Kifaa cha kuwekwa kwenye mkono
chini ya ngozi
Makala haya niliyatoa kwenye blog nyingine, inawezekana umeshayasoma,
lakini nimeona kuwa ni vema niyatoe tena hapa kwa ajili ya yeyote ambaye
hakupata nafasi ya kuyasoma. Hii ni kwa sababu ni makala ya muhimu sana,
yanayotuonyesha tuko wapi katika ratiba ya nyakati, majira na unabii.
Utakaposoma kilichoandikwa humu, itakuwa ni jambo jema kuwapatia hata
wengine unaowafahamu, ama kwa kwa njia ya baruapepe au kwa kuwaambia wasome
makala haya wao wenyewe katika blog hii. Mungu akubariki kwa hilo.
Imeandikwa:
Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa
maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume,
au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze
kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au
hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu
hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. (Ufunuo
13:16-18).
Kumbuka kwamba jina au chapa hii inawekwa kwenye mkono au kwenye kipaji cha
uso!!!
Maneno haya aliyasema Yeye aliye Alfa na Omega, yaani Bwana Yesu, kwenye
mwaka 96. Hiyo ni takribani miaka 1900 iliyopita; maana kitabu cha Ufunuo
kiliandikwa kwenye mwaka 96 baada ya Kristo.
Hebu piga picha kwamba unaishi kwenye miaka hiyo, halafu anatokea mtu mmoja
anakwambia, “Miaka 1900 ijayo watu watakuwa wanawekewa kitu mkononi au usoni
ambacho kitakuwa kinafuatilia nyendo zao zote.” Kwanza hutaelewa, na pili
unaweza kumdhania huyo anayekuambia kuwa amekosa cha kusema au amechanganyikiwa.
Lakini mimi nakwambia, mitazamo ya namna hiyo si ya miaka 2000 iliyopita
tu. Hata sasa hivi ipo kabisa – mitazamo ya kuona kwamba maandiko ya Biblia ni
upuuzi tu usio na maana.
Obama alipoingia madarakani, alikuja na mpango wa kuwapatia huduma za afya
raia wote wa Marekani; mpango unaojulikana kwa jina maarufu kama Obamacare.
Ili kutekeleza mpango huo, uliandaliwa muswada ambao ulipingwa na wengi
lakini hatimaye ulifanikiwa kupita na sasa umekuwa sheria. Labda unajiuliza,
“Kwani mpango afya una ubaya gani?” Kumbuka siku zote kwamba shetani anaitwa
‘kerubi afunikaye’ (Ezekieli 28:14). Kwa hakika, huo ni mpango mzuri kimwili,
lakini kiroho una walakini!
Ili kutekeleza mpango huu, hivi tunavyoongea sasa, kila Mmarekani anatakiwa,
hadi kufikia Machi 2013 awe amewekewa
kifaa ambacho kitawezesha utekelezaji wa mpango huo. Kifaa hicho kinajulikana
kama Radio-Frequency Identification microchip (RFID). Hiki ni kifaa kidogo cha kielektroniki
ambacho kimezidi kidogo punje ya mchele kwa ukubwa.
Baada ya kila mtu kuwekewa kifaa hiki, itaandaliwa orodha ya watu wote
wenye vifaa hivyo. Sehemu ya 2521, uk. 1001, kifungu kidogo cha 1, cha sheria
hii inasema:
The Secretary shall
establish a national medical device registry (in
this subsection referred to as the ‘registry’) to facilitate analysis of
postmarket safety and outcomes data on each
device that – “is or has been used in or on a
patient; and is a class III device; or a class II device that is implantable, life supporting or life sustaining.
Maana yake ni kwamba:
Katibu ataandaa orodha ya kitaifa ya vifaa vya kitabibu (ambayo katika
sehemu hii inaitwa ‘orodha’) ili kuwezesha uchambuzi wa data zitakazopatikana
kutoka kwenye kila kifaa baada ya kifaa kuwekwa
kwa mtu ama ndani
au nje (ya mwili); na kifaa hicho ni cha kundi la III; au ni cha kundi la
II kinachowekwa ndani ya mwili ...
Je, taarifa au data za mtu binafsi atakazoandaa Katibu ni zipi? Sheria
inabainisha kwamba Katibu atakachofanya ni:
including in the registry, in a manner consistent with subsection (f),
approppriate information to identify each device
described in paragraph (1) by type, model, and serial
number or other unique identifiers.
