==== SIKU YA 20 ==== (Matendo 1:8)
* Kim, Joo-Eun
ayashambulia mapepo!
Mchungaji alituambia tusiyaogope
mapepo, bali tuyashambulie moja kwa moja. Alisema kwa ujasiri, “Yakanyageni
na yapeni uchungu! Ng’oeni macho yao na myapondeponde. Yakamateni na kuyatikisa
mahali pote.” Ilikuwa inafurahisha na ilitupa nguvu sana. Kwa kuwa huwa
ninaogopa kirahisi, mchungaji aliniambia nisionyeshe kabisa woga vinginevyo
mapepo yatashambulia zaidi. Niliamua kuwa imara.
Pepo la kwanza nililoliona lilikuwa ni lile ninaloliogopa zaidi. Lilikuwa ni pepo la kike linalovaa gauni jeupe. Lilisababisha mwili wangu kusisimuka wakati linakuja huku likipiga kelele za kutisha. Nilikuwa na wasiwasi, lakini nikakusanya nguvu zangu zote. Nikashika nywele zake na kuzivuta. (Marko 9:23) Likalia, “Aaaa! Niachie! Unaniumiza. Niachie mara moja! Naumia!” Nilivuta bila huruma hadi nywele zake zote zikang’oka. Likalia, “Nywele zangu! Nywele zangu! Kisha likatoweka.
Pepo la kiume lenye kichwa kikubwa lilijaribu kunitisha. Lilinijia huku limepanua kinywa chake. Nilichana hicho kinywa chake na kung’oa macho yake na kuyakanyagakanyaga. Likalia, “Aaah! Macho yangu! Mdomo wangu! Viko wapi? Nitafutieni! Inauma!” Likaanza kuhangaika kutafuta sakafuni lakini halikuona, likaamua kutoweka.
Baada ya hapo pepo lenye jicho kama nusu mwezi lilikuja. Nilichanachana mwili wake vipandevipande na kulipigia kelele. Likakusanya vipande hivyo na kukimbia huku likisema, “Nitakurudia tena. Utaona!”
*
Mikutano ya kipepo na maombi kwa ajili ya silaha za kimbingu
Baadaye, wakati nikiomba, nilisikia
kundi la mapepo likiongea kwenye kona. Niliona mapepo takribani 30 yamekaa
duara yakifanya mkutano. Pepo kiongozi lilisema, “Mtaliacha
Kanisa la Bwana hivihivi? Harakisheni mharibu umakini wao katika kuomba.
Fanyeni jambo enyi wajinga!” Pepo jingine likasema, “Mnamjua yule msichana wa sura mbaya, Joo-Eun? Huyo
msichana anayeitwa Ufuta! Hivi si ni aibu kushindwa na mtu kama huyo?” Na
jingine likapaza sauti, “Vipi kuhusu mimi? Mdomo
wangu ulichanwa! Nilikuwa natoka damu sana.” Jingine likasema, “Ninyi, yaani mlichosema wala si lolote! Mimi nimepoteza
nywele zangu na sasa ni kipara kitupu! Sasa tufanyeje?”
Baadaye, pepo lenye fuvu
lilinishambulia. Kwa hiyo, kwa haraka nikaomba, “Bwana, nipe shoka!” Ghafla,
kukawa na shoka pembeni yangu. Pepo liliponijia, nikachukua shoka lile na
kulipiga kichwani hadi fuvu lote likapasuka vipandevipande.
Lee, Yoo-Kyung: * Yoo-Kyung ashambulia mapepo!
Leo, mara baada ya kuanza kuomba, pepo
la kike lililovaa gauni jeupe lilitokea. Lilikuwa na meno kama ya drakula na
mdomo uliojaa damu. Kwa kuwa halikukimbia baada ya kulikemea, niliamua
kulikamata nywele zake na kulitikisa kwa nguvu, huku nikilizungusha. “Aaaah! Achia nywele zangu. Niachie sasa hivi! Tafadhali!”
lilia. Nilijisikia kutiwa nguvu zaidi. Nikasema, “Ewe pepo mchafu, nimekuwa
nakuogopa sana hadi sasa! Sasa ni zamu yako kukipata unachostahili!” Nililizungusha
mfululizo, huku nikivuta nywele zake na likalia, “Ukifa,
nitahakikisha nakukokota hadi kuzimu!” Baada ya hapo likaondoka.
Pepo lenye kipara lilinijia.
