Thursday, August 23, 2012

Ndugu Waislamu Nisaidieni



Allah katika sura Al-Nisa 4:82 anasema kwamba:

Then do they not reflect upon the Quran? If it had been from [any] other than Allah, they would have found within it much contradiction.

Yaani:

Je, hawaitafakari Quran? Kama isingekuwa imetoka kwa Allah, hakika wangekuta ndani yake sehemu nyingi zinazopingana.


Ni wazi kuwa kile ambacho aya hii inakisema ni kuwa, quran haijikanganyi wala kujipinga hata kidogo. Na kutokana na aya hii, bila shaka Allah pia anamaanisha kuwa kutokuwapo kwa mkanganyiko wowote ndani ya quran ni kipimo tosha kuonyesha kuwa quran imetoka kwa Mungu wa kweli.

Na hiki kusema kweli ni kipimo kizuri cha kuonyesha iwapo jambo limetoka kwa Mungu wa kweli au la; maana Mungu wa kweli, kwa kuwa ni mkamilifu kwa asilimia mia moja, hawezi kusema hivi hapa, kisha aseme vingine kule – maana yeye hasahau kama mwanadamu. Hawezi kusema, “Nilikuwa na mambo mengi au mawazo mengi ndio maana nikasahau.”

Kwa hiyo, kimantiki, vilevile kutokana na aya hii, Allah au Mohammad anamaanisha kuwa, kama tukikuta kuna kupingana ndani ya quran, basi quran itakuwa haijatoka kwa Mungu wa kweli.

Sasa, kama hivyo ndivyo, hebu tuangalie maeneo saba yafuatayo (japokuwa yapo zaidi ya haya) ili tuweze kujua, kutokana na kipimo cha quran yenyewe, kama quran imetoka kwa Mungu wa kweli au la.

Niseme mapema kwamba, mimi si mjuzi wa quran. Kwa hiyo, ninaweza kuwa niko nje kabisa ya maana iliyokusudiwa. Lakini, nikiwa kama mtu ninayejaribu kumtafuta Mungu wa kweli, najaribu kujiuliza maswali katika huko kutafuta kwangu. Hivyo, kama wewe unajua majibu sahihi, nitashukuru kupata msaada wa maelezo yaliyo sahihi.

Nimetumia maandiko kutoka Kiingereza kwa kuwa mimi sifahamu Kiarabu; kisha nikayatafsiri kwa Kiswahili:

1.          Sura Al-Baqara 2:109

Many of the People of the Book wish, through envy, to lead you back to unbelief, now that you have embraced the faith and the truth has been made plain to them. Forgive them and bear with them until Allah makes known His will. He has power over all things.

Hapa quran inaongelea watu wa kitabu (yaani Wakristo), na kusema:

Wengi wa watu wa kitabu, kutokana na wivu wao, wanatamani kuwarudisheni kwenye kutoamini baada ya kuwa mmeamini, pamoja na kwamba ukweli umeshadhihirishwa wazi mbele yao. Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake. Yeye ana nguvu juu ya kila kitu. 

Quran pia inawaagiza Waislamu katika sura Al Imran 3:20  kwamba:

... if they give no heed, then your only duty is to warn them.

Yaani:

... kama wasipowasikiliza, basi ninyi kazi yenu pekee ni kuwaonya tu.

Kwa hiyo, kutokana na aya hizi mbili, yaani Al-Baqara 2:109  na Al Imran 3:20, tunaona mambo yafuatayo:

1.Ni wajibu wa Waislamu kuhubiri dini yao lakini si wajibu wao kuwalazimisha watu kuamini dini yao.
2.Allah kwa wakati wake atawafunulia wale wasioamini ukweli wa mambo.
3.Ni wajibu wa Waislamu kutoa maonyo tu kwa wale wanaowahubiria.

LAKINI, HEBU TAZAMA AYA ZIFUATAZO:

Al-Nisa 4:101

The unbelievers are your sworn enemies.

Yaani, 

Wale wasioamini ni maadui zenu wakubwa.

Vilevile inasema katika sura Al-Tawba 9:3

Proclaim a woeful punishment to the unbelievers.

Yaani:

Tangazeni mapigo makuu (ya ole) kwa wasioamini.

Pia quran inasema katika sura Al-Anfal 8:39

Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.

Yaani:

Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.

Maswali:

1.    Je, aliyempa Muhammad maneno ya 2:109, 3:20 na yale ya 4:101, 9:3, 8:39 ni huyo huyo au ni wawili tofauti?
2.    Iweje aseme kuwa usiwalazimishe watu kuamini bali waonyeni na kuwavumilia tu, kisha anageuka sehemu nyingine na kusema walazimisheni, tena kwa vita?
3.    Je, hii si ishara ya tabia ya usahaulifu ambayo si tabia ya Mungu bali ni ya mwanadamu?
4. Kama ni huyo huyo, je, aya hizi zinafanana au zinapingana?
5.    Kama zinafanana, ni kwa vipi?
6.    Kama zinapingana, huu si ushahidi tayari kuwa quran haitoki kwa Mungu wa kweli kama ambavyo quran yenyewe imeweka kigezo cha kujua hilo? Maana Mungu wa kweli hawezi hata kidogo kusahau jambo alilolisema kabla halafu aje aseme kitu tofauti. Ni viumbe tu ndio wanaweza kusahau na kukosea.

2.          Sura Al-Ankabut 29:6

Quran inasema:

Allah does not need his creatures’ help.

Yaani,

Allah hahitaji kusaidiwa na viumbe wake. (bila shaka ni katika kutekeleza makusudi na mipango yake).

LAKINI QURAN HIYO HIYO INAWAAMBIA WAISLAMU:

Sura Muhammad 47:7

If you help Allah, He will help you and make you strong.

Yaani,

Kama mkimsaidia Allah, yeye naye atawasaidia na kuwafanya kuwa imara.

Maswali:

1.    Umesema huhitaji msaada, kisha unasema tena unahitaji msaada! Je, Mungu anaweza kufanya jambo kama hilo?
2.    Aya hizi zinafanana au zinapingana?
3. Je, hii si ishara kuwa aya hizi zilisemwa tu ili kukidhi mahitaji ya wakati fulani, lakini msemaji alipoona anahitaji kuwafanya watu watende kinyume chake, akajikuta amesema tofauti na alivyosema siku za nyuma?

Na tena quran inasema katika sura Al-Baqara 2:244

Fight for the cause of Allah and bear in mind that He hears all and knows all.

Yaani:

Fanyeni vita kwa ajili ya Allah na mkumbuke kwamba anaona yote na anajua yote.

Maswali:

1.    Kama kweli Allah hahitaji msaada wa viumbe wake; na kama kweli aliumba ulimwengu wote kwa NENO TU, iweje NENO hilo hilo lisiweze kuwabadilisha wanadamu hadi alazimike kuliingiza ndani yao kwa nguvu, kwa vitisho na kwa ukali namna hiyo?

(Ukristo unashinda na kufanikiwa kwa NENO tu. Maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu wetu. Yeye aliumba kwa Neno; na sisi watoto wake, tunaumba kwa Neno hilo hilo. Tunahubiri tu na watu wanaokolewa, wanaponywa, wanalindwa na kusimama na Mungu wa kweli. Huoni kwamba hii hasa ndiyo maana ya nguvu ya Mungu? Hatuhitaji kuchinja au kupiga watu ili wampende Mungu!! Unawezaje, hata tu wewe mwenyewe, kumfanya mwanao au mkeo akupende kwa njia ya vipigo na kulazimisha? yaani, ukitaka mwanao au mkeo akupende utamshikia rungu au panga au bunduki? Je, hiyo si ishara kwamba wewe huna nguvu ndiyo maana unalazimisha? je, huko si kujikanganya maana umetuambia kuwa wewe ni Mungu unayeweza yote?)
2.    Je, Allah anapotaka wanadamu wanaomwamini wafanye vita ili kuwalazimisha wasioamini wamwamini, huko si kutaka msaada kwa viumbe wake?

3.          Sura Al-Shura 42:40

Let evil be rewarded with like evil. But he that forgives and seeks reconcilement shall be rewarded by Allah.

Aya hii inamaanisha kuwa yule anayemwamini Allah akitendewa uovu basi anatakiwa alipe uovu, lakini akisamehe atapata thawabu!

Maswali:

1. Kama aliyetenda uovu anakuwa ametenda jambo baya ambalo halitakiwi na halikubaliki, iweje lile la mlipa kisasi litakiwe na kukubalika? Huku si kujikanganya?
2. Lakini hapo hapo, Allah anasema kuwa mwislamu anayesamehe na kusaka maelewano atapata thawabu kutoka kwa Allah. Unawezaje kukubali vitu viwili vinavyopingana? Kwa mfano, unawezaje kusema kuwa, mtu akikutukana, nawe ukimtukana ni sawa; na usipomtukana ni sawa!
3. Kikubwa kuliko chenzake ni kipi hapa sasa? Je, ni kulipa kisasi au kusamehe? Mbona mambo yenyewe hata hayafanani? Yanawezaje kwenda pamoja?

4.          Sura Al-Kafirun 109:1-6

Say, "O unbelievers, I do not worship what you worship, nor do you worship what I worship. I shall never worship what you worship, nor will you worship what I worship. You have your own religion and I have mine."

Yaani,

Enyi msioamini, mimi siabudu mnachoabudu, wala ninyi hamuabudu ninachoabudu. Mimi kamwe sitaabudu kile mnachokiabudu, wala ninyi kuabudu kile ninachokiabudu. Ninyi mnayo dini yenu, nami nina yangu.

Pia, quran inasema katika sura Al-Baqara 2:256

There shall be no compulsion in religion.

Yaani:

Hakutakuwapo na kulazimishana katika dini.

LAKINI ALLAH HUYO HUYO ANASEMA:

Sura Al-Anfal 8:39

Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.

Yaani:

Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.

Maswali:

1. Aliyemwambia Muhammad asiwalazimishe wasioamini kuamini Uislamu ndiye huyo huyo aliyemwambia afanye vita?
2. Aliyesema kuwa “ninyi msioamini hamtaabudu ninachoabudu” ndiye huyo huyo anayesema ni vita tu hadi dini ya Allah itawale?
3. Na je, aliyesema kuwa hakuna kulazimishana katika masuala ya dini ndiye huyo huyo anayesema watu wake wapigane vita?
4.    Huku si kujipinga mwenyewe?

5.          Sura Al-Baqara 2:177

Righteousness is not that you turn your faces toward the east or the west, but [true] righteousness is [in] one who believes in Allah ...

Yaani:

Haki (mbele za Mungu) haitokani na mtu kugeukia mashariki au magharibi. Mtu mwenye haki ni yule anayemwamini Allah ...

LAKINI QURAN HIYO HIYO INASEMA:

Sura Al-Baqara 2:144

Indeed, we see you look repetedly towards heaven. We will make you turn towards a qiblah that will please you. So turn your face towards the sacred Mosque (qiblah). Wherever you are, turn your faces to it.

Yaani:

Tumekuona unavyoelekeza macho yako mbinguni tena na tena. Tutawafanya muigeukie qiblah itakayowafurahisha. Hivyo, geuzeni nyuso zenu kuelekea msikiti mtakatifu [japo quran zingine zinasema ‘towards al-Masjid al-Haram’ – najiuliza 'Haram' maana yake nini!!]

Maswali:

1.    Kama aliyesema aya hizi mbili ni yuleyule; na ni Mungu wa mbinguni, inakuwaje zinapingana?
2.  Kama zimetoka kwa Mungu wa mbinguni, si jambo la ajabu kuona kwamba hapendi watu waelekeze macho yake kule aliko badala yake waelekeze kwingineko? 
3. Kama wewe tunayekuabudu uko juu, kwa nini hautaki tuelekeza macho yetu huko? Huu si mkanganyiko?
4. Na kama wewe ni Mungu uliye mahali KOTE, kwa nini nielekeze macho yangu sehemu moja?

6.          Sura Al-Nisa 4:135

Believers, conduct yourselves with justice.

Yaani, 

Enyi mlioamini, enendeni kwa njia ya haki.

Hapa Allah anazungumzia juu ya haki.

LAKINI ALLAH HUYO HUYO ANASEMA:

Sura Al-Nisa 4:129

In no way you can treat your wives in a just manner even though you may wish to do that...

Yaani:

Haiwezekani kamwe kwa ninyi kuwatendea haki wake zenu hata kama mngependa kufanya hivyo ...

Maswali:

1.    Aya hizi zinafanana au zinapingana?
2.    Kama hazipingani ni kwa vipi?


7.          Sura Al-Nahl 16:28

The angels will say to those whom they cause to die in purity, ‘Peace be on you.’ Come into paradise for what you did.

Yaani:

[Kuhusu wale wanaoingia mbinguni] – Malaika watasema kwa wale ambao watawafanya wafe katika usafi (utakatifu), ‘Amani na iwe juu yenu. Ingieni paradiso kutokana na matendo yenu.’


LAKINI, QURAN HIYO HIYO INASEMA:


Sura Al-Hijr 15:45-47

Indeed, the righteous will be within gardens and springs, [Having been told], "Enter it in peace, safe [and secure]."  And We will remove whatever is in their breasts of resentment, [so they will be] brothers, on thrones facing each other.

Yaani:

Wenye haki (watakatifu) watakaa kwenye bustani na chemchemi za maji, kwa amani na usalama wataingia humo. Nasi tutaondoa chuki yote ndani ya mioyo yao.

Maswali:

1.   Katika 16:28, inaonekana kwamba watakaiongia peponi ni watu walio safi kwa sababu malaika wamesababisha watu hao wafe wakiwa safi. Lakini 15:45-47 inaonyesha kuwa wataingia peponi wakiwa na chuki mioyoni mwao. Je, chuki ni sehemu ya usafi?
2.    Je, aya hizi zimetoka kwa mtoaji yule yule?
3. Kama chuki ni mbaya kiasi cha kuhitajika kuondolewa mioyoni mwa Waislamu wanaoingia peponi, iweje wakiwa duniani wanaagizwa kuwachukia wale wasio Waislamu (kama tulivyoona kwenye 4:101)?


HITIMISHO

Hizi ni baadhi tu ya aya ambazo zinaonyesha kuwa quran au Allah anasema jambo moja hapa, kisha anajipinga mwenyewe katika sehemu nyingine.

Na ukweli huu, ninavyodhani,unamaanisha kuwa, ama:

1. Si kila aya iliyo kwenye quran ni maneno ya Mungu muumba vyote – maana Mungu huyo hawezi kufanya mambo kama hayo; au
2. Quran haitokani na Mungu bali imetokana na chanzo kingine, ndiyo maana inaonyesha tabia za viumbe za kujisahau au kutojua mambo yote, hususan yajayo.

Nadhani siku ya mwisho Muhammad atawakana watu wote wanaomwamini maana atakuja kusema kwamba, “Mimi niliwaambia kuwa wakitaka kujua kama quran inatoka kwa Allah waangalie kama quran inajikanganya. Sasa waliona kuwa inajikanganaya, lakini wao wakendelea tu kuiamini.

Pia Muhammad atawakana wale wote wanaomwamini na kumfuata kwa sababu yeye mwenyewe anasema wazi katika  sura Al-Ahqaf 46:9,

... nor do I know what will be done with me or you. I follow only what is revealed to me.

Yaani,

... na wala mimi sifahamu kile nitakachotendewa wala kile ninyi mtakachotendewa. Mimi nafuata tu kile ninachofunuliwa.

