==== SIKU YA 22
==== (1 Petro 1:6-9) * Pepo linapiga kinanda
Lee Yoo Kyung
Lee Yoo Kyung
Nilipokuwa
nikiomba, pepo lenye uso mweusi na macho manne lilikuja na kukaa kwenye kiti
cha mpiga kinanda. Likaanza kuhangaika pale huku likijaribu kupiga kinanda.
Huku nikiwa nimekereka, nilipaza sauti na kusema, “Ewe pepo mchafu! Kwa nini
unachezea kinanda cha dada yangu Joo Eun? Kinanda hicho huwa anakitumia wakati
wa ibada za kuabudu.” Likanitukana na kuniambia nifumbe kinywa changu. Kwa
hiyo nikajawa na hasira. “Nini? Unanionyesha dharau? Wewe umekufa!”
Nikalikimbilia na kulikamata. Nikanyonga shingo yake na kupigiza kichwa chake
chini sakafuni.
Mapepo
matatu zaidi yakatokea. Moja lilikuwa kwa umbo la mifupa tu na lilikuwa na
jicho usoni. Lilikuwa likiruka huku na kule kwa mbawa zake kama popo. Nalo
likaenda kukaa kwenye kiti cha kinanda na kuanza kuimba huku likipiga kinanda.
Sauti yake ilikuwa mbaya na muziki wake wala haufuati mapigo ya kimuziki.
“Wewe,
hicho ni kinanda cha Joo Eun. Kwa nini unakigusa? Unasababisha siwezi
kuzingatia maombi yangu!” nilisema kwa sauti. Nikawa nayasikia
yakiongeleshana, “Hawezi kuwa mzingativu.
Tuendelee kupiga kinanda zaidi na zaidi.” Yote yakaanza kubonyeza
kinanda kwa fujo kwa pamoja. Nilihofia kinanda kingeweza kuvunjika. Nikayaambia,
“Ni wazi nyie hamuwezi kunisikiliza.” Nikayakimbilia na kuyakamata yote
kwa mara moja, huku nikiyapiga mateke na kuyazungusha. Huku pua zao zikiwa
zinatoka damu na vichwa vyao vimeumia, yalipiga kelele na kukimbia.
Nikaanza
kuomba tena. Likaja pepo lililovaa vazi jeupe huku mdomo wake unatoka damu.
Lilionekana lina ulemavu huku halina macho, kwa hiyo nikalidhihaki. Likasema, “Haak Sung aling’oa macho yangu. Ndio maana niko hivi. Kwa
nini nyie wawili mnacheka?” Lilikuwa linajaribu kuzua ugomvi na
mimi. Kwa sauti, nikasema, “Bibi yangu anateseka kwa sababu yenu! Kwa nini
alitupwa Kuzimu?” Pepo lile likanidhihaki na kunikera. “Kuzimu ndio mahali pake. Anastahili kuwa pale. Atateswa
hata zaidi.” Kwa hasira, nikaliparua usoni kwa nguvu zangu
zote. Likaanza kuvuja damu nyingi sana na likakimbia.
Nikaanza
kuomba tena, kisha nikaanza kusumbuliwa na pepo jingine. Niliudhika lakini
sikutaka kwenda kulikabili. Nikaamua kutumia mamlaka yangu kwa kusema, “Damu
ya Yesu.” Lakini lenyewe likajibu, “Damu? Damu
ya nani? Damu ya Yesu? Ahaa, damu yako?” “Sawa, kama unatafuta
ugomvi, sogea. Njoo tupigane!” nikasema kwa sauti. Mapepo yakashambulia kwa
makundi, lakini kwa namna fulani, kila nilipotupa mkono wangu, yote yanaanguka
kama kundi. Nikiyapiga tumboni, macho yao yanapasuka. Nikipiyaga puani, pua zao
zinaanza kutoka damu. Nikakamata miguu yao na kuanza kuyazungusha juu. Miguu
hiyo ilikuwa inavutika kama mpira.
Licha
ya kuyatia hasara, yaliendelea kuja na kunighasi. Yalikuwa yanajaribu kunizuia
kuomba. Nikawaza, “Acha tupambane tuone nani atashinda.” Nilitia vidole
puani mwao na kukamata nywele za pepo lolote lililonisogelea karibu. Nilitumia
mikono na miguu yangu kama silaha. Ilishangaza kwamba kila nilivyoendelea
kuyashinda, idadi yao ikawa inaongezeka. Karibu na mwisho, kukawa na mapepo mengi,
mengi sana yasiyohesabika! Yote yalikuja kwa pamoja. Kwa uharaka, nikapaza
sauti “Nisaidie! Harakisha, Roho Mtakatifu! Nisaidie!” Kufumba na
kufumbua, Bwana akatokea. Bwana akayakemea mapepo yale na akanifariji, kwa
kusema, “Bi Madoa (Miss Speckle)! Najua
umekutana na mtihani mkubwa.”
