Friday, March 30, 2012

Kumkabili Goliati Maishani



MUNGU wa mbinguni huzungumza sana kwa mifano kuliko kwa lugha ya kawaida; ya moja kwa moja. Na mfano mkubwa kabisa ni maisha ya Waisraeli. Maisha yao kwa ujumla wake yalikusudiwa kuwa mfano kwa ajili yetu sisi watu wa leo.

Monday, March 26, 2012

Jinsi ya Kuenenda kwa Roho



Maandiko yanasema kwamba: Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. (Warumi 8:6-7).

Ndugu, yapo mashindano makali sana ndani mwetu ambayo yanaendelea kila dakika ya maisha yetu. Mwili unataka hivi na roho inataka vile. Wewe na mimi tuko hapo katikati. Uamuzi unatoka kwetu – ama kufuata mwili au kufuata roho!