Swali ni kwamba, je, kama mtu mwenyewe anakiri kuwa hajui hatima yake wala hatima ya wale wanaomfuata, je, kama ni kweli Mungu wa mbinguni ndiye aliyempatia quran, je, angekaa kimya kweli juu ya suala la HATIMA za wanadamu? Yaani jibu la mtu atakuwa wapi MILELE lingeachwa hewani tu hivihivi? Na kama Muhammad hajui hili na bado anataka watu wamfuate, je, ni hilohilo tu asilolijua au yapo na mengine asiyoyajua? Bila shaka hii inaashiria kuwa yako mengi asiyoyajua.

Sijui kwa kweli! Kama nilivyosema, mimi kwa mambo haya ni maamuma tu. Kwa hiyo, inawezekana niko nje kabisa ya kile kinachomaanishwa. Nitafurahi kama ndugu zangu Waislamu mtanisaidia kujua mambo haya.

Lakini kwa ule upande ambao mimi naufahamu zaidi, yaani Ukristo, Bwana Yesu anasema: Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.  (Yohana 14:6). Yaani, hakuna namna ya kwenda mbinguni isipokuwa kwa kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Hiyo ndiyo namna pekee ya kufika mbinguni. Tafakari!

52 comments:

  1. Ndugu James John,

    Nimekujibu katika link hii,

    Soma jibu lako hapa,

    http://sekenke.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu asante sana kwa jibu majibu yako. Ninayapitia ili nione kile kilichomo. Nashukuru sana.

    ReplyDelete
  3. 1) Aya hi 4:101 inawaelekeza waislamu wafanye nini katika vita (Anae kupiga vita ni adui yako, au sio?aya hii haipingani na aya ya 2:109) aya hiyo inasema hivi,

    Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi (Quran 4:101).

    Na unapo kuwa pamoja nao, ukawasalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na wachukue silaha zao. Na watakapo maliza sijida zao, basi nawende nyuma yenu, na lije kundi jingine ambalo halijasali, lisali pamoja nawe. Nao wachukue hadhari yao na silaha zao. Walio kufuru wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkawa wagonjwa, mkaziweka silaha zenu. Na chukueni hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha(Quran 102).

    Pia aya ya 8:39 ilishuka wakati wa vita (makafiri walikuwa wanawatesa waislamu, Waislamu wanaambiwa wapingane nao (self defence) lakini wakiacha kupigana na nyie na kuwatesa waacheni),

    Aya hiyo inasema hivi,

    Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda. (Quran 8:39).
    Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema (Quran 40).

    2) Kuhusu aya ya 47:7

    Hiyo ni lugha ya mifano (kama unaijua Biblia vizuri, bila shaka unajua maana ya lugha ya mifano)
    Nikisema hivi,

    "Mimi sihitaji shilingi elfu kumi zako lakini ukitoa hizo shilingi elfu kumi kwa ajili ya dini yangu (kama vile kusaidia masikini..) nitahakikisha kuwa kweli unanipenda".

    Hapa kuna contradiction gani ?

    au rafiki yangu mpendwa hajui lugha ya mifano ?

    3) Jiulize kwa nini inchi zote duniani zimeamua kuweka jela ?

    Nadhani jawabu unalijua, au sio ?

    Kuwaadhibu wahalifu au sio ?

    Aya tukufu ya 42:40 inasema hivi,

    Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.
    4) Jibu la swali lako hili lipo hapo juu (katika jawabu namba moja)

    5) Jawabu lako lipo katika aya hii ya Quran Tukufu 2:142,

    Quran Tukufu inasema hivi,

    WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka (Quran 2:142).

    6) Aya hiyo tukufu 4:129,

    Inaelezea ukweli wa mwanamme anapo owa wake zaidi ya mmoja (lazima atampenda mmoja zaidi lakini hata hivyo asimili moja kwa moja akamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa, ajaribu kadiri ya uwezo wako kufanya uadilifu).

    Aya hiyo inasema hivi,

    Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu (Quran 4:129).

    7) Haha Haiiii, rafiki mbona unaanza kudanganya sasa, aya ya 16:28 inasema hivi,

    Ambao Malaika waliwafisha nao wamejidhulumu nafsi zao! Basi watasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya uovu wowote. (Wataambiwa): Kwani! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyo kuwa mkiyatenda (Quran 16:28).

    Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni maovu mno makaazi ya wafanyao kiburi! (Quran 16:129)

    Nimekujibu maswali yako yote (Alhamdulillah), na mimi nakuomba unijibu yangu.

    1) Nani msemaji katika Biblia ?
    2) Je Biblia yote ni maneno ya Mungu ?
    3) Kama Biblia ni maneno ya Mungu kwa nini yanapingana yenyewe kwa yenyewe ?

    Kwa maelezo zaidi soma hapa

    http://www.project-reason.org/bibleContra_big.pdf

    Nasubiri jibu.

    ReplyDelete
  4. UTATU
    Kwa mujibu wa Wakristo wengi, Yesu amekuwa ni Mungu-mtu, mtu kamili na Mungu kamili. Je, kitu chenye mwisho na kile kisicho na mwisho vinaweza kuwa ni kimoja? Kuwa “Mungu kamili” maana yake ni kutokuwa na mwisho na kutohitajia msaada, na kuwa “mtu kamili” maana yake ni kutokuwa na uungu.

    1. Kuwa mtoto ni kuwa chini ya daraja ya uungu na kuwa na uungu ni kutokuwa mtoto wa yoyote. Vipi Yesu atakuwa na sifa ya utoto na uungu kwa wakati mmoja?

    2. Wakristo wanadai kwamba Yesu alidai kuwa yeye ni Mungu wakati walipomnukuu katika Yohana 14:9: “…Aliyeniona mimi amemwona Baba…” Je, Yesu hakusema wazi wazi kwamba: kamwe watu hawakumuuona Mungu, kama inavyosema Yohana 5:37: “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona”?

    3. Wakristo wanasema kwamba Yesu alikuwa ni Mungu kwa sababu alikuwa anaitwa mtoto wa Mungu, Mtoto wa mwanadamu, Masiha, na “mwokozi.” Ezekiel aliandikwa katika Biblia kama ni mtoto wa Mungu. Yesu alinena kuhusu “waletao amani” kuwa ni Watoto wa Mungu. Mtu yoyote aliyefuata matakwa na Mipango ya Mungu alikuwa akiitwa MTOTO WA MUNGU katika utamaduni wa Kiyahudi na katika lugha yao (Mwanzo 6:2,4; Kutoka 4:22; Zaburi 2:7, Warumi 8:14) neno “Messiah” ambalo kwa Kiebrania linamaanisha “Mpakwa Mafuta wa Mungu” sio “Kristo”, wala “Cyrus” na mtu huitwa “Messiah” au “mpakwa mafuta”. Ama kuhusu neno “mwokozi” liliopo katika Wafalme wa pili 13:5, watu wengine walipewa jina hilo vile vile bila ya kuwa miuungu. Kwa hivyo, katika maneno hayo uko wapi uthibitisho unaoonesha kuwa Yesu ni Mungu wakati neno mtoto halikutumiwa kwake peke yake?

    4. Wakristo wanadai kwamba Yesu alikiri kwamba yeye na Mungu walikuwa ni kitu kimoja kwa maana ya Kimaumbile pale anaposema katika Yohana 10:30; “Mimi na Baba tu umoja.”, Baadae katika Yohana 17:21-23, Yesu alinena kwamba wafuasi wake, yeye mwenyewe na Mungu ni kitu kimoja katika sehemu tano. Sasa kwa nini walipe neno “Kitu kimoja” la kwanza maana nyingine tofauti na yale maneno “kitu kimoja” katika sehemu tano nyinginezo?

    5. Je, Mungu ni watatu-katika-mmoja na ni mmoja katika watatu kwa wakati mmoja au ni mmoja kwa wakati huo huo?

    6. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, kwa hiyo hakuna hata mmoja kati ya hao watatu ambae ni Mungu kamili. Tukikubali kwamba huo ndio ukweli, sasa je, wakati Yesu alipokuwa duniani, hakuwa Mungu kamili, wala “Baba aliyembinguni” hakuwa Mungu kamili. Je, hilo halileti mkanganyiko kwa kile alichokuwa akikisema Yesu kila siku kuhusu Mungu wake na Mungu wetu aliyembinguni, Bwana wake na Bwana wetu? Je, hilo vile vile halimaanishi kwamba hakukuwa na Mungu kamili, katika kipindi cha kati ya dai la kusulubiwa na dai la kufufuka?

    7. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, sasa nani aliyekuwa Mungu huko mbinguni wakati Yesu alipokuwa aridhini? Je, hili halileti mkanganyiko na yale aliyokuwa akiyasema mara nyingi juu ya kuwa Mungu aliyembinguni ndiye aliyemtuma?

    8. Ikiwa Mungu ni mmoja na watatu kwa wakati mmoja, je, nani aliyekuwa Mungu huko mbinguni katika zile siku tatu zilizo kati ya dai la kusulubiwa na dai la kufufuka?

    9. Wakristo husema kwamba: “Baba (B) ni Mungu, Mwana (M) ni Mungu na Roho Mtakatifu (R) ni Mungu, lakini Baba si mwana, na Mwana si Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu si Baba”. Kwa hesabu rahisi na kwa kanuni inakuwa hivi, ikiwa B = G, M = G na R = G; kwa kufuatanisha inakuwa B = M = R, wakati sehemu ya pili ya maelezo hayo inaonesha kuwa B№ M№ R (inamaanisha haziko sawa). “Sasa je, huo si mkanganyiko na imani ya Wakristo juu ya utatu wenyewe?

    10. Ikiwa Yesu alikuwa Mungu, kwa nini alimwambia yule mtu aliemwita Yesu “Bwana Mwema” alimwambia asimwite “mwema” kwa sababu hakuna mwema ila Mungu wake aliyembinguni peke yake?

    ReplyDelete

  5. 11. Kwanini Wakristo wanasema kwamba Mungu ni watatu katika mmoja na mmoja katika watatu, wakati Yesu alisema katika Marko 12:29. “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” kama ilivyo katika sehemu nyingi ndani ya Biblia.

    12. Ikiwa kuamini utatu lilikuwa ni jambo la lazima ili uwe Mkristo, kwa nini Yesu hakulifundisha na wala hakulisisitiza jambo hilo kwa Wakristo katika zama zake? Je, vipi hao wafuasi wa Yesu wachukuliwe kuwa ni Wakristo bila ya kulisikia neno utatu? Kama ingekuwa utatu ndio uti wa mgongo wa Ukristo, Yesu angeliufundisha na angeliusisitizia na angeliufafanua kwa watu wake kikamilifu.

    13. Wakristo wanadai kwamba Yesu alikuwa Mungu kama walivyomnukuu katika Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu”. Hayo ni maneno ya Yohana na si maneno ya Yesu, vile vile, neno la kwanza la Kigiriki kwa ajili ya Mungu ni “HOTHEOS” ambalo linamaanisha “Mungu” likiwa na M kubwa, wakati neno la pili la Kigiriki kwa ajili ya Mungu ni “TONTHEOS” ambalo linamaanisha “mungu” likiwa na “m” ndogo. Je, huko si kukosa uaminifu kwa wale waliotafsiri Biblia ya Kigiriki? Je, nukuu hiyo ya Yohana 1:1 iliyotambuliwa na kila mwanazuoni wa Kikristo aliyeisoma Biblia kwamba imeandikwa na Myahudi aitwae Philo Alexandria kabla ya Yesu na Yohana?

    14. Je, neno “god” au “TONTHEOS” pia halikutumika kuashiria wengine kama ilivyo katika Wakorinto 2 4:4 (Na Shetani ndie) mungu wa ulimwengu huu na katika Kutoka 7:1 “Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; ?

    WOKOVU:

    Wakristo wanasema kwamba “MUNGU AEMTOA” mwanawe wa pekee ili kutuokoa sisi”. Je, Mungu alimtoa Yesu kumpa nani wakati yeye Mungu ndiye mmiliki wa ulimwengu wote?

    15. Ikiwa ilikubalika kwa utukufu wa Mungu kuwa awe na watoto, basi angeumba mamilioni ya watoto kama Yesu. Sasa kuna jambo gani kubwa kumhusu huyu mtoto wa pekee?

    16. Kwa nini Biblia inasema kwamba Yesu alitaka kufa msalabani, huku yule mtu aliyesulubiwa pale msalabani alikuwa anapiga kelele “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” kwa mujibu wa Matayo 27:45 na Marko 15:33?

    17. Ikiwa Mungu alitaka kutuokoa, Je, angeshindwa kutuokoa bila kumtoa muhanga Yesu?

    18. Mungu yeye mwenyewe ni haki, na haki inataka kusiwepo na mtu anayepaswa kuadhibiwa kwa madhambi ya wengine, vile vile haipaswi kuadhibiwa watu wengine kwa kuwaokoa wengine: Je! Dai la kwamba Mungu amemtoa muhanga Yesu ili kutuokoa haliteti mkanganyiko kama kweli Mungu ni mpenda haki? Je, Dai hilo halitofautiani na maana halisi ya haki?

    19. Watu wanatoa muhanga vitu vyao ili kupata vitu vingine wasivyokuwa navyo ikiwa haiwezekani kuwa navyo vyote viwili kwa wakati mmoja. Wakristo wanasema kwamba “Mungu alimtoa muhanga mtoto wake wa pekee ili kutuokoa; Tunajua kwamba Mungu ni Mwenye nguvu; Mungu alimtoa Muhanga Yesu kwa nani?

    20. Kutoa muhanga kitu maana yake ni kwamba huwezi kukipata tena kile ulichokitoa; sasa kuna siri gani katika kutolewa Muhanga Yesu wakati Mungu aliweza kumrudisha Yesu baada ya kusulubiwa (kwa mujibu wa maneno ya Wakristo)?

    ReplyDelete
  6. 21. Ikiwa Wakristo wote wameokoka kwa kupitia Yesu na wanakwenda Peponi (kwenye uzima wa milele) bila kujali matendo yao, kwa hiyo mafundisho ya Yesu hayana umuhimu wowote na maana ya maneno “uovu” au “wema” hayana umuhimu wowote. Ikiwa hali sivyo hivyo, kwa hiyo wale Wakristo ambao wanamwamini Yesu lakini hawafuati mafundisho yake wala hawajatubu watakwenda motoni?

    22. Vipi Wakristo wanayachukulia matendo kama kitu kisicho na umuhimu baada ya kuwa kitu kimoja wakati Yesu aliposema katika Matayo 12:36; “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.”?

    23. Wakristo wanasema kwamba watu wanakwenda Peponi kwa kupitia Yesu tu! Wakati Paulo anasema katika 1 Wakorintho 7:8-16 kwamba Mume asieamini anakubalika kwa Mungu kwa sababu anaunganishwa na mke wake na kinyume chake, na watoto wao wasio na dini vile vile wanakubalika kwa Mungu. Kwa hivyo kumbe watu wanaweza kwenda Peponi bila ya kumwamini Yesu; kutokana na maneno hayo.

    24. Vipi Biblia inasema kwamba Waisraeli wote wameokoka ingawa hawamwamini Yesu? Je, Hili halipingani na dai la Biblia ya kuwa njia ya pekee ya kwenda Peponi ni kwa kupitia Yesu tu?

