Kufanywa kuwa ajenti wa
shetani
Sikuwa
na hisia za kibinadamu wala huruma ndani ya moyo wangu tena. Niliingia kazini mara moja na
kuharibu nyumba tano kwa wakati mmoja. Nyumba hizo zilizama ardhini pamoja na
wakazi wake wote. Tukio hili lilitokea Lagos Agosti 1982. Kontrakta aliyejenga nyumba hizo alishikiliwa
kwa kosa la kutoweka msingi imara na alilipa faini kubwa sana. Uharibifu
mwingi unaotokea duniani hivi leo hausababishwi na wanadamu. Kazi ya ibilisi
ni kuiba, kuchinja na kuharibu. Nasema tena, “shetani hana zawadi za bure!”
Niliingia kwenye
kusababisha ajali barabarani, n.k. Moja ambalo ningependa kulitaja lilikuwa
linamhusu kijana mmoja ambaye ndio kwanza alitoka kuokoka na akawa anashuhudia
kuhusu wokovu na ukombozi wake. Alikuwa anasababisha uharibifu mkubwa sana
kwenye ulimwengu wa roho wa giza kwa kufanya hivyo. Kwa hiyo, nilipanga ajali
kwa ajili yake. Siku moja alikuwa akisafiri kwa basi kuelekea Lagos. Kule nako
alikuwa anaenda kutoa ushuhuda wake mahali fulani. Wakati basi likiwa kwenye
mwendo mkali, nililitoa nje ya barabara na likaenda kujigonga kwenye mti. Abiria wote walikufa isipokuwa huyu mwokovu
mpya!
Kupona kwake
kulikuwa kwa miujiza maana alitoka nje ya basi kupitia kwenye buti na akapaza
sauti, “Nimepona! Nimepona!” Tulijaribu kila njia kumfanya aache kushuhudia
lakini tulishindwa.
Kupitia
kwenye TV, tuliweza kumjua mtu ambaye ameokoka hivi karibuni na tungemfuatilia
kwa nguvu ili kuona kama tunaweza kumfanya arudi nyuma. Iwapo baada ya miezi sita
hatujafanikiwa, tunaenda kwenye biashara
yake na kuifanya ifilisike. Kama ni mfanyakazi wa umma, tunamnyanyasa
kupitia kwa bosi wake; na ikiwezekana, tunasababisha bosi wake amfukuze
kazi. Iwapo baada ya yote haya bado anashikilia wokovu wake, ndipo tunakata
tamaa. Lakini kama ikitokea akarudi nyuma, anauawa palepale ili kuhakikisha
kuwa hapati nafasi ya pili ya kutubu.
Niliharibu maisha ya watu kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba Lusifa alifurahi sana na kunifanya kuwa mwenyekiti wa wachawi. Mwezi mmoja baada ya kupewa uenyekiti huo, mkutano uliitishwa. Tulihudhuria mkutano huo tukiwa ndege, paka, nyoka, n.k. Viumbe hawa ni wa muhimu sana kwa sababu zifuatazo:
- Kujigeuza ndege humfanya mchawi awe hatari zaidi.
- Kujigeuza paka kunamfanya mchawi aweze kuwafikia mapepo na pia kuwafikia wanadamu.
- Kujigeuza panya kunamwezesha mchawi kuingia kwenye nyumba za watu kirahisi, na usiku anageuka kuwa kivuli, na kisha mwanadamu na kunyonya damu ya mtu aliyelengwa.
Kwenye mkutano
huu tulikuwa na ajenda moja tu: “Wakristo.” Kisha tulipanga kuwa na mkutano mkuu wa wachawi wa Afrika kwenye
jiji la Benin mwaka 1983. Tulitangaza mkutano huo kwenye magazeti
mbalimbali na kwenye vyombo vingine vya habari. Nguvu zote kubwakubwa za giza
zilikusanywa na tulikuwa na uhakika kwamba hakuna kitakachoharibu mkutano wetu.
Kimsingi, kila kitu kilipangwa vizuri sana na hakukuwa na mwanya wa kutokea
kosa.
