Tuesday, April 3, 2018

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 13


 Related image
==== SIKU YA 22 ==== (1 Petro 1:6-9) * Pepo linapiga kinanda
Lee Yoo Kyung
Nilipokuwa nikiomba, pepo lenye uso mweusi na macho manne lilikuja na kukaa kwenye kiti cha mpiga kinanda. Likaanza kuhangaika pale huku likijaribu kupiga kinanda. Huku nikiwa nimekereka, nilipaza sauti na kusema, “Ewe pepo mchafu! Kwa nini unachezea kinanda cha dada yangu Joo Eun? Kinanda hicho huwa anakitumia wakati wa ibada za kuabudu.” Likanitukana na kuniambia nifumbe kinywa changu. Kwa hiyo nikajawa na hasira. “Nini? Unanionyesha dharau? Wewe umekufa!” Nikalikimbilia na kulikamata. Nikanyonga shingo yake na kupigiza kichwa chake chini sakafuni.


Mapepo matatu zaidi yakatokea. Moja lilikuwa kwa umbo la mifupa tu na lilikuwa na jicho usoni. Lilikuwa likiruka huku na kule kwa mbawa zake kama popo. Nalo likaenda kukaa kwenye kiti cha kinanda na kuanza kuimba huku likipiga kinanda. Sauti yake ilikuwa mbaya na muziki wake wala haufuati mapigo ya kimuziki.
 “Wewe, hicho ni kinanda cha Joo Eun. Kwa nini unakigusa? Unasababisha siwezi kuzingatia maombi yangu!” nilisema kwa sauti. Nikawa nayasikia yakiongeleshana, “Hawezi kuwa mzingativu. Tuendelee kupiga kinanda zaidi na zaidi.” Yote yakaanza kubonyeza kinanda kwa fujo kwa pamoja. Nilihofia kinanda kingeweza kuvunjika. Nikayaambia, “Ni wazi nyie hamuwezi kunisikiliza.” Nikayakimbilia na kuyakamata yote kwa mara moja, huku nikiyapiga mateke na kuyazungusha. Huku pua zao zikiwa zinatoka damu na vichwa vyao vimeumia, yalipiga kelele na kukimbia.

Nikaanza kuomba tena. Likaja pepo lililovaa vazi jeupe huku mdomo wake unatoka damu. Lilionekana lina ulemavu huku halina macho, kwa hiyo nikalidhihaki. Likasema, “Haak Sung aling’oa macho yangu. Ndio maana niko hivi. Kwa nini nyie wawili mnacheka?” Lilikuwa linajaribu kuzua ugomvi na mimi. Kwa sauti, nikasema, “Bibi yangu anateseka kwa sababu yenu! Kwa nini alitupwa Kuzimu?” Pepo lile likanidhihaki na kunikera. “Kuzimu ndio mahali pake. Anastahili kuwa pale. Atateswa hata zaidi.” Kwa hasira, nikaliparua usoni kwa nguvu zangu zote. Likaanza kuvuja damu nyingi sana na likakimbia.

Nikaanza kuomba tena, kisha nikaanza kusumbuliwa na pepo jingine. Niliudhika lakini sikutaka kwenda kulikabili. Nikaamua kutumia mamlaka yangu kwa kusema, “Damu ya Yesu.” Lakini lenyewe likajibu, “Damu? Damu ya nani? Damu ya Yesu? Ahaa, damu yako?” “Sawa, kama unatafuta ugomvi, sogea. Njoo tupigane!” nikasema kwa sauti. Mapepo yakashambulia kwa makundi, lakini kwa namna fulani, kila nilipotupa mkono wangu, yote yanaanguka kama kundi. Nikiyapiga tumboni, macho yao yanapasuka. Nikipiyaga puani, pua zao zinaanza kutoka damu. Nikakamata miguu yao na kuanza kuyazungusha juu. Miguu hiyo ilikuwa inavutika kama mpira.

Licha ya kuyatia hasara, yaliendelea kuja na kunighasi. Yalikuwa yanajaribu kunizuia kuomba. Nikawaza, “Acha tupambane tuone nani atashinda.” Nilitia vidole puani mwao na kukamata nywele za pepo lolote lililonisogelea karibu. Nilitumia mikono na miguu yangu kama silaha. Ilishangaza kwamba kila nilivyoendelea kuyashinda, idadi yao ikawa inaongezeka. Karibu na mwisho, kukawa na mapepo mengi, mengi sana yasiyohesabika! Yote yalikuja kwa pamoja. Kwa uharaka, nikapaza sauti “Nisaidie! Harakisha, Roho Mtakatifu! Nisaidie!” Kufumba na kufumbua, Bwana akatokea. Bwana akayakemea mapepo yale na akanifariji, kwa kusema, “Bi Madoa (Miss Speckle)! Najua umekutana na mtihani mkubwa.”

