Saturday, November 24, 2012

Mwana Mpotevu




Hadithi ya mwana mpotevu inafahamika kwa wasomaji wa Biblia. Vilevile, inafahamika kwa habari ya uhusiano wake na mtu yeyote asiyeokoka; yaani mwana mpotevu anawakilisha watu ambao hawajaamua kumpokea Kristo awe Bwana na Mwokozi wao binafsi. Hadithi hii inaashiria jinsi ambavyo Mungu amempa mtu wa aina hiyo uzima, afya na baraka nyinginezo, lakini badala ya kukaa nyumbani mwa Baba, ameamua kwenda kule duniani na kuishi maisha ya utapanyaji. Hata hivyo, pale anapotambua kuwa amepotea na kuamua kurudi kwa Baba, muda wote Baba yuko tayari kumpokea kwa furaha na upendo mwingi. Sote tuko hivyo. Hapo ndiko tunakoanzia.

Sunday, November 4, 2012

Kuteswa kwa Ajili ya Kristo





Tunaweza kufikiri kuwa tunapita kwenye hali ngumu maishani mwetu. Lakini mara nyingi huwa tunanung’unika tu kwa sababu hatuna nguo, fedha au chakula.

Lakini wapo watakatifu wa Bwana ambao wamepitia mateso mengi kutokana na ushuhuda wao kwa Kristo, Bwana wetu. Ni kwa sababu walimwamini Kristo, matokeo yake wakajikuta kwenye mateso.

Hata leo wapo Wakristo wengi duniani ambao wanateseka kutokana na imani yao kwa Mwokozi. Lakini kwa neema ya Bwana, wameng’ang’ania imani hii.

Majibu ya Ndugu Hamudi - Sehemu ya III


Leo ningependa kuendelea na kujibu maswali ya ndugu yetu Hamudi ambayo aliuliza kufuatia makala niliyoandika katika blog hii, yenye kichwa kisemacho Ndugu Waislamu Nisaidieni.


ROHO MTAKATIFU


Hamudi anauliza: Sehemu pekee katika Biblia alipotajwa Roho Mtakatifu ni katika Yohana 14:26; “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote niliyowaambia. Ni kipi kile ambacho Roho Mtakatifu ameleta au kufundisha kwa miaka 2000 iliyopita?