Ahmed
alikuwa ni injinia. Baadaye alishawishiwa na Ulama mmoja na kupandikiziwa chuki
dhidi ya Wakristo na Wayahudi kiasi kwamba aliamua kuacha kazi yake na kwenda
kusomea masomo ya dini ya Kiislamu (licha ya mama yake kupinga sana).
Masomo hayo
yalimwezesha kuwa hakimu wa mahakama ya sharia. Kutokana na ukandamizaji mkubwa
aliouona kwenye mahakama hizo na kukosekana kwa haki na pia kukosekana kwa msimamo
juu ya tafsiri sahihi ya sheria za kiislamu, moyo wake ulikosa kabisa amani.
Kwa neema
za Yesu Kristo, Ahmed alifunguliwa macho yake na sasa anajiuliza ilikuwaje
akaamini Uislamu?
Ufuatao ni
ushuhuda wake kwa maneno yake mwenyewe ambao ameupa kichwa cha habari: “Njia ya
Allah Kuelekea Jehanamu au Njia ya Yesu Kuelekea Mbinguni.”
*********************
Njia ya Allah Kuelekea Jehanamu au
Njia ya
Yesu Kuelekea Mbinguni
Hadithi ya Kweli
Kila
kitu kilikuwa kinaniendea vizuri wakati mimi (mhandisi wa ujenzi) nilipokuwa
naingia ofisini kwangu kila siku kufanya kazi. Baba yangu alikuwa karani, na
japo mshahara wake hakutosheleza, mama yangu, ambaye alikuwa akitembeza vitu
mtaani, aliweza kupata kipato kilichojazia kwenye upungufu. Kimsingi, alikuwa
ni mama ndiye aliyetulipia watoto wote elimu yetu na matunzo. Nilipopata kazi,
nilimpunguzia mama mzigo mkubwa wa matumizi, lakini baba yangu nilimpa kiasi
kidogo tu kila mwezi.
Dunia
yangu iligeuka ghafla pale nilipokutana na Ulama (mtu mtakatifu wa Kiislamu). Alinieleza
jinsi Waislamu wanavyonyanyaswa na dini zingine na jinsi dunia ilivyosimama
kinyume na Uislamu, huku Marekani ikiwa ndio kinara wa mambo hayo. Aliniambia
kuwa Marekani, kwa makusudi, inalazimisha kuwapo kwa haki za binadamu kila
mahali, maana ziko kinyume na sehemu kubwa ya imani ya Kiislamu, hivyo hilo
linaufanya Uislamu uonekane umepitwa na wakati. Wayahudi nao wanawalaghai
Wamarekani kwa ajili ya maslahi yao ili kuidhibiti Mashariki ya Kati. Allah alishaliona
hili, na kusema kwenye Sura 5.51 ya Quran, kuwa tusiwe na urafiki na Wayahudi
na Wakristo. Lakini nchi za Kiislamu zinaikubalia tu Marekani.
Kukosekana
kwa Maustaadh (walimu wa dini) kwenye eneo langu, kunakowanyima Waislamu welewa
wa kutosha juu ya uzuri na maajabu ya Uislamu, lilikuwa ni jambo jngine
tuliloliongelea kwa kirefu sana. Baada ya mazungumzo ya ushawishi ya miezi
kadhaa, niliulizia kwenye mji mkuu na nikapata taarifa zote kuhusiana na kujiunga
na chuo cha kiislamu. Baada ya kujiuliza sana, ikiwa pamoja na chuki
iliyopandikizwa ndani yangu, niliamua kuacha kazi yangu ya uhandisi, lakini
mama yangu alipinga kabisa. Lakini
mwishowe niliweza kumshawishi kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya Allah, hivyo
nikaenda kujiunga na Chuo cha Kiislamu.
Baada
ya kuhitimu kama Ustaadhi, mara moja nilipangiwa kwenye eneo langu. Hakukuwa na
shule maalum ya Kiislamu, hivyo mwanzoni, niliendesha masomo nyumbani kwangu.
