Sunday, December 15, 2013

Asili hasa ya Uislamu ni nini?




Je, wewe ni Mkristo? Je, wewe ni Mwislamu? Sote tuko kwenye safari ya kuelekea mbinguni huku tukiamini kuwa njia ile tuliyomo ndiyo sahihi; na njia ile waliyomo walio kinyume nasi haiko sahihi.

Ukristo na Uislamu ni dini kubwa ambazo zinadai kuwa zinaabudu Mungu mmoja aliyeumba mbingu na nchi tofauti na dini zingine ambazo zinaabudu miungu mingi. Hata hivyo, zipo tofauti za msingi sana kati ya Uislamu na Ukristo ambazo KATU haziwezi kufanya pande hizi mbili ziwe zote sahihi. Kwa mfano:

Friday, December 13, 2013

Saa 8 mbinguni - Sehemu ya 2




Mchungaji Ricardo Cid


Ndugu msomaji wa blog hii, katika sehemu ya kwanza ya ushuhuda huu tuliona jinsi ambavyo Ricardo amechukuliwa na malaika wa Bwana kupelekwa mbinguni kukutana na Bwana Yesu. Walikuwa wamepita mbingu ya kwanza na wako kwenye mbingu ya pili. Wakati akiwa anaangalia shughuli mbalimbali za mapepo kwenye mbingu hiyo, kwa mbali aliona nyota yenye mwanga mkali ikiwajia pale. Je, hiyo ilikuwa ni nyota ya namna gani? Na je, nini kiliendelea baada ya hapo? Tafadhali karibu kwenye sehemu ya 2 na ya mwisho ya ushuhuda huu wenye ujumbe muhimu kwa Kanisa.

Wednesday, December 11, 2013

Saa 8 mbinguni - Sehemu ya 1





Mchungaji Ricardo Cid



Mchungaji Ricardo alipata mafunuo mbalimbali kutoka kwa Bwana Yesu kuhusiana na hali ya kanisa, haja ya kuwa waombaji wenye bidii, haja ya kujiandaa kwa ujio wa Bwana, unyakuo na kadhalika. Karibu kwenye Sehemu ya 1 ya ushuhuda huu wenye nguvu ambao, kupitia humu, Bwana atasema na moyo wako na kukupatia msukumo mwingine wa kusonga mbele zaidi katika safari hii ya kiroho katika maisha haya ya kimwili.

Wednesday, December 4, 2013

Jiandae kwa kurudi kwa Bwana! Sehemu ya 2




Mpendwa msomaji wa blog hii na mwana wa Mungu aliye hai, hii ni Sehemu ya 2 ya ushuhuda huu. Katika Sehemu ya 1, tuliona safari ya kwanza mbinguni ya dada Bernarda. Katika sehemu hii, anatueleza kile kilichotokea pale Bwana Yesu alipomchukua kwa mara ya pili na kwenda naye mbinguni kisha akamrudisha.