Nawashukuru ndugu Hamudi na Maalim Moses kwa majibu na maswali yenu kuhusu
makala yangu ya Ndugu Waislamu Nisaidieni.
Mimi naamini lengo letu sote ni kumtafuta na kumtii Mungu wetu aliyetuumba,
huku tukiwa na imani kuwa, mwisho wa safari ya maisha haya tutafika kwake
mbinguni. Hata hivyo, leo ninayo maswali mengine kwao na kwa Waislamu wengine.
Mimi naamini kuwa njia pekee ya kufika mbinguni ni Yesu Kristo
tu. Kwa msingi huo, ningependa kuona kuwa si Waislamu tu, bali hata wanadamu
wote wanatambua kuwa Kristo ndiye Mwokozi wetu ambaye pia ni njia ya kufika
mbinguni.
Katika kutekeleza kusudi hilo, ninakutana na changamoto mbalimbali kutoka
kwa watu kama akina Hamudi na Maalim Moses. Na mimi ninafurahi kwa kuwa
zinanifanya nifikirie kwa undani juu ya kile ninachokiamini – maana kuna
maswali mengine ni mazito kwelikweli! Bila shaka Hamudi na Maalim Moses nao
wangependa watu wote tuwe Waislamu kwa kuwa wao nao wanaamini kuwa Uislamu
ndiyo njia pekee ya kufika mbinguni.
Hamudi na Maalim Moses hawako hapa kuhubiri Ukristo. Vivyo hivyo nami siko
hapa kuhubiri Uislamu. Lakini kwa kuwa kila mmoja wetu anaamini kuwa mwenzake
hayuko sawa, ndiyo maana tunajaribu kuitana ili sote tuende mbinguni. Maana mimi
najiuliza, kwa nini Hamudi na Maalim Moses wapotee ilhali mimi niko hapa naujua
ukweli? Naamini na wao nao wanafikiri hivyo hivyo.
Hoja tunazowekeana ndizo sasa zinazofungua ufahamu wetu, na zinamfanya mtu
aone kibinafsi kuwa, “Ahaa, kumbe hii ndiyo kweli niliyokuwa naitafuta!!” Maana
ukweli unapokuwa dhahiri, hata ukibisha kwa nje, moyo wako utasema tu, “Japo
nabisha, lakini kwa kweli niko nje kabisa ya ukweli wenyewe.”
Kwa mantiki hiyo, katika makala haya ninayo maswali kadhaa ambayo si tu
yanatupatia ufahamu juu ya imani zetu, lakini pia yanatuwezesha kutafuta majibu
yanayohusu hatima zetu – si hatima za maisha ya duniani bali ni hatima za roho
zetu, yaani yanatusaidia kujibu swali kuu: “Hivi ni kweli naenda mbinguni au
naenda jehanamu MILELE?”
Yafuatayo ndiyo maswali yangu kwa Hamudi, kwa Maalim Moses na kwa Waislamu wote:
1.
Adamu na Hawa walifukuzwa kwenye Bustani ya
Edeni kutokana na dhambi. Sisi pia tulio uzao wao ni wenye dhambi? Suluhisho la
tatizo hili ni moja tu kulingana na Biblia – Yesu Kristo alikufa msalabani na
kufanyika sadaka au dhabihu ili sisi tusiendelee kuchinja wanyama kila siku kwa
ajili ya dhambi zetu kama torati inavyosema, badala yake tuamini TU katika sadaka ya Yesu na kupokea
msamaha wa dhambi na wokovu wa Mungu bure.
Waislamu hamumwamini Yesu Kristo kama mwokozi aliyefia
dhambi za wanadamu wote. Je, suluhisho la dhambi kwa mwanadamu ni nini? Kwa maana
nyingine, ninyi Waislamu mtaponaje na jehanamu ya moto ilhali ni wazi kuwa
ninyi, kama ilivyo kwa kila mwanadamu, mna dhambi ambazo ndizo hizohizo
zilimtenga Adamu na Mungu?
2. Biblia inasema: Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya
wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na
wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1
Yohana 1:8-9). Kwa hiyo mimi Mkristo nikijikuta nimetenda dhambi nakwenda
mwenyewe kwa Bwana Yesu na kumwambia, “Bwana wangu, nimesema uongo, nimeiba,
nimetukana, nimetamani, … n.k. naomba unisamehe.” Sisubiri hadi mchungaji au
mtu mwingine anikamate kwenye kosa kama polisi wanavyokamata wahalifu.
Ninyi Waislamu mnasema kuwa torati ndiyo njia sahihi ya
maisha ya mwanadamu, kwamba mtu akifanya makosa ni lazima aadhibiwe kama vile
kupigwa mawe, kuchapwa viboko, kukatwa mikono, n.k.