    25. Kwa mujibu wa Wakristo, wale wote ambao hawakubatizwa watakwenda motoni. Kwa hivyo hata watoto wachanga nao watakwenda motoni kwa vile walikufa kabla ya kubatizwa; kwa vile walizaliwa na dhambi la asili la kurithi? Je, hili halipingani na maana ya neno haki; kwanini Mungu awaadhibu watu kwa madhambi wasiyoyatenda?

    ROHO MTAKATIFU

    Sehemu pekee katika Biblia alipotajwa Roho Mtakatifu ni katika Yohana 14:26; “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote niliyowaambia. “Ni kipi kile ambacho Roho Mtakatifu ameleta au kufundisha kwa miaka 2000 iliyopita?

    26. Wakristo wanasema kwamba Msaidizi maana yake ni Roho Mtakatifu (Yohana 14:26) Yesu alisema katika Yohana 16:7-8. “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu;” Hii haiwezi kumaanisha Roho Mtakatifu; kwa vile Roho Mtakatifu inasemekana kwamba alikuwepo hata kabla ya Yesu hajazaliwa kama ilivyo katika Luka 1:41 “Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu”. Hapa, Roho Mtakatifu vile vile alikuwepo wakati wa Yesu: sasa vipi hii imaanishe kwamba ni sharti aondoke Yesu ndipo Roho Mtakatifu aweze kuja?

    27. Katika Yohana 16:7-8, inasema; “Bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” Je, hii “Yeye” hapa inamaanisha nini? Je, viwakilishi hivyo havimaanishi mtu mwanamume?

    28. Je, Roho Mtakatifu anazungumza na Wakristo wema na waovu vile vile? Je, Roho Mtakatifu yu pamoja nao wakati wote au wakati fulani tu? Je, ni wakati gani anaanza kumtembelea mtu atakaye kuwa Mkristo?

    29. Utasemaje kuwa wewe ni Mkristo ikiwa Roho Mtakatifu yu ndani ya Mkristo mwingine? Inakuwaje Wakristo wengi wanawapumbaza watu kwa kudai kwamba Roho Mtakatifu yu ndani yao tu! Na baadaye wanabadilisha dini?

    30. Je, Roho Mtakatifu anaamuru kile ambacho Wakristo wanapaswa kukifanya bila ya uhuru wa kuchagua hata kidogo au anawaongoza tu na wao wana uhuru wa kufuata au kuto fuata?

    ReplyDelete
  7. 31. Ikiwa Roho Mtakatifu anaamuru kile Wakristo wanachopaswa kukifanya, kwa nini Wakristo wanafanya maovu na madhambi? Vipi unaweza kuuelezea ubadilishaji wa dini na kuingia dini na imani mbali mbali kunakofanywa na Wakristo wengi? Je, Wanaambiwa kufanya hayo na Roho Mtakatifu?

    32. Ikiwa Roho Mtakatifu anawaongoza Wakristo tu, na wako huru kufanya wanavyotaka, sasa ni vipi tutajua kwamba waandishi wa Biblia hawakufanya makosa wakati walipoziandika?
    33. Ikiwa Wakristo wanaamini kwamba Roho Mtakatifu huwajia na kuzungumza nao kila siku, kwanini hawamuulizi Roho Mtakatifu kuhusu chapisho lipi la Biblia wanalopaswa kulifuata kwa vile kuna machapisho mengi?

    KAZI YA UJUMBE WA YESU Hivi bila ya kuazima kutoka katika dini na mifumo mingine, Ukristo unaweza kuwapa wanadamu mfumo kamili wa maisha? Huku Ukristo ukiwa umefungika kwa maisha ya kiroho tu na hautoi sheria, sasa vipi jamii itaweza kuamua sheria zipi ni sahihi na zipi ni makosa?

    34. Kwa nini Wakristo wanasema kwamba Yesu alikuja kwa ajili ya ulimwengu mzima wakati yeye alisema kuwa alitumwa kwa Mayahudi tu? Alimwambia yule mwanamke Mkananayo aliyemuomba amtibie bintiye aliyekuwa anasumbuliwa na mapepo: “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” na pia alisema; Si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.” (Matayo 15:21-28).

    KUFUFUKA KWA YESU Ikiwa utasoma Matayo (28: 1-10), Marko (16:1-20), Luka (24:1-12), na Yohana (20:1-18) utakuta habari zenye kutatanisha: Maandika yote hayo yanakubali kwamba kaburi lilikuwa linalindwa kwa muda wa siku tatu. Hata hivyo, maandiko hayo yanaonesha kugunduliwa kwa kaburi kuwa ni tupu katika hali tofauti.

    1 Matayo (28) na Yohana (20) zinaeleza kwamba Maria Magdalena na Maria wengine walikuwa ndio watu wa kwanza kuliona lile kaburi.

    2 Marko (16) inaeleza kwamba Maria Magdalena, Maria mama, James na Salome walikuwa wa kwanza kuliona kaburi likiwa tupu.

    3 Marko (28) inaeleza kwamba kulikuwa na tetemeko la ardhi ambalo lililoondosha jiwe lililokuwa juu ya kaburi. Anasema kwamba Malaika ndie aliesababisha hivyo: Maandiko mengine hayataji kuwepo kwa tetemeko la ardhi.

    4 Matayo na Marko wanasema kwamba mwanamume mmoja tu aliyevaa mavazi meupe ndiye alikuwa malaika.

    5 Luka inasema wanamume wawili waliovalia mavazi meupe, ambao walikuwa malaika, ndio waliokuwa wamekaa juu ya kaburi. Yohana inasema kwamba wale wanawake wawili hawakumkuta mtu yoyote kwa mara ya kwanza walivyokwenda kwenye kaburi, lakini waliporudi tena, waliwaona watu wawili, mmoja alikuwa Malaika na mwingine alikuwa Yesu.

    6 Matayo inasema kwamba, wakati walinzi walipotoa taarifa hizi kwa Kuhani mkuu, yule Kuhani mkuu aliwalipa kiasi kikubwa cha pesa, na kuwaambia “Mnapaswa kusema kwamba wafuasi wake walikuja nyakati za usiku na kuiba mwili wake”. Alidai kwamba askari walichukua pesa na kusambaza habari hiyo na toka hapo, hadithi ilikuwa ni yenye kuzunguka kati ya Wayahudi; mpaka leo (kwa mujibu wa Matayo). Maandiko mengine hayasemi chochote kuhusu jambo hilo.

    ReplyDelete
  8. 35. Ni maelezo yapi ambayo ni ya kweli?

    36. Kwa nini Yesu alipojitokeza baada ya tendo la kusulubiwa inachukuliwa kama ndio kigezo (uthibitisho) wa kufufuka kwake wakati kuna maelezo yasemayo kwamba si yeye aliyesulubiwa wala aliyekufa kwani aliyesulubiwa ni mtu mwingine wakati Mungu akimwokoa Yesu?
    37. Vipi Matayo alijua dai au hoja ya makubaliano kati ya wale askari na yule kiongozi? Hivi mtu hawezi kusema kwamba kuna mtu aliyewalipa wale wanawake kiasi kikubwa cha pesa na akawaambia waeneze maneno yale ya kwamba Yesu alifufuka, pamoja na uthabiti huo huo kama ule wa habari ya Matayo.

    38. Kwanini walimwamini yule mtu aliekuwa na mavazi meupe? Kwa nini walimuamini kwamba alikuwa ni malaika? Maelezo ya Yohana ni ya kustaajabisha sana, kwa vile yeye alisema kuwa Maria hakumtambua Yesu (ni yupi kati ya wale watu wawili) wakati alipokuwa akizungumza nae, hali alimtambua tu wakati yule mtu alipomwita Maria kwa jina lake?

    39. Vipi lile kaburi lililokuwa tupu lina thibitisha kwamba Yesu alisulubiwa? Je, Mungu hawezi kumtoa mtu mwingine kutoka kaburini na kumfufua?

    40. Injili inaaminiwa kuwa ni maneno asilia ya Mungu, yanasadikiwa kwamba yalisemwa na Roho Mtakatifu kwa wafuasi wake ambao waliyaandika. Ikiwa chanzo chake ni kimoja, kwanini yasilingane katika kulizungumzia tukio lile muhimu? (la kufufu Yesu).

    41. Vipi Matayo, Marko, Luka na Yohana waliweza kuchukuliwa kama mashahidi walioona Yesu akifufuka wakati Biblia inatuambia kwamba hakuna mtu aliyemuona Yesu akitoka ndani ya kaburi?
    BIBLIA Ikiwa Wakristo wanachukulia Agano la Kale kwamba ni maneno ya Mungu, kwa nini walibatilisha baadhi ya maandiko katika Agano la Kale ambayo yalikuwa yakizungumzia adhabu (kwa mfano adhabu ya uzinzi)?

    42. Kwanini Marko 16:9-20 haipo kwenye machapisho mengi ya Biblia wakati katika baadhi ya machapisho imejitokeza kama tanbihi ya chini ya ukurasa tu au imewekwa katika mabano? Je, tanbihi ya chini ya ukurasa katika Biblia nayo inachukuliwa kuwa ni maneno ya Mungu, hasa hasa wakati inapozungumzia jambo muhimu kama la kupaa kwa Yesu?

    43. Kwa nini Biblia ya Kikatoliki ina vitabu 73 ndani yake wakati Biblia ya Kiprotestanti ina vitabu 66 tu ndani yake? Wakati zote mbili ya Kikatoliki na Kiprotestanti zinadai kuwa na maneno kamili ya Mungu, ipi inatakiwa iaminiwe na kwa nini; kwa kigezo gani?

    44. Ni wapi zinakotoka hizo tafsiri mpya za Biblia wakati ile Biblia ya asili haipo au haipatikani popote? Maandiko ya kizamani ya Kigiriki ambayo yenyewe ni tafsiri hayafanani na yanatofautiana yenyewe kwa yenyewe.

    45. Unawezaje kuyachukua maandiko ya waandishi ambao kamwe hawakumuona Yesu kwamba ni sahihi, kama vile Marko na Luka?

    ReplyDelete
  9. 46. Kwa nini nusu ya Agano Jipya imeandikwa na mtu ambae kamwe hakuonana na Yesu katika maisha yake? Paulo anadai alionana na Yesu alipokuwa njiani toka Jerusalemu kuelekea Damaskasi bila kutoa ushahidi wowote wa kuonana naye? Paulo alikuwa ndie adui mkubwa wa Ukristo; Je, hilo halitoshi kutilia shaka juu ya usahihi wa kile alichokiandika? Kwa nini Wakristo wanayaita maandiko ya vitabu hivyo vya Agano la Kale kwamba ni “MANENO YA MUNGU” wakati wale waliyoyapitia Biblia ya RSV wanasema kwamba mwandishi wa SAMWELI hajulikani na yule alieandika (na kuyakusanya) maandishi ya kale (KUMBU KUMBU) “HAJULIKANI HUENDA YALIKUSANYWA NA KUHARIRIWA NA EZRA”.!!!
    UTATA

    47. Kulingana na mambo yanayotatanisha katika Biblia, ni vipi Wakristo wanaweza kuamua kwa wingi wa theluthi mbili yapi ni maneno ya Mungu na yapi si maneno ya Mungu kama tangulizi ya baadhi ya Biblia zinavyosema kama ilivyosema ile ya RSV?

    48. Kwanini Luka katika maandiko yake anazungumzia kupaa kwa Yesu kuwa ilikuwa ni siku ya Pasaka, na katika Matendo ya Mitume, maandiko ambayo yanajulikana kama yeye ndiye mwandishi, anasema alipaa siku arobaini baadae?

    49. Ukoo wa Yesu umetajwa katika Matayo na Luka tu. Matayo iliorodhesha vizazi 26 kutoka Joseph hadi Daudi wakati Luka yeye iliorodhesha vizazi 41. ni Joseph tu anayeungana na Daudi katika orodha zote mbili. Hakuna jina jingine hata moja lingana! Ikiwa hayo yalitolewa na Mungu neno kwa neno, vipi yatofautiane? Baadhi wanadai kwamba moja ni kwa ajili ya Maria na moja ni kwa ya Joseph, lakini ni wapi alipotajwa Maria katika maandiko yote mawili?

    50. Ikiwa Musa aliandika vitabu vya kwanza kabisa vya Agano la Kale, Musa aliwezaje kuandika taarifa ya kifo chake mwenyewe? Musa alikufa katika kitabu cha tano akiwa na miaka 120 kama ilivyotajwa katika Kumbukumbu la Torati; 34:5-10

    51. Katika chapisho la King James, kwa nini linaeleza miaka 7 (saba) ya ukame katika Samweli 2 24:13 huku likieleza miaka 3 (mitatu) tu ya ukame katika Mambo ya Nyakati 1- 21:12? Kwa nini yote yalibadilika katika chapisho jipya la kimataifa na machapisho mengine?

    52. Vile vile Katika chapisho la King James, kwa nini inasema kwamba JEHOIACHINI alikuwa na miaka minane wakati alipoanza kuongoza katika Mambo ya Nyakati 2 (21:12) huku ikisema alikuwa na miaka kumi na nane katika Wafalme 2 24:8? Kwa nini baadae zote zilibadilika na kuwa 18 katika chapisho jipya?

    53. Katika machapisho yote, kwa nini yanasema kwamba Daudi aliwauwa waendesha magari ya Farasi MIA SABA wa Kisyria na wapanda farasi arobaini elfu kama ilivyooneshwa katika Samweli 2 10:18 huku ikisema watu elfu saba ambao walipigana kupitia magari ya farasi na wapiganaji wa miguu 40 elfu katika Mambo ya Nyakati 1 19:18?

    54. Katika machapisho yote, kwa nini yanasema kuwa majosho elfu mbili katika Wafalme 1 7:26 huku katika Mambo ya Nyakati 2 4:5 linasema ni majosho elfu tatu?

    55. Katika chapisho la King James, kwa nini linasema kwamba Solomoni alikuwa na vikalio vya farasi elfu nne katika Mambo ya Nyakati 2 9:25, huku likisema kwamba Solomoni alikuwa na vikalio vya farasi arobaini elfu katika Wafalme 1 4:26? Kwa nini yalibadilika yote mawili na kuwa arobaini elfu Katika chapisho jipya?

    56. Mwanzo 1, uumbaji wa Mungu umeanzia majani kisha miti, ndege, nyangumi, ng`ombe na vitambaavyo na mwisho mwanamume na mwanamke. Mwanzo 2, hata hivyo, inauweka uumbwaji wa mwanamume kabla ya ng`ombe na ndege na mwanamke. Baadaye na wanyama. Vipi itawezekana kufafanua haya?

    ReplyDelete
  10. QURAN NA WAKRISTO
    Ketengo hiki hakihitaji wala hakihoji, lakini sana sana kunampatia msomaji baadhi ya aya za Quran ambazo zinauelekeza Ukristo kwa upekee, na watu wa kitabu kwa ujumla. Sehemu kubwa ya Quran inahusika na au inafungamana na Wakristo na Wayahudi na nimeamua kuchagua aya zinazofungamana na maudhui ya makala hii.

    1 “Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; Alimuumba kwa udongo kisha Akamwambia: “Kuwa”; basi akawa.” (Quran 3:59)

    2 “Sema: “Enyi watu mliopewa Kitabu (cha Mwenyezi Mungu. Mayahudi na Manasara)! Njooni katika neno lilio sawa baina yetu na baina yenu: ya kwamba tusimwabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe (Mwenyezi Mungu) na chochote; wala baadhi yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu (au pamoja na Mwenyezi Mungu). Wakikengeuka, semeni: “Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu, (tumenyenyekea amri za Mwenyezi Mungu).”