Yaani: orodha itajumuisha aina ya
kifaa alichowekewa kila mtu, modeli, namba yake, na taarifa zingine za kipekee zinazombainisha
na kumtofautisha na watu wengine.
Sasa, anaposema taarifa zingine za
kipekee maana yake ni nini? Hilo ni neno pana ambalo limewekwa hapo kimtego
na kwa kificho ili kufunika kusudi hasa la mpango wenyewe. Taarifa hizo,
kimsingi, ni kila kitu kinachokuhusu wewe, kwa mfano jina lako, umri, makazi,
urefu, alama za vidole, kundi la damu, rangi ya macho, asili yako, kazi yako,
makosa uliyowahi kufanya, n.k, n.k.
Lakini unaitwa mpango wa afya! Kerubi afunikaye!!
Wanafanyaje ili kukufuatilia? Sheria inaendelea kusema hivi katika ukurasa
wa 503, sehemu E juu ya majukumu ya Katibu:
encourage, as approppriate, the development and use of clinical registries
and the development of clinical effectiveness research data networks from the
electronic health records, post marketing drug and medical
device surveillance efforts.
Pamoja na yote yanayosemwa hapo juu, napenda tuangalie hayo maneno medical device surveillance efforts. Neno
surveillance maana yake ni
kuchunguza; kupeleleza. Hii ina maana kuwa Katibu ataandaa utaratibu
utakaowezesha kuchunguza na kufuatilia kila kifaa. Kwa lugha nyingine ni kwamba
kila aliyewekewa kifaa hiki, wanakuwa wanamfahamu vilivyo na wanaweza kumfuatilia
popote aliko kwa saa ishirini na nne!!
Ni kama ilivyo kwa simu yako, kokote utakakokuwa ambako mtandao
unapatikana, ukiwasha tu simu, mitambo inatambua mara moja kwamba simu namba
fulani imewaka na iko mahali fulani. Tofauti tu ni kwamba, simu unaweza kuzima;
lakini kifaa hiki cha Obamacare hakina swichi ya kuzima; kikiwaka kimewaka
maisha yako yote!!
Kwa mfano, katika ukurasa wa 58, sheria hii inasema: (D) enable the real-time (or near real time) determination of an
individual’s financial responsibility at the point of service and, to the
extent possible, prior to service, including whether the individual is
elligible for a specific service with a specific physician at a specific
facility, which may include utilization of a machine-readable health plan,
where feasible, near real time adjudication of claims.
Maana yake ni kwamba:
(D) kuwezesha
kutambua papo hapo au muda mfupi baadaye kiasi anachodaiwa mtaka huduma ya afya
wakati awapo kwenye kituo cha kutolea huduma na, pale inapowezekana, kabla ya
huduma, ikiwa ni pamoja na kubaini iwapo mhusika anastahili kupata huduma
fulani kutoka kwa mtoa huduma fulani kwenye kituo fulani, jambo ambalo
litajumuisha kuwapo kwa mpango wa afya unaosomeka kwa mashine, na
inapowezekana, kubaini papo hapo kiasi cha malipo ya huduma inayohusika.
Kwa lugha rahisi ni kuwa wanataka mtu akienda hospitali, mitambo imsome
kupitia kifaa kilichomo ndani yake na kubaini kama anastahili kupata huduma
sehemu hiyo. Na yanapotajwa malipo, maana yake ni kuwa kifaa hicho
kimeunganishwa na akaunti yako ya benki. Kwa hiyo, mara tu baada ya huduma,
unakatwa fedha papo hapo, na mtoa huduma naye analipwa papo hapo (ndiyo maana
ya real-time).
Na hii ndiyo maana ya maneno ya uhakika ya Bwana Yesu anaposema kutakuwa hakuna kuuza wala kununua bila kuwa na
chapa ya mnyama!! Huko tunakoelekea ni kwenye ‘cashless society’, yaani hakutakuwa
tena na fedha za noti au sarafu. Fedha yote inakuwa ni ya kielektroniki tu. Ili
ulipe au ulipwe, ni lazima uwe kwenye mfumo wa kielektoniki, yaani uwe na chapa
ya mnyama ndani ya mwili wako.
Sasa, hiyo chapa ya mnyama inawekwaje mwilini? Tazama video ifuatayo nawe
utapata jibu la swali hili.
