Sunday, July 27, 2014

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 4




====  SIKU YA 10  ====

Kim, Joo-Eun: 
Wakati nikiwa nimezama katika kuomba kwa lugha, joka jekundu lilinitokea. Lilikuja kwangu kwa kasi na kunirukia. Lilikuwa na macho kama ya mamba na makucha makubwa makali, na likajaribu kunitisha kwa makucha yake. Moshi unaotia kinyaa ulitoka kwenye pua zake. "Ewe shetani mbaya, ondoka kwangu kwa Jina la Yesu." Nilikuwa napaza sauti kama mwanamke mwenye wazimu. Ndipo joka hilo likaelekea upande wa kaka  Haak-Sung.  Haak-Sung akashtuka. Kuomba
kwake kwa lugha kukawa kwa bidii na kwa sauti zaidi. Alikemea kama nilivyofanya mimi, "Ewe shetani mbaya, ondoka kwangu kwa Jina la Yesu." Mara, lile joka likanijia, na kugeuka kuwa joka jeusi. Kwa kicheko kiovu, likaanza kusema, "Usiombe. Kwa nini unafungua macho bila kutumia nguvu yako wakati wa kuomba? Kama ni hivyo, basi fungua macho yako. Kwani ni lazima ufunge macho yako wakati wa kuomba?  Fungua macho yako sasa hivi? Kwa nini unaomba kwa bidii hivyo siku ya leo?" Lilijaribu kuniondolea uzingativu wangu wakati wa kuomba. Nikapaza sauti tena, "Ewe shetani mbaya, ondoka kwangu kwa Jina la Yesu." Lakini joka lile halikuondoka kirahisi. Kwa hiyo, ilibidi nisisitize Jina la Yesu zaidi. Kwa kusema kwa sauti Jina la Yesu, joka lile lilinigeukia tena kwa macho maovu, likasaga meno yake na kutoweka.  

Mara pepo jingine likanikodolea macho, na kuanza kunijia. Niligundua lilikuwa ni pepo maarufu la kike linaloonekana kwenye sinema nyingi za Kikorea za mambo ya kutisha na kwenye TV. Niliogopa, lakini nikatambua kuwa nikiruhusu tu woga, litapata ujasiri wa kunishambulia. Kwa nguvu zangu zote nilijitahidi kutoonyesha woga, wakati nikipambana nalo kwa maombi. Lengo la pepo hili ni kuwaogopesha watu hadi wafe. Damu ilichuruzika toka kwenye kona za midomo yake, na nywele zake zilikuwa hovyohovyo. Lilitoa sauti mbaya na kicheko cha kutisha. Kwa nguvu zote nilisema kwa sauti, "Ondoka kwangu kwa Jina la Yesu!" nalo likatoweka.
 
Baadaye, Bwana Yesu alinitokea. Hata hivyo, safari hii nilihisi kulikuwa na jambo lisilo sawa. Sikujisikia amani, nikaingiwa na hofu kumwona Bwana. Nikakumbuka mchungaji wangu aliniambia niwe makini, maana shetani huweza kujigeuza malaika wa nuru. Niliambiwa kama nikishindwa kupambanua roho, ama niombe kwa lugha au niijaribu roho kwa kutamka Andiko. Nilimjaribu huyu yesu kwa kunena kwa lugha. Kilichokuwa kimeonekana kama uso wa Yesu, kilianza kumomonyoka na kuwa uso mweusi tii. Shetani alinijia akiwa amevaa sura kama ya Yesu. Macho ya shetani lile yaligeuka pande zote na akawa haondoki akijaribu kuniondolea uzingativu katika kuomba.  

Dada Baek, Bong-Nyo: 
Leo nikiwa naomba kwa lugha, Bwana Yesu alinijia. Nililia, "Bwana, Bwana." Yesu alizungumza akasema, "Acha kulia. Nimekuja kukuchukua hadi Mbinguni. Haya twende." Kulikuwa na huruma kwenye uso wa Bwana akiwa amenishika mkono. Kila ninapotembelea Mbinguni, ninajawa na furaha sana kutokana na maajabu yote ambayo hayana mwisho na ni ya milele. Navutiwa sana na mandhari ya huko. Nahisi kuwa itatuchukua milele kuona na kutembelea Mbingu yote. Yesu aliniambia niende nikaangalie Kanisa la Mbinguni. Mara tulipofika pale, nilibakia mdomo wazi kutokana na uzuri wa jengo hilo. Nikasema kwa mshangao, "Haa!" Nilikuwa nimeshangaa kwelikweli. Lilikuwa jengo kubwa sana. Lilionekana kama vile linaweza kugusa anga la Mbinguni. 

