Naamini umeshasikia mara kadhaa watu wakitaja kile kinachoitwa “sayansi ya
kiafrika”. Kwa kifupi maneno haya yanaongelea kazi za waganga wa kienyeji. Ni
wazi kuwa yanamaanisha upigaji ramli, uaguzi, usafishaji nyota, na hata ulozi
na mengine kama hayo.
Siku hizi watu wengi wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la
kupata “mafanikio”, wakiwamo wanasiasa, wafanyabiashara, wafanyakazi, wake,
waume, wapenzi, wachumba, wanamuziki, na hata wale wanaotaka kuwakomesha
wabaya wao.
Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao
mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza. Angalia basi, mwanga ulio
ndani yako usije ukawa giza.
Basi kama mwanga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu iliyo na
giza, mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikiapo kwa
mwanga wake. (Luka 11:34-36).
Kati ya mambo ambayo adui yetu shetani anajaribu
sana kuyafanya ni kuiba muda ambao tunatakiwa kuwa na Bwana – iwe ni katika
kumwomba, kutafakari, kusoma Biblia, kusikiliza ibada, n.k. Adui anajua kuwa,
kama akiweza kutufanya tutumie muda mwingi kwa ajili ya mambo mengine badala ya
Bwana Yesu, basi mwisho wa safari atakuwa ametunasa, maana Biblia inasema wazi:
Msalaba
wa Bwana wetu Yesu Kristo ndilo jambo kubwa kabisa katika maisha yetu, maana
unamaanisha wokovu. Na wokovu ni kila kitu - uponyaji, msamaha wa dhambi, uzima
wa milele!
Video hii inamwonyesha mtu ambaye ni mzaliwa wa
ukoo wa Abu Bakr Saddiq, ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa Mtume Mohammad. Abu
Bakr Saddiq pia ndiye aliyekuwa Khalifa wa kwanza kwenye ulimwengu wote wa
kiislamu baada ya kifo cha Mtume Mohammad.
Mzaliwa huyu anaitwa Dk. Nasir Siddiki. Yeye pia ametokea kwenye
familia tajiri. Akiwa na umri wa miaka 35 alikuwa tayari ni milionea, huku
akimiliki kila kitu cha kupendeza ambacho unaweza kukifikiria – iwe ni magari
ya kifahari, majumba, nk.
Makala haya niliyatoa kwenye blog nyingine, inawezekana umeshayasoma,
lakini nimeona kuwa ni vema niyatoe tena hapa kwa ajili ya yeyote ambaye
hakupata nafasi ya kuyasoma. Hii ni kwa sababu ni makala ya muhimu sana,
yanayotuonyesha tuko wapi katika ratiba ya nyakati, majira na unabii.
Utakaposoma kilichoandikwa humu, itakuwa ni jambo jema kuwapatia hata
wengine unaowafahamu, ama kwa kwa njia ya baruapepe au kwa kuwaambia wasome
makala haya wao wenyewe katika blog hii. Mungu akubariki kwa hilo.
Kanisa Katoliki limekuwa
likifundisha kwa miaka na miaka kwamba tunaweza kuwaomba watakatifu walioko
mbinguni watuombee kwa Mungu. Je, jambo hili lina ukweli kibiblia? Je, hili ni
fundisho la Mungu au ni la wanadamu? Je, mtu anayefanya hivyo anampendeza Mungu
au anamuudhi?
Hakuna mahali popote
katika Biblia ambapo tumeagizwa kuwaomba watakatifu ili watuombee kwa Mungu. Sasa
haya mafundisho yanatoka wapi? Unawezaje kuwafundisha watu kitu kisicho kwenye
Biblia halafu usiwe na hatia ya kuongeza au kupunguza ujumbe wa Mungu; maana
Bwana anasema kuwa atakayeongeza au kupunguza katika neno lake ana hatia.
(Ufunuo 22:19).
Nani ni "heroes" wa watoto wako. Je, ni wacheza mieleka? je, ni washika bunduki na wauaji wa kwenye sinema na video? Ukimnunulia zawadi mwanao, je, unamletea nini? Je, ni "toy" ya bunduki au ni nini?
Hatima ya mwanao iko mikononi mwako. Kile unachofanya au usichofanya angali bado mchanga ndicho kitakachoamua maisha yake ya baadaye; na hata uzima au mauti ya milele ijayo.
Contina
Mambo
tuliyoyasikia na kuyafahamu, ambayo baba zetu walituambia. Hayo hatutawaficha
wana wao, huku tukiwaambia kizazi kingine, sifa za BWANA, na nguvu zake, na
mambo yake ya ajabu aliyoyafanya. Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, na
sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu wawajulishe wana wao,
ili kizazi kingine wawe na habari, ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na
kuwaambia wana wao. (Zaburi 78:3-5).
Kanon Tipton
Wanao
wakiyashika maagano yangu, na shuhuda nitakazowafundisha; watoto wao nao
wataketi katika kiti chako cha enzi milele. (Zaburi 132:12).
Mwenye
haki aendaye katika unyofu wake, watoto wake watabarikiwa baada yake. (Mithali
20:7).
Hata
mtoto hujijulisha kwa matendo yake; kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
(Mithali 20:11).
Kanon Tipton
Mlee
mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. (Mithali
22:6).