Mwanzoni nilipokuwa nahudhuria kwenye makanisa mengine, watu wengi waliniambia mara nyingi kuwa mimi sikuwa na akili za kutosha. Badala ya kunifundisha namna ya kuomba na kufanya uinjilisti, walinipa tu chakula. Walijaribu tu kunisaidia kwa mahitaji ya kimwili. Kwa hiyo, nilidhani kuwa mimi nilikuwa mtu wa kubeba tu Biblia na kwenda kwenye ibada. Lakini kwa mwongozo wa mchungaji wa kwenye Kanisa la Bwana (Lord’s church), nilianza kunena kwa lugha. Kadiri nilivyoendelea kunena kwa lugha, niliweza kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuomba.  Sasa naweza kuyaona mapepo na ninaweza kupambana nayo. Kila ninapojisikia kama nashindwa kwenye mapambano, ninachofanya tu ni kuliitia Jina la Bwana Yesu. Yeye hunilinda kila wakati. Mwanzoni, nilikuwa naogopeshwa sana na mashambulizi ya mapepo mengi. Lakini hivi sasa siogopi tena, maana Yesu yuko pamoja nami.  Kwanza ushindi ninaopata dhidi ya mapepo umekuwa ni jambo la kuburudisha na kufurahisha.


Kim Joo Eun: * Mapepo yenye vipara yatokea
Leo, pepo jingine lililojifanya kama msichana lilitokea huku limeachama mdomo. Nilimwaga hasira yangu kwake, nikalizaba kibao kwa nguvu sana hadi likavimba kwenye shavu. Nikasema kwa sauti, “Ulimpiga kibao dada Yoo Kyung shavuni, sawa? Utaadhibiwa hata zaidi. Nitakupiga zaidi!” Likalia, “Nisamehe. Sitampiga Yoo Kyung tena. Kweli kabisa!” Nikasema, “Ndio. Wewe ni mwongo kwa asili yako.” Nikang’oa nywele zake zote na kulitupa chini ya kinanda. Kisha nikaona pepo lenye fuvu lenye nywele ndefu nyeupe na macho ya rangi ya machungwa. Nikayachoma macho yake na likaanza kurukaruka kwa mahangaiko kutokana na maumivu makali hadi likakimbia.

* Makanisa Yashindayo
Kadiri nilivyoendelea kuomba, nilihisi kuna harufu nzuri kama ya maua hewani. Bwana akatokea. Kwa hiyo nikamwuliza, “Bwana, hii harufu nzuri hivi inatoka kwako?” Bwana akajibu, “Ndiyo, Madoa. Umeipenda harufu hiyo?” Kwa furaha nikajibu, “Ndiyo Bwana. Ni nzuri sana.” Yesu akaniambia, “Leo unaomba kwa bidii kweli. Nitakuonyesha kitu maalum. Angalia kwa makini hali ya kanisa lako na makanisa ya Korea.” Mara Bwana alipoinua mkono wake, nikapewa maono. Nikaonyeshwa dunia kwa mbali huku kukiwa na mapepo mawili upande huu na huu. Yalikuwa yanazungusha kamba kuzunguka dunia yote kama kwenye mchezo wa rede. Nilipotazama kwa makini, nikaona kwamba ile kamba ilikuwa ni joka refu. Kadiri yalivyozungusha ile kamba, nikaona makanisa mengi ya Korea yakiruka kila kamba ilipoyafikia. Yaliruka na kuruka, huku yakijaribu kujizuia kuanguka. Mengi ya makanisa hayakuanguka mwanzoni, lakini mizunguko ilivyoendelea, yalijikwaa na kuanguka. Nikaona hata kanisa letu likiruka. Sisi hatukujikwaa au kuangushwa na lile joka.

Yesu akasema kuwa kila mzunguko kutoka kwenye yale mapepo ni jaribu linalotakiwa tulishinde. Kama kanisa halikujikwaa na kuanguka, ina maana limeshinda jaribu husika. Kanisa la Bwana (The Lord’s church) lilikuwa na idadi ndogo ya washirika kuliko yote. Makanisa mengine yalikuwa na watu wengi zaidi, lakini mara kwa mara yalijikwaa na kuanguka. Yesu akasema, “Kanisa la Bwana linashinda kwa nguvu sana. Endeleeni kustahimili na kuruka kadiri majaribu mbalimbali yanavyokuja kwenu. Leo, umeomba kwa muda mrefu sana bila kusinzia. Ndio maana nimekuonyesha haya. Omba kwa bidii.”

