Yohana
19:1 Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu,
akampiga mijeledi.
Yohana
19:2 Nao askari wakasokota taji ya
miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau.
Yohana
19:3 Wakawa wakimwendea, wakisema,
Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi.
Yohana
19:4 Kisha Pilato akatokea tena nje,
akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia
yo yote kwake.