Japokuwa nilikuwa nina welewa wa kutosha juu ya elimu ya Uislamu, lakini
kulikuwa na nyakati ambazo nilikuwa
nakwama kujibu maswali ya wanafunzi. Matokeo yake nilianza kuongezea uongo hapa
na pale kwa nia ya kumtetea Allah. Ukweli ni kwamba, wakati wa masomo yangu ya
Uislamu chuoni, kulikuwa na mambo mengi ya kukisia tu yasiyokuwa na ushahidi.
Pale mikanganyiko ilipoibuka ndani ya Quran, ilimalizwa tu kwa kusema ‘Allah
anajua zaidi,’ au kwa kuchanganyachanganya na baadhi ya Hadith, hivyo kufikia
namna fulani ya jibu linalokubalika.
Waislamu wengi wanajua kusoma Kiarabu
kwenye Quran lakini , kwa ujumla, hawaelewi kile wanachosoma. Kwa hiyo, kwa
ujumla Muislamu huwa hajui kile ambacho Quran inasema, hivyo anahitaji Ustaadhi
wa kumwelezea kile kilichomo. Hivyo, huku kuchanganya maelezo na uongo lilikuwa
ni jambo la kawaida kwa ajili ya Allah. Kusema uongo ikawa ni tabia yangu kiasi
kwamba, hata mimi mwenyewe, nikaanza kuuamini huohuo uongo wangu. Chuki dhidi
ya kitu chochote kisicho Uislamu ilikuwa ni sehemu ya mafunzo niliyopata.
Safari
yangu kwenda Makka kwa ajili ya hija ilikuwa ya kuchosha lakini yenye matukio
mengi. Sikupata fursa adimu ya kuangalia ndani ya Kaabah takatifu na miungu
(idols) mitakatifu iliyomo humo ndani, ambayo mtume Muhammad alisaidia kuiweka
humo, kama ilivyoelezwa na Hadithi za Bukhari. Lakini, nilikuwa najiuliza kwa
nini shughuli ya kumpiga mawe shetani kimfano (kwa kupiga mawe nguzo iliyo
kwenye shimo) ilikuwa ni ya muhimu sana kwenye sehemu hiyo. Nilihisi kuwa
ilitosha tu kuangalia utakatifu na si kuwa na shughuli inayomhusu shetani
kwenye sehemu ile, hususani Makka! Kutokana na joto kali, kila mmoja alikuwa
anatoka sana jasho na ananuka. Lakini mkusanyiko wa watu zaidi ya milioni moja
ulikuwa wa kushangaza na wenye vurugu.
Baada ya kurudi kutoka Makka, nilianza kuvaa kofia nyeupe ili kuonyesha kwamba
nimeshatimiza mojawapo ya nguzo 5 za Uislamu (yaani kwenda kuhiji Makka).
Miezi
miwili baadaye, baba yangu alinitembelea ili kutaka nimuunge mkono juu ya wazo
lake la kutaka kuoa mke mwingine. Ili kuhalalisha suala lake, aliniambia kuwa
tayari alishampa mimba huyo msichana wa miaka 19. Nilighadhibika mno! Lakini
sasa Hadithi katika Bukhari zinaniambia kuwa Allah aliumba wanawake kama ‘vitu
vya kuchezea’ kwa ajili ya wanaume. Hata hivyo, nilipomtafakari mama yangu
alivyohangaika kutulisha na kutusomesha, nilimhurumia sana. Bila yeye, baba
yetu asingeweza kutulisha, kutusomesha,
na kutuvika sisi watoto wake. Kutokana na usaidizi wa mama yangu, baba
aliweza hata kufurahia maisha, na baada ya kumtumia kwa miaka hiyo yote,
alikuwa sasa anataka mke mwingine dogodogo, akiwa na umri ulio chini ya nusu ya
umri wake, na mdogo kuliko watoto wake wote watano!
Lakin
Allah ni wa rehema na amewapa wanaume upendeleo kuliko wanawake, maana
mwanamume anaweza kuwa na wake hadi wanne kwa mara moja. Pamoja na kuwa
nilitafuta kila sababu ya kutomwunga mkono baba yangu, nilizungumza na mama
yangu juu ya jambo hilo. Alilia sana; na hata kazini hakwenda siku hiyo.