Mwanzoni
nilipokuwa nahudhuria kwenye makanisa mengine, watu wengi waliniambia mara
nyingi kuwa mimi sikuwa na akili za kutosha. Badala ya kunifundisha namna ya
kuomba na kufanya uinjilisti, walinipa tu chakula. Walijaribu tu kunisaidia kwa
mahitaji ya kimwili. Kwa hiyo, nilidhani kuwa mimi nilikuwa mtu wa kubeba tu
Biblia na kwenda kwenye ibada. Lakini kwa mwongozo wa mchungaji wa kwenye
Kanisa la Bwana (Lord’s church), nilianza kunena kwa lugha. Kadiri
nilivyoendelea kunena kwa lugha, niliweza kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuomba.
Sasa naweza kuyaona mapepo na ninaweza
kupambana nayo. Kila ninapojisikia kama nashindwa kwenye mapambano,
ninachofanya tu ni kuliitia Jina la Bwana Yesu. Yeye hunilinda kila wakati.
Mwanzoni, nilikuwa naogopeshwa sana na mashambulizi ya mapepo mengi. Lakini
hivi sasa siogopi tena, maana Yesu yuko pamoja nami. Kwanza ushindi
ninaopata dhidi ya mapepo umekuwa ni jambo la kuburudisha na kufurahisha.
Kim
Joo Eun: * Mapepo yenye vipara
yatokea
Leo,
pepo jingine lililojifanya kama msichana lilitokea huku limeachama mdomo.
Nilimwaga hasira yangu kwake, nikalizaba kibao kwa nguvu sana hadi likavimba
kwenye shavu. Nikasema kwa sauti, “Ulimpiga kibao dada Yoo Kyung shavuni,
sawa? Utaadhibiwa hata zaidi. Nitakupiga zaidi!” Likalia, “Nisamehe. Sitampiga Yoo Kyung tena. Kweli kabisa!” Nikasema,
“Ndio. Wewe ni mwongo kwa asili yako.” Nikang’oa nywele zake zote
na kulitupa chini ya kinanda. Kisha nikaona pepo lenye fuvu lenye nywele ndefu
nyeupe na macho ya rangi ya machungwa. Nikayachoma macho yake na likaanza
kurukaruka kwa mahangaiko kutokana na maumivu makali hadi likakimbia.
*
Makanisa Yashindayo
Kadiri
nilivyoendelea kuomba, nilihisi kuna harufu nzuri kama ya maua hewani. Bwana
akatokea. Kwa hiyo nikamwuliza, “Bwana,
hii harufu nzuri hivi inatoka kwako?” Bwana akajibu, “Ndiyo, Madoa. Umeipenda harufu hiyo?” Kwa
furaha nikajibu, “Ndiyo Bwana. Ni nzuri sana.” Yesu akaniambia, “Leo unaomba kwa bidii kweli. Nitakuonyesha kitu maalum.
Angalia kwa makini hali ya kanisa lako na makanisa ya Korea.” Mara
Bwana alipoinua mkono wake, nikapewa maono. Nikaonyeshwa dunia kwa mbali huku
kukiwa na mapepo mawili upande huu na huu. Yalikuwa yanazungusha kamba kuzunguka
dunia yote kama kwenye mchezo wa rede. Nilipotazama kwa makini, nikaona kwamba
ile kamba ilikuwa ni joka refu. Kadiri yalivyozungusha ile kamba, nikaona
makanisa mengi ya Korea yakiruka kila kamba ilipoyafikia. Yaliruka na kuruka,
huku yakijaribu kujizuia kuanguka. Mengi ya makanisa hayakuanguka mwanzoni,
lakini mizunguko ilivyoendelea, yalijikwaa na kuanguka. Nikaona hata kanisa
letu likiruka. Sisi hatukujikwaa au kuangushwa na lile joka.
Yesu
akasema kuwa kila mzunguko kutoka kwenye yale mapepo ni jaribu linalotakiwa
tulishinde. Kama kanisa halikujikwaa na kuanguka, ina maana limeshinda jaribu
husika. Kanisa la Bwana (The Lord’s church) lilikuwa na idadi ndogo ya
washirika kuliko yote. Makanisa mengine yalikuwa na watu wengi zaidi, lakini
mara kwa mara yalijikwaa na kuanguka. Yesu akasema, “Kanisa la Bwana linashinda kwa nguvu sana. Endeleeni
kustahimili na kuruka kadiri majaribu mbalimbali yanavyokuja kwenu. Leo,
umeomba kwa muda mrefu sana bila kusinzia. Ndio maana nimekuonyesha haya. Omba
kwa bidii.”
