Monday, June 2, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 6



Sura ya 4: Jinsi shetani anavyopambana na Wakristo


“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” (Efe 6:12) 

Kupambana na Wakristo
Baada ya amri kutoka kwa Lusifa ya kupambana na Wakristo, tulikaa na kupanga njia zetu za kupambana nao kama ifuatavyo:




1. Kusababisha magonjwa.
2. Kusababisha utasa.
3. Kusababisha usingizi Kanisani.
4. Kusababisha machafuko Kanisani.
5. Kusababisha watu kuwa vuguvugu Kanisani.
6. Kuwafanya wasijue Neno la Mungu.
7. Kuwaingiza watu kwenye fasheni na kuiga mambo.
8. Kupambana nao kimwili.

Katika hayo yote hapo juu, nitapenda kuelezea mawili:

1. Kupambana nao kimwili:
Kwa kutumia TV niliyopewa, nilikuwa na uwezo wa kuwatambua Wakristo waliookoka. Hatupambani na wanafiki maana hao tayari ni wa kwetu. Tulikuwa tunawatuma wasichana wetu kwanza kwenye Makanisa makubwa. Ndani ya Kanisa wanakuwa wanatafuna bazoka au kusababisha mtoto awe analia au kufanya chochote kitakachoondoa usikivu wa watu kwenye Neno la Mungu. Wanaweza kuamua kuja kiroho na kusababisha watu kusinzia wakati Neno likihubiriwa.  Mara wanapokuona uko makini kwenye mahubiri, watakungoja nje ya Kanisa na mara unapotoka, mmoja wao atakusalimia au hata kukupa zawadi (na mara zote huwa ni kitu ukipendacho) na atakuwa mkarimu sana. Atafanya kila awezalo, na kabla hujajua lolote, utasahau kila ulichojifunza Kanisani. Lakini kwa Mkristo wa kweli, mmoja wa hawa wasichana ataenda kumsalimia na atataka kujua nyumbani kwako kwa kisingizio kwamba yeye ni mgeni hapo mjini na hawajui Wakristo wengi. Ukimpeleka nyumbani, mara moja atanunua ndizi na Mkristo atachukulia hii kuwa ni ishara ya upendo. Ataendelea kumtembelea na hatimaye ataizima nuru ya Kristo kwake kisha anaacha kuja. Harakati kubwa kwenye Makanisa na feloshipu zilizo hai ni: kuwakatisha tamaa Wakristo ya kusoma na kujifunza Neno la Mungu, hivyo kuwafanya wawe wasiofahamu mamlaka waliyonayo pamoja na ahadi za Mungu kwao. Kwenye viwanja vya mikutano ya Injili, wasichana hawa hutumwa kusababisha watu wasikubaliane na wagombane.

Wakristo wanatambulika kwa njia gani?

Wakristo waliookoka hawajulikani kutokana na Biblia wanazobeba mara kwa mara au feloshipu wanazohudhuria. Wanajulikana kwenye ulimwengu wa roho kutokana na nuru inayong’aa mfululizo kama mshumaa wenye nuru kali kwenye moyo au kwa duara la nuru kuzunguka kichwa au ukuta wa moto ukiwa umemzunguka. Wakati Mkristo anapotembea njiani, tunaona malaika wakitembea naye; mmoja kulia, mmoja kushoto na mwingine nyuma. Hii inasababisha tushindwe kabisa kumkaribia.


Namna pekee ya sisi kufanikiwa ni kumfanya atende dhambi, hivyo kutupa mwanya wa kumfikia. Mkristo anapokuwa anaendesha gari na tunataka kumdhuru, kila wakati tunakuta hayuko peke yake kwenye gari. Mara zote huwa kuna malaika pembeni yake. Yaani, kama Mkristo angejua yale yote ambayo Mungu ameweka kwa ajili yake, asingecheza na dhambi au kuishi hovyohovyo!

2. Kutengeneza Wakristo waliorudi nyuma
Nikiwa kama mwenyekiti niliyeteuliwa na Lusifa, nilikuwa nikituma wasichana kwenye Makanisa yaliyo hai na feloshipu zilizo hai. Wasichana hawa wanakuwa wamevaa vizuri na baada ya mahubiri, hutoka mbele na kujifanya wanaokoka na kwamba wamempokea Kristo, kisha wanaombewa. Mwisho wa feloshipu au ibada wanabakia wakizagaa eneo la Kanisa huku wakimngoja mhubiri, ambaye kwa kawaida anakuwa ana furaha juu ya hawa waumini wapya.

Waumini hawa wanaweza hata kumfuata mhubiri nyumbani kwake. Kama mhubiri hana karama ya kupambanua roho, msichana huyo anamwingiza kwenye dhambi ya uzinzi na uasherati. Hii hutokea mara anapomtamani. Msichana atahakikisha kuwa anaendelea na dhambi hii hadi anapozima kabisa Roho wa Mungu ndani ya mhubiri huyo, kisha anamwacha, anakuwa ameshamaliza jukumu lake.

Hapa ningependa kutoa ushuhuda wa Mtumishi mmoja. Kwenye ulimwengu wa giza wa kiroho anajulikana kama mtu wa Mungu. Kila alipopiga magoti kuomba, kwenye ulimwengu wetu kunakuwa na machafuko. Kwa hiyo tulimtumia hawa wasichana. Mtumishi huyu alikuwa hata akiwalisha lakini hakuwa tayari kunaswa. Walifanya kila walichoweza lakini hawakufanikiwa. Matokeo yake, wasichana hawa waliuawa kwa sababu ya kushindwa kwao.