    3 “Enyi watu mliopewa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahimu, na hali Taurati na Injili havikuteremshwa ila baada yake? Basi je, hamfahamu?”

    4 “Ibrahimu hakuwa Myahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu, mtii; wala hakuwa katika washirikina.”

    5 “Watu wanaomkurubia zaidi Ibrahimu ni wale waliomfuata yeye (katika zama zake) na Mtume huyu
    (Muhammad) na waliomwamini (Mtume huyu). Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa wenye kuamini.”

    6 “Baadhi ya watu waliopewa Kitabu wanapenda wakupotezeni; lakini hawapotezi ila nafsi zao; na (hali wenyewe) hawatambui.”

    7 Enyi mliopewa Kitabu! Mbona mnazikataa Aya za Mwenyezi Mungu, hali mnajua (kuwa ndiyo ndizo)?

    8 Enyi mliopewa Kitabu! Mbona mnachanganya haki na batili, na mnaficha haki, hali mnajua?” (Quran 3:64-71)

    9 “Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa).” (Quran 3:85)

    10 “Na kwa (ajili ya) kusema kwao: “Sisi tumemuua Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mungu,” hali hawakumwua wala hawakumsulubu, bali walibabaishiwa (mtu mwengine wakamdhani Nabii Isa). Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika) hiyo (ya kumwua nabii Isa)wamo katika shaka nalo (jambo hilo la kusema kauawa). Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo) hili (la kuwa kweli wamemwua Nabii isa), ispokuwa wanafuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumwua. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua Kwake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima.” (Quran 4:157-158).

    ReplyDelete
  11. 11 “Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na (ni kiumbe aliyeumbwa kwa) tamko Lake (tu Mwenyezi Mungu) alipompelekea Maryamu. Na ni roho iliyotoka Kwake (Mwenyezi Mungu kama roho nyengine). Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mitume Yake; wala msiseme “watatu …” Jizuieni (na itikadi hiyo); itakuwa bora kwenu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mungu Mmoja tu. Ni mbali na Utakatifu Wake kuwa ana mwana. Ni vyake (vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini; na Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa kutosha. Masihi (Nabii Isa) hataona unyonge kuwa mja wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika waliokurubishwa (na Mwenyezi Mungu hawataona unyonge kuwa waja wa Mwenyezi Mungu). Na watakaoona unyonge uja wa Mungu na kutakabari, basi Atawakusanya wote Kwake (Awatie Motoni). Na ama wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, basi Atawapa ujira wao (sawa sawa), na kuwazidishia fadhila zake. Lakini wale walioona unyonge na kufanya kiburi, basi Atawaadhibu kwa adhabu iumizayo, wala hawatapata rafiki wala msaidizi (yoyote) mbele ya Mwenyezi Mungu. (Quran 4:171-173)

    12 “Na kwa wale waliosema: “Sisi ni Wakristo,” Tulichukua ahadi kwao, lakini wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa, kwa hivyo Tukaweka baina yao (wenyewe kwa wenyewe) uadui na bughudha mpaka Siku ya Kiama. Na Mwenyezi Mungu atawaambia walivyokuwa wakiyafanya. Enyi watu wa Kitabu! Amekwisha kufikieni Mtume wetu, anayekudhihirishieni mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na husamehe mengi. Bila shaka imekwisha kufikieni nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Kitabu kinachobainisha (kila jambo). Kwa (Kitabu) hicho Mwenyezi Mungu huwaongoza wenye kufuata radhi Yake katika njia za salama, na huwatoa katika kiza kuwapeleka katika nuru kwa amri Yake, na Huwaongoza katika njia iliyonyooka. Kwa yakini wamekwisha kufuru wale waliosema: “Mwenyezi Mungu ni Masihi bin Maryamu.” Sema: “Ni nani atakayemiliki (kuzuilia) chochote mbele ya Mwenyezi Mungu kama Yeye angetaka kumwangamiza Masihi mtoto wa Maryamu, na mama yake na vyote vilivyomo katika ardhi?” Na ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake ni wa Mwenyezi Mungu (tu peke yake). Huumba Apendavyo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.” (Quran 5:14-17)

    13 “Bila shaka wamekufuru wale waliosema, “Mwenyezi Mungu ni Masihi (isa) bin Maryamu.” Na (hali ya kuwa) Masihi alisema: “Enyi wana wa Israili! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia Siku ya Kiama).”

    14 Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: “Mwenyezi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu; (Yeye ndiye wa tatu wao).” Hali hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja (tu peke yake). Na kama hawataacha hayo wayasemayo, kwa yakini itawakamata – wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao – adhabu iumizayo.

    15 Je! Hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na kumwomba msamaha? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.

    ReplyDelete
  12. 16 Masihi bin Maryamu si chochote ila ni Mtume (tu). (Na) bila shaka Mitume wengi wamepita kabla yake. (Hawajaona)? Na mamake ni mwanamke mkweli. (Na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na wakenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo)? Tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).

    17 Sema: “Je! Mnawaabudu – badala ya Mwenyezi Mungu (peke yake) – wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukunufaisheni? Na Mwenyezi Mungu ndiye Asikiaye (na) ndiye Ajuaye.”
    18 Sema: “Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu bila haki, wala msifuate matamanio ya watu waliokwisha potea toka zamani; (nao ndio hao wanavyuoni wenu) na wakawapoteza wengi, na (sasa) wanapotea njia iliyo sawa, (hawataki kumfuata Nabii Muhammad).” (Quran 5:72-77)

    19 Na (kumbukeni) Mwenyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryamu! Je, wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu?” aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika. Hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uwongo). Kama ningalisema bila shaka Ungalijua; Unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyo nafsini Mwako; hakika Wewe ndiye Ujuaye mambo ya ghaibu.

    20 “Sikuwaambia lolote ila yale Uliyoniamrisha: ya kwamba, ‘Mwabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu.’ Na nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao; na Uliponikamilishia muda wangu, Wewe ukawa Mchungaji juu yao, na Wewe ni Shahidi juu ya kila kitu.

    21 Ikiwa Utawaadhibu, basi bila shaka hao ni waja wako; na Ukiwasamehe basi kwa hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima; (Hutaambiwa kuwa wamekushinda kuwatia adabu).”

    22 Mwenyezi Mungu atasema: “Hii ndiyo Siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mbele yake mito. Humo watakaa milele. Mwenyezi Mungu amewawia (amewapa) radhi; nao wawe radhi Naye. Huku ndiko kufaulu kukubwa.” (Quran 5:116-119)

    23 Na Mayahudi wanasema: “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;” na Wakristo wanasema: “Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu”; haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale walio kufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!

    24 Wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu na (wamemfanya) Masihi mwana wa Maryamu (pia mungu), hali hawakuamrishwa ispokuwa kumuabudu Mungu Mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Yeye. Ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo.

    25 Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa ispokuwa kuitimiza nuru Yake, ijapokuwa makafiri wanachukia.
    26 Yeye ndiye Aliyemleta Mtume Wake kwa uongofu na Dini ya haki ili Aijaalie kushinda (Dini hii) dini zote; ijapokuwa watachukia hao washirikina.

    27 Enyi mlioamini! Wengi katika makasisi (wanavyuoni wa Mayahudi na Manasara) na watawa (wao) wanakula mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inayoumiza (inayowangoja)

    28 Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika Moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambiwa): “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia (mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya.” (Quran 9:30-35)

    ReplyDelete
  13. MUHAMMAD AU YESU? Wakristo wanadai kwamba utabiri wa Kumbukumbu la Torati 18:18 unamuhusu Yesu na sio Muhammad. Hiyo aya inasema: "Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.” Kumbukumbu la Torati 18-18 Hoja ya pekee wanayoikimbilia katika tafsiri hiyo ni kuwa wote wawili Musa na Yesu walikuwa Mitume. Ingawa hoja hiyo inapingana na madai yao ya kuwa Yesu alikuwa ni Mungu na si Mtume. Mitume wengi wa Kiyahudi walifanana na Musa. Hata hivyo, kama tutamlinganisha Muhammad na Musa, tupata kuwa:

    Muhammad alikuwa ni Mwarabu, na Waarabu wanatokana na Ismaili, mtoto wa Ibrahimu, huku Musa alikuwa ni Myahudi, na Wayahudi wanatokana na Isaka, mtoto wa Ibrahimu, kwa kuwa neno NDUGU ZAO linaashiria watoto wa mtoto wa kwanza kuwa ndugu wa mwingine. Hili halikubaliki kwa Yesu, kwa kuwa alikuwa ni Myahudi.

    Kwa mujibu wa Wakristo, Yesu alienda Motoni kwa siku tatu huku Musa akiwa hajaenda. Kwa hiyo, Yesu si kama Musa. (Katika Uislamu, hakuna yoyote katika hao Manabii watatu aliyeingia Motoni)
    Musa na Muhammad walizaliwa na baba na mama huku Yesu alizaliwa na mama tu.

    Musa na Muhammad walioa na kuwa na watoto, huku Yesu akiwa hajaoa kabisa.
    Musa na Muhammad walipata matatizo na mambo magumu kutoka kwa watu wao mara ya kwanza, lakini mwishoni walikubaliwa na watu wao. Huku Yesu alikuwa amekataliwa na watu wake mwanzoni na anaendelea kukataliwa na Wayahudi hadi leo hii. “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” Yohana 1:11

    Musa na Muhammad walikuwa na nguvu, kando na kuwa Mitume. Wote wawili walitekeleza adhabu kubwa, hilo likiwa ni mfano, huku Yesu hakuwa na madaraka kwa watu wake. “Yesu akajibu, ufalme wangu sio wa ulimwengu huu”, Yesu amesema katika 18:36.

    Musa na Muhammad walileta sheria mpya huku Yesu hakuleta.

    Musa alilazimishwa kuhama alipokuwa mkubwa aende Median huku Muhammad pia, alilazimishwa ahame alipokuwa katika hatua moja ya maisha yake, kuelekea Madina. Huku Yesu hajalazimishwa kuhama katika utuuzima wake.

    Musa na Muhammad wote wawili walikufa vifo vya kawaida na kisha wote walizikwa, huku jambo hilo haliwezi kuongelewa kwa Yesu. Yesu hakuuliwa wala hakusulubiwa kabisa kabisa, kwa mujibu wa Quran na hakufa kwa kifo cha kawaida kama ilivyothibitishwa na Wakristo ambao wanaamini kasulubiwa.

    ReplyDelete
  14. MASWALI YA MWISHO

    57. Kwa nini, ewe kiongozi wa Kikristo, huji kusikiliza na kujifunza dini ya kweli ya Yesu?
    58. Ukiwa kama Mkristo, uliyeusoma Uislamu na ikiwa ni hivyo, je, uliusoma kutoka kwa Waislamu wa kweli?

    59. Kama Mkristo, je, unakubali kwa uadilifu na wema kuwa ni lazima uchunguze kile kinachosemwa na Uislamu juu ya Mungu, Yesu, pamoja na maisha haya na ya baadae?

    60. Kwa kuwa ni Mkristo, je, pia, waamini kile tunacholazimika kuhesabiwa kwa Muumba wetu na kwamba Muumba ni mkamilifu na Muadilifu? Kama muumini mwaminifu kwa Mungu. Je, hulazimiki kutafuta ukweli usiobadilishwa bilia kujali matokeo yake?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hamudi,asante kwa hoja zako ambazo ni wazi zinatoa changamoto isiyo ndogo. Kwa kuwa ni hoja nyingi, itanichukua muda kiasi kupitia moja baada ya nyingine na kujibu. Hizi si za kujibu harakaharaka hata kidogo. Na hata hivyo, siwezi kusema kuwa nitakuwa na jibu la kila moja; ila zile nitakazoweza nitajibu. Mungu akubariki.

      Delete
    2. Shukran bro Hamud jazakallahu khayra

      Delete
  15. Habari Hamudi. Nashukuru kwa majibu yako. Nimejibu kipengele kwa kipengele. lakini kwa kuwa maswlai uliyoniuliza ni mengi, bado naendelea na kujibu mengine yaliyobali.
    Hamudi123 said...
    1) Aya hi 4:101 inawaelekeza waislamu wafanye nini katika vita (Anae kupiga vita ni adui yako, au sio?aya hii haipingani na aya ya 2:109) aya hiyo inasema hivi,

    Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi (Quran 4:101).

    Na unapo kuwa pamoja nao, ukawasalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na wachukue silaha zao. Na watakapo maliza sijida zao, basi nawende nyuma yenu, na lije kundi jingine ambalo halijasali, lisali pamoja nawe. Nao wachukue hadhari yao na silaha zao. Walio kufuru wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkawa wagonjwa, mkaziweka silaha zenu. Na chukueni hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha(Quran 102).

    Pia aya ya 8:39 ilishuka wakati wa vita (makafiri walikuwa wanawatesa waislamu, Waislamu wanaambiwa wapingane nao (self defence) lakini wakiacha kupigana na nyie na kuwatesa waacheni),

    Aya hiyo inasema hivi: Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda. (Quran 8:39).
    Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema (Quran 40).

    Jibu langu:
    Hamudi ingawaje nilikuwa nimeuliza kama sura Al-Baqara 2:109 na Al Imran 3:20 hazipingani na sura kama vile Al-Anfal 8:39, maana hizo mbili za mwanzo zinataka waislamu wasamehe na kuonya tu wale wasiotaka kukubali uislamu huku hii ya mwisho inataka wawalazimishe; lakini wewe unasema kuwa sura kama 4:101 inatoa maelekezo juu ya nini cha kufanya wakati wa vita.

    Ninachokiona hapa hata hivyo ni kuwa, waislamu mnaagizwa kwamba mtu akikukosea basi unatakiwa usikubali kuonewa. Nadhani hilo ni jambo linalojulikana zaidi kwa jina la ‘jino kwa jino’. Na umeniuliza kwamba: “Anae kupiga vita ni adui yako, au sio?”

    Ninashukuru kwamba katika kunijibu maswali yangu, mwishowe umenipa na mimi maswali kupitia “project reason.” Nami kwa kupitia reasoning hiyohiyo, ambayo naamini ni jambo zuri kabisa, ninaona kuwa fundisho hili si practical katika maisha. Mara kadhaa nimesikia wahubiri wa Kiislamu wakisema, “Sisi hatuna tatizo na mtu anayeutakia Uislamu mema.”

    Ndugu Hamudi, nadhani wewe ni shahidi kwamba katika maisha haya, huwezi ukapendwa au kukubaliwa na kila mtu. Upinzani ni jambo ambalo ni la kawaida kabisa. Sasa, ukisema kwamba watu wengine ndio wawe wema kwanza ndipo na wewe ufuate, hiyo ni impractical view of life.

    Ukishajua kuwa kupigwa vita ni sehemu ya maisha na haikwepeki, kuanza kupingana na kila anayekupinga, basi maisha yako yatakuwa ni mzigo mzito sana kwako binafsi. Utakuwa ni mtu uliyejaa uchungu, hasira, chuki, mashindano na mateso moyoni. Mimi siko tayari kabisa kufuata mstari huo. Na ninachoweza kujibu ni kuwa, “Ndiyo, mtu anayenipiga vita ni adui yangu, lakini mimi siko tayari kuwa adui yake.”

    Lakini ufuatao ndio ushauri ulio practical na ambao ni kwa ajili ya usalama wangu na wa dunia nzima. Biblia inasema:
    Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. (Mathayo 5:43-44).