Baadaye, tukiwa tunatembelea Mbingu, Yesu alisema, "Bong-Nyo, hebu twende tukatembelee kilele kirefu kabisa Mbinguni." Tulipofika juu, niliweza kuona sehemu mbalimbali za Mbinguni. Niliona malaika wengi na bustani pana zenye maua aina mbalimbali. Ilikuwa haiwezekani kwangu kuhesabu aina zote za mimea na maua niliyoona. Niliweza kuona bahari isiyo na mwisho, ikiwa na maji angavu kabisa. Kulikuwa na meli nzuri zikiwa juu ya maji.

Baadaye, niliporudi duniani, japokuwa ndio nilitoka tu kutembelea Mbinguni, niliwakumbuka tena wazazi wangu na kaka yangu walioko kuzimu. Nililia kwa saa nyingi, na sikujua cha kufanya. Mara, kikundi cha malaika kumi na tano kilinitokea. "Bwana Mungu ametuamuru kwenda duniani kumfariji Dada Baek, Bong-Nyo.  Hii ndiyo sababu tuko hapa." Walinizunguka na kuanza kunihudumia kwa maneno ya faraja. Mara niliweza kutulia na machozi yangu yalifutwa.

Baadaye tena, niliendelea kuomba. Ghafla, niliona Mbingu zimefunguka, na Mungu Baba alikuwa amekaa kwenye kiti chake cha enzi Mbinguni. Alizungumza na kuniambia nisilie. Roho Mtakatifu alikuja na kuniambia, "Nitakupa wewe na Dada Kang, Hyun-Ja karama ya uponyaji na moto wa Roho Mtakatifu. Lakini ni lazima muwe na shauku kubwa ya karama hiyo na kuitaka kwa bidii." Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Baba, aliniambia, "Bong-Nyo, ukichoka na kuwa dhaifu wakati wa kuomba, nitakupaka mafuta kwa nguvu ya Roho Mtakatifu."

Baada ya kitambo kidogo, Yesu alianza kuongea kwa sauti yenye ukali. Alisema kuwa makanisa na wachungaji wanamwabudu Yeye bure. Wanafuata mapokeo na mafundisho ya wanadamu. Ibada nyingi ni fupi na hazina ujumbe. Kiasi cha muda unaotumika kuabudu na kusifu kimekuwa hakikubaliki. Wanawaza zaidi ni lini ibada itaisha. Muda wa mahubiri umefupishwa. Yesu alikuwa anaeleza huzuni yake. Kwa ujumla, ibada ni za kama saa moja tu. Hata hivyo, ibada nyingi zimekuwa chini ya saa moja. Wana haraka ya kumaliza. Yesu angependa kujidhihirisha kwenye miili ya wahubiri wake, lakini wachungaji wanahubiri kimwili na sio kiroho. Wanaangalia zaidi muda kuliko kuhubiri katika Roho kwa muda kidogo wa kuabudu na wa ibada. Wahubiri wengi wanatumia muda unaobaki kwa mambo binafsi, kwa mfano kwenda kula, kusafiri na waumini, na kupoteza muda kwa mambo yasiyo na maana. Baadhi ya wachungaji wanadanganyika kwa wadada warembo, na wanajali zaidi uzuri wao.

Zaidi ya hapo, baadhi ya wachungaji hawawajali waumini kwa kiwango sawa. Waumini wenye fedha wanaheshimiwa na kupewa muda zaidi kuliko wasio na fedha. Aina hii ya wachungaji hawatumii muda wa kutosha kwa maombi kwa utukufu wa Mungu, bali wanaomba kidogo tu, jambo ambalo linamkosesha raha Bwana wetu. Ujumbe hauongozwi na Roho Mtakatifu. Ujumbe unatokana na nguvu ya uelewa wa mchungaji na mwili wake. Ujumbe usiotokana na Roho Mtakatifu utaishia kwenye mahubiri mafupi yasiyo na nguvu. Wachungaji hawachagui kuongozwa na Roho Mtakatifu bali na waumini. Yesu anatamani sana kuwaongoza wachungaji kwa uweza mkuu kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Lakini wachungaji wao wenyewe walishaacha kutafuta upako wa Bwana. Sasa hivi akili zao za kimwili zinatawala roho zao. Wahubiri wengi hawahisi tena moyo wala shauku ya Mungu.  Mungu anahuzunika sana. Wakati wakipanua au kujenga makanisa, baadhi ya wachungaji hufanya hivyo kwa ajili ya utukufu wao wenyewe na kujikweza.  Mioyoni mwao, jengo ni mnara wa kumbukumbu yao. Aina hii ya wachungaji hutumia muda kidogo sana kwa maombi na wanahangaika zaidi na mali na mambo ya kidunia.