Lee
Haak Sung: * Mapepo
yanayofanana na picha za kwenye mambo ya burudani
Nilipokuwa
naendelea kuomba, pepo moja likanijia. Nilikuwa na hasira sana wakati huo baada
ya kumwona bibi yangu Kuzimu kiasi kwamba nilizimwaga hasira zangu zote kwa
pepo hilo. Niliyachoma macho yake na kuyanyofoa kisha nikayatupia kule. Wakati
wa mapambano haya, nilianza kuwaza kuhusu upanga, na mara upanga ukatokea
mkononi mwangu. Nikafyeka mikono yake. Kila nilipowaza tu kutumia silaha
nyingine, mara ilitokea ama mkononi mwangu au pembeni yangu. Bwana alinipatia
silaha hizi kila nilipoziomba. Nilikuwa nimeshapigana kwa muda mrefu na kuwa na
uzoefu mkubwa bila mimi kujua. Pia nilikuwa nimeshajaa ujasiri na kujiamini.
Pepo
lililojifanya kama binti aliyevaa gauni jeupe likanijia. Lilionekana limefanana
sana na picha (katuni) za kwenye sinema za kutisha. Nilishangaa sana kuona
jinsi lilivyofanana na mojawapo wa wahusika waliobuniwa kwenye tasnia ya
burudani! Hili lilikuwa linafanana kabisa na mojawapo wa wahusika kwa kwenye
filamu moja maarufu ya TV ya Korea ambaye kazi yake ni kuzikokota roho za watu hadi
Kuzimu baada ya kufa. Kwenye maono yale, nikaona mzee mmoja akiwa amelala
sakafuni huku akivuja damu chini ya madhabahu. Huku likimshambulia mzee yule,
pepo lile lilitumia meno yake ya ki-drakula kufyonza damu yake. Baada ya damu
kwisha, lilianza kumla.
*
Mchomo wa sindano ya pepo
Pepo
jingine lilitokea likiwa na mwili kama wa karunguyeye au nungunungu uliojaa
sindano kila sehemu. Nikatupa ngumi yangu kwake. Nilipoligusa tu, nikahisi
maumivu makali sana ya kuchomwa na sindano. Hata baada ya siku za maombi yetu
kwisha, bado mkono wangu ulikuwa na maumivu, ulikuwa mwekundu na umevimba huku
ukiwa na alama za zile sindano. Nilishangaa sana kwamba iliwezekanaje jambo la
kiroho kuacha alama kabisa za kuonekana na maumivu kabisa ya kimwili!
Pastor
Kim Yong Doo: * Kujongea
na kutetemeka kwa mikono
Nilivyoomba
kwa kunena kwa bidii, mikono yangu ikaanza kusogea kidogokidogo juu na chini.
Mara viganja vyangu vikageukiana na kutikisika kwa nguvu, huku mitetemo ikizidi
kadiri muda ulivyoendelea. Nakumbuka niliwahi kumwona mchungaji mmoja alipokuwa
akifanya maombezi kwa watu. Mikono yake nayo ilikuwa inatetemeka. Wakati mikono
yake ikitetemeka hivyo, miujiza mingi ilitendeka. Nikawaza kuwa lazima na mimi
nitakuwa nakaribia kuwa na karama ya uponyaji kama yeye. Mikono yangu ikawa
inajiendea yenyewe kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Nikafungua macho yangu ili
nione na nikajaribu kuizuia isitetemeke, lakini Roho Mtakatifu aliendelea
kuiongoza licha ya utashi wangu na mawazo yangu. Utashi wangu na mawazo yangu
vilikuwa vimeambatana tu na kazi ya Roho Mtakatifu.
Dada,
Baek Bong-Nyo: * Bwana
aijaribu imani yangu
Wakati
nikiomba, Yesu alikuja na kusema, “Bong-Nyo, leo
nataka nikujaribu ili nione ni kwa kiasi gani imani yako imekua. Je, uko
tayari?” Nikajibu kwa ujasiri, “Ndiyo, Bwana. Niko tayari.”
Akatoweka na mara malaika wakaja wakanivisha vazi lenye mabawa. Walipomaliza,
malaika wale nao mara moja wakatoweka.
Kwa
kawaida, Yesu na malaika zake huniongoza hadi Mbinguni au Kuzimu, lakini
haikuwa safari hii. Nikaanza kumlilia Mungu kwa moyo wa dhati. Roho yangu ikaanza
kupaa kuelekea Mbinguni, huku nimevaa lile vazi lenye mabawa. Lakini licha ya
kuomba kwa bidii zote, nikawa napaa chinichini tu. Ilikuwa inaudhi, lakini
sikukata tamaa. Nikaendelea tu kuomba kwa bidii. Muda si mrefu nikawa nimechoka
kabisa. Nikawa sioni kitu chochote; ilikuwa ni giza tu totoro.