    Haya ni maneno ya Bwana Yesu aliye Mfalme wa uzima na amani. This is a practical approach that works. Haijalishi unanichukia, unanipinga, n.k. Lakini mimi siwezi kukubadili wewe wala ulimwengu ili uweze kunipenda mimi. Ninachoweza ni kujibadili mimi mwenyewe kwa kumsamehe yule anayenichukia. Ni practical kushughulika na nafsi moja (yaani ya kwangu) kuliko na maelfu ya nafsi za watu wanaonichukia na kunipinga.

    ReplyDelete
  16. 2) Kuhusu aya ya 47:7, umesema:

    Hiyo ni lugha ya mifano (kama unaijua Biblia vizuri, bila shaka unajua maana ya lugha ya mifano)
    Nikisema hivi: "Mimi sihitaji shilingi elfu kumi zako lakini ukitoa hizo shilingi elfu kumi kwa ajili ya dini yangu (kama vile kusaidia masikini..) nitahakikisha kuwa kweli unanipenda".

    Hapa kuna contradiction gani ? au rafiki yangu mpendwa hajui lugha ya mifano ?

    Jibu langu:
    Samahani Hamudi, sioni mfano au (symbolism) yoyote katika hili. Mfano au symbol ni kitu kama hiki: “Yule bwana ni simba kwelikweli.” Neno “simba” hapa ndio mfano. Maana simba tunamjua na huyu anayeongelewa ni mwanadamu. Kwa hiyo, kwa kuwa yeye si simba, basi neno hili limetumika kuwakilisha nguvu, ujasiri, uimara, n.k. This is symbolism, lakini si katika aya unayoiongelea. Au ukisema, “Maisha ni mtihani”. Neno mtihani hapa ni symbol. Maana mtihani tunajua unafanywa kwenye chumba maalum, kwa usimamizi maalum, na labda kwa kuandika; kitu ambacho sivyo kwa maisha. Bali hapa maisha yanalinganishwa na mtihani kwa maana ya kuhitaji umakini, kufikiri, kuchagua, na kuna kushindwa na kuweza. This is symbolism too.

    ReplyDelete
  17. 3)Umesema: Jiulize kwa nini inchi zote duniani zimeamua kuweka jela ?

    Nadhani jawabu unalijua, au sio ? Kuwaadhibu wahalifu au sio ?

    Aya tukufu ya 42:40 inasema hivi,
    Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.

    Jibu langu:
    Ni kweli Hamudi jela ziko kwa ajli ya wakosaji. Lakini naomba nikuulize maswali haya, ambayo huna lazima ya kunijibu ila utafakari tu. Je, wewe binafsi huwa hukosei? Je, kila unapokosa huwa unaenda kwa bwana jela na kumwambia akuweke jela? Je, kutoka moyoni mwako, kama ukikosa na kukamatwa, kisha ukaambiwa uchague kati ya kufungwa na kusamehewa ungechagua nini?

    Hebu tusiongelee mambo theoretically. Tuende kwenye uhalisia wa mambo katika maisha yetu. Kama ukiwa mkweli kabisa, utatambua kuwa sisi sote ni wakosaji kila siku. Unaweza usiwe mwizi au muuaji, lakini ukawa na wivu. Unaweza usiwe mchawi lakini ukawa na chuki. Unaweza usiwe mzinzi lakini ukawa na hasira, n.k. Kwa hiyo, suala si ukubwa wa dhambi, bali ni ukweli kwamba KILA mwanadamu, kuanzia kiongozi wa dini hadi muumini maamuma, SOTE ni wakosaji!

    Kama hivyo ndivyo, je, tuende jela wote? Tuwe tunapigwa viboko 100 au 20 kila asubuhi na jioni? Je, ni wanadamu wangapi wako tayari kujipeleka mahakamani pale wanapokosa? Waislamu huwa mnawapiga mawe wanaokamatwa kwenye uzinzi, je, wazinzi ni hao tu? Kwa nini wanaopigwa mawe ni wale wanaokamatwa tu? Mbona hatujawahi kusikia mtu ameenda kusema, “Jamani nimezini. Nimekuja mnipige mawe?”

    Jibu ni kuwa njia yenyewe ni impractical. Ipo njia ambayo ni practical kwa ajili ya yeyote aliye tayari kuisikia. Hakuna mwanadamu anayeweza kutimiza sheria ya Mungu kikamilifu. Be frank to yourself and you will see that.

    Hebu sikia yafuatayo Hamudi. Biblia inasema: Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. (Warumi 8:6-8).

    Maandiko haya yanaongelea jitihada za mwanadamu kujaribu kutimiza sheria ya Mungu. Na yako wazi kabisa, jambo ambalo hata sisi wenyewe ni mashahidi katika maisha yetu binafsi, kwamba hata tufanyeje hatuwezi kuwa wakamilifu kwa jitihada zetu.

    Nia ya mwanadamu siku zote ni kwenda kinyume na sheria ya Mungu. Na hili si tu kwa sababu ya uasi, bali tumeumbwa kwa namna ambayo hatuwezi kwa juhudu zetu kuwa watii kwa kiwango anachokitaka Mungu. Unaweza ukajitahidi kwenye maeneo mawili matatu, lakini kwingine utashindwa tu. Kwa mfano, unaweza usiwe mgomvi au mwizi, lakini tamaa na uzinzi vikawa ndiyo shida yako, n.k.

    Sasa nikirudi kwenye hoja, kwamba uovu ni lazima ulipwe kwa uovu, itakuwa ni haki basi kila anayetaka kulipa uovu kwa mwingine, ataje kwanza uovu wake ili ulipwe ndipo alipe kwa mwingine; maana HAKUNA hata mwanadamu mmoja asiyekuwa na uovu.

    Here is the practical way of life:

    Baada ya wayahudi kumpeleka mwanamke aliyekamatwa kwenye uzinzi huku wakiwa wamebeba mawe yao tayari kwa kupiga, Bwana Yesu, Mfalme wa uzima anasema: Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. (Yohana 8:7).

    Sasa kama si kupiga mawe, anataka tufanye nini?
    Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. (Mathayo 6:14-15).

    Hii ndiyo njia inayoendana na uhalisia wa maisha. Kuhukumu si njia inayoendana na maisha. Tatizo linakuja pale mtu anapoishi kwa ajili ya kuwafurahisha wanadamu na kutaka kuonekana kuwa yeye ameshikilia sana dini . Lakini ukiwa ni mtu wa kumtazama Mungu peke yako, kisha ukajipeleleza ndani ya moyo wako kibinafsi bila kujali kuonekana na wengine, utatambua kuwa huna kamwe haki ya kumhukumu mwenzako, maana na wewe umo kwenye kundi lilelile la wahukumumiwa!

    ReplyDelete
  18. 4)Umesema: Jibu la swali lako hili lipo hapo juu (katika jawabu namba moja).

    Jibu langu:
    Jibu hili sijafanikiwa kuliona kama ulivyosema. Bado sioni namna unavyoweza kusema usilazimishe watu kuamini dini yako kisha sehemu nyingine ukasema ni lazima uwalazimishe.

    5) Umesema: Jawabu lako lipo katika aya hii ya Quran Tukufu 2:142,

    Quran Tukufu inasema hivi,
    WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka (Quran 2:142).

    Jibu langu:
    Hamudi sijaelewa hapa. Kama mashariki na magharibi ni ya Mwenyezi Mungu (jambo ambalo ni la kweli kabisa), mbona kila mwislamu anatakiwa kuswali kuelekea upande mmoja tu?

    Rafiki yangu, naamini unafahamu kuwa jambo hili halikuanza na Waislamu, bali lilianza na wayahudi. Wao nao walikuwa wakisali sala zao kuelekea Yerusalemu, wawapo popote pale duniani. Naamini hata sasa wanafanya hivyo.

    Lakini hili ndilo analosema Bwana Yesu Mfalme wa uzima pale alipozungumza na mwanamke kisimani, ambaye naye alikuwa anadhani kuwa kumwomba Mungu ni lazima ukae mkao fulani na uelekee mahali fulani:

    Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.
    Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. (Yohana 4:20-24).

    Ibada ya kweli ni ile ya rohoni. Mungu hakai kwenye upande fualni. Sasa kama wewe uko Afrika Kusini halafu unaposwali unaelekeza mawazo yako Makka, je, utalingana kweli na mtu anayeamini kuwa Mungu yuko humohumo moyoni mwake? Kwa nini umwabudu Mungu aliye maelfu kwa maelfu ya kilometa kutoka mahali uliko badaka ya kumwabudu aliye ndani ya moyo wako? Jesus’ teachings are PRACTICAL and logical, friend.

    ReplyDelete
  19. 6) Umesema: Aya hiyo tukufu 4:129,

    Inaelezea ukweli wa mwanamme anapo owa wake zaidi ya mmoja (lazima atampenda mmoja zaidi lakini hata hivyo asimili moja kwa moja akamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa, ajaribu kadiri ya uwezo wako kufanya uadilifu).

    Aya hiyo inasema hivi,
    Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamngu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu (Quran 4:129).

    Jibu langu:
    Haya Hamudi, hapo sina kikubwa cha kusema. Ila ninachoona ni kilekile kwamba “ajaribu kadiri ya uwezo wake.” Wewe hata mimi tunajua kuwa HUWEZI! Maana, as usual, hili ni jambo ambalo haliendani na asili ya mwanadamu – its unnatural. Kilicho natural ni kupenda mke mmoja/mume mmoja.

    Na kinachoshangaza hata zaidi ni kuwa, je Mungu anaweza kukuagiza ufanye jambo ambalo anajua kuwa utashindwa kisha likakubalika kwake? Maana anasema, kama ulivyonukuu, “Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia.”

    Lakini hivi ndivyo anavyosema Mfalme Yesu: Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao (Waebrania 12:14). Lakini ikumbukwe kuwa sisi wenyewe hatuwezi, bali tunajiachilia kwake atuwezeshaye, maana anasema: Pasipo mimi ninyi hamuwezi lolote. (Yohana 15:5).

    Usipokuwa mtakatifu kama alivyo Mungu, kujitahidi kwako ni kazi bure rafiki.

    7) Umesema: Haha Haiiii, rafiki mbona unaanza kudanganya sasa, aya ya 16:28 inasema hivi,

    Ambao Malaika waliwafisha nao wamejidhulumu nafsi zao! Basi watasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya uovu wowote. (Wataambiwa): Kwani! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyo kuwa mkiyatenda (Quran 16:28).

    Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni maovu mno makaazi ya wafanyao kiburi! (Quran 16:129)

    Jibu langu:
    Asante, Hamudi katika aya hii nimekuelewa. Ni kweli aya hii nilikosea kuiandika kwa usahihi. Haisemi kama nilivyoandika.

    ReplyDelete
  20. Kwanza kabisa ningepena kutanabahisha kwamba,maandishi yangu haya ingawa namjibu Jonh Muhubiri,lakini pia yanawalenga wale wakristo ambao bado wanatafuta kujua Mungu wa kweli na dini ya kweli wayasome mwanzo mpaka mwisho,ama kwa wale wakristo ambao wakereketwa ambao hawaaki kuona na kuujua ukweli hata ukiwa mbele ya macho na kuamua kuendelea kua viziwi,mabubu na vipofu haya si maandishi yao kwani hata wakiwa na ushujaa wa kuyasoma wataendelea kubaki viziwi,mabubu,na vipofu!
    John, kwanza kabisa ningependa kukusifu kwa kazi kubwa na majuhudi yako haya ya kufungua blog yako na kusimama kidete katika kuhubiri dini yako au kuhubiri ''HABARI NJEMA'' na nadhani ingekuwa bora zaidi ukaendelea katika uwanja wako huo.lakini kuona kwamba kumbe umeshamaliza kazi yako au umeshafanikiwa kazi yako kwa kiasi kikubwa kwa kuwahubiria wana imani wenzio wa kikristo ukaona kumbe unao wajibu pia na uwezo pia kuwahubiria na kuwaelimisha waislamu kwa kuingia moja kwa moja na topic ambayo uliipa kichwa cha habari ''Ndugu waislamu nisaidieni''!!!!!??? kichwa chako hicho cha habari kinatofautiana kabisa na maudhuu yenyewe uliyoweka ubaoni.katika maudhui yako hii umejitokeza kama ni mmoja wa wale wahubiri wa kikristo ambao wameisoma vyema Qurani, wameichunguza vya kutosha na kufikia kuielewa vyema na hatimaye wanao wajibu wa kuikosoa Qurani hiyo. kwani uliandika ukiseama kwa kuwaelimisha waislamu na kuwafungua macho kwamba qurani si kitabu kinachotoka kwa Mungu wa kweli ambaye wewe unataka waisilamu wamtafute upya Mungu wao wa kweli,au unataka kuwaelimisha kwamba kuna Mungu mwingine wa kweli na huyu waislamu wanodai kwamba kaleta qurani si wa kweli inabidi wamtafute Mungu wa kweli kwa sababu tu qurani inakanganyana yewe kwa wenyewe kwa hiyo UMETOKA NA JIBU KWAMBA QURANI YA WAISLAMU NI IRRELEVANT !!!!!Uliandika katika utangulizi wako ukisema''.......Na hiki kusema kweli ni kipimo kizuri chakuomyesha iwapo jambo limetoka kwa Mungu wa kweli au la;maana Mungu wa kweli,kwa kuwa ni mkamilifu kwa asilimia mia mia moja,hawezi kusema hivi hapa,kisha aseme vingine kule-maana yeye asahau kama wanadamu.hawezi ''nilikuwa wako na mambo mengi au mawazo mengi nikasahau''kwa hiyo,mantiki,vilevile kutokana na aya hii,Allah au Muhammad anamaanisha kuwa,kama tukikuta kuna kupingana ndani ya Quran,basi Quran itakuwa haijatoka kwa Mungu wa kweli.''

    Na ukaendelea kujieleza,''.......Niseme mapema kwamba,mimi si mjuzi wa wa quran.Kwa hiyo,ninaweza kuwa niko nje kabisa ya maana iliyokusudiwa.''Na ukamalizia maandishi yako kwa kuandika ukisema''......sijui kwa kweli kama nilivyo sema,mimi kwa mambo haya ni maamuma tu,kwa hiyo inawezekana nipo nje kabisa ya kile kinachomaanishwa nitafurahi kama ndugu zangu waislamu mtanisaidia kujua mambo haya'' Sasa hapa sijui unataka kuwaeleza nini waisilamu,je ni kwamba unaongea kitu unachokijua au unabahatisha?sasa katika hoja ya mjadala inabidi topic yako hii waislamu waitupilie mbali, kwani unachokidai kwamba unakijua kumbe ukijui sasa tukuelewe vipi? je upo serious na unachokidai kukijua au ni kuleta uchafuzi tu wa kifikra?kwa kujiita wewe maamuma na unataka uelimishwe na waisilamu.Au wewe ni katika wale tu wahubiri wanaotaka umashuhuri kama ilivyokuwa zama hizi?Badala ya kuendelea katika uwanja wako na ukapata utulivu unataka pia kujiingiza kati uwanja wa waisilamu ambao huna ujuzi nao?!

    Maalim Moses.