Watalebani wakimchapa viboko mkosaji
Swali ni kuwa, kwa nini hatusikii Waislamu wakijipeleka
wenyewe kupokea adhabu hizo baada ya kufanya dhambi? Hatujawahi kusikia
Mwislamu ameenda kusema, “Jamani nimezini kwa hiyo nimekuja mnipige mawe;
Nimeiba, hivyo nimekuja mnikate mkono.” Kwa nini wanaoadhibiwa ni wale TU
wanaokamatwa? Mnataka kutuambia kuwa wakosaji ni hao tu? Kama unaamini kuwa
mzinzi ni lazima apigwe mawe, si uende ukaombe wakupige mawe baada ya kuzini. Kwa
nini hamfanyi hivyo?
3.
Huenda katika swali la hapo juu utajitetea kwa kusema
huendi kwa sababu hujakamatwa (ingawaje Mungu tayari anakuwa ameshakukamata). Sasa,
mbona hatusikii mkiwapiga viboko mia, au kuwakata mikono watoto wenu wenyewe
kwenye familia zenu pale wanapoiba mboga au fedha nyumbani?
Bila shaka wizi ni wizi tu hata kama aliyeufanya ni mtoto.
Ndiyo maana huwa tunawachapa viboko kwa namna ya kawaida isiyo ya kidini. Kwa
nini basi sheria za kiislamu zinakuwa sahihi pale zinapohusu tu watoto wa wengine?
4.
Hivi ni mwanadamu gani anayeweza kusema kuwa anaweza akae
japo siku moja bila kutenda dhambi? Au hata nusu siku? Au hata saa moja tu? Hivi
kuna mtu anaweza kuoga mara moja kwa mwezi halafu akabaki safi kwa mwezi huo
mzima? Mimi naamini hilo haliwezekani. Ukitaka kuwa safi ni lazima uoge kila
siku. Sasa, kama ambavyo jasho, vumbi na harufu mbaya ni uchafu wa mwili, je,
dhambi si ndiyo uchafu wa roho? Na kama dhambi ni uchafu wa roho, “logic” ya
ninyi Waislamu kuwa na mwezi mmoja wa
toba ni nini? Unawezaje kutubu kwa mwezi mmoja halafu eti uwe safi mwaka
mzima?
5. Bila shaka ninyi mnaamini kabisa kuwa Uislamu ni dini
inayowapeleka mbinguni. Pili, mnaamini kuwa mtu akijitoa muhanga kuua makafiri
(yaani akifa huku anatetea dini ya Mwenyezi Mungu), anakwenda peponi moja kwa
moja.
Na bila shaka mnaamini kuwa wale makafiri wanaouawa na
mwislamu kama huyo wanakwenda motoni, maana hata hivyo, wao si ni maadui wa
Allah na dini yake?
Tuchukulie kuwa una watoto watatu – Amri, Hemedi na
Sauda. Amri anakuja kwako na kusema, “Baba, Hemedi na Sauda wamekataa kufua
nguo kama ulivyosema. Kwa hiyo nimewaua.”
Hivi, ni mwislamu gani atakayesema, “Safi sana mwanangu.
Wewe ndiye unayefaa kabisa kuwa mwanangu.”
Mungu ameumba waislamu pamoja na makafiri ambao “hawataki
kufua” – yaani hawataki kushika dini yake. Lakini kuna waislamu leo wanatarajia kuwa baada ya
kufa, labda watamwendea Mungu huyu aliyewaumba wanadamu wote, na kusema, “Baba,
nimeua makafiri mia moja kwa sababu walikuwa hawataki kufuata dini yako” –
ambao maana yake ni kuwa hao mia moja wameenda jehanamu ya moto.
Kwa maneno mengine, mwislamu huyu anachomwambia Mungu
hapo ni hiki: “Baba, nifungulie mlango wa pepo mimi kiumbe wako mmoja maana
nimepeleka viumbe wako mia moja jehanamu.”
Swali ni kwamba: Inawezekanaje wewe ukaenda mbinguni
kutokana na kupeleka wengine jehanamu? Tena wale mia moja ni watoto wa baba
yuleyule unayemwomba akufungulie mlango wa mbingu!
6.
Kama Mungu aliumba mbingu na nchi na kila kitu kwa neno lake tu, iweje leo neno lake hilohilo
lishindwe kubadili tabia tu za watu hadi Uislamu ulazimishe kwa nguvu ya upanga
kuliingiza neno hilo ndani ya wanadamu? Kwa nini nchi za Kiislamu kama vile
Iran, Saudi Arabia, n.k. zina polisi na mahakama kwa ajili ya kuzuia watu kutenda dhambi!!!!! Yaani polisi wanapita
huku na kule kuhakikisha watu hawazini, hawalewi, n.k. Ajabu mno! Hivi ni kweli
Allah anaweza kusema kwa ujasiri kwamba watu katika nchi hizo wanampenda? Si kwamba
watu kama hao wanaogopa tu polisi na mahakama?
