Thursday, August 2, 2012

Wana wa Mungu


Nani ni "heroes" wa watoto wako. Je, ni wacheza mieleka? je, ni washika bunduki na wauaji wa kwenye sinema na video? Ukimnunulia zawadi mwanao, je, unamletea nini? Je, ni "toy" ya bunduki au ni nini?

Hatima ya mwanao iko mikononi mwako. Kile unachofanya au usichofanya angali bado mchanga ndicho kitakachoamua maisha yake ya baadaye; na hata uzima au mauti ya milele ijayo.


Contina

Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, ambayo baba zetu walituambia. Hayo hatutawaficha wana wao, huku tukiwaambia kizazi kingine, sifa za BWANA, na nguvu zake, na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya. Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu wawajulishe wana wao, ili kizazi kingine wawe na habari, ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao. (Zaburi 78:3-5).


Kanon Tipton

Wanao wakiyashika maagano yangu, na shuhuda nitakazowafundisha; watoto wao nao wataketi katika kiti chako cha enzi milele. (Zaburi 132:12).

Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, watoto wake watabarikiwa baada yake. (Mithali 20:7).

Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili. (Mithali 20:11).



Kanon Tipton

Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. (Mithali 22:6).

3 comments:

  1. sema kaka, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, mtoto mdogo unakuta mama yake mzazi anatukana matusi ya nguoni na mtoto yupo anasikia, what do you expect?unadhani mtoto atakuwa mstaarabu?
    mtoto jumapili hapelekwi kanisani eti amechoka alale, unadhani akikua atajua umuhimu wa kanisa, lazima wakirsto tubadilike jamani, misingi ya dini izingatiwe kwenye malezi, tusitegemee kufuga mtoto wa simba bandani halafu tutegemee atageuka ng'ombe ukubwani

    Barikiwa mtumishi

    ReplyDelete
  2. Ulichosema ndugu yangu ni kweli. Ni jambo la muhimu sana kuwalinda watoto kwa kuwakabidhi kwa Mungu ili Neno lake na Roho wake wawalinde.

    ReplyDelete