==== SIKU YA 21 ====
Kim,
Joo-Eun:
Nilikuwa kwenye moto, nikiomba kwa
kunena. Madragoni (mazimwi) matatu ya kutisha yakatokea. Dragoni la kwanza
lilikuwa na michoro mingi na maumbo ya duara kwenye mwili wake wote mwekundu.
Dragoni la pili lilikuwa na mistari myekundu na buluu ya wima iliyochanganywa
pamoja kiasi kwamba ilinifanya kuchanganyikiwa nilipoitazama. Dragoni la tatu
lilikuwa na mistari ya buluu na njano ya ulalo iliyochanganywa pamoja. Yalikuja
kama vile yanataka kunimeza mzimamzima, lakini nilipaza sauti mara tatu kwa
uthabiti, “Kwa Jina la Yesu, ondokeni kwangu!” Yakakimbia.
Nilipoangaza angaza macho, nikaona
mapepo yaliyokuwa yamekaa kwenye duara yakijadiliana jambo. Kiongozi wao
akaliambia pepo mojawapo lililokuwa kipara, “Wewe,
safari hii utaenda kujaribu!” Kwa haraka lilikuja kwangu, lakini
kama ilivyokua mwanzo, nilikamata kichwa chake na kukivuta huku na kule.
Nikatoboa macho yake, likakimbia. Kisha pepo lenye vidole kama mkasi likanijia.
Lilikuwa linakwaruza ubao. Sauti iliyokuwa inatoka sikuweza kuivumilia. Kwa
hiyo nikalivunja vidole vyake na kuliparua usoni kwa vidole hivyo. Likasema, “Wewe, nirudishie vidole vyangu! Kwa nini unachukua vidole
vyangu? We kisumbufu kidogo, usinichezee! Kwa nini imani yako imekua kiasi
hiki?” Baada ya kusema hivyo, likatoweka.
Niliendelea kuomba kwa nguvu. Joka
kubwa lilitambaa kuelekea kwangu huku lionyesha uso wa hasira. Magamba yake
yalibadilika rangi mbalimbali na lilikuwa linaleta na kuondoa mkia wake karibu
na mimi. Nililikamata na kulitupia ukutani. (Marko 16:17,19)
Kisha pepo jingine lilitokea ambalo lilikuwa limefungwa bandeji mwili mzima. Lilinifanya nikumbuke katuni ya kichina inayoonyesha pepo aitwaye ‘Kang-She.’ Likasema, “Tazama we mtoto, hii inafurahisha kwelikweli!” Likaanza kufungua zile bandeji. Chini ya bandeji kulikuwa na wadudu wengi, majongoo na matandu yalitambaa juu ya mwili wake wote. Huku nikiwa nimesikia kinyaa sana, kwa haraka nilimwita Yesu, na akatokea. Akalikamata lile pepo na kulitupa chini. “Yesu asante sana!” nilisema. Akatabasamu na kupapasa kichwa changu taratibu. “Mpendwa wangu Ufuta, imani yako imeongezeka sana! Omba kwa bidii.” Leo Yesu alikuwa amevaa vazi maalum la dhahabu lenye moyo mwekundu kifuani mwake unaotoa rangi mbalimbali.
Baada ya Yesu kuondoka, pepo lililojifanya kama bibi kizee, lilitokea. Lilikuwa limevaa nguo nyeusi na kushikilia shoka refu. “Acha kuomba! Utaomba wakati mwingine. Si lazima uombe leo, sawa? Kwa nini umeng’ang’ania kuomba leo? Omba kesho. Yesu atakutana na wewe ukiomba kesho. Fanya hivyo.” Likarudia kusema hivyo kwa sauti zaidi. Kwa hiyo na mimi nikaliambia kwa sauti, “We kizee mwenye sura mbaya, kwa Jina la Yesu, ondoka kwangu!” Likatoweka.
Lee, Yoo-Kyung:
Wakati nikiomba, pepo moja lilinijia na
kusema, “Wewe! Hivi hujui kuwa unatakiwa kuniomba
msamaha?” Sikuamini kile nilichokisikia. Kwa hiyo, nikalikamata na
kulizaba kibao usoni. Lakini na lenyewe likanizaba kibao usoni kwangu, huku
likisema, “Unathubutu kunipiga kofi? Njoo hapa.