Tulijadili kwa kirefu suala la mke wa pili. Aliposema kuwa hatakubaliana na
kuwapo mke wa pili, nilimwambia kuwa hakuwa na namna, maana baba angeweza
kumtaliki bila ridhaa yake na bado akamwoa mwanamke huyu. Na hiyo ina maana
kuwa, mama angetakiwa kuondoka na kuwaacha wanawe, kwa kuwa katika Uislamu
watoto ni wa baba na si wa mama. Jambo hili lilimwumiza hata zaidi.
Wakati baba yangu alipomleta mkewe mpya nyumbani, mama yangu alitumia muda
wake mwingi nje ya nyumbani, lakini huku akileta fedha kidogo tu. Hali hii
ilimfanya baba yangu awe na mzigo mkubwa zaidi, maana hakuwa na fedha za
kutosha kwa ajili yake mwenyewe; na kila wakati mama alipokuwa nyumbani, hali inakuwa ni kama uwanja wa vita. Sisi watoto
tulilikuwa tukibakia tu na mama yangu, na kumwacha huyu mwanafamilia mpya peke
yake hadi pale baba anaporudi nyumbani kutoka kazini.
Wakati huu, nilipandishwa cheo, na kulikuwa na wakati ambapo nilikaa kama
hakimu wa mahakama za sharia (Mahakama ya Kiislamu). Uzoefu niliopata kutokana na
mkasa wa mama yangu mwenyewe, ulikuwa kila wakati umo moyoni mwangu, na
sikuweza kukubaliana kabisa na amri za Allah na kupuuza upendo, huduma na
umuhimu ambao mama yangu alitupatia sisi sote. Hali hii ilikuwa na athari
kwenye utoaji wangu wa hukumu kwa baadhi ya kesi katika mahakama za sharia.
Nimeshuhudia kiburi na majivuno ya wanaume dhidi ya wake zao wa kiislamu, na
wengi wa wanawake hawa, kama ilivyokuwa kwa
mama yangu, walichangia sana kwa ajili ya watoto wao na nyumba zao, na waliletwa
kwangu huku mara nyingi wakiwa wamepigwa sana, yote haya yakiwa yameruhusiwa
kwenye Uislamu na Allah.
Kwa mara ya kwanza, nilidhani kuwa haya yalikuwa mambo tu ya kipekee na nikawaza
kuwa Allah hawezi kukosea katika amri zake. Lakini kadiri nilivyoendelea kuona wanawake
zaidi na zaidi (mara nyingi wakiwa na umri wa miaka 35 na zaidi; na mmoja
alifika mahakamani akiwa amefungwa POP kwenye mkono wake mzima wa kushoto na
mguu wa kushoto, huku akiwa kwenye kiti cha magurudumu), mimi nilianza kuwa na
mashaka, na nilianza kusoma sana vitabu vya Kiislamu kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi
bora na wenye utu kuhusiana na jinsi wanawake wa Kiislamu wanavyotendewa na
waume zao, na tabia ya wanaume wa Kiislamu kutoa talaka kirahirahisi, n.k,
lakini bila mafanikio yoyote. (Ndoa katika
Uislamu si sakramenti mbele za Mungu, lakini ni mkataba tu wa kawaida – mara
nyingi ukifanyika kwa mdomo tu - kati ya muoaji na baba wa mwanamke au mzee wa
karibu; na mkataba huu unaweza kuvunjwa wakati wowote anapoamua mume, bila
ridhaa ya mke wake. Hali hii mara ilinifanya nikasirike sana, maana katika
ujana wake, mwanamke anakuwa ametumiwa kama mke wa upendo, kisha anakuja
kutelekezwa tu baadaye, kama karatasi ya chooni). Lakini, sikuweza kupata suluhisho
lolote lenye utu dhidi ya unyanyasaji huu na suala lililozagaa la talaka katika
Uislamu. Hili lilinizidishia tu hali ngumu.
