Sura ya 7: Kazi za Maajenti wa Shetani
“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza
kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya
majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” (Eph 6:11-12).
Kitabu hiki
hakitakuwa kimekamilika iwapo hakitaweka wazi mbinu mbalimbali za utendaji kazi
za hizi nguvu za giza. Pia ni muhimu kwamba namna mbalimbali za kujidhihirisha
kwao nazo ziwekwe wazi.
Jambo moja ni dhahiri nalo ni, ibilisi
ama atakufanya uamini kuwa yeye hayupo au kwamba shetani ni mawazo tu mabaya;
au atakufanya uone zaidi nguvu zake kuliko nguvu za Mungu. Wakati Biblia
inasema: “kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya
majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho,” Biblia hiyohiyo pia inasema kuwa
silaha za Mkristo dhidi ya ibilisi na maajenti wake “si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata
kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na
kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii
Kristo” (2 Kor
10:4-5). Vilevile
Maandiko yanasema wazi: “Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu
alidhihirishwa, ili azivunje kazi za ibilisi.”
(1Yoh 3:8)
Na Yesu alizivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa
ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. (Kol 2:15).
Maandiko
yanasema, “Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako.” Kwa hiyo, mwana wa Mungu ni
lazima uwe mwangalifu kukiri Neno la Mungu, ambalo Mungu alishaahidi kuwa
atalitimiza haraka. Kuna ukiri wa aina tatu uliotajwa kwenye Neno la Mungu:
1. kukiri kuwa Kristo Yesu ni Bwana.
2. Kukiri imani katika Neno, katika Kristo na katika Mungu Baba.
3. Kukiri dhambi.
Tunaposikia neno “kukiri,” ni rahisi kuwazia dhambi. Maana ya kukiri kwenye kamusi ni:
1. Kukiri kile tunachoamini.
2. Kushuhudia kile tunachokijua.
3. Kuwa shahidi wa kile tulichokipokea.
Kwa hiyo, inasikitisha kwamba
kila tunapotumia neno ‘kukiri’ mawazo mengine hukimbilia kwenye dhambi. Hapa
mwandishi anamtia moyo mwana wa Mungu kuanza kukiri kile ambacho Mungu amesema.
Wewe ambaye ulikuwa umekufa kutokana na dhambi zako Mungu alikufufua pamoja na
Kristo na kukuketisha juu sana kuliko ufalme uwao wote katika Kristo Yesu. Kwa
hiyo, Wakristo wanatakiwa watambue mahali kule walikoketishwa. Ni lazima wajue
kuwa wanatenda kazi kutokea kule juu sana; juu ya shetani na maajenti wake.
Bwana Yesu amewapa nguvu na mamlaka
yote kama ambavyo amewapa kila kitu kinachohusiana
na uzima na ucha Mungu. (2Petro 1:3). Mungu hakupanga kwamba mazingira
yawatawale watoto wake, bali Neno la Mungu kwenye kinywa cha Mkristo ndilo liyatawale
mazingira na matukio. Mungu ameongea kwenye Yer 23:29 akisema: “Je!
Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande
vipande?”
Wakristo, yaani waliookoka, ni
lazima watambue kuwa, Jina la Yesu linapotamkwa, kinachotoka kwenye vinywa vyao
ni moto. Mkristo anaposimama kwenye mamlaka aliyopewa na Kristo na akatoa amri
kwa Jina la Yesu, moto unabubujika toka kinywani mwake na pepo yeyote
anayetawala matukio na mazingira ni lazima atii! Yesu yuko hai leo ili
kuhakikisha kuwa kila Neno lake linatimia. Napenda pia kusisitiza jambo ambalo
Wakristo wengi hawalizingatii, lakini ambalo shetani analitumia. Pale Petro
alipomwonyesha Yesu mtini ulionyauka kwa kuwa aliulaani, Bwana alisema:
(Kulingana na Mathayo) Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo
la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima
huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba
katika sala mkiamini, mtapokea. (Mat 21:21-22).
(Kulingana na Marko)
“Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione
shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. (Mark
11:22-23).