Lee Haak Sung: * Mapepo yanayofanana na picha za kwenye mambo ya burudani
Nilipokuwa naendelea kuomba, pepo moja likanijia. Nilikuwa na hasira sana wakati huo baada ya kumwona bibi yangu Kuzimu kiasi kwamba nilizimwaga hasira zangu zote kwa pepo hilo. Niliyachoma macho yake na kuyanyofoa kisha nikayatupia kule. Wakati wa mapambano haya, nilianza kuwaza kuhusu upanga, na mara upanga ukatokea mkononi mwangu. Nikafyeka mikono yake. Kila nilipowaza tu kutumia silaha nyingine, mara ilitokea ama mkononi mwangu au pembeni yangu. Bwana alinipatia silaha hizi kila nilipoziomba. Nilikuwa nimeshapigana kwa muda mrefu na kuwa na uzoefu mkubwa bila mimi kujua. Pia nilikuwa nimeshajaa ujasiri na kujiamini.

Pepo lililojifanya kama binti aliyevaa gauni jeupe likanijia. Lilionekana limefanana sana na picha (katuni) za kwenye sinema za kutisha. Nilishangaa sana kuona jinsi lilivyofanana na mojawapo wa wahusika waliobuniwa kwenye tasnia ya burudani! Hili lilikuwa linafanana kabisa na mojawapo wa wahusika kwa kwenye filamu moja maarufu ya TV ya Korea ambaye kazi yake ni kuzikokota roho za watu hadi Kuzimu baada ya kufa. Kwenye maono yale, nikaona mzee mmoja akiwa amelala sakafuni huku akivuja damu chini ya madhabahu. Huku likimshambulia mzee yule, pepo lile lilitumia meno yake ya ki-drakula kufyonza damu yake. Baada ya damu kwisha, lilianza kumla.

* Mchomo wa sindano ya pepo
Pepo jingine lilitokea likiwa na mwili kama wa karunguyeye au nungunungu uliojaa sindano kila sehemu. Nikatupa ngumi yangu kwake. Nilipoligusa tu, nikahisi maumivu makali sana ya kuchomwa na sindano. Hata baada ya siku za maombi yetu kwisha, bado mkono wangu ulikuwa na maumivu, ulikuwa mwekundu na umevimba huku ukiwa na alama za zile sindano. Nilishangaa sana kwamba iliwezekanaje jambo la kiroho kuacha alama kabisa za kuonekana na maumivu kabisa ya kimwili!

Pastor Kim Yong Doo: * Kujongea na kutetemeka kwa mikono

Nilivyoomba kwa kunena kwa bidii, mikono yangu ikaanza kusogea kidogokidogo juu na chini. Mara viganja vyangu vikageukiana na kutikisika kwa nguvu, huku mitetemo ikizidi kadiri muda ulivyoendelea. Nakumbuka niliwahi kumwona mchungaji mmoja alipokuwa akifanya maombezi kwa watu. Mikono yake nayo ilikuwa inatetemeka. Wakati mikono yake ikitetemeka hivyo, miujiza mingi ilitendeka. Nikawaza kuwa lazima na mimi nitakuwa nakaribia kuwa na karama ya uponyaji kama yeye. Mikono yangu ikawa inajiendea yenyewe kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Nikafungua macho yangu ili nione na nikajaribu kuizuia isitetemeke, lakini Roho Mtakatifu aliendelea kuiongoza licha ya utashi wangu na mawazo yangu. Utashi wangu na mawazo yangu vilikuwa vimeambatana tu na kazi ya Roho Mtakatifu.


Dada, Baek Bong-Nyo: * Bwana aijaribu imani yangu
Wakati nikiomba, Yesu alikuja na kusema, “Bong-Nyo, leo nataka nikujaribu ili nione ni kwa kiasi gani imani yako imekua. Je, uko tayari?” Nikajibu kwa ujasiri, “Ndiyo, Bwana. Niko tayari.” Akatoweka na mara malaika wakaja wakanivisha vazi lenye mabawa. Walipomaliza, malaika wale nao mara moja wakatoweka.

Kwa kawaida, Yesu na malaika zake huniongoza hadi Mbinguni au Kuzimu, lakini haikuwa safari hii. Nikaanza kumlilia Mungu kwa moyo wa dhati. Roho yangu ikaanza kupaa kuelekea Mbinguni, huku nimevaa lile vazi lenye mabawa. Lakini licha ya kuomba kwa bidii zote, nikawa napaa chinichini tu. Ilikuwa inaudhi, lakini sikukata tamaa. Nikaendelea tu kuomba kwa bidii. Muda si mrefu nikawa nimechoka kabisa. Nikawa sioni kitu chochote; ilikuwa ni giza tu totoro.

