(Waebrania
11:35-40)
|
Hii ni sehemu ya mwisho ya ushuhuda wa Jim McCoy aliyekuwa mwanafunzi wa mwanamke mchawi kule Marekani, lakini akaokolewa na Bwana Yesu na kutolewa ndani ya vifungo vya mauti.
.........................................
Mojawapo ya mambo hayo ni kuhakikisha kuwa
Wakristo lazima wakubaliane na imani ya New Age, watii mafundisho yake,
vinginevyo ni lazima waharibiwe. Kinachoongelewa
hivi sasa ni juu ya kuwatowesha kabisa! Kama unadhani kuwa mipango hii ni
maneno tu, basi umekosea sana. Haya ni mambo ya kweli kabisa! Mimi mwenyewe
nimekuwa nikifanyia kazi mipango hii na nimeona jinsi inavyoenezwa. Leo,
nilipoongea na ndugu mmoja, nilimwambia kuwa Mshauri wa Umoja wa Mataifa wa
masuala ya New Age kule Marekani alishaagiza nchini gilotini
100,000 (gilotini ni mtambo wa kukatia shingo za watu), kwa ajili ya
kuwaua wale Wakristo wasiokuwa tayari kuonyesha ushirikiano. Vilevile, katika
nchi nyingine mipango kama hiyo inaendelea kuandaliwa. Lakini kumbuka kuwa hizi
si ndoto bali ni mambo halisi yanayotokea sasa hivi. Mshauri wa Umoja wa
Mataifa ni taasisi muhimu katika kuwezesha sheria hizi zianze kufanya kazi.
Lakini hali halisi nyingine ni ukweli
kwamba Bwana Yesu Kristo anakuja kwa ajili ya bibi harusi wake, ambaye naye ni
lazima asiwe na waa wala kunyanzi lolote (Efe. 5:27).
Kumpokea Yesu kama Mwokozi wako binafsi
kwenye maisha yako peke yake haitoshi kukuponya wewe. Ni lazima pia ufanye
uamuzi wa kubadilika moyo wako chini ya uongozi wake, na kuwa kiumbe kipya. Kwa
njia hii ndipo utaweza kusimama kinyume na wale manabii na hayo makundi ya
uongo. Tuna watu duniani kote ambao wanahatarisha maisha yao ili kuharibu
mafundisho hayo ya New Age na ninajua kuwa wengi katika jamhuri ya Cheki
wanajitahidi kufanya vivyo hivyo. Unaweza kuuliza, “Nawezaje kufanya hivyo bila
kufanya mapinduzi? Nawezaje kushiriki kibinafsi katika vita hii ya kiroho?”
Sasa siongelei juu ya kumwaga damu au kupigana kimwili bali ninachosema ni
kuwa, tumia zile zilaha ambazo Bwana Yesu ametupatia.
Yafuatayo ni mambo muhimu ili kuweza
kupigana vita hivi:
1) Kwanza ni kubatizwa kwa Roho Mtakatifu,
maana bila Roho Mtakatifu hutaweza kujua namna sahihi ya kuzitumia silaha hizo.
2) Silaha yenye nguvu zaidi na inayofaa
zaidi dhidi ya New Age na mambo mengine ya uongo ni kuhubiri Injili kwa nguvu
kwa mataifa yote kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo, hivyo kuwa na nguvu kwenye
jamii yako. Bwana Yesu anarudi hivi karibuni (Ufu. 22:20) na uombe kuwa akukute
uko tayari, na uko nje kule ukiwahubiria watu Injili yake. Ni lazima
kuwajulisha watu, na kuwaepusha watoto mashuleni na mambo haya. Ni lazima
ufanye uinjilisti na kufanya kazi chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu ili kwamba
jamii yenu isivunjike tena na watu kuibiwa. Nyie vijana ndio msingi wa kesho.
Ni lazima mzuie mambo haya kwa kizazi hiki na vile vijavyo. Msipofanya hivyo,
hali itakuwa mbaya sana. Msikubali uinjilisti uzimike kwenye nchi yenu. Ni
lazima muwafundishe watoto na
kuwaonyesha kuwa Yesu Kristo kweli anajishughulisha na maisha ya watu. Ni
lazima muwe na ushuhuda ulio hai juu ya Bwana.