Bwana
anatuonyesha nguvu ya maneno na pia anamtia moyo Mkristo kusema kitu maalum
wakati akiwa anaomba na katika kutumia mamlaka yake. Baadhi ya Wakristo
huuambia mlima ung’oke lakini hawauambii uende wapi. Yesu alisema kuwa ukiuambia mlima, “Ng'oka ukatupwe baharini …” Hebu tuchukue mfano wa kutoa
mapepo. Baadhi ya Wakristo huyafunga na kuyafukuza mapepo bila ya kuyaambia
yaende wapi. Hii ni hatari. Unapolifunga pepo, linafungika. Kama ukilitoa bila kulipeleka mahali maalum litabakia
hapo karibukaribu. Kama pepo likikemewa tu litoke kwa mtu, linaweza baadaye
kurudi na kumwingia yeyote asiye Mkristo. Kwa hiyo, Wakristo wanatakiwa kuwa
waangalifu wanaposhughulika na mapepo. Hakikisha kuwa pepo limefungwa, limetolewa na
limepelekwa sehemu maalum (na limepigwa marufuku kurudi kumwingia mtu tena).
Baadhi ya
Wakristo wanapoomba husema, “Nakuteka ewe pepo kwa Jina la Yesu.” Kwenye
ulimwengu wa roho, hapo unaliona kabisa pepo likiwa limesimama likisubiri amri
inayofuata. Lakini kama Mkristo akiishia tu hapo, anakuwa hajamsaidia yule
mwenye shida. Usichezecheze na ibilisi. Hauwezi kuchezacheza mbele za adui
yako. Mungu amekutuma kwenye huduma ya kuwafungua watu na ya upatanisho (kuwapatanisha
watu na Mungu). Kwa hiyo, ni lazima uwe mwangalifu kutenda kazi iliyokamilika.
Narudia tena: unapomfunga pepo, anafungwa.
Unapomtoa na kuamuru aende mahali fulani, anatoka na kwenda huko.
Maadamu tu kama huchezi na dhambi bali unaishi ndani ya mapenzi ya Mungu, amri
yoyote utakayotoa kwa ibilisi au maajenti wake kwa Jina la Yesu, ni lazima waitii!
Mungu ameahidi kulitimiza kila Neno lake.
Tunapokuwa sasa
tunaelekea kwenye hatua ya pili, yaani udhihirisho wa shetani na maajenti wake,
napenda uweke aya zifuatazo moyoni mwako:
1. “Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.” (Kol 2:10).
2. “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” (Luk 10:19).
3. “Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako…. Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.” (Isa 54:15, 17).
Makanisani
Sisi ni
mashahidi leo kwamba kuna watu wengi waliopagawa na mapepo makanisani. Wengine
hata hunena kwa lugha au kutoa unabii. Ni wale tu walio na Roho wa Mungu
wanaweza kuwatambua watu hawa. Lakini tuko hapa kuwajadili maajenti wa shetani
walioko makanisani. Hatuko hapa kujadili wanachama wa vyama vya siri vya
kishetani walioko makanisani (ambao baadhi yao hata ni viongozi wa Kanisa) –
hao tunajua wapo. Ninaoongelea ni wale wanaokuja kama maajenti wa shetani:
2. Kutawanya makanisa.
3. Kuwafanya watu wasinzie wakati ibada inaendelea.
4. Kusababisha mambo mbalimbali yanayoondoa usikivu wakati wa ibada.
5. Kuwaleta watu kwa shetani.
Kwa kuwa nilishasema mambo kadhaa
kuhusiana na mambo haya kwenye sura ya tatu, nitawapa tu ushuhuda wa kile
ambacho kilitokea si muda mrefu uliopita. Wakristo wanatakiwa kutii kila Neno
la Bwana Yesu Kristo kwa sababu, wasipotii wanakuwa kwenye hatari ya kuanguka
pale shetani au maajenti wake wanapoweka kikwazo kidogo tu mbele yao. Wakristo
wameitwa watoke gizani ili waje
kwenye nuru ya ajabu ya Mungu mwenyewe.
Wakristo wameitwa ili kujitenga kabisa
na dunia na yale yaliyo ya dunia. Maandiko yanasema, “Tokeni
kati yao, Mkatengwe nao,”
(2 Kor.
6:17).