Siku moja niliitwa kwenye ofisi ya mufti. Niliambiwa niunde kamati ya kujaribu kusanifisha (to standardize) hukumu za mfumo wa mahakama wa Kiislamu unaotumika katika mahakama za Sharia. Unajua, kwa sababu Qur'ani, Hadith, na Sunah hazisemi kwa hakika nini cha kufanya (kwa mfano, Allah anasema katika Sura 4.34, kwamba 'mke mkaidi ni lazima apigwe na mume wake na kutengwa hadi ajirekebishe. Lakini haisemi kwamba apigwe mara ngapi, sehemu gani ya mwili wake, apigwe lini, kama ni mjamzito au la, kwa lazima au la, kwa mikono au mjeledi, kwa sababu zipi, nk. Suala hilo limeachwa mikononi mwa mume kuamua. Mara nyingi walikuja kwetu wanawake na kutuonyesha alama za vipigo kwenye miili yao, lakini hakukuwa na kitu katika Uislamu cha kukomesha hali hii, isipokuwa pale ambapo mwanamke alivunjwa mifupa, ambapo nako tulimshauri tu mume, kama ilibidi).
Kama mashahidi 4 walitoa ushahidi wa wizi wa mwanamume na mkono wake wa
kulia ukakatwa kama adhabu, na wakati mwingine baadaye, ikiwa mmoja wa
mashahidi alikiri kutoa ushahidi wa uongo chini ya shinikizo (maana kushuhudia
uongo ni jambo la kawaida katika mahakama za sharia), matokeo yake nini basi?
Kulikuwa vurugu nyingi kutokana na kwamba mahakimu tofauti wanatafsiri Uislamu
kwa namna mbalimbali. (Uislamu hauko wazi kupokea mawazo ya sasa, kama kutumia
DNA, au mifumo ya uhasibu, au uhalifu wa kwenye mtandao, n.k. lakini umeng’ang’ania
mifumo yenye umri wa miaka 1,100 toka kwa mababu, na kutaka itumike kwenye
maisha ya leo).
Watuhumiwa katika mahakama zetu walianza kuchagua kuwapo wakati kukiwa na baadhi
ya majaji na kutokuwapo kukiwa na majaji wengine. Hivyo, unaweza kuwa na msururu
mrefu kwa ajili ya majaji wachache lakini hakuna kesi kwa majaji wengine.
Wanasheria hawakuhitajika katika Uislamu, lakini huwa tunapata mashahidi wa
uongo wengi wanaokuja na kuwatuhumu kwa mambo mbalimbali watu ambao wana
uhasama nao. Nilipoanza kazi yangu kwa kusanifisha hukumu, nilianza kupata
matatizo mbalimbali, hoja mbalimbali, n.k. kutoka kila upande na nikaishia tu
kuchukiwa na wengi. Hakukuwa na mahakimu wawili ambao walikuwa wanatafsiri kwa
namna ileile Qur'ani na adhabu zinazotakiwa kutolewa. Hawakuweza hata
kukubaliana juu ya mtazamo mpana wa tafsiri na adhabu (kwa mfano, muda wa chini
au wa juu wa kifungo cha mtu gerezani, nk). Malalamiko makuu kutoka kwa majaji hao
yalikuwa ni kusema, ‘hili halimo ndani ya Quran.’
Mwishowe, mpango ule mzima uliondolewa, na Haki za Kiislamu ziliruhusiwa kutolewa
kulingana na tafsiri na welewa wa kila hakimu kuhusu Uislamu; na machafuko yanaendelea
hadi leo hii. Mimi nilivunjwa sana moyo kusema kweli. Kusema kweli, kwa kila
kushindwa kwa Waislamu, kuna angalau ‘conspiracy’ moja ya Wakristo/Wayahudi
inayowalaumu Waislamu.
Waislamu hawatakaa wakubali kwamba mfumo wao wa utoaji haki wenye umri wa
miaka 1,100 umepitwa na wakati. Ni rahisi kwao kulaumu nchi za Magharibi na
kusema, 'Hawauelewi Uislamu', kuliko kujaribu kuhalalisha Uislamu, kwa sababu Waislamu
wanajua kwenye akili zao kuwa, mfumo huo utaonekana kuwa wa kikatili (barbaric)
na uliopitwa na wakati, na pia kwa sababu Qur'ani yenyewe inapingana na aya
zake zinaweza kutafsirika kwa namna nyingi (open ended), na pia kutojua maana halisi ya aya katika
Qur'ani. Kwa hiyo, ni rahisi kulaumu nchi za Magharibi kuwa 'hazina welewa' na
kuwaacha wakishangaa, wakati ukweli ni kuwa nchi za Magharibi ziko sahihi
kabisa kuhusiana na mawazo yao juu ya Uislamu.