Lakini ghafla,
Wakristo wa Naijeria waliingia kwenye maombi na sifa kwa Mungu wao. Mipango
yetu yote ilisambaratika! Si tu hivyo, lakini pia walisababisha vurugu kubwa sana kwenye ulimwengu wa giza. Matokeo yake,
mkutano ule wa wachawi haukuweza
kufanyika Naijeria. Wakristo ni
lazima watambue kuwa mara waingiapo kwenye sifa za kweli kwa Mungu Mwenyezi,
kunakuwa na matatizo na kuchanganyikiwa baharini na angani; na maajenti wa
shetani wanakosa mahali pa kupumzikia. Maombi ni kama kutupa mabomu na kila
mtu anakimbia ili kuponya maisha yake.
Kama
Wakristo wangetambua na kutumia nguvu na mamlaka ya Mungu waliyopewa, wangetawala
masuala ya mataifa yao! Ni Wakristo tu ndio wana uwezo wa kuokoa taifa.
Baada ya
mkutano ule kushindikana, ambapo baadaye ulifanyikia Afrika Kusini, niliitwa
tena baharini. Nilipofika kule, niliambiwa kuwa baharini ndiko kutakuwa
nyumbani kwangu kwa kudumu, na duniani nitakuwa nakwenda tu kama kuna jambo
gumu la kufanya. Nilikabidhiwa majukumu
mapya – kubuni hirizi na dawa kwa ajili ya waganga wa kienyeji, kuwa msimamizi
wa chumba cha kuongozea (control room) na kutuma zawadi, kufungua
makanisa ya majoho meupe - white garment churches (nyumba za maombi), kufungua
zahanati za uzazi (maternities), kufungua maduka na kuyafanya yakue, kutoa ‘watoto’
na fedha. Nitayaelezea mambo haya moja baada ya jingine:
- Kufungua makanisa ya majoho meupe - white garment churches
- atakubali kutupatia roho moja au mbili kila mwaka.
- akifikia ngazi fulani kwenye kanisa, ataingizwa kwenye kundi letu.
- hakuna mshirika atakayeruhusiwa kuingia kwenye nyumba ya maombi akiwa amevaa viatu.
Anapokubaliana
na masharti haya, anapewa kitu kama “white gravel”, mifupa wa binadamu, damu
na hirizi, vyote vikiwa kwenye mtungi wa kienyeji. Kisha ataelekezwa akaufukie
mtungi huo na vitu vilivyomo mbele ya kanisa na kuchimbia msalaba juu yake. Baada
ya kufanya hivyo, ni msalaba tu ndio utakaokuwa unaonekana. Atashauriwa ajenge
kidimbwi au beseni ambamo mapepo yataendelea kuweka maji maalum. Haya ndiyo
maji ambayo utawasikia wachungaji hao wakiyaita "maji matakatifu."
Watu wengi
wanaposumbuliwa na mapepo wanaenda kwa hawa “manabii” ili yakatolewe. Ukweli ni
kwamba, wanaenda kuongezewa tu mapepo zaidi. Shetani hawezi kumtoa shetani
mwenzake. (Luka 11:17-19). Atakachofanya huyu nabii ni kumwombea huyo
mshirika, kisha anampa kitambaa chekundu akaweke nyumbani kwake. Halafu atamshauri
awe anaomba huku amewasha mshumaa na ubani. Kwa kufanya hivi, mtu huyo anakuwa
anatukaribisha sisi kwenye nyumba yake. Wakati mwingine mshirika anaweza
kuambiwa alete mbuzi, n.k. kwa ajili ya kafara. Kafara hizi ni kwa jili yetu
ili tuweze kuja kusaidia kumponya. Nabii anakuwa hana nguvu ya kutibu au kuponya.
- Kufungua zahanati za uzazi
Kama mwanamke akija kwetu kutaka msaada wa kufungua zahanati ya uzazi na kuifanya ikue, atapewa masharti:
Mwezi mmoja utateuliwa na sisi ambapo watoto wote watakaozaliwa katika mwezi huo kwenye zahanati hiyo, watakufa. Lakini wale wanaozaliwa kwenye miezi mingine, wanaishi.