Hata hivyo, wanachofanya polisi
ni kuzuia watu kutenda dhambi kwa nje. Je, moyoni inakuwaje? Au hamjui kwamba
wizi, uzinzi n.k. haukai mwilini bali moyoni? Maskini wee! Mbona Mungu wenu
kawaacha mnahangaika peke yenu? Mnahangaika kutafuta waumini kwa kutumia
upanga! Mkishawapata mnahangaika kuwalinda kwa polisi na mahakama ili wasitoke!
Mnahangaika kuzuia dini zingine kuhubiriwa kwenye nchi za Kiislamu ili watu
wasijui ukweli utakaowafanya wauache Uislamu! Kweli ndugu zangu mnatia huruma
kupita kiasi.
7.
Kama Uislamu ungekuwa na neno la kweli, kwa nini nchi za
kiislamu zinaogopa na kupiga vita kabisa Ukristo kuhubiriwa humo? Je, hii si
ishara kuwa mnafahamu kuwa watu watajua kweli ambazo zitawafanya waukimbie
Uislamu?
Natumaini ndugu zangu Hamudi na Maalim Moses na Waislamu wengine mtanisaidia kupata majibu ya maswali haya. Nawaalika mpokee wokovu wa Yesu Kristo kungali mapema, maana mlango wa wokovu utafika mahali utafungwa na wale wote ambao watakuwa wako nje, kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, gharika itawakumba. Na gharika ya sasa si ya maji, bali ni ya moto. Bwana Yesu akubariki ndugu msomaji.
rafiki yangu mzanzibari aliniambia mtume alisema vita vya kueneza uislam vimeisha, jihad iliyobaki ni mtu kupigana vita vya jihad ndani ya nafsi yake mwenyewe yaani mtu kupigana vita vya kuushinda mwili na nafsi yake dhidi ya matendo maovu.KAMA KWELI HAYO NI MANENO NA MAAGIZO YA MTUME MOHAMAD KIPENZI CHA WAISLAMU, HAKIKA MTUME HANA MFUASI HATA MMOJA! inasikitisha sana waislamu si wafuasi wa mtume wala si wafuasi wa YESU. kwa maneno mengine kulingana na maagizo hayo hapo juu ya mtume mohamad kipenzi cha waislamu,siku ya hukumu atawaambia ingawa niliwaagiza katika mafundisho yangu ya mwanzo kuwa mchukie adui zenu, mkate wezi mikono, wazinzi wapigwe mawe na mpigane jihad kwa ajili ya dini ya allah LAKINI MWISHO NILIWAAMBIA JIHAD IMEISHA JIHAD IMEBAKIA KWAKO MWENYEWE DHIDI YA NAFSI NA MWILI WAKO( yaani hakuna tena chuki dhidi ya wasiokuwa waislamu, hakuna kutetea dini ya allah, kukata watu mikono n.k) sasa ndugu zangu waislamu kwa muhamad kipenzi chenu hampo, kwa yesu hampo! mpo wapi? mmeamriwa kuwalinda na kuwahami wasiokuwa waislamu, kutokuharibu makanisa wala kuiba au kuchukua kwa nguvu mali ya kanisa na masinagogi. ni kwamba hamsomi QURAN au mnasoma QURAN nyingine tofauti na ile niliyoisoma? ( siku ya sabasaba ktk banda la wahamadiya), nilipowauliza kwa upole kwanini waislamu wanachoma makanisa kwa kigezo cha kuitetea dini ya allah, nao vijana wawili waliokuwepo wakanifungulia sura ( nimeisahau) niligutuka sana kwani niliyoyasoma ni kinyume 100% na imani na matendo ya waislamu. mwisho wakaniambia wao wahamadia wanafuata mafundisho ya muhamed ndio maana hawasapoti mambo yanayoshabikiwa na waislamu wengine na ndio maana waislamu wengine wanawakataa wahamadia .kwamba wao wanapigania ustawi wa jamii kama vile kufadhili na kujenga miradi ya maji, hospital, shule, misikiti n.k. kwa misingi hii huenda wahamadia ndio waislamu wengine hawa ni wafuasi wa dini iliyojificha ndani ya uislamu lakini si uislamu. --castor
ReplyDelete54 inasema siku kazaa lakini 69 inataja kwa idadi kabisa
ReplyDelete