Nikakumbuka kwamba Bwana alisema anataka kujaribu imani yangu. Kwa hiyo, nikaendelea kuomba. Kwa bahati mbaya, kila kikwazo unachoweza kukifikiria kilinitokea na nikajikuta nimerudi kulekule nilikoanzia. Hadi sasa, kila nilipoomba kanisani, Bwana alikuja kwangu na kunionyesha kila kitu. Nilishakuwa na majivuno bila kujua. Nikakumbuka swali ambalo niliwauliza malaika waliokuwa wakinivika vazi la mabawa muda mfupi uliopita. Niliwauliza Yesu alikuwa wapi na wao walinijibu, “Sasa hivi, anasubiri kukutana na wewe kwenye kilimia (the Milky Way).” Kwa bahati mbaya, wakati huo, nilichelewa kwa sababu nilikuwa napaa kwa kasi ndogo sana. Imani yangu peke yangu haikuwa na uwezo wa kunipaisha kwa umbali ule.

Nikaomba kwa dhati kabisa kwa muda mrefu, lakini bado nilikuwa sioni chochote. Mawazo mengi yalipita akilini mwangu na nikaanza kutubu. Bila ya msaada wa Yesu, sikuweza kufanya chochote. Nilijihisi kama naendelea kuzama kwenye bwawa. Hali hisia zile ikaendelea hadi nilipojihisi nimefungiwa ndani ya kitu fulani. Kulikuwa na vitu vinatembea mbele ya macho yangu na nikatambua kuwa tayari nilikuwa Kuzimu, nikiwa nimefungiwa kwenye chumba cha giza.

Kwenye giza hilo, hakuna kilichokuwa kinaonekana. Mapepo yalikuwa yanajazana kunizunguka. Mapepo yasiyo na idadi yalianza kung’ang’ania miguu yangu kwa nguvu yasitake kuniachia. Yalinibana na kunivuta mikono, miguu na mwili kiasi kwamba nikawa siwezi kusogea kabisa. Nikaanza kunena kwa lugha, lakini ghafla matusi yakaanza kunitoka mdomoni bila mimi kupenda.

 “Nyie, mapepo machafu! Kwa nini mnanisumbua? Ishieni zenu huko muachane na mimi!” Sikuweza kujizuia kulaani. Lugha zote chafu ambazo nilijifunza huko nyuma, kabla ya kukutana na Yesu, ziliporomoka kutoka kinywani mwangu. Lakini haikujalisha ni kiasi gani nimeyatukana yale mapepo, hayakuacha kufanya mashambulizi yao kwangu. Nikaita, “Yesu, tafadhali nisaidie!”

Nikaendelea kumwita Bwana na kunena kwa lugha kwa bidii. Baada ya muda nisioujua, niliweza kwa namna fulani kuponyoka kutoka Kuzimu na kuanza kupaa kuelekea Mbinguni. Nikawa naomba huku napaa. Kwenye anga, mapepo yeye nguvu yakaanza kunifukuza. Nikaweza kuona waziwazi msururu usio na mwisho wa mapepo mengine nyuma yao. Nilidhani kuwa sasa nilikuwa niko salama baada ya kuponyoka kutoka Kuzimu. Badala yake kumbe nilikuwa naenda kukabiliana uso kwa uso na mapepo yenye nguvu zaidi. Nikajihisi nimeingia kwenye matatizo makubwa.

Bado nilikuwa simuoni Yesu au malaika wowote. Nikawaza, “Ina maana nitakabiliana na hili jeshi la mapepo peke yangu!” Sikuwahi kuwaza nitakabiliana na vita kama ile. Sikujua kuna majeshi ya mapepo kwenye anga ambayo kazi yao ni kuwapinga Wakristo, kwa lengo la kuzuia maisha yao ya maombi. Kama mtoto mchanga anavyotembea kwa furaha huku ameshikilia mkono wa baba yake, ndivyo ambavyo Yesu mara zote alikuwa akiniongoza kwenda Mbinguni na Kuzimu. Nilikuwa nimejaa ushamba fulani huku nikidhani kuwa kila kitu ni rahisi rahisi tu. Kumbe nilikuwa nikiomba bila kujali sana.

