Tuesday, April 3, 2018

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 13


 Related image
==== SIKU YA 22 ==== (1 Petro 1:6-9) * Pepo linapiga kinanda
Lee Yoo Kyung
Nilipokuwa nikiomba, pepo lenye uso mweusi na macho manne lilikuja na kukaa kwenye kiti cha mpiga kinanda. Likaanza kuhangaika pale huku likijaribu kupiga kinanda. Huku nikiwa nimekereka, nilipaza sauti na kusema, “Ewe pepo mchafu! Kwa nini unachezea kinanda cha dada yangu Joo Eun? Kinanda hicho huwa anakitumia wakati wa ibada za kuabudu.” Likanitukana na kuniambia nifumbe kinywa changu. Kwa hiyo nikajawa na hasira. “Nini? Unanionyesha dharau? Wewe umekufa!” Nikalikimbilia na kulikamata. Nikanyonga shingo yake na kupigiza kichwa chake chini sakafuni.

Wednesday, March 21, 2018

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 12


==== SIKU YA 21 ====
Kim, Joo-Eun:
Nilikuwa kwenye moto, nikiomba kwa kunena. Madragoni (mazimwi) matatu ya kutisha yakatokea. Dragoni la kwanza lilikuwa na michoro mingi na maumbo ya duara kwenye mwili wake wote mwekundu. Dragoni la pili lilikuwa na mistari myekundu na buluu ya wima iliyochanganywa pamoja kiasi kwamba ilinifanya kuchanganyikiwa nilipoitazama. Dragoni la tatu lilikuwa na mistari ya buluu na njano ya ulalo iliyochanganywa pamoja. Yalikuja kama vile yanataka kunimeza mzimamzima, lakini nilipaza sauti mara tatu kwa uthabiti, “Kwa Jina la Yesu, ondokeni kwangu!” Yakakimbia.

Monday, December 11, 2017

Kubatizwa kwa Moto Uwakao - 11


 
==== SIKU YA 20 ==== (Matendo 1:8)
* Kim, Joo-Eun ayashambulia mapepo!
Mchungaji alituambia tusiyaogope mapepo, bali tuyashambulie moja kwa moja. Alisema kwa ujasiri, “Yakanyageni na yapeni uchungu! Ng’oeni macho yao na myapondeponde. Yakamateni na kuyatikisa mahali pote.” Ilikuwa inafurahisha na ilitupa nguvu sana. Kwa kuwa huwa ninaogopa kirahisi, mchungaji aliniambia nisionyeshe kabisa woga vinginevyo mapepo yatashambulia zaidi. Niliamua kuwa imara.