Sunday, May 27, 2012

Je, Sabato Ni Siku Katika Juma?



Sabato ilianzia wakati wa uumbaji ambapo baada ya siku sita za uumbaji, Mungu alipumzika siku ya saba. 

Imeandikwa: Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya, akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. (Mwa. 2:2-3).

Hatimaye ulifika wakati ambapo Mungu aliwatoa wana wa Israeli kutoka utumwani Misri; ndipo aliwapa amri juu ya sabato. 

Monday, May 21, 2012

Furaha Katika Roho Mtakatifu



Mara kadhaa nimesikia watu wakisema, “Nikienda kanisani najisikia raha kweli; lakini nikitoka, hali ya uzito wa moyo inanirudia tena.”
Ndugu, Biblia inasema: Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Rum. 14:17).

Hebu tujiulize swali hapa. Sehemu nyingine tunaposoma, Bwana anasema kwamba:

  • Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo. Mimi nimeushinda ulimwengu. (Yohana 16:33)
  • Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. (Mt. 10:22);

Sunday, May 13, 2012

Kuishi Maisha ya Aina Mbili


UTANGULIZI

Mwandishi mmoja alimwuliza Bwana Yesu: Katika amri zote ni ipi iliyo kuu? (Mk. 12:28).

Bwana alimjibu: Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. (Mk. 12:29-30). Hicho ndicho kipimo cha utimilifu wa utii.