    ReplyDelete
  21. sasa mimi sijui kwamba ni msaada gani huo unaotaka waisilamu wakusaidie,wakati wewe mwenyewe umekuja kuwaelimisha na kuwafumbua macho kwamba kitabu chao si sahihi na wala hakitoki kwa Mungu wao,kwani uwoga wako ulikuwa ni nini mpaka ukajiita maamuma wakati wewe ni muhubiri wa dini?kwa nini tu usije na maudhui kwamba unawachallenge waislamu kwamba kitabu chao si cha kweli kwa sababu tu kinasigana chenyewe kwa chenyewe?nadhani waislamu wangekuelewa yema na wakakupa umuhimu na wakawa tayari kuichukua changamoto hiyo.Lakini hata hivyo waisilamu wamekuja kupambana na changamoto hiyo kama inastahiki kuitwa changamoto kwa kukuchukulia kama ni PROVOCATEUR tu na waislamu hawakukunyamazia.Na nayashukuru sana majuhudi ya kazi njema yaliyofanywa na Mahmuud na Hamuud, kwa kukuwekea wazi kile ambacho wewe umekitilia mashaka lakini kwa vile jukumu la kuamini au kutoamaini ni jukumu la mwanadamu mwenyewe ukitaka amini na ukitaka usiamin, lakini ukweli umeshabainishwa.Jonh, mimi kwa upande mwingine kabisa kwa kukuelimisha wewe kama ni mkristo au hata waislamu wenzangu kwamba Qurani haisomwi hivyo au haichunguzwi hivyo kama ulivyofanya wewe.Ukweli ni kwamba wewe Jonh na mafano wako ni watu ambao mnaingia ndani ya Qurani tayari ukiwa na fikra tangulizi,au itikadi nyingine au hata muono mwingine kabisa na mnaingia katika qurani na kutaka kuthibisha hayo.kwa mfano kama wewe,umekuja na fikra tangulizi kwamba ni lazima uthibitishe kwamba Qurani si ya kweli, na wala haitoki kwa Mungu,kama hali ni hiyo na mfano wake utakuta Qurani inakusubiri kwa unalolitaka, kwa maana, wewe na mfano wako mnanyofoa aya kutoka huku na kule,mnazipindisha mnavyotaka kama unga wa ngano uliokandwa na kuzibinya na kuzikata manavyotaka ili mfikie kuthibitisha kile mlichokuja nacho, na kuziweka,kutozielewa na kuzisoma nje kabisa ya mukqtadha(out of context)na unatoka na jibu la EUREKA!!!!! kwamba nimegundua mambo ambayo waislamu wenyewe hawayajui kwa hiyo wache niwaelimishe!!!!!sasa leo kuna watu kama wewe wanaingia ka kuingia katika qurani na wanadai kwamba waisilamu hatakiwi kuswali na atakeyeswali atapata adhabu kali kama aliivyoonya Mungu katika sura ya 107aya ya 4 ''OLE WAO WANAO SWALI''!!!na kasimama hapo na ansema quran inasema hivyo kwamba waisilamu hawatakiwi kuswali!wengine wa mfano wako wanakuja na hoja kwamba Qurani inaruhusu kuwaoa watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa kuelewa wanakusomea sura ya 65 aya 4 ''.............,PAMOJA NA AMBAO HAWAPATI HEDHI.............''!!!na wengine wanakwambi kwamba Qurani imeruhusu ushoga na ubasha wanakusomea sura ya 42 aya ya 50 ''Au huwachanganya wanamume na wanawake,''!!!Na wengine wanakuelimisha historia ya waarabu kabla uisilamu kwamba walikuwa wanwaoa mama zao waliowazaa kwa kusomea mwanzo wa aya ya 23 ya sura ya 4''Mmeharimishiwa(kuwaoa) mama zenu,.....'' Kwa mifano hiyo na mingineyo inategemea ni fikra gani ya utangulizi uliyo nayo na ukaingia nayo katika Qurani ukanyofoa nyofua na kuziweka na kuzisoma aya nje ya MUQTADHA (out of context)kwa hiyo Jonh wewe umenyofua nyofua,kuzikata kata,kujifanya kutozielewa makusudio(kumbe unazielewa) umezisoma na kuziweka aya za qurani nje ya Muqtadha(out of context)na umetoka na EUREKA!!! Ebu Jonh muhubiri, kama wewe unasoma Qurani na kuichunguza unatoka na neno la AHLUL KITABU kwamba linaashiria WAKRISTO tu je uona tayari umeshaingia na fikra ya utangulizi???

    Maalim Moses.

    ReplyDelete
  22. John Muhubiri, Qurani si super market ukaingia humo ukachagua na kununua unavyovitaka na unavyovipenda na ukatoka na ukasema kwamba bidhaa nyingine hazina umuhimu wala thamani.Qurani inajitegemea yeyewe kwa yenyewe haitaji resource za nje ili uifahamu au uielewe inajifasiri yewewe kwa wenyewe wala haitaji tafsiri za watu ili uilewe,na yale majuhudi yaliyofanywa na wafasiri kama wanadamu ni majuhudi yao binfsi kwa vile walivyoielewa Qurani na wala hawa-represent maana na kusuduo la mwenyewe aliyeileta Qurani na ndio maana ALLAH(S.W) akaonyo katika sura ya 3 aya ya 7 aliposema''7.Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye
    maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama
    wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna,
    na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na
    wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka
    kwa Mola wetu Mlezi, Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili''Je Jonh ulilisoma kemeo hilo?jibu hapana na kemeo hilo kwa wale wote wanaokisoma kitabu hiki cha Qurani aidha wawe waisilamu wenyewe au wasiokuwa waisilamu,sasa wewe Jonh kama ni muhubiri wa INJILI unasema kwamba hata lugha iliyoshushiwa Qurani ya kiarabu uielewi, vipi leo uwe bingwa wa kuipitia,kuichunguza na kuichambua Qurani na kutoka na EUREKA?!!!!!Mfano wako wewe Jonh,ni sawa na mtu aliyesikia mara nyingi tu kwamba kuna hekalu limejengwa kwa ufanisi wa hali ya juu,madhubuti maridadi na uishiwi hamu la kulijua na kulitembelea hekalu hilo,wewe ukasema wait a minute!mimi Jonh nitalikosoa hekalu hilo na kuthibiitisha kwamba limejengwa kimakosa na foundation yake si madhubuti na linaweza kuanguka wakati wowote endapo tetemeko la ardhi likipiga au kimbunga kikipiga,naam,ukaenda ukalitembelea ukaliangalia na ukatoka ukawaambia watu kwamba mimi nilijua kabisa tangu mapema kwamba hekalu hili lilijengwa vibaya na litaanguka tu kwa vile foundion yake si imara, ulipoulizwa kama umesomea uhandisi wa majengo au una ni mkandarasi wa majengo unawajibu wasikilzaji wako,ah,mimi hata kuchanganya zege siju,i lakini mimi naona hivyo!!!wasikilizaji wako aidha watakuona hujui unaloliongea au watakuona ni mwendawazimu!!! sasa mimi siwezi kusema kwamba wewe ni mwendawazimu, isipokuwa,masikini hujui unaloliongea umenyofoa aya huku na kule na kuingia na fikra ya utangulizi na kudai kwamba hekalu lenyewe FOUNDATION yake siyo madhubuti.John kitabu cha Q urani kimeshushiwa kwa ufunuo kwa Muhammad kwa miaka 23!iNa hakikuja kwa wakati mmoja kama Taorati au Injili,na mitume yake kuanza kazi ya kufundisha wafuasi wao,na baada mitume hiyo kuondoka jukumu la kuhifadhi vitabu hivyo lilikua mikononi au mabegani mwa wataalamu wao wa kidinii na wafuasi wao

    Maalim moses

    ReplyDelete
  23. Lakini wataalamu wao hao wa kidini, angalia John,baada ya kuvihifadi wenyewe vitabu vyao viongozi wa dini hizi mbili za kiyahudi na kikristo wakaingiza mikono na miguu yao humo kwa tamaa za kidunia kwa kuwa na madaraka makubwa ya kidini na kijamiii na kudai kwamba huo ndio muradi au makusudio ya Mungu,je Injili ina version ngapi?je ni mara ngapi majopo ya wataalamu wa kidini ya kikkristo wamekaa kuangalia upya wapi sawa na wapi si sawa katika Injili?je watu kweli wana haki ya kukikosoa kitabu cha Mungu wa kweli au kuweka wanayoyata na wanayaona wao,kupunguza au kuzidisha au kuna mambo ambayo hayaingii aklini ambayo wazee wao wa awali waliingiza ndani ya Injili na Taurati?Je hukumbuki Jonh, komangano la kwanza na la pili la Nicaea?Ambapo walifikia kuweka itikadi ambayo mnaamini hadi leo hii kwamba ndio itikadi sahiiya dini yenu?Nadhani unajua hapa nini ninachokusudia nayo ni itikadi ya TRINITY au UTATU kwa nini isiwe itikadi ya UUNE?maana katika itikadi yenu Mama wa mtoto wa mungu(MARIA) naye ni Mungu!Au ni sababu gani za kimsingi ambazo komangano hilo la Nicaea walimsahau mama wa mtoto wa Mungu(MARIA)KUWA NAE NI MUNGU?!!topic ya itikadi yenu hii nitaindika huko mbeleni.Wayahudi nao wataalamu wao wa kidini, wao wakajaza yaliyokuwemo na yasiyokuwemo katika Taurati kitabu ambacho nyinyi wenyewe wakristo mnaona haya hata kukifanyia marejeo na kama mnarejea humo basi mnachagua story kwa mpito tu,marejeo yenu yote ni Injili tu na kma mtafanya marejeo katika Taurati basi manarejea sana kitabu cha Psalms kwa vile ibada yenu ni mziki, kuimba na kupiga makofi(kama mapagani)na psalms ndiyo marejeo yenu makubwa ya nyimbo na ibada zenu.Je John unataka kuniambia Jesus wa kihistoria na wanafunzi wake, ndio ulikuwa utaratibu wao huo wa kuabudu?Au mmezusha tu baada ya kukosa kujua jinsi gani Jesus wa kihistoria alivyokuwa anaabudu na wanafunzi wake? Lakini Allah(s.w)hakutaka tena Qurani kuwaachia tena wataalamu wa kidini na waumini wake jukumu la kuiangalia na kuilinda,yeye mwenyewe akachukua jukumu la kuingalia na kuilinda aliposema katika sura ya 15 aya ya 9''Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakao ulinda''

    maalim Moses

    ReplyDelete
  24. Kama kweli wewe Jonh ni mchambuzi wa dini na kusoma historia zake, je ujapata mshangao wa kihistoria baada ya kufa Mtume Muhammad na kuzuka kwa mgogoro wa utawala wa kisiasa na kugawanyika kwa waisilamu wemyewe mapaka kufikia kupigana civil war kwa tamaa ya madaraka?lakini waisilamu pamoja natofauti zao za kisiasa walikaa mbali sana na Qurani na hakuna mtu au kikundi iliyoigusa kwa kutia mkono au miguu kwa kudai masilahi yake au kubadilisha sura au aya kwa maislahi ya kidunia na kisiasa kama walivyofanya wazee wa kiyahudi na wa kikristo?je hujaliona hilo?na hadi keo hii kitabu hiki alichoshushuwa Muhammad tangu miaka 1400 iliyopita kimebaki INTACT kwa kusoma na kuandikwa?Na kwa waislamu wenyewe ikitokea mesoma ovyo kwa makusudi au kwa kutokujua, basi utakumbushwa kwamba unesoma vibaya, kwani kusoma kwako vibaya kunaweza kupelekea kubadilisha maana kabisa.Na Qurani ndio kitabu pekee duniani muumini wa kitabu hicho ana uweo wa kukihifadhi kwa moyo, hakuna hata kitabu chochote kile ambacho waumini wake wanaweza kukisoma kwa moyo kuanzia A-Z je uoni kwamba mwenyewe Allah(s.w)amechukua jukumu la kukihifadhi kitabu chake?Au amulioni hilo?amulijuwi hilo au hata kulitafakari na kulizingatia kwamba kitabu hiki ni kitabu pekee cha kwelina cha haki, ambacho kinatoka kwa MUNGU MMOJA WA KWELI,HANA MKE,HANA MTOTO NA WALA HANA MSHIRIKA KATIKA UTWALA WAKE,mbapo nyinyi hamuamini hivyo!!!Qurani ambayo sura zake na aya zake zilikuwa zinashuka kwa matakwa,mahitaji na changamoto mbali mbali katika miaka 23.Je umeingia katika Qurani ukasoma hoja ya wale makafiri jamaa zake Mtume muhamad ambao walimwambia wewe ni mzushi,muongo,mshairi,mwendawazimu,mchawi,badilisha qurani hii utelete qurani nyingine,simulizi za kale,umekuwa ukiandikiwa asbuhi na jioni na hoja kemkem ambazo kwa wakati wao huo walikuwa na haki ya kuifanyianyia changamoto Qurani hiyo ili wapate kujua kwamba ni kitabu cha kweli na haki na ndio moja ya jibu ni hii aya ambayo wewe umeifanya ndio mada ya mjadala huu angalia jibu lingine alilowaambia-si wao tu bali hata na sisi waisilamu wenyewe-sura ya ya 47 aya ya24''Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?Angalia tena jibu lingine hili katika sura ya 54,aya ya''Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo aneyekumbuka?

    Maalim Moses

    ReplyDelete
  25. Je umeyasoma na majibu mengine ya Qurani kwa chnagamoto zao hizo,jawabu hapana,je unazijua na umezikusanya na kuzichambua aya au sura za aidha zilizoshuka wakati wa Makkah kwa miaka 13 na zile ambazo zilishuka wakati wa Madina kwa miaka 10 kwa matakwa,mahitaji na changamoto mbali mbali?jibu hapana na je uliiweka maudhui yoyote au kuitafuta au kujiuliza swali lolote na ukazikusanya aya zote ndani ya qurani zinazoziongelea au kujadili kuhusu kadhia,swali au changamoto hiyo ukaiyona Qurani inakupa jawabu gani?jawabu hapana,je hata wewe mwenyewe kama ni muhubiri wa Injili je ulizikusanya sura au aya zote katika qurani ambazo zinzoongelea kuhusu itikadi ya dini yako kisha ukapata jibu la mwisho kwamba qurani inakwambia nini?hukufanya hivyo na hutofanya hivyo kwa woga wa kuukuta,kuujua na kuutambua ukweli mezani ambao nyinyi hamuhutaki,na nakuwekea changamoto hiyo mbele ya waumini wako na waisilamu tuziksanye aya na sura zote katika Qurani ambazo zinzoongelea kuhusu itikadi ya dini yenu kisha tuone ukweli upo wapi kisha tuapishane mbele ya Allah (s.w) kwamba anaekataa ukweli lana ya Allah(s.w),malaika zake na walimwengu wote ziwashukie.Hakika huwezi kufanya hili na hutolifanya .Sasa iwapo waarabu wenyewe wakati Qurani ilipokuwa inashuka mpaka imemalizika kushuka kwa miaka 13 ya Makka na miaka 10 ya madina walipewa changamoto moja ambayo mpaka leo hii ipo hai na inawanataka wale wate wasio amini Qurani hii ni maneno ya Allah(s.w) wathibitishe kinyume chake kwa kuandika Qurani yao aidha kwa majuhudi binafsi au hata walijikusanya wanadamu na majini na hadi leo hii na mapaka dunia inakwisha hakuna alieweza na atakaeweza kupambana na changamoto hiyo.Na nilidhani wewe kama muhubiri wa Injili ungeweza kutuletea changamoto hii tungekuelewa vyema kama uwezo huo unao.lakini waarabu wenyewe walishindwa pamoja na kuwa mabingwa katika lugha yao mama ya kiarabu hadi leo hii watu na majini wameshindwa kufanya hivyo na watashindwa kufanya hivyo.Allah(s.w) anaiweka changamoto ubaoni akisema;

    Maalim Moses

    ReplyDelete
  26. katika sura ya 2 aya ya 23-24 '' NA IKIWA MNA SHAKAKWA HAYO TULIYOMTEREMSHIA
    MJA WETU BASI LETENI SURA MOJA YA MAFANO WAKE,NA MUWAITE MASHAHIDI WENU BADALA YA MWENYEZI MUNGU IKIWA MNASEAMA KWELI'' NA MKITOFANYA-NA WALA HAMTOFANYA KAMWE-BASI OGOPENI MOTO AMBAO KUNI ZAKE NI WATU NA MAWE WALIO ANDALIWA HAO WALIO KANUSHA''
    Kisha akawaambia tena katika sura ya 17 aya ya 88 '' SEMA:WANGELIKUSANYIKA WATU NA MAJINI ILI WALETE MFANO WA HII QURANI BASI HAWALETI MFANO WAKE,HATA WAKISAIDIANA WAO KWA WAO''
    Na katika sura ya 10 aya ya 38 Allah(s.w)kawaoneni huruma kwa kuona labda changamoto ni kubwa mno kuandika kitabu kizima itakuwa ni tabu kwenu basi andikeni sura moja tu(fupi au ndefu) aliposema ''JE! NDIYO WANASEMA AMEIZUA?SEMA:HEBU LETENI SURA MOJA MFANO WAKE NA MUWAITE(KUKUSAIDIENI)MUWAWEZAO,ISIPOKUWA MWENYEZI MUNGU,IKIWA NYINYI MNASEMA KWELI''
    Allah(s.w)akaendelea kuwawekea changamoto hiyo akiwaambia katika sura ya 11 aya ya 13 '' AU WANASEMA: AMEIZUA? SEMA: BASI LETENI SURA
    KUMI ZILIZO ZULIWA MFANO WA HII, NA WAITENI
    MUWAWEZAO BADALA YA MWENYEZIMUNGU, IKIWA MNASEMA KWELI''.Changa moto ipo mbele yenu na si kwenu tu kama wakristo au wayahudi bali kwa walimwengu wote wenye mashaka na hii Qurani wanatakiwa wafanye hivyo,nasi tumo miongoni wa wenye kusubiri.