Bwana aliponiambia mambo haya, niliona uso wake ukionyesha huzuni. Japokuwa wahubiri wengi wanaweza kujitapa kuhusiana na majengo mazuri, Mbingu zinaona mambo hayo kuwa ni madogo sana. Njia za Mbingu ni za juu sana kuliko njia za dunia. Kitu ambacho duniani kinaonekana ni kikubwa sana, Mbinguni kinaweza kuonekana kidogo sana. Yesu aliniambia: "Si wachungaji wote ni waovu. Hata hivyo, wasio watii ni lazima waadabishwe. Kama wasipotubu, nitawatupa jehanamu. Kule watateswa. Baada ya muda mfupi nitakupeleka kule ukawaone baadhi yao ambao walishatangulia huko."

Baadaye siku hiyo, nilihitaji msaada toka kwa Bwana ili kuelewa baadhi ya vitu. Baadhi ya waumini, ambao walishakuwa Wakristo kwa miaka na miaka, waliniambia kuwa mtu akifa, anaingia Mbinguni au kuzimu. Walisema kuwa mtu aliye hai hawezi kutembelea Mbinguni wala kuzimu. Walisema ni upuuzi tu kuamini kitu kama hicho. Walibeza mikutano yetu ya maombi na kuomba kwetu kwa muda mrefu. Pia walisema kuwa Mchungaji Kim na kanisa lake wanaweza kuwa ni kikundi cha imani za kishetani (cult).  Kwa hiyo, niliomba, "Tafadhali Bwana, vipi kama kanisa letu ni cult? Nini kitatokea kwa familia yangu?" Bwana akasema, "‘Cult’ ni nini? Watu wanalaumiana na kuhukumiana kwa sababu ya tofauti zao, madhehebu na mafundisho yao. Wanatenda dhambi. Hata hivyo, mimi nafurahishwa na kanisa lenu. Wewe na waumini wa kanisani kwenu mnaomba bila kukoma usiku kucha. Wale waliowatesa na kuwaita imani ya kishetani watajua kuwa Mimi ni hai na ni Bwana. Mmepokea karama ya uponyaji wa wagonjwa na uwezo wa kutoa pepo. Pia mnaishi kwa kumfuata Roho Mtakatifu." Yesu akaendelea kusema, "Watu wanaohukumiana na kulaumiana watapata hukumu ya kutisha sana. Usikubali wakupoteze. Ninaguswa sana na maombi yenu. Msiogope. Nitakulinda wewe na kanisa lenu. Japokuwa ni shauku yangu kujidhihirisha kwa watu wangu wote na kuwapatia karama za rohoni, lakini hawanitafuti. Wengi hawaombi sawasawa na mapenzi yangu."  Nikamwuliza, "Yesu, nini kitatokea kwa kanisa?" Yesu akasema, "Mna bahati kujazwa na Roho Mtakatifu na kupokea kipawa cha kunena kwa lugha haraka hivi. Moto mtakatifu utaenea na kupokewa na kusanyiko lote."

Wakati wa ibada ndefu, Mchungaji Kim alitoa mahubiri yenye nguvu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Baadhi ya watu wanaweza kuwaza kuwa tutasinzia kwa kuwa ibada ni ndefu. Hata hivyo, mahubiri, sifa, kuimba na kuabudu vinafanyika kwa moyo sana kiasi kwamba tunakuwa tumejaa nguvu zinazotuwezesha kuendelea usiku kucha hadi siku inayofuata. Siku moja, mchungaji wetu alihubiri kwa nguvu sana kiasi kwamba uso wake uligeuka na kuwa mwekundu. Wakati wa mahubiri, niliona maono ya kiti cha enzi cha utukufu cha Mungu. Mungu Baba alikuwa akimimina mafuta ya upako. Ilionekana kuwa Roho Mtakatifu anampaka mafuta mchungaji kwa moto. Niliweza kumwona Mungu Baba akimimina mfululizo moto na mafuta ya upako juu ya mchungaji. Mahubiri yakawa na nguvu na ya kuvutia zaidi. Nilimwona Bwana Yesu akicheka kwa furaha. Bwana alimwambia malaika mmoja arekodi kwa bidii matukio ya ibada ile. Malaika aliitikia na kutii. 

Nikamwuliza Yesu juu ya kanisa liiloenea duniani kote, likiwa na matawi mengi, hata Korea. Wengine husema kuwa idadi yao ni kubwa kwa sababu ya historia na utamaduni wao.  "Je, na wao ni waumini kama sisi?" nilimwuliza Yesu. Yesu akasema, "Kama wananiamini Mimi, basi wataokolewa. Lakini kanisa hilo linashusha hadhi ya Neno la Mungu kwa kulishirikisha na dunia.