Nilitembea usiku kucha kwenye mitaa ya
Prague. Nimetembea usiku kucha kwenye mitaa ya Brno, na kile nilichoona ni
kibaya sana. Watoto walikaa mitaani wakiwa wamelewa chakari, huku wakicheza
muziki wa rock ambao unawaharibu ufahamu wao. Kuna makahaba wengi wa umri mdogo
tu. Watoto hawa; vijana hawa wanaelekea kwa kasi shimoni, kwenye uangamivu. Kwa
hiyo, ninyi walimu, wazazi na yeyote mwenye ushawishi, wafundisheni Injili ya
Yesu Kristo. Hilo ndilo tumaini pekee kwa ajili yao na hata kwenu ili msije
kutumbukia kwenye mafundisho ya New Age. Kama nilivyosema kabla, wanaharakati
wa New Age na waabudu shetani wamelenga hasa kwa vijana. Ni lazima tuwe makini
na tabia za vijana kwenye makanisa. Vijana ndio msingi wa jamii. Hao ndio taifa
lenyewe.
Inasikitisha lakini ukweli ni kwamba New
Age wako makanisani tayari miongoni mwa vijana. Pia kwenye sehemu mbalimbali za
jamii wameshaingia. Vilevile kwenye nafasi za juu za kitabibu kupitia “holistic
teaching”. Haya ni mafundisho yanayosema kuwa mwanadamu ni kiumbe ambaye tayari
ameshakuwa mkamilifu.
Namna zote zile mbadala za utabibu ziko
chini ya mafundisho haya. Wanasaikatria (psychiatrists) wote wanaotoa huduma
zao kwa kutumia upigaji taswira kichwani (visualization) na kufikiria (imagination),
wanaamsha nguvu za maono (psychic power) ndani ya mtu. Hii ina maana kuwa
mtaalamu wa eneo hilo anakuwa anaingiza ndani yako mawazo fulani anayotaka uwe
unayaona, hivyo kukuongoza katika welekeo fulani ambao anautaka yeye. Hii ni
mbinu ambayo shetani ataitumia ili kukutoa nje ya mpango aliokuandalia Mungu.
Eneo la tiba mbadala linajumuisha njia
kama tibavitobo na tibamgandamizo
(acupuncture and
acupressure). Niliongea na baadhi ya madaktari nchini kwangu na pia na
baadhi ya Wakristo ambao wamewahi kutumia aina hizi za uponyaji. Walikuwa na
anwani inayoonyesha kampuni fulani ya kule Kalifonia, ambayo hujishughulisha na
huduma hizi. Nilibaini kuwa kampuni hii ina malengo ya kuhakikisha kuwa sindano
zote zinatoka mahali pamoja kisha zisambazwe duniani kote.
Niliwauliza kama jambo hili linafanyika
kwa maslahi ya lile Baraza la Ulimwengu
nao wakanithibitishia kuwa hilo ni
kweli. Pia nilitafuta ni wapi hizi sindano zinazotumika kwenye tibavitobo zinakotoka.
Na sasa naweza hata kuwaonyesha nyaraka zinazothibitisha kuwa ni kweli kwamba
kila sindano inatoka kwa makuhani wa kibudha. Kuna kiwanda kikubwa
kinachozizalisha, kisha hao makuhani huzifanyia maombi yao kabla ya kusambazwa
duniani kote. Kwa namna hiyo, ile laana yao inasambaa kote. Tangu wakati wa hizo
sindano kutengenezwa hadi zinapotumiwa kwa mgonjwa, ile sala ya kuhani inakuwa
inafuatana na hiyo sindano.
Nyuma ya matumizi ya hizi sindano ziko
nguvu za kiroho ambazo huathiri aina fulani ya nguvu (energy) ndani ya
mwanadamu na hatimaye kumharibu. Zinaweza kupoza maumivu kwa muda tu lakini
watu wanakuwa chini ya hiyo nguvu. Kwa kifupi ni kuwa sindano hizi zina nguvu za
kipepo na za imani za kipagani za mashariki nyuma yake. Hapa tena shetani
anawadanganya watu na wakati huu anapitia kwenye mgongo wa sayansi. Wakristo
wengi hutumia tiba mbadala, badala ya kukimbilia uponyaji wa Bwana Yesu. Yeye
ni yuleyule, hajabadilika. Nilijua hilo pale nilipokabiliwa na kifo kutokana na
kansa na nimonia nilipokuwa nikiishi kwenye kile kijumba chenye baridi kali.
