walikujibu? karibia mwaka sahvi unapita sioni majibu?
ReplyDeleteShalom Nicky. Asante kwa maoni yako. Bwana akubariki sana; tuzidi kusimama imara kwa Bwana tukimtanguliza Yeye katika mambo yote maishani mwetu.
DeleteKuhusiana na yale maswali ambayo niliuliza ndugu zetu waislamu, sijapata jibu hata moja hadi leo. Ukweli ni kwamba maswali hayo hawawezi kuyajibu kwa sababu Uislamu hauna majibu juu ya mambo yake. Ndiyo maana inabidi utumie kulazimisha mambo kwa kuwa akili ya kawaida tu haikubaliani na mambo yake.
Na kusema kweli, sikuyaweka hapa ili wanipatie majibu (maana najua hawawezi kuyapata), bali nimeyaweka ili wajihoji na kujipima juu ya hayo wanayoyaamini; ili yamkini watambue hatari waliyomo na kuja kwa Mwokozi wetu na wao, Yesu Kristo, ambaye ndiye PEKEE njia, na KWELI, na uzima.
Ubarikiwe na Bwana, Nicky.
Barikiwa mpendwa kwa kutuwekea shuhuda zenye kujenga IMANI ZETU. Mungu wangu azidi kukutumia katika huduma hii hujui wangapi wanabadirisha maisha yao na wangapi wanarekebishwa kiimani ila ni kusudi la YESU KRISTO ALIE HAI kufanya ujumbe wake upite kwa walio wake. MUNGU azidi kukubariki.
ReplyDeleteAsante sana Upendo kwa maoni yako yenye kutia moyo. Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.
DeleteAmen nimebarikiwa na we uvarikiwe
ReplyDelete