Mapepo yale yaliweka vikwazo zaidi kwa kila hatua niliyopiga, ili kunizuia kupiga hatua kwenda mbele. Nililia kwa maombi ya dhati kabisa. Machozi na jasho vilitiririka mwilini mwangu. Pepo moja likapaza sauti, “Wewe, tazama pale! Kuna maombi mengine kutoka duniani yanapanda juu!” Kisha jingine likasema, “Hayo maombi hayana hata nguvu wala mamlaka.” Kama vile mtu anayechuma matunda na kuyala, mapepo yale yaliyakamata na “kuyala” maombi yale kutoka duniani.

Hapo nikajua kuwa kumbe maombi yasiyo na nguvu ni kazi bure. Maombi yanayofanywa huku mtu anasinzia, haelekezi moyo wake sawasawa, yaliyojaa fikra za kibinadamu, yaliyojaa ubinafsi, yahusuyo mambo tu ya kimwili na maombi ya nyuso mbili – yote hayo hayana nguvu yoyote. Hayo yalikuwa ni “matunda” yaliyopendwa sana na mapepo na yaliliwa mara moja.

Nikajua sasa kuwa ni maombi tu yaliyojaa shauku kubwa sana ya kufa na kupona na maombi yaliyojaa vilio vya kweli ndiyo yanayopenya anga na kufika hadi Mbinguni. Nikajua sababu kwa nini mchungaji wetu huwa analia kwa sauti na kwa kuzama sana anapokuwa anaomba. Mara nyingi nilikuwa nakerwa na mchungaji, na kuwaza, “Hakuna hata watu wengi humu kanisani. Kwa nini anapaza sauti kiasi hiki? Kwani ni lazima apayuke hivyo?” Kusema kweli, kuna nyakati nilijilazimisha tu kuomba japokuwa nakuwa nakerwa na vilio vikubwa vya mchungaji wetu. Nikaanza kuomba msamaha kwa kule kukerwa kwangu. Sasa najua kwa uhakika kabisa kwa nini tunatakiwa kuomba kwa namna ile.

Nikaendelea kuomba, bila kujua muda gani umeshapita. Na pale nilipokuwa nimechoka na kuishiwa kabisa nguvu ndani yangu, nikaona kwa mbali nyota nyingi kutoka kwenye kilimia (the milky way) zikiangaza. Mara moja, nikakusanya kila nguvu iliyokuwa imebakia ndani yangu na kuanza kuomba kwa kunena. Nikafika kwenye kilimia huku nimechoka kabisa, lakini pale ndipo mpendwa wangu Yesu aliponisalimu kwa furaha.

Mara Yesu aliponiona, alitoa tabasamu pana na kusema, “Bong-Nyo, umefanya vizuri kabisa. Najivunia wewe!” Nilikuwa nina hasira kiasi wakati huo, kwa hiyo nikamuuliza Yesu,“Bwana, kwa nini umenifanyia hivi? Bora basi hata ungenieleza kabla. Unawezaje kuniacha tu bila hata ya kunidokezea?” Nilipomaliza kuongea, Yesu alicheka tu. Na baada tu ya maneno machache na Bwana, akatoweka tena! Ghafla, kila kitu kikawa giza na mara nikajikuta nimesimama kwenye ukingo wa Kuzimu.

Bwana ameniacha kwa mara nyingine kupima imani yangu! Mara pepo lililoonekana kama pomboo lilijaribu kunishambulia na kuning’ata, huku likiwa limepanua kinywa chake; likionyesha meno yake makali. Nikafanya kama nataka kuliparua na nikasema kwa sauti, “Njoo unichukue kama unaweza.” Pepo lile likatoweka.

Kukawa na kibarabara chembamba mbele yangu. Nikaanza kutembea kukifuata. Nikatembea kwa muda ndipo nikaona kuna kitu kinanijia. Nilipokikaribia, nikaona ni pepo linalotia kinyaa, lenye kichwa lakini hakuna macho wala pua. Kutoka sikio lake la kushoto hadi la kulia kulikuwa na mkato mkubwa kwenye uso wake na meno yake yalikuwa makali kama ya papa.

Nilipokabiliana nalo uso kwa uso, pepo hilo nikasema, “We! Nimeshapambana na kuyashinda mapepo makubwa kuliko wewe na kuyashinda. Wewe si lolote kwangu. Ndani yangu umo moto uliotengenezwa na Mungu wa Utatu. Utateketea na kugeuka majivu mara utakapogusa mwili wangu. Kama huamini njoo upambane na mimi.”

Pepo lile likaogopa na kukimbia mbio. Nikatembea peke yangu kwenye barabara ile ndefu isiyo na mwisho na ikaonekana kama nazidi kuzama ndani zaidi ya Kuzimu. Nilikuwa naogopa na kutetemeka ndani yangu, lakini sikutaka kuonyesha hofu yangu. Hivyo ikabidi niwe nimetuliza akili yangu.

