Wednesday, February 20, 2013

Manyanyaso na Ukandamizaji Mkubwa wa Wanawake Katika Nchi za Kiislamu




Kati ya mambo ya kusikitisha sana ni jinsi wanawake katika nchi za Kiislamu wanavyonyanyaswa na kukandamizwa. Ni wanadamu ambao Bwana Yesu amewaumba na kuwapa heshima kubwa lakini maskini wamejikuta katika nchi ambazo Mungu anayeabudiwa huko amewapokonya ile heshima na kuwatwika mateso makali ambayo hata ni vigumu kueleza. Mungu huyo amewapa wanaume mamlaka ya kuwafanyia chochote watakacho, lakini bahati mbaya sana, kile wanaume hawa wanachofanya ni masikitiko matupu.


Wanawake katika nchi hizi wanapigwa, wananyimwa elimu, wanalazimishwa kuolewa wakiwa na umri mdogo, wanalazimishwa kuolewa na wanaume wasiowachagua wao, na hata wanauawa kinyama.


Kama mambo haya yangekuwa yanafanyika kutokana na masuala ya kimila, hilo ni jambo linaloeleweka kwa sababu zipo mila na desturi nyingi, katika makabila mengi, ambazo tunajua kuwa ni potofu, na ndiyo maana zinasemwa kuwa zimepitwa na wakati; na kila juhudi zinafanywa ili kuzitokomeza. Inaeleweka kuwa washika mila hao wanafanya hivyo kwa kutoelewa. Na asili ya mila hizi potofu ni kutokuwa na elimu sahihi na kutomjua Mungu wa kweli. Ndiyo maana watu hawa wanapoelimishwa, mambo hayo yanakoma.


Lakini hali ya wanawake katika nchi za Kiislamu si hivyo. Ukandamizaji, manyanyazo na mateso haya wanafanyiwa kwa jina la dini na Mungu anayeabudiwa na jamii hizi. Kwa maana nyingine ni kuwa, haya ni mazao au matunda ya Mungu huyo. Kwa hali ya kawaida tungetegemea kuwa Mungu awe ni kimbilio la wale walio na shida, lakini kama Mungu anakuwa ndiye chanzo cha mateso, watu watakimbilia wapi?


Kwa kuwa haya ni mambo yaliyo kinyume na ubinadamu, wapo baadhi ya wanawake wanaojaribu kupaza sauti zao katika jitihada za kupingana na manyanyaso na mateso haya makubwa


Hebu soma zaidi kwa kubofya hapa.

8 comments:

  1. asalaam aleykum,

    ni mara ya kwanza kuiona hii site yako na nimo naiangalia SI KWA JICHO LA kupuuza bali KUONA NINI UMEANDIKA kwani wengi huwa hawapendi UKWELI....amabpo UKWELI hat ikiwa baba ake mtu kauwa atoe ushahidi hivi ndivo KUran Kareem inavyoeleza.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Salim asante kwa kutembelea blog yangu. Asante pia kwa mtazamo wako ulio sahihi kabisa kwamba ukweli unaweza kuwa mzito sana kubeba lakini kwa mtu mkomavu ataukubali ingawaje unamwumiza. Nitafurahi kama utanielimisha pale ambapo nimekosea nami sitasita kukubaliana na ukweli. Karibu tuelimishane na kurekebishana. Mungu akubariki.

      Delete
    2. Nasema..
      mbona blog yako haichukua maandishi kama unavyoandika wewe na mara inajificha nilikuwa nakujibu kutoka na aya ulizotaka kujuwa mara imekwnda invisible kuna tatizo lelote?

      Delete
    3. Kuhusu blog yangu kujificha, Salim sina uhakika ni kwa sababu gani lakini kwa upande wangu sijaweka labda setting yoyote inayokataa aina fulani ya maoni. Mimi ninakaribisha kila aina ya maoni. In fact, nimeiseti kwa namna ambayo upande wa comments sifanyi moderation yoyote. Comment inaingia kama inavyotumwa na mwandishi wake. Huenda kulikuwa na tatizo lingine tu nje yangu. Please, keep trying. Sana ninachojua ni kuwa comments hazitakiwi kuzidi herufi takriban 4000 hivi. Zikizidi inakuwa vizuri uivunje mara mbili au tatu.