Nitakuua!” Nilikuwa nimejawa na hasira. Kwa hiyo, nikayang’oa macho
yake na kuyatupa chini. Shavu langu likaanza kuvimba na sikuweza kusahau jinsi
kujisahau kidogo tu kulivyosababisha mimi nikazabwa kibao na yule pepo.
Muda mfupi baadaye, pepo la kike
lililovaa vazi jeupe lilitokea. Lilikuwa linalia machozi. “Hii si sawa kabisa! Mwanaharamu yule, Haak-Sung, amenipiga
na kile kijitu kisumbufu, Joo-Eun, nacho kimenipigapiga!”
Nikalisubiri lifike karibu kisha nikang’oa macho yake kwa vidole vyangu.
Likarukaruka kwa maumivu na likakimbia. Pepo jingine la kike likasema, “Wewe, unadhani utabaki salama kwa haya unayotufanyia?” Nikashika
nywele zake, nikalizungusha kisha nikalitupilia mbali nami. Nikasema, “Yesu
nipe shoka.” Kwa kutumia shoka, nikakata kichwa cha pepo yule na kukipasua.
Huku kichwa chake kikiwa kimekatika, likanijia na kusema kwa sauti, “Wewe, hata husikii huruma kwangu?” Likawa
linazunguka likitafuta kilipo kile kichwa chake, huku likisema, “Kichwa changu kiko wapi? Uso wangu uko wapi?”
Baadaye, nilitaka kumwona Yesu.
Nikamwita kwa nguvu zangu zote, “Baba! Baba!” Yesu akanisalimia kwa
tabasamu pana, “Mpendwa
wangu Ufuta, umefanya vizuri sana. Yoo-Kyung wangu anaweza peke yake kuyashinda
mapepo kikamilifu kabisa.” Pia akasema, “Yoo-Kyung, Mchungaji Kim atakapokuita, ‘Sesame’
(Ufuta) wakati wa ibada, uitike kwa nguvu kabisa. Kuitika kwa nguvu nayo ni
imani. Umenielewa?” Nikasema, “Ndiyo, Bwana. Amen.”
Baada ya muda mfupi, baadhi ya malaika
walikuja, wakasema, “Dada Yoo-Kyung, umeyashinda mapepo. Wewe si wa kawaida.
Songa mbele! Na mapepo yakikushambulia tena, uyashinde tena kama ulivyofanya
hadi sasa!” Wote wakanishangilia. Yesu alinichukua kwenda kutembelea
Mbinguni. Nilipofika pale, Yae-Ji na mimi tulianza kucheza mbele za Bwana.
Tukamwomba “Bwana, tafadhali mimina machozi ya toba kwa Shemasi Shin Sung-Kyun,
na Joseph. Wote wawili wanatamani kuomba sala ya toba kwa machozi lakini
hawawezi kulia.” Lakini Bwana akajibu, “Naweza tu kutoa machozi ya toba kama watu wanaomba kwa moyo kabisa kwa
toba kwa mioyo yao.” Tulisindikizwa kurudi hadi Kanisani. Yesu aligusa
shavu langu nilikokuwa nimezabwa kibao na yule pepo na akasema, “Mpendwa Yoo-Kyung, uwe imara.
Umeelewa?” Kisha akapunga mkono na kutoweka.
Lee, Haak-Sung: * Pepo lenye msumeno wa mnyororo
Wakati nikiomba kwa kunena, mapepo
matatu yalinivamia kwa mara moja. Moja lilikuwa na uso wa binadamu na mwili wa
dragoni. Jingine lilikuwa ni mifupa tu. Na la tatu lilikuwa limevaa kinyago cha
chuma. Cha ajabu, lilikuwa limebeba msumeno mkubwa wa mnyororo (chainsaw) na
lilijaribu kukata mikono yangu. Ilinibidi niwe makini sana. Kama ningepoteza
uzingativu wangu hata kwa sekunde moja, lile pepo lingenikata. Sikuwa tayari
kupoteza. Kwa hiyo, nilikwepa na kukimbia mashambulizi. Kisha wakati wa
kushambuliana, nililipokonya ule msumeno na nikalifyeka mikono yake. Likawa linapiga
kelele huku yale mengine mawili yakanikimbia.
Baadaye, pepo jingine lilinijia.