Kama akikubali, naye pia atapewa hirizi inayowavuta watu kuja kwenye zahanati yake. Zahanati za namna hii zipo Onitsha, Lagos, n.k. Viatu haviruhusiwi ndani ya zahanati hizo.
- Kufungua maduka
- Kutoa watoto
Ningependa kusema kuwa utasa mara nyingi husababishwa na mapepo hapa duniani, lakini mtu wa namna hiyo atakuwa na watoto baharini. Kwa hiyo, ningependa kuwausia wana wa Mungu kuwa ni vema kumsubiri Mungu maana Yeye hutoa watoto halisi.
- Kutoa fedha
Chochote atakachoamua kutoa ni lazima kitoke kwenye tumbo lililomzaa na yeye. Jambo muhimu la kukumbuka ni kuwa, wakati wa kumuua huyo aliyetolewa, mtu aliyemtoa atapewa mkuki au mshale. Ndugu zake watafanywa wapite kwenye kioo. Mara atakapomwona yule aliyemchagua, ataambiwa amchome na anapofanya hivi, nduguye huyo atakufa papohapo kokote kule aliko.
Ziko njia nyingine mbalimbali lakini katika zote hizo, kitu kimoja anachofanya shetani ni kwamba, anahakikisha kuwa kwenye hizo njia mbalimbali, mtoaji kafara ndiye anayehusika na kifo cha aliyetolewa kafara kwa kumfanya ampige au amchome mtu huyo.
Kumbuka, shetani hana zawadi za bure!!
asante sana na mungu akubariki. mbona sehemu ya pili na ya tatu hazipo? kuna ya 1,4 na 5 tu .kama ni ukijaliwa plz ziweke pia
ReplyDeleteShalom, shalom.
DeleteSehemu zote zipo angalia tu vizuri utaziona.
Bwana akubariki.
Shalom hongera sana kwa shuhuda kemkem unazotupa. Mungu akubarikisana. Tupe basi mwendelezo Wa 6 na 7
DeleteShalom mpendwa.
DeleteNimekuwa kwenye ratiba ngumu sana kwa kipindi sasa ndio maana sijaweza kuendeleza sehemu zinazofuata, lakini Bwana ni mwema, sehemu hizo naziweka ndani ya siku tatu hivi.
Ubarikiwe nawe pia.
SHUHUDA HIZI ZINAJENGA SANA UFALME WA MUNGU.HASA SISI WAHUBIRIRI TUNAPATA UJASIRI SANA KWA KUJUWA SIRI ZA ADUI YETU MKUU SHETANI.UBARIKIWE SANA TUNASUBIRI MUENDELEZO WA SHUHUDA HII KUOKOLEWA NGUVU ZA SHETANI.
DeleteMUNGU AKUBARIKI SANA MTUMISHI KWA KUWEKA SHUHUDA HIZI ZINATUYSAIDIA SAANA KUSIMAMA NA KUTAMBUA YA KUWA MUDA WETU U MFUPI SAANA...ENDELEA KUTULETEA SHUHUDA ZINGINE..
ReplyDeleteshalom, shalom. asante sana kwa maoni yako na Mungu azidi kukubariki na kukuinua. Namshukuru Bwana sana kama kazi hii inaleta mchango kwenye mwili wa Kristo.
Deleteumekuwa kimya sana mtumishi kwa sehemu ya 6 na ya 7 ya ushuhuda huu.nimeifuatilia kwa wiki 3 sasa bila mafanikio.tafadhali mtumishi ninaomba utuwekee sehemu hizo.shuhuda hizi zinatujenga sana na kuinua imani zetu.na MUNGU muweza wa yote akubariki sana.
ReplyDeleteShalom, najitahidi kufanya hivyo ndugu yangu. Mungu wetu ni mwaminifu, atafanya uwezekano upatikane tu. Bwana akubariki.
Deleteni ushuhuda mzuri hongera na pole
ReplyDeleteKaka mbona kimya sana siku hizi,tume miss shuuda na mafundisho yako tafadhari tukumbuke tafadhari!!!
ReplyDelete