Nikakumbuka
kwamba Bwana alisema anataka kujaribu imani yangu. Kwa hiyo, nikaendelea
kuomba. Kwa bahati mbaya, kila kikwazo unachoweza kukifikiria kilinitokea na
nikajikuta nimerudi kulekule nilikoanzia. Hadi sasa, kila nilipoomba kanisani,
Bwana alikuja kwangu na kunionyesha kila kitu. Nilishakuwa na majivuno bila
kujua. Nikakumbuka swali ambalo niliwauliza malaika waliokuwa wakinivika vazi
la mabawa muda mfupi uliopita. Niliwauliza Yesu alikuwa wapi na wao walinijibu,
“Sasa hivi, anasubiri kukutana na wewe kwenye kilimia (the Milky Way).” Kwa
bahati mbaya, wakati huo, nilichelewa kwa sababu nilikuwa napaa kwa kasi ndogo
sana. Imani yangu peke yangu haikuwa na uwezo wa kunipaisha kwa umbali ule.
Nikaomba kwa dhati kabisa kwa muda mrefu, lakini bado nilikuwa sioni chochote. Mawazo mengi yalipita akilini mwangu na nikaanza kutubu. Bila ya msaada wa Yesu, sikuweza kufanya chochote. Nilijihisi kama naendelea kuzama kwenye bwawa. Hali hisia zile ikaendelea hadi nilipojihisi nimefungiwa ndani ya kitu fulani. Kulikuwa na vitu vinatembea mbele ya macho yangu na nikatambua kuwa tayari nilikuwa Kuzimu, nikiwa nimefungiwa kwenye chumba cha giza.
Kwenye giza hilo, hakuna kilichokuwa kinaonekana. Mapepo yalikuwa yanajazana kunizunguka. Mapepo yasiyo na idadi yalianza kung’ang’ania miguu yangu kwa nguvu yasitake kuniachia. Yalinibana na kunivuta mikono, miguu na mwili kiasi kwamba nikawa siwezi kusogea kabisa. Nikaanza kunena kwa lugha, lakini ghafla matusi yakaanza kunitoka mdomoni bila mimi kupenda.
“Nyie, mapepo machafu! Kwa nini mnanisumbua?
Ishieni zenu huko muachane na mimi!” Sikuweza
kujizuia kulaani. Lugha zote chafu ambazo nilijifunza huko nyuma, kabla ya
kukutana na Yesu, ziliporomoka kutoka kinywani mwangu. Lakini haikujalisha ni
kiasi gani nimeyatukana yale mapepo, hayakuacha kufanya mashambulizi yao
kwangu. Nikaita, “Yesu, tafadhali nisaidie!”
Nikaendelea
kumwita Bwana na kunena kwa lugha kwa bidii. Baada ya muda nisioujua, niliweza
kwa namna fulani kuponyoka kutoka Kuzimu na kuanza kupaa kuelekea Mbinguni.
Nikawa naomba huku napaa. Kwenye anga, mapepo yeye nguvu yakaanza kunifukuza.
Nikaweza kuona waziwazi msururu usio na mwisho wa mapepo mengine nyuma yao.
Nilidhani kuwa sasa nilikuwa niko salama baada ya kuponyoka kutoka Kuzimu.
Badala yake kumbe nilikuwa naenda kukabiliana uso kwa uso na mapepo yenye nguvu
zaidi. Nikajihisi nimeingia kwenye matatizo makubwa.
Bado
nilikuwa simuoni Yesu au malaika wowote. Nikawaza, “Ina maana nitakabiliana
na hili jeshi la mapepo peke yangu!” Sikuwahi kuwaza nitakabiliana na vita
kama ile. Sikujua kuna majeshi ya mapepo kwenye anga ambayo kazi yao ni
kuwapinga Wakristo, kwa lengo la kuzuia maisha yao ya maombi. Kama mtoto
mchanga anavyotembea kwa furaha huku ameshikilia mkono wa baba yake, ndivyo
ambavyo Yesu mara zote alikuwa akiniongoza kwenda Mbinguni na Kuzimu. Nilikuwa
nimejaa ushamba fulani huku nikidhani kuwa kila kitu ni rahisi rahisi tu. Kumbe
nilikuwa nikiomba bila kujali sana.
Mapepo
yale yaliweka vikwazo zaidi kwa kila hatua niliyopiga, ili kunizuia kupiga
hatua kwenda mbele. Nililia kwa maombi ya dhati kabisa. Machozi na jasho
vilitiririka mwilini mwangu. Pepo moja likapaza sauti, “Wewe, tazama pale! Kuna maombi mengine kutoka duniani
yanapanda juu!” Kisha jingine likasema, “Hayo
maombi hayana hata nguvu wala mamlaka.” Kama vile mtu anayechuma
matunda na kuyala, mapepo yale yaliyakamata na “kuyala” maombi yale kutoka
duniani.
Hapo
nikajua kuwa kumbe maombi yasiyo na nguvu ni kazi bure. Maombi yanayofanywa
huku mtu anasinzia, haelekezi moyo wake sawasawa, yaliyojaa fikra za
kibinadamu, yaliyojaa ubinafsi, yahusuyo mambo tu ya kimwili na maombi ya nyuso
mbili – yote hayo hayana nguvu yoyote. Hayo yalikuwa ni “matunda” yaliyopendwa
sana na mapepo na yaliliwa mara moja.
Nikajua
sasa kuwa ni maombi tu yaliyojaa shauku kubwa sana ya kufa na kupona na maombi
yaliyojaa vilio vya kweli ndiyo yanayopenya anga na kufika hadi Mbinguni.
Nikajua sababu kwa nini mchungaji wetu huwa analia kwa sauti na kwa kuzama sana
anapokuwa anaomba. Mara nyingi nilikuwa nakerwa na mchungaji, na kuwaza, “Hakuna
hata watu wengi humu kanisani. Kwa nini anapaza sauti kiasi hiki? Kwani ni
lazima apayuke hivyo?” Kusema kweli, kuna nyakati nilijilazimisha tu kuomba
japokuwa nakuwa nakerwa na vilio vikubwa vya mchungaji wetu. Nikaanza kuomba
msamaha kwa kule kukerwa kwangu. Sasa najua kwa uhakika kabisa kwa nini tunatakiwa
kuomba kwa namna ile.
Nikaendelea
kuomba, bila kujua muda gani umeshapita. Na pale nilipokuwa nimechoka na
kuishiwa kabisa nguvu ndani yangu, nikaona kwa mbali nyota nyingi kutoka kwenye
kilimia (the milky way) zikiangaza. Mara moja, nikakusanya kila nguvu iliyokuwa
imebakia ndani yangu na kuanza kuomba kwa kunena. Nikafika kwenye kilimia huku
nimechoka kabisa, lakini pale ndipo mpendwa wangu Yesu aliponisalimu kwa
furaha.
Mara
Yesu aliponiona, alitoa tabasamu pana na kusema, “Bong-Nyo,
umefanya vizuri kabisa. Najivunia wewe!” Nilikuwa nina hasira
kiasi wakati huo, kwa hiyo nikamuuliza Yesu,“Bwana, kwa nini umenifanyia
hivi? Bora basi hata ungenieleza kabla. Unawezaje kuniacha tu bila hata ya
kunidokezea?” Nilipomaliza kuongea, Yesu alicheka tu. Na baada tu ya maneno
machache na Bwana, akatoweka tena! Ghafla, kila kitu kikawa giza na mara nikajikuta
nimesimama kwenye ukingo wa Kuzimu.
Bwana
ameniacha kwa mara nyingine kupima imani yangu! Mara pepo lililoonekana kama
pomboo lilijaribu kunishambulia na kuning’ata, huku likiwa limepanua kinywa
chake; likionyesha meno yake makali. Nikafanya kama nataka kuliparua na
nikasema kwa sauti, “Njoo unichukue kama unaweza.” Pepo lile likatoweka.
Kukawa
na kibarabara chembamba mbele yangu. Nikaanza kutembea kukifuata. Nikatembea
kwa muda ndipo nikaona kuna kitu kinanijia. Nilipokikaribia, nikaona ni pepo
linalotia kinyaa, lenye kichwa lakini hakuna macho wala pua. Kutoka sikio lake
la kushoto hadi la kulia kulikuwa na mkato mkubwa kwenye uso wake na meno yake
yalikuwa makali kama ya papa.
Nilipokabiliana
nalo uso kwa uso, pepo hilo nikasema, “We! Nimeshapambana na kuyashinda
mapepo makubwa kuliko wewe na kuyashinda. Wewe si lolote kwangu. Ndani yangu
umo moto uliotengenezwa na Mungu wa Utatu. Utateketea na kugeuka majivu mara
utakapogusa mwili wangu. Kama huamini njoo upambane na mimi.”
Pepo
lile likaogopa na kukimbia mbio. Nikatembea peke yangu kwenye barabara ile
ndefu isiyo na mwisho na ikaonekana kama nazidi kuzama ndani zaidi ya Kuzimu.
Nilikuwa naogopa na kutetemeka ndani yangu, lakini sikutaka kuonyesha hofu
yangu. Hivyo ikabidi niwe nimetuliza akili yangu.
Nikaendelea
kutembea kwenye ile barabara. Nikaona jani kubwa mbele yangu ambalo lilionekana
kuwa na uhai. Jani lile lilijifungua na kujifunga na likajaribu kunimeza.
Lakini nikasema kwa sauti, “Sawa! Nimekuja hapa mahususi kukuua wewe! Haya
tuone nani atapona.” Nikalishambulia kwa nguvu na mara lile pepo
likatoweka.
Nikaendelea
mbele. Nikaona kuna makundi ya mapepo, kama wadudu, pande zote za barabara
yaliyojaribu kunishika. Nikasikia milio ya kutisha ya mapepo iliyofanya mwili wangu
usisimuke. Nikasikia milio mingi tofauti, lakini nikaipuuza na kuendelea mbele
huku nikiomba kwa kunena kwa sauti. Nikapaza sauti, “Mungu wa Utatu! Nipe
nguvu! Nipe nguvu na uwezo wa kimwili na kiroho!” Nikaomba kwa dhati na ghafla, moto Mtakatifu ukaanza kuwaka ndani yangu.
Huku
nikijiuliza nimetembea umbali kiasi gani, nikadhani nimeona mwisho wa barabara
ile kwa mbali. Ghafla, mwanga mkali ukatokea mbele yangu na ikawa ni Yesu. Nikapatwa
na mshangao na kuvutiwa sana. “Ndio! Hatimaye nimeokolewa, Bwana!” Nikamkimbilia
na kumkumbatia. Bwana akanishikilia kwa nguvu kwa mikono yake na kusema, “Mpendwa wangu sana Bong-Nyo, umepambana na mengi hadi
kufika hapa! Kaa pembeni yangu na mimi nitakupa yaliyobakia.” Nikabakia
kwenye mikono ya Bwana na kufumba macho yangu ili kupumzika. Je, ilikuwa
inatokea tena? Nilipofungua macho yangu, Bwana alikuwa haonekani tena.
Nikawaza, “Nawezaje kuwa tena kwenye chumba hiki cha giza Kuzimu?” Haikujalisha
ni kwa sauti kiasi gani nimemwita Bwana, mwangwi tu wa utupu ulinijibu!
Nikamwita Bwana, lakini hakuwapo. Sikuweza tena kujizuia kuwaza kwamba Yesu
amenidanganya. Yesu akasema kwa waziwazi, “Bong-Nyo,
umefanya vizuri. Karibu unamaliza, kwa hiyo kuwa mvumilivu na upumzike hapa.”
Baada ya kusema haya, na nilipokuwa najisikia niko salama, akanijaribu tena.
Hasira
yangu haikuisha. Nikagundua kuwa nimefungiwa ndani ya sanduku la chuma kama
mnyama wa kwenye bustani ya wanyama. Kulikuwa na mapepo yasiyo na idadi yenye
sura tofauti yakizunguka lile sanduku na kunikodolea macho, huku yakijaribu
kunihoji maswali. Yalinikodolea macho, na kunidhihaki na kucheka. Kulikuwa na
maelfu ya mapepo ya kijeshi yaliyovaa helmeti za mafuvu.
Mapepo
yale yalikuwa makini kunitazama wakati nikiwa nimefungiwa kwenye lile sanduku
la chuma. Nikasema kwa sauti, “Nyie wanaharamu, ni akina nani nyie? Mnatoka
wapi?” Yakajibu, “Tumetoka kuzunguka huku na kule.
Na wewe je? Kwa nini uko humu?” Nikaeleza kwamba Yesu amenileta humu
Kuzimu, lakini ameniacha ndiyo sababu nilikuwa hapo peke yangu. Baada ya kusikia
hayo, yakanidhihaki yakisema, “Wewe, Bwana wako
wala hatakurudia tena. Huu ndio mwisho wako!”
Nikaanza
kuomba kwa sauti kwa kunena. Macho ya yale mapepo yaliyovaa helmeti za mafuvu
yakaanza kugeuka kuwa mekundu. Yakanitazama kwa hasira kali. Nguvu ya kuomba
kwa kunena ilikuwa inayalemea na nikagundua kuwa yameanza kubadilika. Kwa hiyo
nikaomba kwa nguvu hata zaidi. “Mungu wa Utatu, nigeuze niwe moto wako
uteketezao!” Mapepo yote yakavamia lile sanduku la chuma kutaka kuliharibu.
Lakini moto Mtakatifu uliowaka ndani yangu ukayateketeza yote na kuyageuza kuwa
majivu. Lakini vyuma vya lile sanduku havikuharibika, bali vilibakia kama
mwanzo.