Nikalidanganya linisogelee kwa kuliambia, “Wewe, njoo hapa nikufundishe
jambo la kufurahisha. Njoo huku! Fanya haraka!” Pepo lile likawa na
wasiwasi na likagoma kuja. “Wewe! Kweli nina kitu kizuri cha
kufurahisha kwa ajili yako. Njoo uone!” nikasema, lakini bado
halikuniamini. Likaniuliza, “Unaahidi kuwa
hautaniadhibu?” Nikajibu, “Kwa nini nikuadhibu? Nilitaka tu
kukuonyesha jambo la kufurahisha. Kwa hiyo njoo hapa.” Likaja karibu
nami huku likiwa limechangamka. Lilipokuwa karibu, nikakamata mkono wake na
kuanza kulizungusha hewani, kisha nikalitupa likajibamiza ukutani.
Baadaye kidogo, nikasikia sauti kubwa
za miguu inayotembea kama ya kikosi cha askari. Ilikuwa kama mamia ya miguu
ikitembea kwa pamoja. Mara nikaona kundi kubwa la mapepo likinijia, yote yakiwa
yamevalia sare za kijeshi. Nilijua kuwa mapepo yanayokuja kunishambulia
yalikuwa yakiendelea kuwa yenye nguvu zaidi kuliko yaliyotangulia. Lakini
nilipotaja Jina la Yesu, yote yakatoweka.
Kim, Yong-Doo:
* Mikono yote iligeuzwa kama keki iliyopinda
(pretzel)
Nilikuwa nikimlilia Bwana huku mikono
yangu ikiwa imeinuliwa juu kwa takribani dakika 30. Mikono yangu ilianza
kuzunguka tena na tena. Mkono wangu wa kushoto ulianza kujisogeza kutokea ndani
kwenda nje, ukifuatiwa na mkono wangu wa kulia, nao ukifanya kama wa kushoto.
Ghafla, mikono yote ikaanza kujinyonga kuelekea nje kama keki iliyopinda na
ikabakia kwenye mkao huo. Ulikuwa ni mkao mbaya na wenye mateso na mgumu
kustahimili. Kisha mikono yangu kila mmoja ukaanza kujinyonga kuelekea upande
tofauti na mwingine, kutokea nje kuja ndani; ndani ya dakika moja tena. Kwanza
mkono wangu wa kushoto, kisha wa kulia. Halafu nikabakia kwenye mkao huo nao
kwa dakika 30 zingine. Kwa sababu jambo
hilo lilikuwa linatendeka polepole, nilikosa uvumilivu na nikaanza kuingiwa na
hasira.
Nikalalamika, “Bwana, kwa nini
unanifanya niteseke kiasi hiki? Kama utanigeuza ndani nje, basi bora ufanye
haraka. Mbona kama unacheza nami? Unanifanyia nini hiki sasa? Nimechoka. Si
itakuwa bora kwetu sote kama utanipa mara moja hicho ninachotaka?” Nikaanza
kumshambulia Bwana kwa malalamiko yangu, “Bwana, kama ungenipiga tu kwa moto
wako Mtakatifu na kufungua macho yangu ya kiroho, si itakuwa bora kwa upande
wako na wangu? Nani ataweza kupokea
vipawa vya rohoni kama utafanya mambo kuwa magumu kiasi hiki?”
Niliomba na kudai vipawa vya
rohoni. Nililia, nilipiga kelele kwa
nguvu zangu zote. Lakini Bwana aliendelea kurudia kazi za Roho Mtakatifu kupitia
kunyonga mikono yangu. Alifanya hivi mara nyingi. Nikawaza, “Hivi anataka
kunipa vipawa gani hasa vya rohoni? Hii ni aina gani ya vipawa jamani?”
Nilikuwa nimekereka sana na nilitamani jambo lile lingefanyika kwa haraka.
Lakini Bwana wala hakuwa na haraka kama mimi. Badala yake, nilikerwa na mwendo
wake wa polepole.
Ilikuwa ni takribani saa nne baadaye,
ndipo kunyonga kwa mikono yangu kulipokoma na ikaanza kusogea kuanzia mbele
kwenda nyuma. Nilijaribu kwa kila njia kuituliza mikono yangu, lakini kule
kutetemeka kwake kuliendelea. Kwa kweli,
ilikuwa inachekesha. Niliambiwa kupitia unabii kuwa nilikuwa kwenye mchakato wa
kupokea kipawa cha uponyaji na nguvu ya miujiza.
