Utangulizi kutoka kwa blogger
Je, unahisi kuwa una huzuni kubwa isiyoweza kuondoka, umekata tama,
unajiona huna maana, unahisi kama vile Mungu amekudanganya au amekuacha;
unahisi kama vile Mungu si wa kuaminiwa
au Neno lake si la kuaminiwa, unahisi kuwa Mungu hasikii maombi yako, hakupendi;
unahisi kwamba umeshapoteza wokovu wako, au unahisi kuwa umetenda sana dhambi
kiasi kwamba Mungu hawezi kukusamehe tena?
Napenda nikuletee habari njema kwamba, bado liko tumaini, tena kubwa
sana kwa ajili yako. Karibu usome ushuhuda huu ambao, si tu ni ushuhuda wa
mpendwa aliyepita kwenye mapito kama hayo, lakini pia ni somo zuri mno kiasi
kwamba, kama kawaida, Mungu anayo mengi ya kutufundisha kupitia mambo ambayo
wengine walipitia kama sisi na wakashinda kwa neema ya Mungu ambayo iko kwa
ajili ya kila mwanadamu, ukiwamo na wewe. Pendo la Mungu ni zaidi ya maji ya
bahari, hivyo hakika kabisa unayo sehemu yako humo ambayo inakungoja uingie na
kupokea.