Kati ya mambo ya
kusikitisha sana ni jinsi wanawake katika nchi za Kiislamu wanavyonyanyaswa na
kukandamizwa. Ni wanadamu ambao Bwana Yesu amewaumba na kuwapa heshima kubwa lakini
maskini wamejikuta katika nchi ambazo Mungu anayeabudiwa huko amewapokonya ile
heshima na kuwatwika mateso makali ambayo hata ni vigumu kueleza. Mungu huyo
amewapa wanaume mamlaka ya kuwafanyia chochote watakacho, lakini bahati mbaya
sana, kile wanaume hawa wanachofanya ni masikitiko matupu.
Wednesday, February 20, 2013
Tuesday, February 19, 2013
Bahasha za Zaka Makanisani Zinatoka Wapi?
Je,
ni huduma kwanza au ni roho kwanza?
Wapendwa nawasalimu katika
jina la Bwana wetu, Yesu Kristo.
Katika safari yetu ya
kiroho tunakutana na mitihani na changamoto mbalimbali ambazo, ama zinatujenga
au, kwa bahati mbaya, wakati mwingine zinatubomoa.
Lakini tunapokutana na
changamoto kutoka kwa watu wasiomjua Mungu, hilo halitusumbui sana, maana
tunajua kuwa kwa hao hilo ni jambo la kawaida. Mtihani mkubwa unakuja pale
tunapopambana nazo kutokea kwa wale wanaomjua Mungu, na hasa kama ni vongozi
wetu wa kiroho.
Nimekuwa nikijiuliza juu
ya suala moja ambalo, nafikiri, limekuwa likifanyika kimazoea zaidi kuliko
kimaandiko. Hili ni suala la ulipaji wa zaka.
Subscribe to:
Posts (Atom)