Kwa hiyo, nilijibadili kuwa mwanamke na kwenda kwake; na kwa maneno na vitendo, nilijaribu kumshawishi, lakini alishindikana. Hili lilinikera sana, kwa hiyo niliamua kumuua kimwili kabisa. Siku moja huyu mtumishi alisafiri kwenda mji wenye soko wa Oduekpe. Nilimwangalia na alipokuwa ameinama kupatania bei, nilikamata lori moja lililokuwa limejaza mapipa ya mafuta na kulielekeza pale alikokuwa. Lori hilo liligonga nguzo ya umeme mkubwa na kuanguka katikati ya soko na watu wengi walikufa lakini huyu mtumishi alipona. Jinsi alivyopona, kwa kweli ni muujiza. Siku nyingine nilimwona akisafiri kwenda kwenye mji wa Nkpor kwa mguu. Hapo tena nilielekeza kwake lori lililokuwa linakuja mbele yake likiwa limejaza viazi. Lori hilo lilielekea moja kwa moja kwenye barabara mpya ya kwenda makaburini na kuua watu wengi; lakini huyu Mtumishi alipona tena! Baada ya hapo tulikata tamaa. Bado yuko hai hadi leo!

Kwa sababu ya Mkristo mmoja, ibilisi anaweza kuamua kuua roho nyingi, akidhani kuwa ataweza kumuua na huyo, lakini mara zote huwa anashindwa. Matukio haya yalitokea kwa Wakristo wengi bila ya wao kujua, lakini Mungu wao kila mara aliwaokoa. Tatizo ni kuwa, ibilisi huwa hakati tamaa.  Mawazo yake huwa mara zote: “Naweza kufanikiwa.” Lakini huwa hafanikiwi. Ilmradi tu Mkristo anatembea na pendo la Mungu na anabakia ndani yake na hanaswi na masumbufu ya maisha, ibilisi hawezi kamwe kufanikiwa, hata kama atajitahidi kiasi gani! Ni yule asiyeamini tu ndiye anayeweza kupatwa na ibilisi.  

Ukandamizaji wa Wakristo

Jambo hili hutokea zaidi ndotoni. Mkristo anaweza kuota mambo yafuatayo:
1. Ndugu aliyekufa akija kumtembelea.
2. Makundi ya watu yakimfukuza.
3. Marafiki wakiogelea mtoni.
4. Marafiki wakimletea chakula na kumwambia ale.
5. Mwanamke asiyeolewa au hata aliyeolewa akifanya mapenzi na mwanamume. Hili lisiposhughulikiwa linaweza kusababisha hata utasa. Au mwanamke mwenye mimba anajiona akifanya mapenzi na mwanamume. Hili lisiposhughulikiwa, linaweza kusababisha kuharibika kwa mimba.


Kama Mkristo akiota mambo hayo hapo juu, asiyapuuze; bali anapoamka, ajichunguze na kutubu dhambi yoyote anayoijua mbele za Mungu; ayafunge mapepo hayo yote na kumwomba Mungu arejeshe chochote ambacho kinaweza kuwa kimechezewa au kuharibiwa. Hili ni la muhimu sana. Mtu ni lazima pia aombe msaada na ushauri kwa Mkristo aliyekomaa kiroho na kiimani.

Kuleta roho za watu kwa ibilisi

Yesu Kristo alipokuwa anaondoka hapa duniani, aliwapa agizo wanafunzi wake: “Enendeni ulimwenguni kote mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu.” Wakati Wakristo wengine wanangoja muda unaofaa ili kutii amri hiyo, ibilisi naye amewapa agizo hilo maajenti wake. Tofauti tu ni kwamba, maajenti wa ibilisi wana bidii zaidi kuleta roho kuliko Wakristo!

Mojawapo ya maeneo ambako ibilisi anapata roho za wanadamu ni kwenye shule za sekondari, hasa shule za wasichana. Baadhi ya wasichana hupelekwa kwenye shule za sekondari kama wanafunzi. Tunawapatia nguo za ndani za kisasa na za gharama kubwa. Hili ni jambo la kwanza kabisa, kwa sababu kwenye mabweni ya shule za wasichana wanapenda kutumia nguo za ndani tu. Ajenti wetu huwa hapungukiwi na kitu chochote – vipozodi, nguo, nguo za ndani, vitabu, mahitaji mbalimbali na fedha. Huwa anapewa sabuni maalum ya kuogea ambayo anamwazima mwanafunzi yeyote anayekuja kuomba. Msichana atakayetamani kuwa kama yeye anavutwa awe rafiki yake. Polepole, ajenti wetu atatukutanisha sisi na msichana huyo. Hapo tutamtembelea kimwili kabisa na tutaanza kumletea zawadi na kumpatia mahitaji yake. Kwa njia hii, ataungana nasi kwa kupenda yeye mwenyewe. Hatimaye na yeye ataleta mwingine na kadhalika. Hii inachukuliwa kama wajibu maalum na unafanyika kwa malengo ya kufanikiwa kabisa.

Jambo moja ni lazima lieleweke: shetani huwa hamlazimishi mtu yeyote. Anachofanya ni kukuvutia kwa njia fulani ili uje wewe mwenyewe. Ndiyo maana Biblia inasema: “Mpingeni shetani naye atawakimbia” (Yakobo 4:7). Eneo jingine linaloleta roho kwa ibilisi ni utoaji wa lifti. Tunakuwa tunawatuma wasichana wetu mabarabarani, na mara zote wanakuwa ni wasichana warembo wakiwa wamevaa vizuri. Utawakuta pia mahotelini na kupitia njia hii, tunawapata wanaume na wanawake.  Watu unaoona wanatangazwa magazetini kuwa wamepotea, hupotea kupitia kuwapa lifti wasichana wasiowafahamu. 

Kwa hiyo, ni lazima uwe makini na mtu unayempa lifti kwenye gari yako.

No comments:

Post a Comment