Nikaendelea kutembea kwenye ile barabara. Nikaona jani kubwa mbele yangu ambalo lilionekana kuwa na uhai. Jani lile lilijifungua na kujifunga na likajaribu kunimeza. Lakini nikasema kwa sauti, “Sawa! Nimekuja hapa mahususi kukuua wewe! Haya tuone nani atapona.” Nikalishambulia kwa nguvu na mara lile pepo likatoweka.

Nikaendelea mbele. Nikaona kuna makundi ya mapepo, kama wadudu, pande zote za barabara yaliyojaribu kunishika. Nikasikia milio ya kutisha ya mapepo iliyofanya mwili wangu usisimuke. Nikasikia milio mingi tofauti, lakini nikaipuuza na kuendelea mbele huku nikiomba kwa kunena kwa sauti. Nikapaza sauti, “Mungu wa Utatu! Nipe nguvu! Nipe nguvu na uwezo wa kimwili na kiroho!” Nikaomba kwa dhati na ghafla, moto Mtakatifu ukaanza kuwaka ndani yangu.

Huku nikijiuliza nimetembea umbali kiasi gani, nikadhani nimeona mwisho wa barabara ile kwa mbali. Ghafla, mwanga mkali ukatokea mbele yangu na ikawa ni Yesu. Nikapatwa na mshangao na kuvutiwa sana. “Ndio! Hatimaye nimeokolewa, Bwana!” Nikamkimbilia na kumkumbatia. Bwana akanishikilia kwa nguvu kwa mikono yake na kusema, “Mpendwa wangu sana Bong-Nyo, umepambana na mengi hadi kufika hapa! Kaa pembeni yangu na mimi nitakupa yaliyobakia.” Nikabakia kwenye mikono ya Bwana na kufumba macho yangu ili kupumzika. Je, ilikuwa inatokea tena? Nilipofungua macho yangu, Bwana alikuwa haonekani tena. Nikawaza, “Nawezaje kuwa tena kwenye chumba hiki cha giza Kuzimu?” Haikujalisha ni kwa sauti kiasi gani nimemwita Bwana, mwangwi tu wa utupu ulinijibu! Nikamwita Bwana, lakini hakuwapo. Sikuweza tena kujizuia kuwaza kwamba Yesu amenidanganya. Yesu akasema kwa waziwazi, “Bong-Nyo, umefanya vizuri. Karibu unamaliza, kwa hiyo kuwa mvumilivu na upumzike hapa.” Baada ya kusema haya, na nilipokuwa najisikia niko salama, akanijaribu tena.

Hasira yangu haikuisha. Nikagundua kuwa nimefungiwa ndani ya sanduku la chuma kama mnyama wa kwenye bustani ya wanyama. Kulikuwa na mapepo yasiyo na idadi yenye sura tofauti yakizunguka lile sanduku na kunikodolea macho, huku yakijaribu kunihoji maswali. Yalinikodolea macho, na kunidhihaki na kucheka. Kulikuwa na maelfu ya mapepo ya kijeshi yaliyovaa helmeti za mafuvu.

Mapepo yale yalikuwa makini kunitazama wakati nikiwa nimefungiwa kwenye lile sanduku la chuma. Nikasema kwa sauti, “Nyie wanaharamu, ni akina nani nyie? Mnatoka wapi?” Yakajibu, “Tumetoka kuzunguka huku na kule. Na wewe je? Kwa nini uko humu?” Nikaeleza kwamba Yesu amenileta humu Kuzimu, lakini ameniacha ndiyo sababu nilikuwa hapo peke yangu. Baada ya kusikia hayo, yakanidhihaki yakisema, “Wewe, Bwana wako wala hatakurudia tena. Huu ndio mwisho wako!”

Nikaanza kuomba kwa sauti kwa kunena. Macho ya yale mapepo yaliyovaa helmeti za mafuvu yakaanza kugeuka kuwa mekundu. Yakanitazama kwa hasira kali. Nguvu ya kuomba kwa kunena ilikuwa inayalemea na nikagundua kuwa yameanza kubadilika. Kwa hiyo nikaomba kwa nguvu hata zaidi. “Mungu wa Utatu, nigeuze niwe moto wako uteketezao!” Mapepo yote yakavamia lile sanduku la chuma kutaka kuliharibu. Lakini moto Mtakatifu uliowaka ndani yangu ukayateketeza yote na kuyageuza kuwa majivu. Lakini vyuma vya lile sanduku havikuharibika, bali vilibakia kama mwanzo.

