==== SIKU YA 23 ==== (1 John 3:7-10)
Mchungaji Kim Yong Doo: * Mama Kang, Hyun
Ja alishambuliwa na mapepo baada ya kujisahau
Kwenye
saa 5 kamili asubuhi, mke wangu, Joseph, Joo Eun, na mimi tulisimama mbele ya
mgahawa unaotazamana na jengo la Chama cha Ushirika cha Kilimo. Mke wangu
alipoanza kutembea, alishambuliwa na kuanguka chini. Alianguka kwa nguvu sana
kwenye barabara ngumu ya lami, takribani mita tano kutoka kwangu, utadhani
alikuwa anateleza kwenye barafu. Jambo hilo lilitokea kwa haraka sana,
hatukupata muda wa kumdaka wakati alipotupwa hivyo. Alipiga kelele za maumivu
na sote tukamkimbilia ili kumsaidia ainuke. Viganja vyake vyote vilikuwa
vimechanika, kucha zimevunjika, na mikono ilikuwa imefunikwa na damu.