Alikuwapo
huyu dada mmoja, dada J (sitataja jina lake). Alikuwa ameokoka na akawa
mshirika kamili wa Kanisa moja lililo hai. Baadaye alihamishia ushiriki wake
kwenye dhehebu langu. Alishiriki katika kazi zote za Kanisa na alikuwa na bidii
sana. Lakini tabia yake ilianza kutia mashaka wakati fulani. Kwa hiyo, wachache
wetu tuliamua kwenda kumtembelea nyumbani kwake ili kujua kilichokuwa
kinamsumbua. Wakati tukimhoji, mapepo yalilipuka ndani yake na kuanza kutuambia
kuwa alikuwa ni ajenti wao kwenye Kanisa letu. Mapepo haya yalitolewa ndani
yake na akafanyiwa huduma ya kufunguliwa.
Tulimwuliza,
“Dada, inakuwaje wewe ni mshirika wa Kanisa la kiroho na bado ukawa ajenti wa
shetani?” Alituambia yafuatayo: Haya yalianza siku moja baada ya ibada ya
Jumapili. Dada mmoja (ambaye alidhani alikuwa akimwamini Kristo), alimwendea na
kuomba kuwa karibu naye kwa sababu, alidai kuwa alivutiwa na maisha ya Kikristo
ya dada J. Dada J alikubali kuwa rafiki yake bila kuwa wasiwasi. Wote walienda
nyumbani kwa dada J na huyo aliyeomba urafiki alileta ndizi na karanga, ambazo
wote wawili walizila. Alikaa na dada J kwa muda kisha akaondoka.
Akawa akija
mara kwa mara kumtembelea dada J huku akimletea zawadi mbalimbali. Zawadi hizo
ni pamoja na magauni, viatu, fedha, n.k. Wakati mwingine huyo rafiki wa dada J
alikuwa akija na wasichana wengine wengi. Haya yaliendelea kwa muda na yule
dada alipoona amefanikiwa kuzima nuru ya Kristo ndani ya dada J, alibadili
mbinu na kuanza kumtembelea dada J kiroho. Hapo dada J alipewa nguo nyekundu,
jiwe la kwenye maji, pete kwa ajili ya kidole gumba cha mguu wa kulia na mkufu
wa kuvaa mguuni. Kwa kuwa dada J alishakula sana nao na alishapokea zawadi zao
nyingi sana, hakukuwa na njia ya kukataa. Aliingia agano nao na akaanza
kuhudhuria mikutano yao. Alikuwa sasa anaweza kujigeuza nyoka, popo, n.k. Ndipo
akawa ajenti wao kwa lengo la kuvuna roho kwa ajili yao kutoka Kanisani.
Mungu asifiwe kwa kuwa sasa
ameshafunguliwa! Zawadi zote alizokuwa amepewa ziliharibiwa na sasa ana furaha
tena katka Bwana. Mpendwa msomaji, hii yote ilianza na urafiki usio wa kawaida,
na kwa kuwa dada J hakuwa na karama ya kupambanua roho, na hakuwa macho kama
Bwana anavyotuagiza, yaani “Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, ” (Marko 14:38), dada huyu alipotoka
na kuangukia mikononi kabisa mwa adui; na mbio zake zingeweza kuishia kuzimu
kwa sababu ya uzembe.
Unaweza kuwatambua maajenti wa
shetani kirahisi kutokana na mambo yafuatayo:
- wanavaa pete kwenye moja ya vidole vyao gumba, mkufu
kwenye mguu, pete ya puani, bangili za ajabuajabu, n.k.
- wanaingia Kanisani au kwenye feloshipu na kuwa na bidii sana katika shughuli za kikundi au Kanisa, kwa ajili ya Mkristo mmoja tu ambaye wanamfuatilia. Baadhi huwa na tabia zisizo za kawaida na wengine ni waovu, n.k.
Ndiyo maana
mwana wa Mungu anatakiwa kumwomba Mungu ampe karama ya kupambanua roho, ili
aweze kuwatambua mara anapowaona. Mara wanapogundua kuwa umewajua,
wanahakikisha hauji karibu yao. Sababu ni kuwa mkubwa wao atawaonya kuhusiana
na wewe!