Kwa mara nyingine tena, milio ya wanyama mbalimbali na mapepo ikasikika kote na ikawa kana kwamba nilishakuwa pale kwa miezi kadhaa. Haikujalisha ni kwa bidii kiasi gani nililia na kupiga mateke na kupaza sauti, hakukuwa na njia ya kutoka kwenye sanduku lile pale Kuzimu. Kidogokidogo, moyo wangu ukaanza kuchoka. Subira yangu kwa Bwana ikabadilika kutoka kwenye kungoja kwa shauku na kuwa maumivu ya moyo, lakini sikuacha kuomba.

Niliomba, “Bwana, nahitaji nguvu. Nipe nguvu! Pia, naomba karama ya uponyaji na unijaze kwa moto ili niweze kuyeyusha sanduku hili la chuma nitoke hapa.” Nikafungua macho yangu na nikawa bado nimo ndani ya sanduku lile. Hakuna ndoto wala tumaini kwenye sanduku la Kuzimu! Haikujalisha ni kwa nguvu kiasi gani nimemwita Bwana, bado nilikuwa nimenaswa ndani ya lile sanduku! Je, hii ina maana kuwa nitateseka milele humu Kuzimu? Sikuwa tena na nguvu za kutosha ndani yangu hata za kunyanyua kidole, nikaanguka tu kwenye kona mojawapo. Ilikuwa kama vile nilishanaswa humo sandukuni kwa miezi minne.

Baadaye, nikaanza kupiga kelele tena, “Bwana, nisaidie! Uko wapi?” Sikuona hata kivuli cha Bwana wangu. Mapepo yaliendelea kuvuta na kutesa mwili wangu na nikaendelea kupigana nayo kwa siku 15. Kwenye lile sanduku, niliweza kuhisi kabisa siku zikipita.

“Bwana, nisaidie! Tafadhali nitoe humu. Nisaidie kutoka mahali hapa!” Nilikuwa kama najiomba tu mwenyewe. Nikasikia mtu akicheka. Nikasema kwa sauti, “He! Ni sauti ya Bwana!” Bwana akatokea katikati ya mwanga mzuri na kuliangaza lile sanduku lenye giza pamoja na maeneo ya karibu kwa mng’ao wake.

Yesu akaanza kucheka kwa sauti hata zaidi akisema, “Mpendwa Bong-Nyo, umejisikiaje huku Kuzimu?” Nikamhoji Bwana, “Aah Bwana. Kwa nini umenifanyia hivi? Hivi umeamua kunifanya niteseke? Kwa nini umefanyia hivi?” Nilikuwa nimejaa huzuni kubwa wakati nikimimina malalamiko yangu, na Bwana akajibu, “Samahani. Nilitaka kukujaribu wewe kibinafsi; ni kwa kiasi gani imani yako imekomaa!” Sikuwa na cha kusema zaidi kwa hilo.

Nilipohoji ni wapi Bwana alikuwa, alinijibu kwamba alikuwa duniani akitembelea makanisa mbalimbali ili kuwaangalia na kuwahudumia kondoo wake awapendao. Nikakiri kwa Bwana hisia zangu za ndani kabisa na kumwomba msamaha. “Bwana, nilikuwa na uchungu na kukuchukia wewe sana wakati nikiwa nimefungiwa kwenye sanduku hili Kuzimu. Unisamehe.” Sauti yangu ilibadilika kwa malalamiko na hisia za kujihurumia wakati hisia hizo zikijidhihirisha. “Bwana, nilikwama ndani ya sanduku hili kwa miezi minne.” Nikaanza kulia.

Bwana aliendelea kucheka kwa sauti na mimi nikasema kwa nguvu, “Kwa nini unafurahia hivyo kuniona nina huzuni na nikiteseka? Nimeteseka kiasi hiki Kuzimu, lakini kwa nini unacheka kana kwamba lilikuwa ni jambo la kufurahisha? Je, unafurahia kuniona nikiteseka?” Akajibu kwa upole, “Bong-Nyo, ilikuwa ni miezi miwili tu tangu uanze kuhudhuria kanisani, lakini imani yako imekua sana. Najivunia wewe!” Akanipigapiga mgongoni.

Yesu akaniondolea vazi lililochakaa ambalo nilivaa kule Kuzimu na akawaamuru malaika wanivike kwa mavazi safi, yanayong’aa na yenye mabawa. Akasema, “Umestahimili mambo mengi. Kwa hiyo, sasa tukatembelee Mbinguni!” Alinishika mkono na tukaanza kupaa kuelekea Mbinguni. Leo ilikuwa ni siku ngumu kuliko siku yoyote niliyowahi kuiona maishani mwangu.