Kwa vile Qur'ani ina kupingana kwingi pamoja na mambo ambayo yamepitwa na
wakati, Mwislamu kamwe hawezi kujadiliana na asiye Mwislamu, kwa sababu yule
asiye Mwislamu anaweza kutumia Quran dhidi yake. Kwa hiyo, inakuwa ni bora tu
kusema, 'Wewe haujui uzuri wa Uislamu’ ili kukwepa aibu. Huu ndio mtazamo wa Mwislamu
wa kawaida. Kwa ujumla, Mwislamu hawezi kustahimili mzaha. Huu ndio ukweli
wenyewe. Ukiendelea kubishana naye inakuwa ni afadhali kwake). (Nenda kwa
tovuti www.answering-islam.org na uone mwenyewe orodha ndefu ya utata ulio ndani
ya Quran).
Siku moja, mimi nilimkuta mama yangu akimeza vidonge na nikaja kugundua kuwa vilikuwa vya kuondoa maumivu. Nilimpeleka hospitali kufanyiwa vipimo na akakutwa ana kansa. Ni lazima alikuwa nayo kwa muda mrefu, maana ilishaenea kote mwilini. Aliteseka kila siku. Miaka miwili baadaye, alifariki. Sisi ndugu tuliumia sana. Ulimwengu wangu ulibomoka kabisa kutokana na tukio hili. Nilijaribu kujisahaulisha kwa kufanya kazi, lakini nikawa nachanganyikiwa zaidi na zaidi kutokana na kukosa majibu sahihi.
Kwa mfano, ubakaji ulihitaji mashahidi 4 ili kumtia hatiani mbakaji, kitu
ambacho kimsingi hakiwezekani. Kwa hiyo, mara zote nililazimika kuwaachia huru
wabakaji. Na wakati mwingine, mbakaji huyohuyo aliletwa tena mahakamani baada
ya kumbaka msichana mwingine, na bila mashahidi 4, sikuwa na cha kufanya zaidi
ya kumwacha huru tena. Maisha ya wasichana wasio na hatia yanaharibiwa kwa jina la Uislamu. Japokuwa
nilijua fika kwamba huyu ni mbakaji, lakini bado Uislamu haukuruhusu mimi kuona
haki ikitendeka. Mbaya zaidi, ikiwa mahakama ya Kiislamu haikulichukulia hilo
kuwa ni tukio la ubakaji, basi msichana aliyebakwa anahukumiwa kupigwa mawe
hadi kufa kwa ajili ya kupata mimba nje ya ndoa.
Yule bibi wa Kikristo jirani yangu, aliyeishi nyumba chache tu kutoka kwangu, aligundulika kuwa ana kansa. Familia yake ya Kikristo iliomba kwa Isa Al-Masih (Yesu Kristo) kila usiku ili aweze kupona haraka kule hospitalini. Niliwaza kuwa walikuwa wanapoteza tu muda, kwa sababu bila ya huruma za Allah, ni lazima tu bibi angekufa. Lakini wiki tatu baadaye, nilishtuka nilipomwona mwanamke huyo akishughulikia maua yake mbele ya nyumba ya mtoto wake.
Nilipiga moyo konde na kwenda kuongea naye. Aliniambia kuwa, kwa neema ya
Yesu Kristo aliye Bwana, maombi yake yalijibiwa, na sasa yeye alikuwa amepona kikamilifu. Mwanawe alitoka nje na
kunikaribisha ndani kwa ajili ya kunywa chai. Baada ya kuzungumza kwa kirefu,
nilirudi nyumbani kwangu nikiwa nimechanganyikiwa huku nikijiuliza, kwa nini Allah
hakumwangalia mama yangu, ambaye alikuwa Mwislamu nzuri, mwenye umri mdogo, na
asiye na dhambi, lakinibadala yake huyu bibi mzee, ambaye ana imani kubwa kwa
huyu Isa Al- Masih (Yesu Kristo) aliponywa kabisa? Niliwaza, huenda hii ikawa ni kazi ya shetani.