Dada Baek Bong-Nyo: * Ziara nyingine Kuzimu
Nilikuwa nafurahia uchezaji wa kiroho
na kuomba kwa kunena. Malaika kumi walishuka kutoka Mbinguni ili kunichukua
hadi kwa Yesu. Nilipofikishwa kwa Yesu, alisema, “Mpendwa wangu Bong-Nyo, kama unavyojua, mchungaji
wako Kim anaandika kitabu juu ya Mbinguni na Kuzimu. Ningependa kumchukua Mchungaji
Kim pamoja nami hadi Kuzimu na kumwonyesha kile anachotakiwa kuandika kuhusina
na Kuzimu, lakini macho yake ya rohoni hayajafunguka bado. Sina namna ila
kukuchukua wewe, ili kuwezesha kuandikwa kwa usahihi mambo ya Kuzimu. Wewe peke
yako ndio ninaweza kukupeleka kule. Kwa hiyo nakuomba uvumilie kwa muda kidogo.
Haya twende tukatembelee Kuzimu pamoja.”
Mara tulikuwa tunatembea kwenye
barabara ya Kuzimu. Harufu mbaya ya nyama zilizooza ilifanya tumbo langu
livurugike na kulikuwa na giza lisilo na mwisho. Nilishikilia kwa nguvu mkono
wa Bwana. Kule Kuzimu, kuna mateso tu milele. Tulifika mahali ambapo watu
waliokuwa kwenye shimo lenye moto walikuwa wakilia na kuomba msaada. Moto
ulikuwa mkali sana. Kulikuwa na watu wengi wasio na idadi, wote wakiwa uchi,
wakirukaruka na kupiga kelele ndani ya pipa kubwa sana. Nikamwona baba yangu
tena. Alianza kulia, “Bong-Nyo, unafanya nini hapa? Siwezi kuvumilia maumivu
ya moyo kila wakati ninapokuona. Nisamehe sana kwa yote niliyokutendea. Nadhani
hiyo ndiyo sababu niko hapa nikilipia yale niliyotenda.” Sikuweza
kusema neno lolote, lakini nililia tu mfululizo. Maumivu yaliyoko Kuzimu ni
makubwa mno kuliko mateso ambayo baba yangu alinisababishia duniani. Kile
kilichonipata duniani kilikuwa si lolote si chochote.
Pepo moja kubwa lilikuwa linafurahia
kuwakatakata watu kwa fyekeo kubwa (scythe). Lilikuwa linaimba na kuimba.
Lilimnyakua baba yangu na kuanza kumkatakata, kama ambavyo tunakatakata chakula
cha tambi nyumbani. “Ahhhh! Tafadhali niokoe! Naomba! Tafadhali niueni tu!” Vilio
vya maumivu na mateso vya baba yangu vilinifanya nizimie. Bila ya kuwapo Bwana
karibu yangu, ningezimia mara nyingi tu. Hakuna mwisho wa mateso kule Kuzimu.
Unakuwa umelaaniwa kwa majuto ya milele. Hakuna tena matumaini. Njia pekee ya
kuepuka kwenda Kuzimu ni kumpokea Yesu kama Mwokozi wako na kuishi kwa
uaminifu.
Tuliendelea mbele, huku tukiacha nyuma
vilio vya maumivu makali vya baba yangu. Baada ya kutembea kwa muda, niliona
mti mbele yangu. Nilipofika karibu, nikamwona mama yangu, mdogo wangu wa kiume,
shemeji yangu na mpwa wangu, wote wakiwa uchi, huku wakiwa wamening’inizwa
mtini kwa vifundo vya miguu yao. Pembeni yao kulikuwa na pepo lililokuwa refu
kuliko mlima. Nilimtazama mama yangu na yeye akaniona, huku akiwa kaning’inia
mtini. Wengine nao waliniona na kuanza kunililia. “Bong-Nyo, kwa nini uko
hapa kama huwezi kutusaidia? Kwa nini umekuja tena? Je, unapenda kuniona nikiwa
kwenye mateso kiasi hiki?”
