Mwanadamu
alivyoumbwa
Tukisoma Biblia kuhusiana
na uumbaji wa mwanadamu, imeandikwa hivi:
Bwana Mungu akamfanya mtu
kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
(Mwanzo 2:7).
Kulingana na andiko hili,
tunajifunza yafuatayo:
(a) Mwanadamu
ana sehemu kuu mbili.
(b) Sehemu
ya kwanza ni mavumbi, yaani mwili unaoonekana
kwa nje na tunaweza kuugusa.
(c) Sehemu
ya pili ni pumzi ya uhai ambayo iko ndani na hatuwezi
kuiona wala kuigusa.
(d) Mavumbi
pamoja na pumzi ya uhai yanaunda nafsi hai.