Nililikamata na kulikandamiza chini kwenye shingo yake. “Aaagh! Ninakufa hapa. Acha kunikandamiza kichwa!” lilipiga
kelele. Nilikuwa najisikia raha sana. Nilikandamiza hata zaidi hadi likapasuka.
Kisha nikalitandika ngumi hadi likaenda kuangukia kwenye kona.
Wakati naendelea kuomba, Yesu alitokea
na kuniambia, “Mpendwa
wangu Yoo-Kyung, imani yako imekua sana. Unaweza kuyaumiza mapepo kwa mkono
wako sasa.” Alitabasamu. Nikasema, “Yesu, nataka kuenda
Mbinguni!” Akasisitiza kwamba tukatembelee kuzimu.
Tulipofika kuzimu, tulienda kwenye
sehemu ambako kulikuwa na sufuria kubwa la chuma, jekundu kutokana joto la
moto. Yesu akasema, “Yoo-Kyung,
angalia kwa makini ndani ya sufuria uone nani yumo humo.” Niliangalia
kwa makini na nikamwona bibi yangu yumo ndani, pamoja na mwanamume mwingine.
Walikuwa wakirukaruka huku wakipiga kelele “Aaah! Tafadhali, kuna joto kali
sana humu!”
Bibi yangu aliponiona, akasema, “Yoo-Kyung,
siwezi kustahimili joto hili zaidi! Tafadhali msaidie bibi yako. Mwombe Bwana
anisaidie kutoka humu.” Hakujua cha kufanya. Alikuwa akikimbia huku na huku
kama kwa wazimu. Nguo yake nyeupe ilikuwa inawaka moto. Bibi yangu alipaza
sauti, “Yoo-Kyung, nafurahi kwamba uko hapa. Tafadhali, nakuomba unitoe
hapa! Siwezi kuvumilia joto hili tena.” Nilijaribu kumtoa kwa kunyoosha
mkono wangu, lakini Bwana alinikumbusha kwa msisitizo mkubwa kwamba
nisingeweza. “Yesu, moyo wangu unaumia kumuona kwenye maumivu makali kiasi
hiki. Nifanye nini sasa?” nililia.
Yesu alinikumbatia kwa nguvu na kufuta machozi yangu. Tulianza kuondoka,
lakini mapepo ya kutisha yakatokea mbele yetu. Yesu akapaza sauti akisema,
“Mkimsumbua Joo-Eun au
Yoo-Kyung, nitawatupa mara moja kwenye shimo la moto Kuzimu!” Liliinamisha
kichwa chake na kutoweka. Yesu alinishika mkono na kuniongoza kurudi kanisani
na yeye akarudi Mbinguni.
Lee, Haak-Sung: * Pepo lenye kinyago cha chuma
Wakati nikiomba, pepo la kiume
lililojaa misuli na limevaa kinyago
cheupe cha chuma usoni lilianza kutikisa upanga mkubwa kuelekea kwangu.
Sikuogopa. Badala yake nilikamata
upanga wake na kulipiga kichwani kwa upanga huo. Nikawa nasikia chuma kwa chuma
vikigongana kwa sauti. Nikatoa kinyago chake na nikaona mafunza yanayotia
kinyaa yamejaa usoni kwake.
Baada ya muda kidogo, pepo lenye pembe
kila sehemu lilikuja limebeba ubao mkubwa mweusi. Likasema, “Acha kuomba. Acha kuomba!” Sikulijali na
nikaendea kuomba kwa kunena kwa lugha. Likaanza
kukwaruza ule ubao. Sikuweza kuvumilia kelele zake. Nikaziba masikio yangu na
kusema kwa sauti, “Shetani, kwa Jina la Yesu, toweka!” Liliendelea tu
kukwaruza ubao ule huku likisema, “Yaani,
raha kwelikweli!” Nikapaza sauti, “Yesu, tafadhali nisaidie.
Pepo hili ovu linanitesa!” Yesu akatokea kwenye mwanga na pepo lile
likakimbia bila hata kugeuka nyuma.
Pepo jingine lilitokea ambalo lilikuwa
linafuka moshi. Mara ule moshi ukawa na umbo la binadamu. Niliweza kuona watu wamenaswa ndani ya ule
moshi, wakiomba msaada. Nilitambua kuwa pepo hili lilikuwa limemeza watu.
Nikaanza kuomba kwa kunena, huku nikimwita Yesu. “Yesu, nisaidie! Pepo
linataka kunimeza. Fanya haraka unisaidie!” Nilipoita hivyo, Bwana akatokea mara moja na kuyaharibu mapepo yale.
No comments:
Post a Comment