Je, umewahi kusikia juu ya ile inayoitwa Injili ya
Barnaba? Hii ni injili ya namna gani?
Injili ya Barnaba ni kitabu kikubwa karibu sawa na Injili zote za kwenye Biblia zikichanganywa pamoja. Injili hii inapendwa na kusambazwa sana kwenye ulimwengu wa Kiislamu, wakidai kwamba ndiyo injili sahihi kabisa.
Injili hii inadai kwamba iliandikwa na mmojawapo wa mitume wa Yesu Kristo aliyeitwa Barnaba.







