Katika Sehemu ya 1 na ya 2 tuliona jinsi
ambavyo Jim McCoy aliingizwa kwenye vifungo vya kipepo na mwanamke mchawi
(lakini kwa ridhaa ya McCoy mwenyewe); lakini akajikuta kwenye mateso mengi.
Hatimaye Bwana Yesu alimhurumia na kumtoa kwenye vifungo hivyo.
Katika sehemu hii, McCoy anaendelea
kueleza mbinu na hila zinazotumika leo duniani; ambazo shetani na maajenti wake
wanafanya juhudi za kuzieneza kote duniani ili, sit u watu wanaomkataa Yesu,
bali hata Wakristo waweze kunaswa katika mtego na kuishia jehanamu.