Je, wewe ni Mkristo? Je,
wewe ni Mwislamu? Sote tuko kwenye safari ya kuelekea mbinguni huku tukiamini
kuwa njia ile tuliyomo ndiyo sahihi; na njia ile waliyomo walio kinyume nasi haiko
sahihi.
Ukristo na Uislamu ni dini
kubwa ambazo zinadai kuwa zinaabudu Mungu mmoja aliyeumba mbingu na nchi tofauti
na dini zingine ambazo zinaabudu miungu mingi. Hata hivyo, zipo tofauti za
msingi sana kati ya Uislamu na Ukristo ambazo KATU haziwezi kufanya pande hizi
mbili ziwe zote sahihi. Kwa mfano:
- Ukristo unaamini kuwa Yesu ni Mungu na Uislamu unaamini kuwa Yesu si Mungu. Haiwezekani kamwe Ukristo ukawa sahihi katika hili na Uislamu ukawa sahihi katika hili. Ni lazima uwe ni upande mmoja TU ulio sahihi katika jambo hili.
Hali ni hiihii katika
mambo mengine mengi. Kwa mfano:
- Ukristo hauamini hata kidogo kwamba Muhammad ni mtume wa Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo; lakini Uislamu unaamini hivyo.
- Ukristo unaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka; lakini Uislamu hauamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka.
- Ukristo hauamini kuwa kuna Mwislamu YEYOTE atakayekwenda mbinguni kwa kupitia imani ya Uislamu; lakini Uislamu unaamini hivyo; n.k., n.k.
Kwa kuwa haiwezekani pande
zote mbili zikawa sahihi, lazima kuna upande uliodanganywa; na Biblia ilishaonya
tangu karne nyingi kabla kwamba yuko Ibilisi audanganye ulimwengu wote. (Ufunuo 12:9).
Je, asili ya Uislamu ni
nini? Hata kama wewe ni Mkristo, ni muhimu kuyajua haya maana tunao ndugu zetu
wengi walio upande wa pili. Ndugu zetu hawa si kwamba hawataki kwenda mbinguni;
la hasha! Mbingu wanaitaka sana. Tena wapo wengi walio na juhudi kubwa kuliko
hata sisi tulio Wakristo. Lakini juhudi na nia njema huwa si jibu na suluhisho
la shida yoyote. Ni lazima hizi zichanganywe na maarifa sahihi.
Hata Waswahili wanasema:
Penye nia pana njia. Lakini kama una nia ya kwenda mji ulio kaskazini lakini
ukapanda gari inayokwenda magharibi ni vigumu sana kufikia lengo. Nia ya kweli
ni LAZIMA iungane na maarifa ya kweli!
Uislamu umetokea wapi? Tafadhali
weka maarifa haya kwenye blog yako; kwenye facebook; kwenye tweeter; n.k.;
huwezi kujua utasababisha wokovu kwa nani.
Bofya HAPA ili kufahamu zaidi.
No comments:
Post a Comment