Nilipomwita Yesu, alikuja kwenye maisha yangu na kuniponya kabisa. Yesu Kristo
ndiye tunayemuhitaji.
Jamhuri ya Cheki hivi sasa inayo fursa
kubwa inayoweza kuitumia, nami ninaomba kuwa muitumie na kwamba New Age
wasilete uovu wao kwenye nchi yenu. Naomba kwamba maisha yenu yawe mikononi mwa
Yesu Kristo; ili muweze kupigana hii vita kubwa kabisa, ambayo si yenu tu bali
ni ya mataifa yote na Wakristo wote. Hatari hiyo kubwa ni kundi la New Age.
Soma ufunuo 21:7-8. Ndiyo, uongo huo upo hapa sasa hivi! New Age yote ni
uchawi; kila kitu kinachohusiana na mambo haya ya giza – yaani imani yao.
Wanataka kumleta Lusifa. Hatuko hapa kuwachukia wao, lakini ni lazima tuuchukie
uongo na udanganyifu huo ambao umewanasa. Fanyeni kazi ya kueneza Injili ambayo
ametuagiza Yesu; leteni wanafunzi kutoka mataifa yote. Asanteni.
Malengo
ya New Age
- Mpango
wenye dondoo kumi na tatu -
Na 1) kuanzisha umoja kwa dunia yote, dini
ya NEW AGE na mfumo wa kisiasa na kijamii unaofanana duniani kote.
Na 2) dini ya dunia, yaani NEW AGE itaimarishwa
kwa kutekeleza ibada ya sanamu iliyokuwa ikifanyika katika Babeli ya zamani,
ambako ndiko zilikoshamiri imani za siri (mystical cults), uchawi, uabudu
shetani na ufisadi (immorality).
Na 3) kuukamilisha mpango pale atakapokuja
masihi wa NEW AGE, Mpingakristo ambaye namba yake ni 666, ambaye atakuja katika
mwili ili kuwaongoza wale wote walioungana katika dini moja ya kilimwengu ya NEW
AGE na kuusimamia huo mpango mpya wa dunia.
Na 4) kuleta dini ya NEW AGE ili
kuwasaidia viongozi wa kiroho (mapepo) kuja na kuandaa njia ya Mpingakristo.
Huyu mtu, ambaye ni mungu wa NEW AGE, atatangazwa kuwa ni Mwalimu mkubwa katika
dunia.
Na 5) kaulimbiu kuu ya hii dini ya
kilimwengu itakuwa ni: “Amani ya dunia!” “Upendo!” na “Umoja!”
Na 6) Mafundisho ya NEW AGE yatafundishwa
na kuenezwa kila mahali duniani kote.
Na 7) viongozi na waumini wa NEW AGE watakuwa
wakisambaza uongo, kwamba Yesu si Mungu wala si Kristo.
Na 8) Ukristo na dini zingine zitakuwa ni
sehemu ya dini ya kilimwengu ya NEW AGE.
Na 9) kanuni za Kikristo ni lazima
zichafuliwe ili watu wazitilie mashaka na kuachana nazo.
Na 10) Watoto ni lazima wadanganywe na
wakiwa mashuleni, wafundishwe mafundisho ya NEW AGE.
Na 11) wadanganyifu wataudanganya
ulimwengu kwa kuuambia kuwa mwanadamu ni mungu.
Na 12) sayansi na dini ya kilimwengu ya NEW
AGE zitaungana pamoja.
Na 13) Wakristo watakaokataa mpango wa NEW
AGE watashughulikiwa. Ikibidi, wataharibiwa na dunia “itasafishwa” – yaani
watauawa ili wasiwepo kabisa.
Hapa chini, nimechagua mafundisho ya aina
kuu tatu ulimwenguni ili kukufanya uelewe zaidi mafundisho ya NEW AGE – Ukristo, uasili [naturalism – ambayo inajumuisha kutoamini mungu kabisa
(atheism) na ubinadamu (humanism)], kisha New
Age. Haya ni makundi matatu ya msingi – kile wanachoamini, misimamo yao na
tofauti kati yao:
UKRISTO
Unaamini yafuatayo:
1) Mungu: anajua yote; ana nguvu zote; ni
Muumbaji wa mwanadamu na ulimwengu.
