Tuesday, June 24, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 10




Sura ya 8: Silaha za Mwamini


- Jina la Yesu
- Damu ya Yesu
- Neno la Mungu
- Sifa za Mkristo


Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.” (Efe 6:10-11). 

“Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.” (Ufu 12:11).

Sunday, June 22, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 9




Sura ya 7: Kazi za Maajenti wa Shetani

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” (Eph 6:11-12). 

Kitabu hiki hakitakuwa kimekamilika iwapo hakitaweka wazi mbinu mbalimbali za utendaji kazi za hizi nguvu za giza. Pia ni muhimu kwamba namna mbalimbali za kujidhihirisha kwao nazo ziwekwe wazi.

Tuesday, June 17, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 8




Sura ya 6: Majaribu na Ushindi

Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.” (Yohana 10:27-28) 

Baada ya kumpokea Kristo, jambo la kwanza lililotokea lilikuwa ni kutoweka kwa zawadi zote ambazo nilipewa kule baharini, yaani teleskopu, TV, mashati, picha nilizopiga kwenye maabara za ndani ya bahari na picha za malkia wa pwani ambazo zilikuwa nyumbani kwangu.

Saturday, June 7, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 7



Sura ya 5: Kukutana kwangu na Yesu Kristo

Mwezi wa February 1985, tulikuwa na mkutano wetu wa kawaida baharini. Baada ya hapo niliamua kusafiri hadi Port Harcourt kwenye Jimbo la Rivers, kumtembelea mke wa marehemu mjomba wangu. Nilikutana na mtu aliyeitwa Anthony. Alikuwa na karakana yake kule Nwaja Junction, kwenye barabara ya Trans-Amadi, Port Harcourt, Jimbo la Rivers. Alituma ujumbe niende kwake na kwa kuwa kwenye kundi letu tuna sheria kwamba usikatae wito, niliamua kwenda. Nilienda kwake mchana siku ya Alhamisi. Alianza kwa kusema, “Mungu amenipa ujumbe kwa ajili yako.” Alitoa Biblia yake na kuanza kuhubiri. Kulikuwa na Wakristo wengine watatu wamekaa (mwanamume na wanawake wawili). Aliendelea na mahubiri yake kwa muda mrefu na sina uhakika kama niliyasikia yote. Hatimaye aliniambia nipige magoti kwa ajili ya kuombewa. Nilitii na nikapiga magoti kimyakimya.

Monday, June 2, 2014

Niliokolewa Toka Kwenye Nguvu za Giza - Sehemu ya 6



Sura ya 4: Jinsi shetani anavyopambana na Wakristo


“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” (Efe 6:12) 

Kupambana na Wakristo
Baada ya amri kutoka kwa Lusifa ya kupambana na Wakristo, tulikaa na kupanga njia zetu za kupambana nao kama ifuatavyo: