Monday, December 11, 2017

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 11


 
==== SIKU YA 20 ==== (Matendo 1:8)
* Kim, Joo-Eun ayashambulia mapepo!
Mchungaji alituambia tusiyaogope mapepo, bali tuyashambulie moja kwa moja. Alisema kwa ujasiri, “Yakanyageni na yapeni uchungu! Ng’oeni macho yao na myapondeponde. Yakamateni na kuyatikisa mahali pote.” Ilikuwa inafurahisha na ilitupa nguvu sana. Kwa kuwa huwa ninaogopa kirahisi, mchungaji aliniambia nisionyeshe kabisa woga vinginevyo mapepo yatashambulia zaidi. Niliamua kuwa imara.

Pepo la kwanza nililoliona lilikuwa ni lile ninaloliogopa zaidi. Lilikuwa ni pepo la kike linalovaa gauni jeupe. Lilisababisha mwili wangu kusisimuka wakati linakuja huku likipiga kelele za kutisha. Nilikuwa na wasiwasi, lakini nikakusanya nguvu zangu zote. Nikashika nywele zake na kuzivuta. (Marko 9:23) Likalia, “Aaaa! Niachie! Unaniumiza. Niachie mara moja! Naumia!” Nilivuta bila huruma hadi nywele zake zote zikang’oka. Likalia, “Nywele zangu! Nywele zangu! Kisha likatoweka.

Pepo la kiume lenye kichwa kikubwa lilijaribu kunitisha. Lilinijia huku limepanua kinywa chake. Nilichana hicho kinywa chake na kung’oa macho yake na kuyakanyagakanyaga. Likalia, “Aaah! Macho yangu! Mdomo wangu! Viko wapi? Nitafutieni! Inauma!” Likaanza kuhangaika kutafuta sakafuni lakini halikuona, likaamua kutoweka.

Baada ya hapo pepo lenye jicho kama nusu mwezi lilikuja. Nilichanachana mwili wake vipandevipande na kulipigia kelele. Likakusanya vipande hivyo na kukimbia huku likisema, “Nitakurudia tena. Utaona!”
* Mikutano ya kipepo na maombi kwa ajili ya silaha za kimbingu

Baadaye, wakati nikiomba, nilisikia kundi la mapepo likiongea kwenye kona. Niliona mapepo takribani 30 yamekaa duara yakifanya mkutano. Pepo kiongozi lilisema, “Mtaliacha Kanisa la Bwana hivihivi? Harakisheni mharibu umakini wao katika kuomba. Fanyeni jambo enyi wajinga!” Pepo jingine likasema, “Mnamjua yule msichana wa sura mbaya, Joo-Eun? Huyo msichana anayeitwa Ufuta! Hivi si ni aibu kushindwa na mtu kama huyo?” Na jingine likapaza sauti, “Vipi kuhusu mimi? Mdomo wangu ulichanwa! Nilikuwa natoka damu sana.” Jingine likasema, “Ninyi, yaani mlichosema wala si lolote! Mimi nimepoteza nywele zangu na sasa ni kipara kitupu! Sasa tufanyeje?”

Baadaye, pepo lenye fuvu lilinishambulia. Kwa hiyo, kwa haraka nikaomba, “Bwana, nipe shoka!” Ghafla, kukawa na shoka pembeni yangu. Pepo liliponijia, nikachukua shoka lile na kulipiga kichwani hadi fuvu lote likapasuka vipandevipande.

Lee, Yoo-Kyung: * Yoo-Kyung ashambulia mapepo!
Leo, mara baada ya kuanza kuomba, pepo la kike lililovaa gauni jeupe lilitokea. Lilikuwa na meno kama ya drakula na mdomo uliojaa damu. Kwa kuwa halikukimbia baada ya kulikemea, niliamua kulikamata nywele zake na kulitikisa kwa nguvu, huku nikilizungusha. “Aaaah! Achia nywele zangu. Niachie sasa hivi! Tafadhali!” lilia. Nilijisikia kutiwa nguvu zaidi. Nikasema, “Ewe pepo mchafu, nimekuwa nakuogopa sana hadi sasa! Sasa ni zamu yako kukipata unachostahili!” Nililizungusha mfululizo, huku nikivuta nywele zake na likalia, “Ukifa, nitahakikisha nakukokota hadi kuzimu!” Baada ya hapo likaondoka.

Pepo lenye kipara lilinijia. Nililikamata na kulikandamiza chini kwenye shingo yake. “Aaagh! Ninakufa hapa. Acha kunikandamiza kichwa!” lilipiga kelele. Nilikuwa najisikia raha sana. Nilikandamiza hata zaidi hadi likapasuka. Kisha nikalitandika ngumi hadi likaenda kuangukia kwenye kona.


Wakati naendelea kuomba, Yesu alitokea na kuniambia, “Mpendwa wangu Yoo-Kyung, imani yako imekua sana. Unaweza kuyaumiza mapepo kwa mkono wako sasa.” Alitabasamu. Nikasema, “Yesu, nataka kuenda Mbinguni!” Akasisitiza kwamba tukatembelee kuzimu.

Tulipofika kuzimu, tulienda kwenye sehemu ambako kulikuwa na sufuria kubwa la chuma, jekundu kutokana joto la moto. Yesu akasema, “Yoo-Kyung, angalia kwa makini ndani ya sufuria uone nani yumo humo.” Niliangalia kwa makini na nikamwona bibi yangu yumo ndani, pamoja na mwanamume mwingine. Walikuwa wakirukaruka huku wakipiga kelele “Aaah! Tafadhali, kuna joto kali sana humu!”

Bibi yangu aliponiona, akasema, “Yoo-Kyung, siwezi kustahimili joto hili zaidi! Tafadhali msaidie bibi yako. Mwombe Bwana anisaidie kutoka humu.” Hakujua cha kufanya. Alikuwa akikimbia huku na huku kama kwa wazimu. Nguo yake nyeupe ilikuwa inawaka moto. Bibi yangu alipaza sauti, “Yoo-Kyung, nafurahi kwamba uko hapa. Tafadhali, nakuomba unitoe hapa! Siwezi kuvumilia joto hili tena.” Nilijaribu kumtoa kwa kunyoosha mkono wangu, lakini Bwana alinikumbusha kwa msisitizo mkubwa kwamba nisingeweza. “Yesu, moyo wangu unaumia kumuona kwenye maumivu makali kiasi hiki. Nifanye nini sasa?” nililia. Yesu alinikumbatia kwa nguvu na kufuta machozi yangu. Tulianza kuondoka, lakini mapepo ya kutisha yakatokea mbele yetu. Yesu akapaza sauti akisema, “Mkimsumbua Joo-Eun au Yoo-Kyung, nitawatupa mara moja kwenye shimo la moto Kuzimu!” Liliinamisha kichwa chake na kutoweka. Yesu alinishika mkono na kuniongoza kurudi kanisani na yeye akarudi Mbinguni.

Lee, Haak-Sung: * Pepo lenye kinyago cha chuma
Wakati nikiomba, pepo la kiume lililojaa misuli  na limevaa kinyago cheupe cha chuma usoni lilianza kutikisa upanga mkubwa kuelekea kwangu.

Sikuogopa. Badala yake nilikamata upanga wake na kulipiga kichwani kwa upanga huo. Nikawa nasikia chuma kwa chuma vikigongana kwa sauti. Nikatoa kinyago chake na nikaona mafunza yanayotia kinyaa yamejaa usoni kwake.

Baada ya muda kidogo, pepo lenye pembe kila sehemu lilikuja limebeba ubao mkubwa mweusi. Likasema, “Acha kuomba. Acha kuomba!” Sikulijali na nikaendea kuomba kwa kunena kwa lugha.  Likaanza kukwaruza ule ubao. Sikuweza kuvumilia kelele zake. Nikaziba masikio yangu na kusema kwa sauti, “Shetani, kwa Jina la Yesu, toweka!” Liliendelea tu kukwaruza ubao ule huku likisema, “Yaani, raha kwelikweli!” Nikapaza sauti, “Yesu, tafadhali nisaidie. Pepo hili ovu linanitesa!” Yesu akatokea kwenye mwanga na pepo lile likakimbia bila hata kugeuka nyuma.

Pepo jingine lilitokea ambalo lilikuwa linafuka moshi. Mara ule moshi ukawa na umbo la binadamu.  Niliweza kuona watu wamenaswa ndani ya ule moshi, wakiomba msaada. Nilitambua kuwa pepo hili lilikuwa limemeza watu. Nikaanza kuomba kwa kunena, huku nikimwita Yesu. “Yesu, nisaidie! Pepo linataka kunimeza. Fanya haraka unisaidie!” Nilipoita hivyo, Bwana akatokea mara moja na kuyaharibu mapepo yale.

No comments:

Post a Comment