2) Mwanadamu: aliumbwa na Mungu kwa sura
ya Mungu. Anatakiwa kujikana na kumtukuza Muumba.
3) Kweli: ni thabiti, haibadili, inaweza
kujulikana (yaani, inawezekana kujua jema na baya).
4) Mwongozo
wa mwanadamu na kanuni za maisha: Neno la Mungu Muumba ambaye ameumba vyote. “Ee Bwana, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake;
kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.” (Yer.
10:23)
5) Kristo: ni Yesu, Mzaliwa wa kwanza wa
Mungu, Mwokozi na Bwana wetu.
6) Tatizo la mwanadamu: Chanzo cha dhambi:
kutomfuata Mungu.
Suluhisho: Imani na utii kwa Mungu – Yesu
Kristo.
7) Familia: ilianzishwa na Mungu na
inaongozwa na kanuni za kimaadili. Kwa njia hii, ndoa pamoja na watoto
wanalindwa.
8) Kifo: ni kuingia katika ulimwengu
mwingine, ambako roho inaendelea kuishi milele, ama mbinguni au jehanamu.
9) Malengo: kumfundisha kila mtu kuhusu
Mungu na Yesu Kristo ili kwamba kuwepo na uzima tele sasa na milele.
HITIMISHO:
Mwanzo, Mungu alimuumba mwanadamu kwa sura
yake. Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na
baada ya kufa hukumu (Ebr. 9:27)
UASILI (NATURALISM)
Unaamini yafuatayo:
Na 1) Mungu: hakuna muumba aliye na nguvu
zisizo za kibinadamu. Mawazo kuhusu Mungu yalitokana tu na jamii za zamani
ambazo hazikuwa na ustaarabu wala maendeleo, bali zilijaa ushirikina tu.
Na 2) Mwanadamu: alitokea kwa bahati tu
kutokana na mabadiliko (evolution). Wanamkana Muumba na kujitukuza wao wenyewe.
Na 3)
Kweli: ni jambo linalotegemeana na hali ya mambo; inaweza kubadilika
tena na tena (yaani, kilicho kweli sasa, kinaweza kisiwe kweli baadaye). Kila
mtu kibinafsi ndiye mwenye kuamua kweli ni ipi kwake. Imani yao ni kuwa, “wewe
fanya kile ambacho roho yako inapenda.”
Na 4) Mwongozo wa mwanadamu na kanuni za
maisha: hakuna mamlaka iliyo nje ya mtu; kinachomwongoza mwanadamu ni sayansi
na ufahamu wake binafsi. “Ninawaza. Nina hisia. Niko sawa tu.” Maadili
yanategemeana na hali.
Na 5) Kristo: ni mwalimu, mwanamaadili,
hana asili ya uungu.
Na 6) Matatizo ya mwanadamu: ni matokeo ya
kukosa elimu. Pia ni matokeo ya kuwa na dini.
Suluhisho: maarifa, elimu, kumwelewa
mwanadamu, sayansi na teknolojia.
Na 7) Familia: ni kundi la watu wanaoishi
pamoja; kila mtu yuko huru kuamua juu ya kanuni za kufuata maishani.
Na 8) Kifo: ndio mwisho wa mwanadamu;
hakuna mbingu wala jehanamu.
Na 9) Malengo: kutengeneza jamii timilifu
duniani (utopian society) kupitia serikali ya kijamii ya kilimwengu.
HITIMISHO: mwanadamu ana wema ndani yake.
Wazo la Mungu lilitokana na jamii za kale ambazo hazikuwa na elimu. Mwelimishe
mwanadamu ili ajue kuwa Mungu hayupo.
NEW AGE MOVEMENT
Wanaamini yafuatayo:
Na 1) Mungu: kila mtu na kila kitu ni
mungu.
Na 2) Mwanadamu: ameendelea kimwili,
lakini bado anaendelea kupiga hatua kiroho. Wanamkana Muumba na kujitukuza
wenyewe.
Na 3) Kweli: ufunuo unatoka kwa mtu
mwenyewe au kutoka kwa “viongozi wa kiroho” (spiritual guides). Kwa hiyo, ni
kutoka kwa mwanadamu hadi kwa mwanadamu mwingine.