Vilevile, tazama video ifuatayo uone jinsi chapa ya mnyama inavyofanya
kazi. Video hii si sinema ya kubuni. Ni hali halisi kabisa. Humo ndani utamwona
kijana ambaye ni mtu wa kujirusha; mtu wa viwanja.
Katika klabu anayoipenda kuna wateja wa aina mbili – wa kawaida na VIP. Wateja
wa kawaida ni wale wanaolipa kwa fedha za noti na sarafu. VIP ni wale wanaolipa
kwa mfumo huu ambao tunauzungumzia.
Kwanza kijana alienda kuwekewa kifaa hicho. Anapofika klabu, mitambo ya
pale inamtambua mara moja. Hata malipo yake ya tiketi na vinywaji yanafanyika ‘automatically’.
Pia, utaona jinsi ambavyo mdhibiti wa mitambo anavyoweza kuwafuatilia wenye
hiyo chapa kupitia kwenye skrini. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa wale watakaopokea
chapa ya mnyama!!
Rafiki, napenda nikueleze kabisa jambo moja. Kwa kuwa mpango huu ni wa
kishetani, lengo lake HASA si kutoa afya au kudhibiti biashara na fedha na
uchumi. Lengo lake hasa ni kuipata ROHO YAKO. Kwa hiyo, kuna mengi ambayo yamefichika
humo.
Kwa nini Bwana Yesu anatoa onyo lifuatalo? Na mwingine, malaika wa tatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu
awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika
kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya
ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe
cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika
watakatifu, na mbele za Mwana- Kondoo. (Ufunuo 14:9-10).
Kwani chapa ina shida gani? Ni wazi kabisa kwamba, teknolojia iliyopo
imefikia juu sana kiasi kwamba, watakapokuwekea chapa ya mnyama, si tu
watadhibiti nyendo zako na fedha zako, bali wataweza kudhibiti hata mawazo,
akili, na hisia zako kutokea mbali.
Na kwa sababu shetani hataki uende mbinguni; na mbinguni hakuna anayeweza
kwenda bila kumkubali Yesu moyoni na kumkiri kwa kinywa chake mwenyewe, basi,
akili yako ikishatekwa, unakuwa huna tena kamwe uwezo wa kuokoka.
Japokuwa tunaongelea jambo hili kana kwamba ni habari ya taifa la Marekani, kumbuka
kwamba tumeliangalia kiroho, si kimwili. Na kama hili ni suala la kiroho, ni wazi kuwa
shetani si mtawala wa Marekani. Anaitwa ni mungu wa duania. Kwa hiyo, lengo
lake ni kutawala dunia yote na kuizamisha pamoja naye katika jehanamu!
Ushauri
Ushauri mkubwa kabisa ninaokupa ni “OKOKA SASA!” Njoo kwa Yesu upone.
Lakini kwa wewe ambaye humtaki Yesu na umeamua ama kung’ang’ania dini au
dunia, weka maneno haya moyoni mwako ili, endapo wakati huu utakukuta, ujue cha
kufanya – maana wakati huo, nakuhakikishia kabisa – ubishi wote ulio nao utakuishia
kabisa!
- Usikubali kamwe kupokea chapa ya mnyama mkononi au usoni mwako.
- Ukikataa, shetani hatafurahi hata kidogo, maana unamzuia kukutawala na kukupeleka motoni.
- Hutaweza kununua chochote (dawa, chakula, nk). Kwa hiyo, utakuwa na maisha ya mateso makubwa mno.
- Utawindwa kama mnyama kila sehemu. Hivyo, maisha yako yatakuwa ya mashaka mengi. Na wakikukamata, watakupa nafasi ya kukubali chapa hiyo, au wakuue. Kubali ufe!
- Kanuni ya kwenda mbinguni ni moja tu: kumkiri Bwana Yesu kwa kinywa chako mwenyewe na kuamini moyoni mwako mwenyewe kuwa alifufuka kutoka katika wafu. Itakulazimu ufanye haya ndipo hata wakikuua, utaingia mbinguni. Vinginevyo, unaweza usipokee chapa, ukauawa, na bado mbinguni usiende.
Shetani anakuja; na Yesu naye
anakuja. Utakuwa upande gani? Wakati wa kuokoka ni sasa. Chukua hatua upate
salama ya roho yako.
No comments:
Post a Comment