Siku ya pili, mawazo juu ya huyu bibi hayakunitoka kabisa. Niliamua kuwa ni
lazima nipate jibu juu ya suala hili. Baada ya kutoka kazini, nilienda tena
kwenye nyumba hii ya Wakristo kwa lengo la kuonyesha kuwa hii nadharia ya huyu Yesu
Kristo si ya kweli na pia kwenda kuwaomba wanipatie Injili yao (Agano Jipya).
Mwanzoni, walikuwa wanasitasita, maana nchi yangu ni nchi ya Kiislamu, na
kuhubiri Ukristo kwa Mwislamu kutasababisha kupata kila aina ya adhabu.
Baadaye, mtoto wa kiume katika familia hii ya Kikristo aliniashiria kwa macho Biblia
yake iliyokuwa juu. Niliichukua (Hii ilimaanisha kuwa hakunipa yeye, bali niliichukua
kwa ridhaa yangu kutoka kwenye nyumba hiyo. Hivyo, asingetuhumiwa kwa kunipa vitu
vyenye kufuru).
Usiku ule nilisoma Injili ya Mathayo na kupitia sehemu zingine mbalimbali
za Biblia. Nilishangaa kwa jinsi Biblia ilivyokuwa imeandikwa kwa mpangilio
mzuri, na ilikuwa rahisi kufuatilia mambo yaliyoandikwa humo. Lakini ninahitajika
welewa zaidi juu ya mambo yaliyomo humo na umuhimu wake. Kwa hiyo, nilianza
kwenda mara kwa mara kwenye nyumba hii ya Wakristo, lakini nyakati za usiku, ili
majirani wasije wakanishuku. Kutokana na kujua nafasi yangu katika jamii, wenyeji
wangu walikuwa na wasiwasi wa kitendo changu kuwaingiza kwenye matatizo. Siku
zikawa wiki, na nilikuwa nikiwahi nyumbani kila siku ili kwenda kusoma zaidi Biblia.
Nilipenda sehemu ambapo Yesu Kristo anasema, yeyote asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga
jiwe mwanamke aliyekamatwa kwenye uzinzi. Kuna upendo mwingi sana kwa ajili ya
kila mmoja katika Injili (Agano Jipya). Mahangaiko yote na msongo uliokuwa
ndani yangu ulianza kupungua, kadiri nilivyoendelea kujisikia amani na utulivu
kwa huyu Yesu Kristo. Lakini chuki yangu dhidi ya dini zote nyingine ilikuwa
bado imo ndani yangu.
Mimi daima nimekuwa nikijiuliza, kwa nini ni wanawake wa kiislamu tu ndio huona vivuli ya mizuka na kupagawa ama kwa pamoja au mmoja mmoja katika madarasa, viwanda, nk iwe ni usiku au mchana? Hili si tu ni jambo la kawaida katika nchi yangu, lakini katika nchi nyingine pia. Mwislamu hatakiwi kupiga au kuweka picha ya kitu chochote hai (ikiwa ni pamoja na wanadamu), na jambo hili kwangu nililiona halina maana, kwani ningependa kuweka picha za familia yangu kwa ajili ya uzao wangu. Dome of the Rock katika Yerusalemu ilijengwa takriban miaka 60 (685-691 BK) baada ya Mtume Muhammad kufa (Juni 8, 632 BK kule Makka). Hakukuwa na kitu cha maana kuhusiana na Uislamu katika Palestina wakati wa kifo chake. Basi kwa nini mwili wa Mtume Muhammad kwenda Yerusalemu kupaa hadi Mbinguni, wakati ingefaa zaidi apae kutokea Kaabah kule Makka, ambako ndiko mahali patakatifu zaidi katika Uislamu? Mashaka haya makubwa daima yalinisumbua, na hakukuwa na majibu, hata kutoka kwa wenzangu wakubwa na na wenye hekima zaidi.
*******************
Tafadhali endelea kusoma sehemu ya pili kwa kubofya HAPA.
No comments:
Post a Comment