    Jonh,Qurani ni kitabu ambacho kina muda wa miaka 1400,kipo mbele yako wameshindwa waarabu wenyewe kukifanyia changamoto wa zamani mpaka wa leo ambao lugha yao ni tajiri sana na moja ya kuendelea kubaki lugha ya Kiarabu hai ni kutokana na Qurani wataalamu wa lugha wanasema lugha uzalika ukua uzeeka na kufa kwa sababu mbalimbali, ebu angalia lugha hizi ambazo zinazingatiwa zimekufa(.Neo-Hittite - Liburnian - Akkadian - Aramaic - Avestan - Church Slavic - Messapic - Eteocretan - Eteocypriot - Egyptian (Ancient) - Elamite - Etruscan - Geez - Mycenaean Greek - Gothic - Hittite - Hieroglyphic Luwian - Middle Hittite - Marsian - Milyan - Minaean - Kawi - Khotanese - Latin - Langobardic - Noric - North Picene - Numidian - Old Aramaic - Moabite - Old Chinese - Old Hittite - Minoan - Old Ossetic - Old Persian - Oscan - Old Tamil - Pahlavi - Paelignian - Phoenician - Palaic - Pyu (Myanmar) - Sanskrit - Sabine - Sicel - Sogdian - South Picene - Sumerian - Sicanian - Sorothaptic - Tokharian B - Tangut - Thracian - Tartessian - Ugaritic - Marrucinian - Aequian - Aquitanian - Bactrian - Camunic - Celtiberian - Cisalpine Gaulish - Chorasmian - Carian - Dacian - Edomite - Eblan - Epi-Olmec - Faliscan - Galatian - Harami - Hadrami - Hernican - Hattic - Hurrian - Iberian - Illyrian - Indus Valley Language - Lycian - Lydian - Lemnian - Ligurian (Ancient) - Alanic - Lepontic - Lusitanian - Cuneiform Luwian - Elymian - Median - Ancient Macedonian - Meroitic - Ancient North Arabian - Phrygian - Parthian - Punic - Qatabanian - Raetic - Sabaean - Scythian - Sidetic - Sakan - Transalpine Gaulish - Tokharian A - Early Tripuri - Umbrian - Urartian - Venetic - Vandalic - Volscian - Vestinian - Zhang-Zhung - Mysian - Kaskean - Pali).

    Maalim Moses

    ReplyDelete
  27. Je Jonh, unajua kwamba Jesus alihubiri Injili kwa lugha ya ARAMAIC?na unadhani kwa kufa kwa lugha hiyo baada ya kufa kwa Jesus je wafuasi wake walihubiri kwa lugha gani akiwemo Paulo mtengenezaji wa pili wa chistianity baada ya Jesus?je kama Paulo alihubiri kwa lugha ya Hebrew je unadhani na kuamini kwamba alikijua ki-Aramaic sawa sawa mapaka afikishe mradi wa Injili ya jesus kama Jesus mwenyewe alivyohubiri kaika lugha ya ARAMAIC?Ebu angalia vitabu vya dini hizi mbili za kiyahudi na kikristo baada ya wazee wao kutia mikono na miguu yao,ndani yake unakuta kuna story za ajabu ajabu,itikadi za ajabuajabu,lugha za kihunihuni na lugha za matusi(vulger language) na itikadi ambazo zinagongana kati ya TAURATI NA INJILI.Sasa ebu tuiangalie Qurani,na kwa vile bahati mbaya hujui kiarabu,ningekuomba uombe msaada japo kwa kuwauliza waisilamu na wasiokuwa waisalmu wanaokijua kiarabu jinsi gani Allah(.w)alivyokishusha kitabu chake,kwanza lugaha aliyoitumia,maneno alivyochagua na kuyapanga,mpaka herufi alivyozitumia na kuziweka mahala pake ili kuleta maana aliyoksudia kwa makini zaidi ambapo mwanadamu hana uwezo huo,na ndiyo maana waarabu walishindwa kuleta mfano wake kwa kukosa jibu la busara au kuamini walidai tu kwamba Muhammad ni mshairi na mchawi na Qurani yenyewe ni uchawi!Na ndio maana literature ya kiarabu kwa mabingwa wa lugha hiyo hadi hii leo bado inawashangaza!!je kweli kama tukitumia mantiki yetu huru na uhuru wa kufiri bila ya vikwazo tunaweza kudai kwamba kitabu hiki Qurani si maneno ya Allah(s.w)au kimeandikwa na Muhamad katika karne ya saba AD?!!!!!
    John,Qurani ipo mbele yako tangu miaka 1400 iliyopita,na kama kweli unataka uongofu(nina mashaka kama kweli unautaka uongofu)Qurani itakuongoa na kukuonyesha njia iliyonyoka na hilo ni jukumu lako na sio jukumu la Roho Mtakatifu kama ulivyodai katika moja ya post yako,ni mwanadamu ndie mwenye jukumu la kuchagua na kuamini kwa uhuru wake ukitaka amini na kama hutaki usiamini ni uhuru wa mwisho huo kwa mwanadamu na majukumu utayabeba wewe mwenyewe mbele ya Allah(s.w)na wala hatobeba JESUS WALA ROHO MTAKATIFU kama mnavyodai na kuamini.

    ITIKADI YENU INAYOJENGA MNAYOAMINI NI BATILI BATILI BATILI!!!!!
    Jonh,uliandika kwamba Mungu wa kweli ni mkamilifu kwa asilimia mia moja,swali ambalo mimi nakuuliza Jonh,Je ni Mungu gani huyu unayemkusudia hapa?Je ni Mungu Baba,Mungu Mama(Maria),Mungu mtoto(jesus)au Mungu roho Mtakatifu,au Mungu wote hao wanne hatimaye wanageuka na kuwa Mungu moja?!! mantiki ya kikikrısto kuhusu Mungu ni mantiki ya kujichanganya na kujidanganya, kwa vile nyinyi si watu wa kukaa na kuhoji kuhusu itikadi yenu mmezaliwa umejikuta wakristo mmepandikizwa na kunyonyeshwa itikadi ya utatu au uune ndiyo Mungu wenu!!John,mimi nakuomba ebu kaa pembeni acha kila kitu huwe huru wa mawazo tuanze kujadili itikadi yenu hi ya utatu au uunei bila ya taathira ya kuzaliwa kwako na kuwa muhibiri wa Ijili,Mantiki kwa itikadi yenu inasema hivi;hapa kwa waisilamu naomba mniwie radhi,si kwamba nakufuru bali naiweka picha katika fremu yake sahii kwa waumini wa kikristo

    Maalim Moses

    ReplyDelete
  28. Kama tunakubaliana kiitikadi kwamba Mungu ni mkamilifu kwa asilimia mia moja na hana upungufu wowote,hana mwanzo wala hana mwisho ni mwenye uhai wa milele,hasau wala kukumbushwa asinzii wala halali muumba mbigu,ardhi na walimwengu:naona wakristo mpaka hapa tupo pamoja,sasa mnachotufundisha nyinyi na kuitikadi mbona kinagongana na itikadi ya awali ya taswira ya Mungu.Nyinyi mnaamini kwamba baada ya kuwepo Mungu baba akajiona mpweke,akaona upweke huu ni lazima nitafute mke,akatafuta mke ambaye ni Maria,alipokuwa na mkewe maria akaona bado kuna mapungufu ikabidi ashauriane na Maria kuzaa mtoto tena wazae mtoto mmoja tu!hata hivyo wakaona bado kuna mapungufu wanahitaji msaidizi wa kusidiana kulea mtoto na wakamleta Roho Mtakatifu llakini huyu roho mtakatifu anakuwa msaidizi wa Mungu baba,Mungu,mama, na Mungu mtoto,ROHO HUYU ANAWAHUDUMIA HAWA MIUNGU MINGINE,wanamrusha popote wanapotaka kama hali inahitaji kufanya hivyo.Mungu baba siku moja aliwaita Mungu Mama na Mungu Mtoto na Mungu Roho mtakatifu wakashauriana kwamba inabidi kumuumba mwanadamu na kumleta duniani,na siku ya kuchukua maamuzi hayo wakawaita na malaika kuwashauri ushauri ambao wao hawatokua na maamuzi na wakatoa maamuzi kwamba wanataka kumuumba mwanadamu na mkewe,ingawa malaika mmoja alipinga kuumbwa kwa mwanadamu huyo na mkewe,lakini hatimaye waungu walishinda na kupitisha maamuzi yao hayo wakamuumba mwanadamu na mkewe na wakamuweka peponi au katika bustani ambayo hakukuwa humo tabu,shida wala kuteseka,loo!kumbe yule malaika aliepinga kuumbwa kwao akawafuata humo akawashawishi kwamba eti waungu walifanya makosa kukuumbeni wanadamu na mkitaka muishi kama malaika inabidi mkiuke maagizo yake aliyowapeni.mwanadaamu na mkewe walimkubalia malaika huyo ambaye anajulikana kama shetani,wakaenda kinyume na maagizo ya Mungu Baba au wote waungu wanne.hatimaye wakaondolewa katika bustani na kuletwa hapa duniani kwa kosa hilo la mume na mke,mke akapewa adhabu yake na mume akapewa adhabu yake na kizazi chao kikaukumiwa kwamba kitarithi madhambi waliyofanya wazazi wao, dhambi ya asili(original sin).Na baada ya miaka mingi kupita waungu hawa wanne waliona jinsi gani kizazi cha mwanadamu huyu na mkewe wanavyotenda maovu,ufisadi,na madhambi mengine makubwa makubwa,ikabidi wakae tena kitako washauriane nini cha kufanya bila ya kuwaita malaika, wakaamua kuwaletea watu wanadamu wa mfano wao(mitume) ili wawaonye na kuwaweka katika maadili mema ambayo miungu waliyaona bora kwa wanadamu.Lakini hata hivyo wanadamu hao waliendelea kukiuka maagiza ya miungu.Baada miaka mingi kupita,Miungu hiyo ilikiri na kuona kwamba wamefanya makosa makubwa kumuumba huyu mwanadamu ambaye anafanya uovu na ufisadi katika dunia na hasa baada ya kuwarithisha wanadamu hawa dhambi iliyotendwa na wazazi wao(dhambi asili) wakakaa tena kitako na kufikiri upya nini cha kufanya na kuamua, na mara hii tena katika kikao hichi cha pili malaika hawakushirikishwa.Miungu hiyo minne ilikubaliana kwa pamoja kwamba kwa vile tumewarithisha dhambi ya wazazi wao sasa wakati umeshafika wa kutolewa mtoto wetu KAFARA kwa ajili ya madhambi yote ya wanadamu au dhambi asili waliyorithi toka kwa wazazi wao!!!!!Wakaulizana je

    Maalim Moses

    ReplyDelete
  29. ni jinsi gani ya kumtoa mtoto wetu huyu KAFARA?Mungu Baba akaamua kwa kusema kwamba wewe mke wangu utangulie kwenda duniani katika umbile la kibinadamu,kisha huyu Mungu Roho mtakatifu atakuwa anakuja mara kwa mara kukutembelea na kuandaa mazingira mazuri ya kuja kwa mtoto wetu,naam,Mungu mama akaja duniani katika umbile la kibinadamu na kwa kukubaliana na Miungu mingine afikie kwa wayahudi na yeye mwenyewe ajulikane kama myahudii na kujificha katika dini ya kiyahudi,lakini ajabu ya mambo Mama huyu Mungu hata siku moja hakuwaambia wayahudi kwamba amekuja kujiandaa kuzaa mtoto wa Mungu akficha siri hiyo, na wakati ulipofika Mungu Roho Mtakatifu kwa maamrisho ya Mungu Baba akamtia Mungu MWANA katika tumbo la Mungu Mama na akazaliwa kama wanavyozaa wanawake wengine wa kibinadamu,lakini kwa vile Mungu Mama hakuwaambia wenyeji wake na kuendelea kuficha kama yeye ni Mungu Mama, wayahudi wenyeji wake hawakukubali kwamba Mungu Mama amezaa Mtoto bila ya kuolewa na hatimaye yeye na mtoto wake wakahukumiwa ifuatavyo; mama ni malaya na mtoto ni wa haramu!!!!!sasa baada ya yote hayo leo Mungu Mtoto ndie amekuwa center ya imani na itikadi ya wa wakristo katika dini yao,unawasikia JESUS MAISHA,JESUS UWOKOVU,JESUS UHAI,JESUS NJIA YA KUFIKA KWA MUNGU BABA,JESUS MFUTA MADHAMBI,JESUS NDIO KILA KITU!!na unapoendelea kusikiza mahubiri yaho mpaka unafikia kuamini kwamba Mungu Baba na Mungu Mama wapo likizo ya muda mrefu na hawana kazi ya kufanya mapaka siku ya dunia kwisha,na hii dunia inaendeshwa na kutawaliwa na Mungu Roho Mtakatifu na Mungu mtoto ndio wao wawili wanaekwenda mbio katika kuendesha shughuli za kila siku za huu ulimwengu na viumbe vyake.Ukisikia mkristo anasema tumsalie Bwana basi Bwana huyo ni Jesus!tumsifu Bwana basi Bwana huyo ni Jesus!Tumuombe Bwana basi Bwana huyo ni Jesus!!Tatizo lenu wakristo mmechagua njia fupi(shot cut)kwamba JESUS amebeba madhambi yenu kwa hiyo mpo huru kufanya chochote kile kilikuwa kizuri au kibaya muda wa kudumu Jesus kabeba madhambi hayo!!!je mnatutaka na sisi waisilamu tuamini hivyo wakati tunajua wazi kwamba kwa mafunzo ya Qurani yetu hakuna mwanadamu anayebeba madhambi ya mtu mwingine hata sheria za kimataifa inalikubali hilo leo haileti mantiki madhambi kama ya akina Hitler,Stalin,Pol Pat, na mafano wao ayabebe Jesus na watu hao wakakae kwa amani na usalama katika mamlaka ya Miungu hiyo minne!!!Cha kushangaza zaidi kwa nini mnafanya madhambi na kwenda kuungama madhambi yenu kwa wakuu wenu wa kidini wakati Jesus ameyabeba?kwa nini mnafanya mambo na matendo mema hapa duniani wakti mmeshahakikishiwa kuingia kitka ufalme wa miunguyenu peke yenu?!!kwa nini msijiunge tu na walevi,majambazi,wezi,wazinifu na mafisadi wa dunia?!!!