Yesu akaniambia kuwa pepo lile lilikuwa
ni la pili kwa ukubwa kule Kuzimu. Lilikuwa linapenda kuwapiga watu na kubandua
nyama za miili yao. Kisha linawatupa bila huruma motoni. Nilitamani
nilichanechane! Lilimwamuru mmoja wa walio chini yake kuweka chombo kikubwa
kilichojaa wadudu chini ya watu wa familia yangu. Wadudu hawa walikuwa kama funza,
wakiwa na meno makali na macho yaliyong’aa sana. Walipanda hadi kwa wale ndugu
zangu na kuanza kuwatafuna nyama za miili yao bila huruma. Walichimba kote
kwenye miili yao, hata macho na pua zao. Nikawasikia wote wakilia, “Ahhhh!
Tafadhali niokoe! Bong-Nyo! Dada mkubwa! Aaaa! Shemeji! Tafadhali
niokoe! Shangazi! Tafadhali nisaidie!” Mara nyama yote ikawa
imekwisha na wale wadudu wakaendelea kuchimba hata ndani ya mifupa yao. Moyo
wangu uliumia sana kujua kwamba hali hii ingeendelea milele. Pamoja na kumwomba
sana Yesu asaidie, alichoweza tu kusema ni, “Siwezi kufanya hivyo. Muda huo ulishapita!”
Yesu alinipeleka hadi kwenye mlima
mkubwa sana. Niliona watu wamesimama kuuzunguka huku wakiwa wamekata tamaa.
Walionekana wamechoka na wamevimba kutokana na kupigwa sana. Pembeni yao
kulikuwa na pepo linalotisha, ambalo lilianza kunidhihaki, likisema, “Nakuona hapa mara kwa mara. Umefuata nini tena leo?”
Nilijawa na hasira, nikaanza kulilaani, “Wewe, we ni mwanaharamu! Natamani
nikuchane vipandevipande kama ulivyofanya kwa familia yangu, kisha nikutupe
kwenye shimo la moto! Nitakupata tu!” Pepo lile likadhihaki kwa sauti
hata zaidi, “Unalia kwa sababu unaniogopa. Hiyo
inanifanya nifurahi! Utafanya nini sasa?” Nikasema, “Yesu, nataka
kuliua pepo hilo. Nalichukia pepo hilo! Bwana, kwa nini umesimama tu na
haufanyi lolote? Nionyeshe chochote!” Yesu alinyanyua mkono wake wa kulia
na kuuzungusha. Mara moja mwili wa pepo lile ukapooza na halikuweza kusogea,
kama nguzo ya jiwe. Mara watu wote walifunikwa na wadudu mbalimbali, ambao
walikuwa wanakula nyama za miili yao. Vilio vya watu wale vilirindima kwenye
anga lote la Kuzimu.
* Kukutana na Rais aliyepita wa Korea
Tuliendelea mbele, na Yesu akasema, “Roho utakazokutana nazo sasa ni
zile unazozifahamu sana, kwa hiyo tazama kwa makini.” Nikamwona rais
aliyepita wa Korea. Kulikuwa na joka kubwa jeupe limemviringa mwili wake na
nyoka wengine kadhaa wa rangi mbalimbali walikuwa juu yake. Alisema, “Ahhh! Acheni kunikosesha pumzi!
Tafadhali acheni! Niokoe tafadhali!” Lakini licha ya maumivu yale makali,
alianza kuongea na mimi akisema, “Wewe ni nani? Kwa nini uko hapa? Mimi
nilikuwa rais wa Korea, nikiwa na hadhi zote, lakini sasa ninateseka hapa
Kuzimu. Wachungaji wengi walijaribu kunishauri niende kanisani, lakini
niliwapuuza wote. Nilipuuza kile walichonieleza kuhusu Kuzimu na sikuwahi
kudhania kuwa kuna sehemu kama hiyo. Mwanangu bado hamjui Yesu na nina wasiwasi
sana juu ya hilo. Mwanangu anatakiwa amkubali Yesu akiwa bado yuko hai na
apokee wokovu ili aje aishi Mbinguni. Natamani ningeweza kwenda sasa na
kumweleza mwanangu ukweli huu. Lakini
siwezi. Sasa nifanyeje? Ahhh! Moyo wangu unauma sana.” Alimwomba
Yesu, lakini Yesu alimsikiliza tu bila kusema neno lolote.
No comments:
Post a Comment