Na 4) Mwongozo wa mwanadamu na kanuni za
maisha: sayansi na “mungu aliye ndani ya mwanadamu” ndio wanaounda dini. Msingi
wa maamuzi: upendo kwa jirani, umoja wa kilimwengu.
Na 5) Kristo: ni mmoja kati ya wengi,
ambao walileta michango katika mpango wa kiroho.
Na 6) Matatizo ya mwanadamu: yanasababishwa
na utengano kati ya umoja (the oneness) toka kwa kila mmoja na toka kwenye
maumbile ya asili (nature).
SULUHISHO: mabadiliko juu ya ufahamu (consciousness)
katika umoja na “mungu ndani ya moyo wa mwanadamu.”
Na 7) Familia: kutokana na kurudi tena
duniani baada ya kufa (reincarnation), kila roho inachagua familia iitakayo
kabla ya kuzaliwa; na kwa jinsi hii, mafungamano yanakuwa thabiti.
Na 8) Kifo: ni kama kiinimacho tu; ni
kubadilika na kuingia kwenye maisha mengine ya mwili kwa njia ya kuzaliwa kama
kiumbe mwingine (reincarnation).
9) Malengo: kuunda jamii timilifu (utopian
society) kupitia dini ya kilimwengu na serikali moja ya ulimwengu wote.
HITIMISHO: Mungu ni hai kabisa kwa sababu
MIMI MWENYEWE NI MUNGU na ataendelea kuwapo baadaye kupitia maisha ya wanadamu
wengine.
Mpokee Yesu leo.
Kama unahubiri, fanya kazi kwa bidii.
Jungu la uovu linakaribia kumwaga duniani kile ambacho kimekuwa
kinapikwa. Lakini kwa walio ndani ya Yesu, milango ya kuzimu haitaliweza
Kanisa!
………………………………………
Neno la mwisho toka kwa blogger:
Duniani hivi sasa kuna uovu mwingi na
mkubwa na wa kutisha unaoendelea kusukwa na shetani kupitia wanadamu
wanaomtumikia. Lengo ni kushika madaraka ili maamuzi mbalimbali yaweze kufanywa
yanayowanyima watu uhuru wa kumwabudu Kristo ili kwamba giza la kuzimu liweze
ufunika kabisa ufahamu wa mwanadamu. Kristo ndiye NURU pekee kwetu.
Biblia inasema vizuri sana: Ndani yake ndimo ulimokuwa
uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza
halikuiweza. (Yohana 1:4-5).
Lakini liko tatizo moja kubwa:
Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala
ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. (Yoh
1:10-11).
MARANATHA!
………………………………….
Kama ungependa kusoma ushuhuda huu kwa Kiingereza, bofya HAPA. Lakini kwa sasa uko kwenye Word Document ambayo itabidi u-dowload. Utaangalia upande wa chini na kubofya link ya Disciple of a Witch.
Asante sana umenipaisha tena kiroho nitazidi kuhubiri.Ubarikiwe sana.
ReplyDeleteAmen. Ubarikiwe na Bwana na azidi kukupaisha hadi utimilifu wa Kristo kwenye eneo alilokuitia katika Jina la Yesu.
ReplyDeletebarikiwa sana mtumishi wa mungu ushuhuda huu umenigusa na umenikumbusha sana wakati mungu aliposema nami nikasomee psychology chuo kikuu.....mwanzo nilipata shida sababu kuna aina ya vitabu nilikuwa nikivisoma mungu anizuia kwa namna flani vinaitwa SELF HELP BOOKS....nilichogundua psychology baada kuanza kusoma psychology chuoni ni hivi.....psychology yenye misingi mizuri ni ile ambayo inamkubaliana na neno la mungu (school of thought) lakini kuna baadhi ya wasisi walidiriki hata kusema dini ni moja ya ugonjwa wa akili ambao utatibiwa na psychotherapist mfano Sigmund Freud.....hivyo psychology ipo parts ambayo inamkubali mungu na haina tatizo ila ipo nyingine part kama...Self help books, Telepathy,psychic na nyingine mtumishi wa mungu huyo alizozitaja....kanisa tuwe macho...Bwana Yesu atusaidie
ReplyDelete