Masokoni
Maajenti hawa
wanatenda kazi kwa njia mbalimbali masokoni. Sokoni ni eneo lao mojawapo
kubwa la kufanyia kazi, kama ambavyo kwenye mahoteli ni eneo wanakosubiria
wanaume. Sokoni, ndiko wanakonasia mawindo yao,
baadhi ya wanawake wajawazito ambao huwasababishia mimba zao
kuharibika ili waweze kupata damu kwa ajili ya akiba zao za damu. Baadhi ya
watu, maajenti hawa huwasindikiza hadi kwenye nyumba zao ili waweze kwenda huko
usiku. Hii hutokea kwa wasio waamini! Baadhi ya vitu vya kuvutia vinavyouzwa
sokoni, kama vile mikufu, rangi za midomo, marashi na vyakula kama dagaa aina
ya “Queen of the Coast” n.k., vina asili za ajabu.
Kuna vitendo
fulanifulani ambavyo Wakristo wanatakiwa kuwa makini navyo, maana unaweza
kumwona mwanamke au mwanamume ambaye atakugusa ghafla tumboni au sehemu yoyote
ya mwili wako, na jambo hilo likasababisha ugonjwa. Kwa hiyo, Mkristo
anatakiwa, akiona hivi, akemee kwa mamlaka ya Jina la Yesu, huku akitawanya na
kuharibu mipango ya ibilisi, n.k. Na hakika yake, kila utakachokitawanya au
kukifunga hapa duniani, kitatendeka vivyo hivyo. (Mat 16:19, Mat 18:18).
Shughuli za kitamaduni
Ni muhimu
pia kutambua kuwa watu wengi huingizwa kwenye shughuli za shetani au kuingiwa
na mapepo kupitia shughuli nyingi za kitamaduni, kama vile sherehe na ngoma. Nyingi
ya tamaduni zetu zina ushetani ndani yake. Wengine hupagawa kupitia
marafiki, na wengine kupitia kusoma baadhi ya maandiko au vitabu vya hadithi. Mapepo
huzungukazunguka karibu na kila sanamu. Hutenda kazi kupitia ibada ya sanamu
(Zakaria 10:2). Kama sehemu muhimu ya dini, ibada ya sanamu ni kuvipa nguvu ya
kiungu vitu vya kawaida na kutoa heshima ya kiungu kwa kiumbe (Rum 1:18-22). Maandiko
yanaita ibada ya sanamu kuwa ni ukahaba wa kiroho (Yeremia 3:8-10). Kwa hiyo,
mwana wa Mungu hatakiwi kuwa na uhusiano wowote, wa moja kwa moja au usio wa
moja kwa moja, na ibada ya sanamu. Kile kinachoitwa maisha ya juu, juju na
muziki wa disko vina uvuvio wa shetani na mapepo.
Nakumbuka,
kabla Bwana hajaniokoa, kwenye mkutano mmojawapo tuliofanya na shetani,
alisema, “Dunia hii ni yangu na naenda kuitawala kwa nguvu zangu, na
nitawaharibu wote wanaomwamini Yule Mwenye Haki.” Shetani huwa hataji Jina la
Yesu. Mtu yeyote akifanya hivyo mbele zake, anakuwa kwenye hatari ya kupoteza
maisha yake. Aliahidi kutufanya sisi tuliokuwa maajenti wake, magavana, n.k.
Shetani ni mwongo na hakika ni baba wa uongo. Kulikuwa pia na mipango ya
kuwanyamazisha Wakristo wa Naijeria kwa kupiga marufuku uingizaji wa Biblia na
maandiko mengine ya Kikristo.
Huwa
anatenda kazi kupitia wasioamini walio kwenye nyadhifa za utawala, kwa kuanzisha
sera na programu zilizo kinyume na Ukristo. Pia anaanzisha vituo vya uponyaji
ambavyo vitaonekana ni vya kiroho kabisa; na kupitia hivyo, ananasa roho za
watu. Hivi kwa kawaida hujulikana kama nyumba za uponyaji wa kiroho na
zimetuzunguka kila upande. Hapa miujiza mingi ya uongo hutendeka ili
kuwadanganya washiriki wake. Shetani anajua sana juu ya kuja mara ya pili kwa Yesu Kristo na
kila wakati huwahimiza maajenti wake kuharakisha na kuwa na bidii katika
operesheni zao. Kila wakati husema, “Hatuna tena muda wa kutosha.” Wapendwa
wana wa Mungu, shetani halali. Kwa nini wewe ulale?
ITAENDELEA ....
ubarikiwe john .....
ReplyDeleteama akika mungu atupiganie nasi twajinyenyekeza mbele zake
ReplyDelete