      Delete
  2. bbrother
    nasema barua nimekuletea; NASEMA KUWEKA PICHA YA MWANAMKE APIGWA MAWE KUTOA REFERENCE ZA ISLAM sioni kwamba CHRISTIITY haina sheria hizo UNWJUWA VYEMA IMO KATIKA BIBLE jee wewe unaona haya yatendwayo na kundi jingeni lindosari?
    makristo hawaaply kwa nini? na tukisema waislamu wakiapply unakuwa na lakuzungumzi kuonesha ubaya UBAYA ZAIDI NI KWA WASIOFUATE SHERIA ZA KITABU CHAO.
    NAULIZA
    huku kuowa MWAMUME KWA MWAMUME IMO KATIKA BIBLE?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kwenye Biblia adhabu hizi zimo. In fact, ukichunguza kwa makini ni kwamba, amri zilizo kwenye Quran zimetoka kwenye torati iliyo kwenye Biblia. Na jambo hili nimeshaliongelea kwa kina na mara nyingi tu.

      Lakini kwa kifupi ni kwamba, nakuomba usome makala yangu niliyoiita: MAJIBU YANGU KWA IBRABURA – SEHEMU YA 2. Hapo utaona maelezo yangu juu ya kwa nini hatutakiwi kufuata sheria za torati literally.

      Kuhusu wanaume kuoana wao kwa wao, Biblia inasema wazi kuwa: Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti (1 Wakorintho 6:9). Kwa hiyo, Salim, anayefanya hivyo anakuwa yuko kinyume na Neno la Mungu kwenye Biblia.

      Lakini hili ni tofauti na Mwislamu anayempiga mawe mzinzi. Huyu hayuko kinyume na maagizo ya Quran bali anakuwa anatenda sawasawa na quran inavyoagiza.

      Swali linalokuja ni kwamba, Quran inakubali kabisa kwamba Biblia ni Neno la Mungu, ingawaje Biblia haisemi chochote juu ya Quran. Sasa kama Quran inakubaliana na hilo, kwa nini sasa ikachukua ukweli nusu? Je, si Quran inayosema kuwa Injili kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu (Al- Imran 3:2-3; Al- Ahqaf 46:12)? Na je, si Quran inayoagiza wale wanaoiamini kuwa waamini Biblia (Al-Nisa 4:136)?

      Sasa, mbona basi ikaagiza nusu tu ya kile ambacho Biblia inaagiza – yaani watu wapigwe mawe, ilhali utimilifu wa jambo hilo umeachwa?

      Kwa hiyo Salim, I don’t look at people and think of them as Muslims or Christians, but I see them as human beings.

      Being humans, we ALL have ONLY ONE problem - Sin. And sin has ONLY ONE end - Hell. And sin has ONLY ONE solution – the blood sacrifice of Jesus.

      I cannot keep quiet and see you get lost simply because you are Moslem [as I said, I don’t see you that way even though that is how you see yourself]. One day you will understand what this means, Salim.

      And one more thing about killing sinners, we only have just one life, if you kill that sinner, are you not condemning that person to ETERNAL hell because you are denying such a one an opportunity of repentance?

      Would you be ready for that yourself; or are you supporting it because your subconscious assumption tells you that you yourself will never be in such a circumstance?

      Delete
  3. kwa upande wangu ndo mara ya kwanza kupitia blog yako na nimegundua kua hujakomaa katika mambo ya dini na mbaya zaidi unaonyesha ni mvivu wa kufikiri na huna busara.pia hufanyi tathmini ya kina kwa kile unachozungumza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom brother Mohamed. Asante kwa kutembelea blog hii. Asante pia kwa maoni yako.

      Inawezekana kabisa nikawa kama unavyosema - sijakomaa katika dini, ni mvivu wa kufikiri na sina busara, maana watu wa aina hizo wapo (au tupo) hapahapa duniani.

      Naamini kuwa sitakuwa peke yangu mwenye mitazamo ya namna hii. Naamini pia hii ni fursa mojawapo ya wewe kutusahihisha na kutusaidia kuwa katika mstari ule ambao unaamini kuwa ni sahihi. Tafadhali tusaidie tu. Mungu akubariki.

      Delete