    Maalim Moses

    ReplyDelete
  30. Maswali ya kujiuliza ni mengi tu lakini tunaendelea kuuliza, je ni kweli kwamba wanadamu wamerithi dhambi ya asili toka kwa mwanadamu wa kwanza na mkewe? Mpaka waungu wanne waamue kumtoa mtoto wao KAFARA?na kama hivyo ndivyo ilivyo kwa nini Mungu Baba aamue kuwaleta mitume na manabii lukuki iwapo tu anajua kwamba ameeshafanya kosa kubwa la kuwarithisha wanadamu dhambi ya wazazi wao?kwa nini Mungu Mama asiwatangazie mapema wenyeji wake(mayahudi) kwamba yeye yupo kwao kwa ajili ya kumzaa mtoto wa Mungu?Na siri ipi iliyopo mpaka MTOTO WA MUNGU AZALIWE KATIKA UGENI WA KIYAHUDI? Na kwa nini Mungu asubiri kwa miaka yote hiyo na kusema kwamba ungofu wa mwanadamu upo katika kumuamini mwanangu?na vipi kuhusu wale watu(vizazi)vya kale ambavyo hawakumuona Jesus,kumjua au kumsikia na ambao hawakumuamini?kwa nini wasemehewe madhambi yao wakati hawakumjua huyu Mtoto wa Mungu?Na kwa nini kuwe na siku ya hukumu ambapo mtoto wa Mungu atakaa kuliani mwa baba yake wakati wakitoa hukumu?(hapa sijui Mungu Mama na Mungu Roho matakatifu wataka upande gani)sasa je hukumu hiyo ni ya nini wakati Mungu mwana Kashatolewa KAFARA kwa walimwengu wote?Hii ndio itikadi yenu na dini yenu wakristo ili mujikinaishe wenyewe itikadi hiyo inabidi kutowapa umuhimu au nafasi mitume mingine ambayo ameileta Mungu Baba au hata kuikataa na kuipinga kama mnavyomkataa na kumpinga Mtume Muhammad.Naam,inabidi mfanye hivyo kwani kuamini kwamba Jesus ni mwanadamu na mtume,mjumbe wa Mungu ametumwa kama walivyotumwa mitume mingine ukristo utakuwa haupo tena utaanguaka na aidha ujaribu kuwa myahudi na wayahudi ni ya matumbo 12 tu au uingie dini ya walimwengu wote ambayo ni dini ya kiisilamu nanyi hamlitaki hilo.kwa hiyo itikadi yenu hiyo ya waungu watatu au wanne kwa mmoja haileti maana wala haikubaliki kimantiki ni itikadi ambayo wameiingiza mababu zenu katika Injili ya kweli kupitia Paulo na wengineo waloandika Ijili tofauti.Hiyo ni itikadi ya kipagani ambayo unaikuta katika MYTHOLOGY katika dini za wagiriki wa kale ,wamisri wa kale na mapagani wa wa kale wa ulaya.Lakini kama mnamtafuta Mungu wa kweli kwa sifa kamili za uungu mtafuteni katika Taurati na katika Qurani mtakuta humo ambaye NI MUNGU MMOJA TENA MMOJA PEKEE HANA MWANA WALA MKE WALA MSHIRKA KATIKA UUNGU NA UTAWALA WAKE, AMBAYE ANAUENDESHA HUU ULIMWENGU PEKE YAKE NA NDIYE ATAKAYESIMAMIA SIKU YA HUKUMU PEKE YAKE BILA MKE WALA MTOTO WALA ROHO MATAKATIFU HUYU NDIE MUNGU ALIELETA MITUME YOTE NA MANABII WOTE WANADAMU AKIWEMO JESUS KWA UJUMBE MMOJA TU HAKUANA MUNGU WA KWELI ISIPOKUWA NI YEYE TU NA HAKUNA APASAE KUABUDIWA KWA HAKI NA KWELI ISIPOKUWA NI YEYE TU PEKE YAKE.ANGALIENI ITIKADI HIYO KATIKA TAURATI NA QURANI MTAIKUTA HAI NA NDIO CENTER YA CRY BATTLES YA MITUME YOTE,KWA NINI MUMPUUZE BABA WA MITUME IBRAHIMU, NA AMBAYE ALIYEIZATITI ITIKADI HIYO YA KUMPWEKWESHA MUNGU PEKE YAKE?KWA NINI MUMPUUZE NABII NA MJUMBE MUSA AMBAYE ALIZIDI KUIPIGANIA ITIKADI HIYO KWA NGUVU ZAKE ZOTE KWA WATU WAKE AMBAO WALIISHI KATIKA UTAMADUNI WA KUABUDU MASANAMU WALIPOKUWA MISRI NA WAKAFANYA KOSA HILO WALOPOKUWA KATIKA JANGWA LA SINAI?JE HAMUONI,HAMSIKII NA WALA HAMUONGEI??!!!

    Maalim Moses

    ReplyDelete
  31. Je wewe Jonh unamjua na kumuamini mungu huyu mmoja kama walivyofundisha mitume yote ya kibinadamu akiwemo JESUS? au bado unaendelea kuamaini kwamba miungu mnne kwa mmoja ndie Mungu wa kwel?i kama utanisoma kwa akili ya wazi isiyovishwa magubigubi nadhani utanielewa na kuanza kufikiria upya na kutafuta ukweli ambao ni nuru katika Qurani mpira upo uwanjani kwenu na wala haupo uwanjani kwetu.Na ndugu zangu waisilamu mtaniwia tena radhi kwa kutolea mfano huu wa itikadi ya wakristo kwa kuweka katika utaratibu huu ambao wao wanaouamini.Ewe Mungu Moja nimefikisha ujumbe, naomba uwe mwenye kushuhudia!!!
    Maalim Moses.

    ReplyDelete
  32. Maalim Moses, asante sana kwa kutembelea blog hii na kutoa yaliyo moyoni mwako kwa wingi namna hii. Ninapitia kila kitu ulichoandika kisha nitasema kile ambacho nimeelewa, ili yamkini, kwa neema ya Mungu tunayemtafuta kwa bidii zote namna hii, tuweze kufika mahali pazuri - iwe ni kupitia Uislamu au Ukristo - maana naamini kuwa tunachokitafuta ni MAPENZI HALISI ya Mungu.

    Maana swali kubwa ni kuwa, je, hayo mapenzi ya Mungu yamo kwenye kitabu gani hasa?

    Asante sana.

    ReplyDelete
  33. Rafiki, James John,

    Aya ya 8:39 ilishuka wakati wa vita (makafiri walikuwa wanawatesa waislamu na wanawapiga Waislamu , Waislamu wanaambiwa wapingane nao , in self defence) lakini wakiacha kupigana na nyie na kuwatesa waacheni),

    Aya hiyo inasema hivi: Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda. (Quran 8:39).

    Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema (Quran 8:40).

    Unataka nikulitee chinja chinja iliopo katika Biblia ?

    (Mie ni Hamudi123, nazo account mbili). Nasubiri majibu ya maswali yangu (yote).

    ReplyDelete
  34. Ndugu. Ama m/mungu ni mkubwa. Akktaka ujue utajua na asipotaka hutojua. Kafiri ni mtu mpingaji hasa anapinga juu ya m/mungu uwepo wake.

    ReplyDelete
  35. Quran ni kitabu kilicho barikiwa na kipo wazi. Mada zote zinazozungumziwa hapo zinaeleweka na wala hazijichanganyi ila huyo anaye tafsiri hiyo tafsiri ndio anajichanganya mwenyewe wala sio quran. Msaada amtafute sheikh anaye tambulika ili amfahamishe makusudio ya tafsiri ya quran tukufu.

    ReplyDelete
  36. Aya nyingi za quran naweza kusema zote zinahitaji hekima ya hali ya juu.utulivu na kuwa tayari kitafakari neno kwa tafakari/tafakuri ya hali ya juu. Imekaa hasa kisayansi

    ReplyDelete
  37. Wakristo wachache kama huyo hapo juu ni vema angesema ukweli lengo lake na wala asinge danganya. Tayari naye namuona yupo katika aya moja ambayo quran inawataja watu wa stile hiyo(sito itaja aya hiyo)

    ReplyDelete
  38. Lakini aya hiyo inazungumzia watu wenye kuisoma quran kwa lengo la kutafuta upogo. Na m/mungu aliyetukuka ameweka wazi kabisa katika aya hiyo. Allahu akbar. (waislamu kwa yakini mwenyezi mungu ametoa kitabu kwa haki na bila ya hiki kitabu basi tungeangamia kwa upotofu)

    ReplyDelete
  39. Nimepitia katika mitandao hoja za wakristo wenye kusema uongo kama ule wa nataka kujifunza nk kumbe la. Wote mada zao kwangu zinajirudia na zinaonesha wazi hawana elimu ya kuweza kuielewa quran. Wengi wanao ielewa wapo wazi tena wanahofu juu ya mwenyezi mungu.

    ReplyDelete
  40. Wengi wa wakristo mfano wa huyo jamaa hapo juu(lakini sio wote) hawana hofu ya mungu. Wao wanaona ni kawaida tu, heshima haipo. Naamini waislamu wote wanaheshima sana kwa m/mungu na akitajwa nyoyo zao zinakuwa katika hali fulani...

    ReplyDelete
  41. Watu hasa wakristo someni someni tafuteni mashekhe wanaojulikana ninamaana wenye weledi ili wawajuze mambo mazuri mnayo yakosa kutoka katika quran.Quran ni rehma kwa watu wote,uliza kwa wajuzi utafahamu vema na utapata faida pia. Katika uislamu hakuna mambo ya uzushi. Kila kitu kina sababu kama ilivyo hesabu au sayansi.na dini ya islam imekamilika, inamaana haiitaji ziada. hivyo utapewa ujumbe wa lailaha illallah.

    ReplyDelete
  42. Yesu alitoa angalizo. Waislamu tumshukuru m/mungu kwa kweli yeye anatuhurumia sana na anajua shetani ni adui yetu wa wazi.na watu waliopita wamepotezwa na huyu iblis. Hakuna hoja hata moja baada ya kuangalia kwa karibu zinazosemwa na makafiri ila zina majibu katika quran hiyo hiyo. Hili ni katika mambo yanayo nishangaza sana na zaidi quran ilivyo ni miujiza ya kuendelea. Yanayosemwa japo na huyo jamaa ni mambo madogo sana,yapo mambo ambayo quran inajibu kwa kushangaza... Vijana someni quran kwa tafakuri someni tena someni mtaona mambo. Hakika mwenyezi mungu anaona na anayo habari ya yote. Tumuombe msamaha kwa makosa yetu madogo na makubwa... Na makafiri washindwe kabisa.

    ReplyDelete
  43. mada nzuri, wachangiaji mmeharibu. mngekuwa mnaulizana maswali kiasi, majibu yakishatolewa mnauliza mengine. sasa kwa hapo yajibiwe ya john au abdul au hamad au mzizimkavu? wabongo bana!!!

    ReplyDelete
  44. Tunasubiri majibu ya bro hamud kutoka kwa John kuh utatu,roho mtakatifu,na mengineyo

    ReplyDelete
  45. Tafsiri hizi sio za kweli kabisa. Mwandishi pamoja na wasomaji ili uamini kuwa mwandishi wa mada hii ametafuta fitna kama quran yenyewe iliwezakuwatambua watu ni katika surat imrani 2:7 “Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.”

    Wasomaji rejeeni hizo nukuu za aya alizozirejea kwny mada yake na tafuteni tafsiri mtabaini kuwa hakuwa na weledi wa kutoka katika kunukuu maana halisi

    Angalieni alivyonukuu na maana halisi hizo chache hapo chini


    Al-Nisa 4:101

    The unbelievers are your sworn enemies.

    Yaani,

    Wale wasioamini ni maadui zenu wakubwa.

    Maana halisi ni

    “101. Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.”

    Vilevile inasema katika sura Al-Tawba 9:3

    Proclaim a woeful punishment to the unbelievers.

    Yaani:

    Tangazeni mapigo makuu (ya ole) kwa wasioamini.

    Maana halisi

    3. Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina. Basi mkitubu itakuwa kheri kwenu, na mkigeuka basi jueni kuwa nyinyi hamumshindi Mwenyezi Mungu. Na wabashirie makafiri kuwa watapata adhabu chungu.

    Pia quran inasema katika sura Al-Anfal 8:39

    Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.

    Yaani:

    Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.

    Maana halisi
    39. Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda.

    “ sura hiyo Al anfal ni sura ya vita... wakati huo waislam wanapigana vita ndiyo aya hiyo ilishuka”

    ReplyDelete
  46. Mwandishi naona umetafsiri out of content kwny Surat Baqara aya 109.. Kwa kusema

    " Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake."

    Uhalisia wa maneno hayo katika Quran ni

    Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake.
    kwa kiarabu ni
    فَاعۡفُوۡا وَاصۡفَحُوۡا حَتّٰى يَاۡتِىَ اللّٰهُ بِاَمۡرِهٖ

    "faoAAfoo waisfahoo hatta yatiya Allahu bi amrihi"

    Hivyo sio kweli hiyo conclusion yako ya kusema "Allah kwa wakati wake atawafunulia wale wasioamini ukweli wa mambo."

    ReplyDelete
  47. Ukweli ni kuwa hakuna anayejua kitabu kamili cha mwenyezi mungu shetani hujitahidi kwa kila njia ili awe na wafwasi cha muhimu ni kuwa mwamini mungu jinsi ulivyo mchukulia kwa nafsi yako. Ole wao wanaopinga neno la mungu pasipo kujua wanaopinga ukweli wa mungu, siku hiyo utakuwa pekee yako.TAFUTA majibu yako mwenyewe bali usitafutiwe wala wakutafutie. Mungu awe nasi.

    ReplyDelete
  48. Lakini katika injili rumi si Kuna kisa Kuna watu walitaka kumdhuru mtume SAW bahati nzuri Kuna mkatoliki akamuwai mtume njiani akamwambia usipite njia hii Kuna watu wa nataka kukudhuru na kweli mtume alibadili njia akasalimika je waislam wanajua ukaribu wa mtume SAW na wa katoliki.. Hasa waislam wa sasa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sijaelewa unamaanisha nini unaposema iNJILI RUMI - kama ni Waraka wa Warumi haiwezekani, maana uliandikwa miaka zaidi ya 500 kabla ya Muhammad kuzaliwa.

      Delete