==== SIKU YA 19 ==== (Waebrania 10:35-39)
Shin
Sung-Kyung: * Shemasi Shin Sung-Kyung
alicheza uchezaji wa kiroho
Nilikuwa
naomba kwa kunena kwa lugha na mwili wangu ukajisikia kama moto unaowaka. Nje
baridi ilikuwa kali sana na ilifikia hadi nyuzi hasi 10 na tulizima mitambo
yote ya kupasha joto. Ndani ya kanisa kulikuwa baridi. Lakini Roho Mtakatifu
alikuwa juu yetu kiasi kwamba baridi ile kali hata haikutusumbua kwa kuwa Bwana
aligeuza miili yetu kuwa kama moto unaowaka. Ilitubidi kuvua makoti yetu mazito
ambayo huwa ni kwa ajili ya kipindi cha baridi kali na tukabaki tu nguo za
mikono mifupi.