Tukiwa tunajadili kanisa hili, katika maono, nilionyeshwa mfalme wa mapepo. Pepo hili ovu lilionekana lina wasiwasi juu ya mipango yake kuhusiana hasa na kanisa hilo. Yesu akasema, "Watu wa Mungu wengi sana hawana ufahamu juu ya ibilisi na mapepo waovu. Watu wangu wanaishi kwa uaminifu maisha yao bila kutafakari sana juu ya adui. Hata hivyo, ibilisi atajaribu kuzuia kazi yenu. Iweni na ujasiri."

Baadaye, wakati naomba pembeni ya mchungaji, pepo kubwa sana jekundu lilitokea. Jitu hilo lilingilia mlango wa mbele. Lilionekana kuwa refu hadi mawinguni. Sura yake ilijaa ghadhabu. Lilikuwa linachezeshachezesha pua yake. Joka lile liliongea, "Ninajaribu kuingia ndani ya mwili wako. Unawezaje kupingana na mimi! Mimi ni mfalme wa kuzimu! Wote kule kuzimu wananitii mimi na kwa hofu. Wewe ni nani hasa? Wewe si lolote si chochote! Huna haki ya kuweka wazi uwepo wangu. Aha. Sasa najua wewe ni nani. Mmoja wa watumishi wangu ameshaniambia wewe ni nani. Mwanzoni nilishamwagiza huyo mtumishi wangu awadanganye wengi na kuwapeleka kuzimu. Lakini alirudi bila mafanikio. Nilipomwuliza kwa nini alishindwa, alisema, ‘Mfalme wangu, inabidi uje mwenyewe uone kwa nini ni vigumu. Nilidhani nitawashawishi kirahisi watu wajiue. Lakini maombi ya Wakristo yana nguvu sana.’ ‘Ndio unasema nini?’ nilimkemea mtumishi wangu. Ilibidi nije kuthibitisha maneno ya mtumishi wangu. Yalikuwa ya kweli. Karibu ilikuwa haiwezekani kushindana na maombi haya.

Japokuwa joka lile lilitutisha na kutukemea, tuko salama kwa sababu Yesu anatulinda. Joka lile lilitoa lugha chafu, kisha likasema, "Nimeshazuiliwa." Yesu akamjibu yule joka, "Unadhani uko wapi hapa? Usilete fujo na ghasia. Ukimgusa hata mtu mmoja kwenye Kanisa la Bwana (The Lord's Church), utaadhibiwa, na Baba yangu atakupiga." Joka lile lilijaa huzuni na ghafla likatoweka. Yesu akasema, "Joka lile kule kuzimu lilijaribu kuwadanganya ninyi kama mfalme wa mapepo. Hii ni mara ya kwanza ya udhihirisho wa hilo joka. Mara zote limekuwa likituma walio chini yake duniani kutekeleza maagizo yake. Ombeni kwa bidii na bila kukoma. Mara zote iweni waangalifu na msiwe na hofu, maana Utatu Mtakatifu wa Mungu utawalinda."

Mchungaji Kim, Yong-Doo: 
Ilikuwa ni Jumanne, na nje barafu ilikuwa ikidondoka, huku halijoto ikiwa nyuzi 15 chini ya sifuri. Licha ya hali ya hewa kuwa hivyo, washirika wetu wanne walitoka kwenda kushuhudia. Lakini kabla ya kufanya hivyo, walikuwa wakijiandaa kwa bidii kwa maombi na nguvu za Roho Mtakatifu. Na Bwana alikuwa akiwapa upako wa moto mtakatifu. Hao wanne walijadiliana mchezo wa kutumia ili waweze kushuhudia kwa mafaniko zaidi. Walijua kuwa malipo mazuri sana yanawangojea kwa kufanya kazi ya Bwana bila kuchoka. Wote walirudi wamechelewa sana, na walikuwa wamejawa na furaha. "Mchungaji, hatukujua kuwa kushuhudia ni jambo la kuburudisha kiasi hiki," walisema. 

2 comments:

  1. Jina la BWANA YESU libarikiwe! James umetumika vema ktk kutenda kusudi la MUNGU, ubarikiwe. Umekuwa kimya ni kitambo kirefu sasa, tushirikishe ulipo.

    ReplyDelete
  2. Tafadhali Ndugu James ,tunabarikiwa na post zako -Ongeza nyingine tafadhali

    ReplyDelete