Kwa
mara nyingine tena, milio ya wanyama mbalimbali na mapepo ikasikika kote na
ikawa kana kwamba nilishakuwa pale kwa miezi kadhaa. Haikujalisha ni kwa bidii
kiasi gani nililia na kupiga mateke na kupaza sauti, hakukuwa na njia ya kutoka
kwenye sanduku lile pale Kuzimu. Kidogokidogo, moyo wangu ukaanza kuchoka.
Subira yangu kwa Bwana ikabadilika kutoka kwenye kungoja kwa shauku na kuwa
maumivu ya moyo, lakini sikuacha kuomba.
Niliomba,
“Bwana, nahitaji nguvu. Nipe nguvu! Pia, naomba karama ya uponyaji na
unijaze kwa moto ili niweze kuyeyusha sanduku hili la chuma nitoke hapa.” Nikafungua macho yangu na nikawa bado nimo
ndani ya sanduku lile. Hakuna ndoto wala tumaini kwenye sanduku la Kuzimu! Haikujalisha
ni kwa nguvu kiasi gani nimemwita Bwana, bado nilikuwa nimenaswa ndani ya lile
sanduku! Je, hii ina maana kuwa nitateseka milele humu Kuzimu? Sikuwa tena na
nguvu za kutosha ndani yangu hata za kunyanyua kidole, nikaanguka tu kwenye
kona mojawapo. Ilikuwa kama vile nilishanaswa humo sandukuni kwa miezi minne.
Baadaye,
nikaanza kupiga kelele tena, “Bwana, nisaidie! Uko wapi?” Sikuona hata
kivuli cha Bwana wangu. Mapepo yaliendelea kuvuta na kutesa mwili wangu na
nikaendelea kupigana nayo kwa siku 15. Kwenye lile sanduku, niliweza kuhisi
kabisa siku zikipita.
“Bwana,
nisaidie! Tafadhali nitoe humu. Nisaidie kutoka mahali hapa!”
Nilikuwa kama najiomba tu mwenyewe. Nikasikia mtu akicheka. Nikasema kwa sauti,
“He! Ni sauti ya Bwana!” Bwana akatokea katikati ya mwanga mzuri na
kuliangaza lile sanduku lenye giza pamoja na maeneo ya karibu kwa mng’ao wake.
Yesu
akaanza kucheka kwa sauti hata zaidi akisema, “Mpendwa
Bong-Nyo, umejisikiaje huku Kuzimu?” Nikamhoji Bwana, “Aah Bwana.
Kwa nini umenifanyia hivi? Hivi umeamua kunifanya niteseke? Kwa nini umefanyia
hivi?” Nilikuwa nimejaa huzuni kubwa wakati nikimimina malalamiko yangu, na
Bwana akajibu, “Samahani. Nilitaka kukujaribu
wewe kibinafsi; ni kwa kiasi gani imani yako imekomaa!” Sikuwa
na cha kusema zaidi kwa hilo.
Nilipohoji
ni wapi Bwana alikuwa, alinijibu kwamba alikuwa duniani akitembelea makanisa
mbalimbali ili kuwaangalia na kuwahudumia kondoo wake awapendao. Nikakiri kwa
Bwana hisia zangu za ndani kabisa na kumwomba msamaha. “Bwana, nilikuwa
na uchungu na kukuchukia wewe sana wakati nikiwa nimefungiwa kwenye sanduku
hili Kuzimu. Unisamehe.” Sauti
yangu ilibadilika kwa malalamiko na hisia za kujihurumia wakati hisia hizo
zikijidhihirisha. “Bwana, nilikwama ndani ya sanduku hili kwa miezi minne.” Nikaanza
kulia.
Bwana aliendelea kucheka kwa sauti na mimi nikasema
kwa nguvu, “Kwa nini unafurahia hivyo kuniona
nina huzuni na nikiteseka? Nimeteseka kiasi hiki Kuzimu, lakini kwa nini
unacheka kana kwamba lilikuwa ni jambo la kufurahisha? Je, unafurahia kuniona
nikiteseka?” Akajibu kwa upole, “Bong-Nyo,
ilikuwa ni miezi miwili tu tangu uanze kuhudhuria kanisani, lakini imani yako
imekua sana. Najivunia wewe!” Akanipigapiga mgongoni.
Yesu
akaniondolea vazi lililochakaa ambalo nilivaa kule Kuzimu na akawaamuru malaika
wanivike kwa mavazi safi, yanayong’aa na yenye mabawa. Akasema, “Umestahimili mambo mengi. Kwa hiyo, sasa tukatembelee
Mbinguni!” Alinishika mkono na tukaanza kupaa kuelekea Mbinguni.
Leo ilikuwa ni siku ngumu kuliko siku yoyote niliyowahi kuiona maishani mwangu.