Ilichukua roho yangu miaka mitatu kutoka duniani hadi kwenye kilimia (the Milky Way) na nikatumia miezi minne na nusu Kuzimu. Ilionekana kama miaka mitatu na nusu imepita haraka sana. Mapepo kwenye anga na ya kule Kuzimu yalikuwa imara na yenye nguvu sana. Nisingechukua dakika moja au hata sekunde moja kwenye mapambano nayo na kushinda bila ya ulinzi wa Bwana. Nilipofika Mbinguni, malaika wengi walitabasamu na kunifariji. “Dada, umefanya vizuri sana!” Maneno ya malaika yaliinua moyo wangu. Kila ninapokuwa Mbinguni, magumu yote niliyokutana nayo Kuzimu nayasahau.

Sijui mambo mengi, maana nimekuwa nahudhuria kanisani kwa miezi miwili tu sasa. Kutokana na kile nilichokiona kwenye sinema na kwenye mahubiri, nimejifunza kidogo kuhusu mtu aitwaye Musa ambaye aligawa bahari. Nilimwomba Yesu aniruhusu nimwone Musa japo mara moja tu. Yesu aliniongoza hadi kwenye ufukwe wenye mchanga wa dhahabu. Kwa upole, malaika walinipeleka kule. Mara tu Yesu alipoita jina la Musa, Musa alikuja kwangu na kunisalimu kwa heshima, “Karibu mbinguni!” Musa alikuwa mrefu na mzuri.

* Kushuhudia miujiza ya Musa Mbinguni

Yesu alinitambulisha kwa Musa. Nikasema, “Musa, sikujui vizuri, lakini nafahamu kidogo kwa sababu nilisikia mahubiri ya mchungaji wangu kuhusiana na wewe.” Akajibu, “Oh, kweli? Dada, nafurahi kwamba uko hapa!” Nikaendelea kusema, “Ulipokuwa duniani, haukugawa bahari na kutenda miujiza mingi?” Musa kwa unyenyekevu akasema, “Sikufanya chochote, lakini alikuwa Mungu aliyenipa mimi nguvu na nilichofanya mimi ni kutii tu.” Nikasema, “Mimi nimeshahudhuria kanisani kwa miezi miwili tu hadi sasa, lakini mara tu niliposikia habari zako, nilitamani sana kukutana na wewe. Lakini Bwana mara nyingi hunipeleka kutembelea Kuzimu, kwa hiyo kukutana na wewe haikuwa rahisi. Natamani kushuhudia baadhi ya miujiza yako. Je, unaweza kunionyesha baadhi yake?”

Yesu alimruhusu Musa ajenge mlima mkubwa wenye mchanga wa dhahabu. Kufumba na kufumbua, kukawa na vilele viwili vya milima. Nikampa changamoto ajenge nyumba ya ghorofa 600. Aliinua tu mkono wake hewani na kuuzungusha mara moja na zikatokea ghorofa 680 mbele yangu.

Nikabakia kinywa wazi. Akanitengenezea ngazi ya dhahabu kutoka duniani hadi Mbinguni. Musa akafanya miujiza mingine mingi ambayo haiwezi kuelezeka kwa maneno. Nikasema, “Musa, unisamehe kwa imani yangu ambayo bado haijakomaa. Samahani na najisikia aibu kwa kukujaribu hivyo na kukuuliza maswali mengi.” Akajibu, “Usijali kuhusu chochote na hata kama bado una maswali mengine, usisite kuuliza.”

Nikaomba kuona kugawanywa kwa bahari kama ilivyoandikwa kwenye Biblia. Kuona hili lilikuwa ni jambo la kuogofya na kushangaza sana. Yesu alikuwa anatazama kimya pembeni yangu. “Yesu, Musa, mimi ni mwamini mpya na sijui mambo mengi, kwa hiyo nadhani nimekuwa wazi sana kuhusu maswali yangu. Tafadhali mnisamehe. Samahani. Nikirudi tena kanisani, nitaandika na kumshirikisha mchungaji wangu kile nilichokiona, ili kwamba auelezee ulimwengu.” Yesu akasema, “Musa, Dada Baek Bong-Nyo anatakiwa arudi duniani, kwa hiyo muage.” Kwa heshima, Musa aliinamisha kichwa chake na kusema, “Kwa heri dada.”

Yesu akanielezea, “Hata Mbinguni, Musa huwa yuko na kazi nyingi muda wote. Huwa anasafiri kote Mbinguni na ana mambo mengi ya kuyafanya.” Sitasahau nilivyokutana na Musa Mbinguni. Yesu aliniongoza kurudi kanisani na nikamalizia maombi yangu.

No comments:

Post a Comment