Ilichukua
roho yangu miaka mitatu kutoka duniani hadi kwenye kilimia (the Milky Way) na
nikatumia miezi minne na nusu Kuzimu. Ilionekana kama miaka mitatu na nusu
imepita haraka sana. Mapepo kwenye anga na ya kule Kuzimu yalikuwa imara na
yenye nguvu sana. Nisingechukua dakika moja au hata sekunde moja kwenye
mapambano nayo na kushinda bila ya ulinzi wa Bwana. Nilipofika Mbinguni,
malaika wengi walitabasamu na kunifariji. “Dada, umefanya vizuri sana!” Maneno
ya malaika yaliinua moyo wangu. Kila ninapokuwa Mbinguni, magumu yote
niliyokutana nayo Kuzimu nayasahau.
Sijui
mambo mengi, maana nimekuwa nahudhuria kanisani kwa miezi miwili tu sasa.
Kutokana na kile nilichokiona kwenye sinema na kwenye mahubiri, nimejifunza
kidogo kuhusu mtu aitwaye Musa ambaye aligawa bahari. Nilimwomba Yesu aniruhusu
nimwone Musa japo mara moja tu. Yesu aliniongoza hadi kwenye ufukwe wenye
mchanga wa dhahabu. Kwa upole, malaika walinipeleka kule. Mara tu Yesu alipoita
jina la Musa, Musa alikuja kwangu na kunisalimu kwa heshima, “Karibu mbinguni!” Musa alikuwa mrefu na
mzuri.
*
Kushuhudia miujiza ya Musa Mbinguni
Yesu
alinitambulisha kwa Musa. Nikasema, “Musa, sikujui vizuri, lakini nafahamu
kidogo kwa sababu nilisikia mahubiri ya mchungaji wangu kuhusiana na wewe.”
Akajibu, “Oh, kweli? Dada, nafurahi kwamba uko hapa!” Nikaendelea
kusema, “Ulipokuwa duniani, haukugawa bahari na kutenda miujiza mingi?”
Musa kwa unyenyekevu akasema, “Sikufanya chochote, lakini alikuwa Mungu
aliyenipa mimi nguvu na nilichofanya mimi ni kutii tu.” Nikasema, “Mimi
nimeshahudhuria kanisani kwa miezi miwili tu hadi sasa, lakini mara tu
niliposikia habari zako, nilitamani sana kukutana na wewe. Lakini Bwana mara
nyingi hunipeleka kutembelea Kuzimu, kwa hiyo kukutana na wewe haikuwa rahisi.
Natamani kushuhudia baadhi ya miujiza yako. Je, unaweza kunionyesha baadhi
yake?”
Yesu alimruhusu Musa ajenge mlima mkubwa wenye mchanga wa dhahabu. Kufumba na kufumbua, kukawa na vilele viwili vya milima. Nikampa changamoto ajenge nyumba ya ghorofa 600. Aliinua tu mkono wake hewani na kuuzungusha mara moja na zikatokea ghorofa 680 mbele yangu.
Nikabakia
kinywa wazi. Akanitengenezea ngazi ya dhahabu kutoka duniani hadi Mbinguni.
Musa akafanya miujiza mingine mingi ambayo haiwezi kuelezeka kwa maneno.
Nikasema, “Musa, unisamehe kwa imani yangu ambayo bado haijakomaa. Samahani
na najisikia aibu kwa kukujaribu hivyo na kukuuliza maswali mengi.” Akajibu, “Usijali kuhusu chochote na hata
kama bado una maswali mengine, usisite kuuliza.”
Nikaomba kuona kugawanywa kwa bahari kama ilivyoandikwa kwenye Biblia. Kuona hili lilikuwa ni jambo la kuogofya na kushangaza sana. Yesu alikuwa anatazama kimya pembeni yangu. “Yesu, Musa, mimi ni mwamini mpya na sijui mambo mengi, kwa hiyo nadhani nimekuwa wazi sana kuhusu maswali yangu. Tafadhali mnisamehe. Samahani. Nikirudi tena kanisani, nitaandika na kumshirikisha mchungaji wangu kile nilichokiona, ili kwamba auelezee ulimwengu.” Yesu akasema, “Musa, Dada Baek Bong-Nyo anatakiwa arudi duniani, kwa hiyo muage.” Kwa heshima, Musa aliinamisha kichwa chake na kusema, “Kwa heri dada.”
Yesu
akanielezea, “Hata Mbinguni, Musa huwa yuko na
kazi nyingi muda wote. Huwa anasafiri kote Mbinguni na ana mambo mengi ya
kuyafanya.” Sitasahau nilivyokutana na Musa Mbinguni. Yesu
aliniongoza kurudi kanisani na nikamalizia maombi yangu.
No comments:
Post a Comment